Milton Mahanga: RC Makonda jisafishe na kashfa hii au jiuzulu

Hakika mimi nimejifunza kwa mh makonda kutokukata tamaa ukweli kama hiyo cv ni yake anastahili kuwa Rais wa nchi hii amepigania masomo bila kuchoka kama amefeli darasa la saba mara tatu lakini bado alipambana mpaka chuokikuu hakika huyu anastahili pongezi sana.
Mhe saluti kwako endelea kupambana usiogope wakosoaji wewe ni mfano wa kuiga kwa vijana
Hatahivyo cheo cha mkuu wa mkoa ni kidoga sana kutokana na juhudi zako
 
Et makonda ana chet cha div 0 ?????? alaf et mnadai miaka ya nyuma MTU alikua akipata div 0 anapewa cheti jaman kwan makonda kazaliwa mwaka gani kama sio 1980's sa miaka hyo kulikua na chet chenye div 0? Acheni mbwembwe ww mwenye div 1 tuambie ww ni mkuu wa mkoa gani sasa
 
Kweli mkuu jamaa kahaso Sana ila kilichomualibia Ni kukosa nidhamu ya matumizi..
Mzee Warioba alimchunia tu Kijana akajua kijana anapambania Tumbo na Kipind kile alikua na mtetezi Marehemu........

Kijana akaona ndo mfumo uo wakujipatia Vyeo sasa Ameingia Choo Cha watoto wadogo wa Kike........

Angetuliaga tu afanye yake ila tu Kama ni kweli jamaa ndo DAUDI BASHITE.......!
 
LeMutuz baharia, Bwana mkubwa mvuvi, hawa jamaa tungewapa Mv Dar es Salaam, wangeingizia nchi kipato kikubwa sana.

Yaani Mkuu hiyo team bomba sana. Tungepata [emoji886],salmons,vibua vya kutosha soko lote la ferry lingefurika.
 
Ukiona zinakuchosha ZIMA DATA.
 
Asante kaka hebu waambie naona Vijana wanamoto sana
 
VIPI CV YA KIELIMU YA MWENYEKITI FREEMAN MBOWE AU BWANA GASTURA NAE VIPI AJIUZULU UENYEKITI AU MNAMSHAURIJE??
Ha ha ha! Nadhani Freeman Mbowe ni yeye yule tangu 1961 hadi mwisho wa maisha yake. Freeman amebaki kuwa Freeman tangu mwanzo wa maisha yake.

Wife enzi hizo alitaka eti kubadili jina baada ya kumwoa achukue la kwetu; nikamwambia mama; baki na jina lako mimi ni mumeo tu sio babako baki na jina la kwenu huko ulilosomea. Ukishaona figisu figisu za kubadili majina ujue hapo kuna "kiza". Kuna mchezo mchafu unataka kuchezwa na wengi wamefanya hivyo.
 
huyu jamma sijui mahanga na muona bonge la gharasha hivi huyu si alituhumiwa kuwa na vyeti feki vya phd yake vip alishaawahi kulitolea maelezo japo kidogo
Nyie watu mnachekesha sana! Hajawahi kulitolea maelezo basi yatoeni hayo maelezo kama mnayo kama alivyofanya yeye kwa "mtuhumiwa". Kama mnao ushahidi wa vyeti vyake feki wekeni ushahidi huo hadharani mtakuwa mmelisaidia sana taifa.
 
