Milton Mahanga: RC Makonda jisafishe na kashfa hii au jiuzulu

Milton Mahanga: RC Makonda jisafishe na kashfa hii au jiuzulu

foggery kwa ubushi wangu lawyer umeondoa credibility ya chochote atakachokifanya mbele za raia kwa sasa hivi makonda jina lake limeandikwa kwa chaki kwenye blackboard hata upepo ukipita unalifuta(he is exposed na ni mtuhumiwa)
 
Kwa uandishi wako hutofautiani na unayemtetea. Waliofeli miaka ya nyuma hata ukiwa na 35 ulikuwa unapata cheti je unajua hilo?
Unapo Zunguamzia miaka ya Nyuma unanaanisha kuanzia mwaka gani labda?
 
Anaandika Milton Mahanga
RC MAKONDA JISAFISHE NA KASHFA HII AU JIUZULU

Hebu Mkuu wetu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, kama hii "CV yako" inayotembea mitandaoni ikisemekana imethibitishwa na Mchungaji Gwajima ni ya uongo, tunaomba uikanushe na uweke CV yako ya kweli ili kuweka heshima yako na nafasi yako, na ili sisi wakazi wako wa Dar es Salaam tuwe na imani na wewe bosi wetu. La sivyo kama ni kweli chukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu nafasi yako ya ukuu wa mkoa.
=========================

CV YA PAUL MAKONDA

1. Alizaliwa tar.15/02/1981 katika kijiji cha Koromije, wilaya ya Misungwi, mkoa wa Mwanza.

2. Majina yake halisi ni Daudi Albert Bushite

3. Alianza darasa la kwanza mwaka 1988 katika shule ya msingi Koromije akitumia majina ya Daudi Albert Bushite. Mwaka 1991 alifeli darasa la 4, akarudia.

4. Mwaka 1992 alifeli tena na hivyo akahamishiwa Mwanza mjini, ili aweze kusoma na kupata masomo ya jioni (tuition).

5. Mwaka 1996 alihitimu darasa la 7 lakini hakuchaguliwa kuendelea na elimu ya sekondari katika shule ya serikali.

6. Mwaka 1997 akajiunga na kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamba.

7. Mwaka 2000 akahitimu kidato cha 4 na kupata daraja sifuri (division zero).

8. Mwaka 2001 akatumia cheti cha Ndg.Paul Christian Muyenge (chenye div.3 ya points 25) kujiunga na chuo cha uvuvi Nyegezi (Nyegezi Fisheries Training Institute) kwa masomo ya Certificate akahitimu mwaka 2002.

9. Mwaka huohuo 2002 akitumia cheti cha Ndg.Paul Christian Muyenge, alijiunga na Chuo cha uvuvi Mbegani Bagamoyo kwa masomo ya Diploma ya uvuvi (ORDINARY DIPLOMA IN MASTER FISHERMAN, NTA LEV.6), na kuhitimu mwaka 2005.

10. Mwaka 2003 alikutana na Ndg.Benjamin Sitta (mtoto wa Marehemu Samwel Sitta, ambaye ni Mayor Kinondoni kwa sasa). Wakawa marafiki.

11. Mwaka 2005 baada ya kuhitimu Stashahada yake ya uvuvi, aliomba admission Chuo cha Kilimo Sokoine kusoma shahada lakini akakosa nafasi.

12. Baada ya kukosa nafasi alienda kuishi nyumbani kwa Marehemu Sitta akiwa kama rafiki wa Ben (mtoto wa Sitta). Kwakuwa alitoka familia duni, Sitta aliahidi kumsomesha elimu ya juu.

13. Mwaka 2006, alipata udahili Chuo cha ushirika na biashara Moshi (wakati huo kikiwa chuo kikuu kishiriki cha SUA), kwa kutumia vyeti vyake vya certificate (ya Nyegezi) na diploma (ya Mbegani).

14. Alidahiliwa kwa course ya BA in Cooperate Management &Accounting. Mwaka 2007 alimaliza first year lakini akashindwa kuendelea na 2nd year baada ya kupata Suplementary 6 kati ya Course 8 alizokua akisoma (akawa discontinued).

15. Mwaka huohuo 2007 akaomba Admission upya. Akamaliza first year akiwa na carriers 3 ambazo alienda nazo 2nd year. Mwaka 2008 akiwa 2nd year akapata supplementary 4 kati ya course 8 alizokua akisoma. Akawa na mzigo wa carry over na supplementary. Akaamua kuacha chuo.

16. Mwaka 2008 akaenda kujaribu kuomba udahili chuo kikuu SUA kwa mara nyingine lakini akakosa.

17. Mwaka 2009 akarudi tena MUCcoBS kwa udahili mpya. Akaachana na CMA akachagua Community &Economic Development (CED).

18. Mwaka 2012 akahitimu shahada ya kwanza ya Community &Economic Development kwa jina la Paul C Makonda badala ya majina yake halisi ya Daudi A Bushite

19. Jina Makonda analitumia baada ya kula kiapo mahakamani kubadili jina. Cheti cha Form four kinasomeka Paul C Muyenge lakini vyeti vya elimu ya juu vinasomeka Paul C Makonda baada ya kuapa mahakamani.

20. Ndugu Daudi Albert Bushite ameoa (tangu mwaka 2009) lakini hajabahatika kupata mtoto. Na ndiye mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa sasa.
Daudi BASHITE...
 
Angekuwa mpambanaji asingefoji vyeti.......angepambana kiuhalisia kutimiza malengo yake.......mpk kufoji vyeti ni wazi alikata tamaa ndio akatafuta mkato.......hata hivyo nampogeza alipofikia sio pakubeza.
alichoweza ni wachache wanakithubutu
 
And that is what makes a man the really man
Really ni uhalisia..sasa huo uhalisia kwa bwana. DAUDI BASHITE upo wp?na VYETI vya mwenzie?uhalisia wake ni DAUDI BASHITE.. na sio PAUL MAKONDA...
 
Daudi wewe ni mwamba ulimshinda hadi goliatl mwili nyumba amka pambana hata kama vyeti ni vya Paul piga kazi usiogope though Acha mbwembwe na ujuha. ...
 
At least ungetoa mfano wa nape nauye ambaye alifeli ila hakufoji vyeti akahustle kwa kuunga unga unga weeeeee hadi leo hii ana Masters bila kufoji vyeti wala shortcut.

Sasa kituko ni wwe kumsifia makonda ambaye kahustle kwa kufoji vyeti??? Ungesema alifeli afu akaendelea kuunga unga hadi leo hii ndobapate degree hapo ningekuelewa ila kwa kutumia jasho la mtu mwingine ili aendelee ma shule sio kuhustle ni UHUNI......
 
alichoweza ni wachache wanakithubutu

Maisha ya kufoji foji na kuunga unga mbona rahisi sana na kila mtu anaweza akiamua..
Issue ni kutumia akili kufanya vizuri darasani na kunyooka mpaka chuo kikuu na si kuunga unga.
 
Back
Top Bottom