Nakubaliana nawe mkuu alafu samahani ni Mkuru na si mkura najua ni typing error tu lakin nilikua najaribu tu kumpa mawazo tofauti kama ulivochangia mwenzangu yeye ndo mwenye pesa mwsho wa ciku mwamzi mkuu ni yeye lakn akhasante tupo pamoja
samahani mkuu
ni mawazo mazuri ila hilo la kilimo cha kitunguu ni bora zaidi cha muhimu ni kufanya utafiti wa masoko hasa nchi za jirani
ahsante Sana Mkuu!!
Jaribu kuangalia pia uwezekano wa kufungua duka la nafaka za vyakula mbali mbali kaa vile mchele n.k. ambavyo unaagiza au unavifuata Dubai. Nimewahi kusikia hii nayo ina faida kubwa sana ila sina details.
Kiongozi, kila kitu nilichotaka kukwambia ushaambiwa.
ukishindwa yote, jaribu kusoma alama zanyakati... i mean, 2015 hii hapa..jaribu kuwekeza kwenye uheshimiwa..!!
Duhh,katika Post zote tangu nimejiunga Jamii forum sio siri hii imekaa kiaina yake.Nimeipenda Sana.Wajameni nina 5M ninataka izunguke ilinipate japo pesa ya kulipia mtoto ada bila kubangaiza.
Msaada wenu wa mawazo nitauheshimu sana na kama nikifanikiwa na idea ya mtu baada ya miaka miwili au mitatu sitamsahau japo kwa zawadi ya shukurani.
Mwenzenu kwenye matatizo na raha.
Inategemea na sehemu ulipo:
(1)Binafsi ningekushauri ufungue duka la spare za pikipiki kwa mtaji huo almost utapata unit atleast kumi za vipuri mhimu kulingana na sehemu husika.
2) Jikite kwenye kilimo cha matikiti maji. Anza na ekari mbili kwa mtaji wa 2M. Ukitaka mchanganuo wa kilimo hiki nitakuelekeza hapahapa jukwaani.
Bajaj sasa hivi ni biashara ngum sana,wanalia watu na wengi wanatoka kwenye soko.Itakuwa kama kesi ya pick up yako.Nashukuru. Biashara za vyombo vya usafiri zimenishinda ndugu yangu, nilikuwa na pick up ilileta faida kwa muda baadaye madereva wakaanza kuleta pesa ndogo na hicho kiduchu nilichopata kiliishia garage. Wewe kwa experience yako unadhani Bajaj itakuwa tofauti?
Mkuu xfactor wanunuzi wanakuja shamba mkuu kama utalihudumia shamba ipasavyo na kupata mavuno mazuri.
Mhimu:
Tafta soko kabla hujalima.
Epuka walanguzi hasa wale wa meza za sokoni, ukifanya nao biashara usiruhusu aje shamba. Kama atahitaji mzigo, mpelekee sample na sisitiza shehena anayohitaji na usizidishe. Hakikisha bei ni flat rate kabla ya delivery.
Usimamizi ndiyo kila kitu ili kuyafikia malengo yako.
Twendeni shamba, Hima sasa!!
Mkuu xfactor,
Mito ipo mingi tu. Cha mhimu ni target ya soko na roho ya uthubutu. Mwenzenu nilirudisha vyeti kijiji kwa Mama nikaukana utumwa japo haikuwa jambo dogo kushawishi wazazi. Ila penye nia pana njia na sio jambo dogo kuacha kazi na kuamua kufanya yako tena maporini!
Mkuu xfactor,
Mito ipo mingi tu. Cha mhimu ni target ya soko na roho ya uthubutu. Mwenzenu nilirudisha vyeti kijiji kwa Mama nikaukana utumwa japo haikuwa jambo dogo kushawishi wazazi. Ila penye nia pana njia na sio jambo dogo kuacha kazi na kuamua kufanya yako tena maporini!
Mchanganuo wa kilimo cha matikiti;
1)Kawaida ekari moja ina sqm4000
2)spacing ya matikiti ni m1.5shimo na m1.6 mstari. Acha mashina2 na matunda3 kila shina.
3)tumia mbegu ya hybrid aina ya sukariF1 ambapo kwa ekari moja itakugharimu Tshs260k
Tumia mbolea ya kinyesi cha kuku kama itapatikana kilahisi au nenda dukani kwajl ya mbolea ya kupandia na kuboresha matunda ambayo haitazidi tsh200k.
4) waterpump ya kichina horsepower5.5 3" inatosha kumwagilia eneo kubwa hata ekari5 na gharama yake(complete) haizidi tsh800k.
5)gharama ya kulima +viuatilifu haizidi tsh400k.
6) bei ya kuuza shambani kwa tikiti moja la hybrid ni tsh1500 na inachukua siku60 kukomaa.
Ukishusha hesabu hapo juu utapata kifuatacho:
4000/(1.5*1.6)*2*3*1500= TSH 15,000,000/=
COST(TSH 1,660,000/=)
FAIDA= TSH14,600,000/=
Fanya umepata faida ya TSH 10,000,000/=
cc WILE xfactor Zanzibar spices BAK etc
Umetafutaje hela wakati hujui cha kufanyia? Anyway, fuga kuku wa mayai itakutoa sana mjini ama anzisha nyama choma kijiwe!!