Kwanza Mr.Milton Mahanga, Mimi nakushangaa sana we we binafsi kuibeba hoja ya uhalali wa vyeti vya Mh. Rc Makonda, ningependa sana utujibu sisi wana Dsm kwa maswali haya yafuatayo:
1. Kwanini uhoji Elimu ya Rc Makonda baada tu ya mchakato wa kupambana na mihadarati? Tatizo lako ni nini ? Hasira yako juu ya vita hii ni nini ?
2. Kwa nini wewe utembee na madai ya Mch. Gwajima? Je kwanini malalamiko ya Gwajima unayaamini na kuyafanya ndiyo msingi wa madai yako? Kwa nini usimfuate Gwajima au yule mtoto wa Sitta ili akuthibitishie kuwa nikweli Rc alitumia cheti chake?
4.Je unamtaka Rc Makonda kujiudhuru ili uendeleze biashara yako ya mihadarati? Huoni kuwa biashara yako hii ni hatari sana kwa mstakabali WA nguvu kazi ya Taifa hili? Je kazi anazozifanya Rc Makonda ziko chini ya kiwango? Je kushughulikia vita dhidi ya madawa ya kulevya hakuna maana kwa vile tu Gwajima kaguswa?
5.Kama Rc Makonda alifeli masomo nakuishia Std 7 sasa amewezaje kujiendeleza hadi kufanikiwa kufika huko alikofikia? MTU ambaye hats Secondary amefika kwa Magumashi anaweza kuongelea mambo yanayouhusu Mkoa wetu wa Dsm kwa ufasaha kiasi ambacho huenda ni wakuu wa Mkoa wa Dsm wachache sana kuwahi kutokea ktkt historia ya Taifa hili, kwa uchace naweza kukumbusha; Rc. Mama Chipungahelo, Rc.Makamba, Rc, Kandoro na Rc Makonda.
6. Nikuonavyo Mimi We we Milton Mahanga, huenda yafuatayo nidhahili mbele yako,
(a). Huenda wewe Unajishughulusha na Madawa ya kulevya.
(b). Huenda wewe umetumwa na kulipwa na Watuhumiwa wa madawa ya kulevya akina, Mowe, Gwajima na wengineo ili ujaribu kumvunja moyo Rc Makonda jambo ambalo hatutegemei Kamwe. Makonda ni jasiri, Makonda ni Msomi wa Ukweli na ni kiongozi mahiri asiyeteteleka hats kidogo, na ni muelwa, nikiongozi sahihi na hatababaishwa na Unafiki na Uzushi wa kizandiki unaoletwa mitandaoni na watu ambao wana miyo na mitizamo ya KISHETANI, hawana Huruma na vijana, watoto, watu wetu kuangamia kwa madawa haramu ya kulevya, watu kama akina Milton Mahanga wao wanajali matumbo yako zaidi pale wanapolipwa hivyo visenti ya kununulia MB wanakuwa tayari kuuza uhai wa watu wengine, na wanadiriki kukatisha tamaa juhudi chanya za vita dhidi ya madawa ya kulevya, vita ambayo kila Mtanzania mwenye Huruma na Taifa hili hawezi kuhangaika na ujinga na upuuzi WA kuhoji Elimu ya Rc Makonda nahata kufikia hatua ya kumtaka ajiudhuru !!!!!. Huh ni ujinga na upumbavu uliopitiliza, na unafaa kupuuzwa na kila Mtanzania mpenda Maendeleo.
MH. MKUU WA MKOA MAKONDA ENDAPO UTAYAONA MAWAZO YANGU HAYA, NAKUSHAURI IFUATAVYO;
1.ACHANA NA UPUUZI HUU, HUNA HAJA YA KUJIBU UJINGA.
KAMA WAO WANATATIZWA NA ELIMU YAKO, WAO NDIYO WATHIBITISHE SIYO WEWE WANAYEKUTUHUMU NDIYO UTHIBITISHE. WAJIBU WA MTU ANAYEKUTUHUMU NIKUTHIBITISHA PASIPO SHAKA KWAMBA TUHUMA DHIDI YA MTUHUMIWA NI ZA KWELI.

ULIWAHI KUONA WAPI MTU ANATUHUMIWA WIZI, YEYE MWENYEWE TENA ATHIBITISHE KUWA NI MWIZI AU SIYO MWIZI. MAKONDA OYEEEEEEE.
 
Punguani kweli wewe! Ikithibitika ni forgery mahali pake ni jela, viboko, na kazi ngumu. Acheni kuupamba uhalifu kwa lugha laini. Eti mpambanaji; mbona hakupamba huko O-Level? Watu wameumia, wame-toil vya kutosha halafu wengine kiusanii usanii wana-excel? Kama Serikali imeamua kuweka level ground iwe kwa wote na sio kuumiza wengine na kupendelea wengine.
 
Pumbavu ..
 
Nimesoma wasifu unaozunguka humu kumhusu mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Mhe huyu ni mpiganaji na mpambanaji ambae hakati tamaa pamoja na kufeli kwake lakini bado alihakikisha anataifuta elimu, CV inaonesha alifeli mara mbili darasa la nne hapa angeliweza kukataa tamaa na kuacha shule lakini bado alipambana, hata chuo kikuu amedisco mara mbili lakini hakukata tamaa bado alipambana kuhakikisha anapata Elimu, huu ni mfano bora wa vijana inabidi kupambana kama alivyopambana mkuu wa mkoa.

PAUL MAKONDA:
1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya
Misungwi, mkoa wa Mwanza.
2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bashite
3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya
msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bashite .
Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.
4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza
mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).
5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa
kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.
6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya
sekondari ya Pamba.
7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri
(division zero).
8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg. Paul Christian
Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha
uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa
masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.
9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg. Paul Christian
Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa
masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN
MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.
10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg. Benjamin Sitta (mtoto wa
Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Meya wa Kinondoni kwa
sasa). Wakawa marafiki.
11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi,
aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada
lakini akakosa nafasi.
12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa
Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta).
Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha
elimu ya juu.
13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara
Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa
kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya
Mbegani).
14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management &
Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa
kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati
ya Course 8 alizokuwa akisoma (akawa discontinued).
15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza
first year akiwa na carries 3 ambazo alienda nazo 2nd year.
Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya
course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na
supplementary. Akaamua kuacha chuo.
16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu
SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.
17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya.
Akaachana na CMA akachagua Community & Economic
Development (CED).
18. Mwaka 20012 akahitimu shahada ya kwanza ya
Community & Economic Development kwa jina la Paul C
Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi Albert Bashite
19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani
kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge
lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda
baada ya kuapa mahakamani.
20. Ndugu Daudi Albert Bashite ameoa (tangu mwaka 2009)
lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye Mkuu wa Mkoa wa
Dar es Salaam kwa sasa.
 
kweli nimeamini..ki.laza hutetea kila.za mwenziwe......dogo haelewi anazungumzia nini.....
 
Sasa nimeamini, Mtu mpaka apate njia, kweli. Historia ya Mtu ni Msitu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…