Milton Mahanga: RC Makonda jisafishe na kashfa hii au jiuzulu

Milton Mahanga: RC Makonda jisafishe na kashfa hii au jiuzulu

Nakumbuka k/ndoni alisema hajaridhika na watumishi hewa waliopatikana bwana yule akamsifia sana. Nadhani huu ni muda sasa bwana yule kuwasifia waliowezesha kujua malaika mdg kafoji csee
 
Mwacheni apumue haa!
ushauri wa bure kwa Makonda tunaomba uikanushe na uweke CV yako ya kweli ili kuweka heshima yako na nafasi yako, na ili sisi wakazi wako wa Dar es Salaam tuwe na imani na wewe bosi wetu. La sivyo kama ni kweli chukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu nafasi yako ya ukuu wa mkoa.
Tuliambiwa hukuna jiwe litakalosalia bila kugeuzwa.
 
Wanamajibu yao mepesi sana, wanasema eti ni mambo ya mtandaoni, mara wanaomchafua ni wauza madawa ya kulevywa.
Hahahaaaaa, hapa hata wale wafunga kamba zake za viatu Clouds hawaliongelei hili, wala hawampigii simu mubashara atoe maelezo.

Sipati picha kama angekuwa mh. Mbowe ndiyo kanunua cheti, mikutano na waandishi wa habari ingekuwa imefanyika kama 6 mpaka sasa.
<<Mungu wa mbinguni hafanyiwi usanii>>.
Makonda anaogopa nini kuonyesha vyeti kuondoa utata huu. Ukweli siku zote haupingiki
 
Naunga mkono hoja. Sisi wengine tulimkubali sana hadi tukampigia chapuo
Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam

Na baada ya kuamsha vita ya madawa ya kulevya, tukampigia chapuo lingine
Baada ya Magufuli, 2025 Makonda atatufaa sana, kwasababu ana uthubutu kuliko hata JPM!. Apunguze....

Paskali
Kaka pasco hatukatai makonda anauthubutu lakini tunataka uthubutu utakaoendana Na sheria Na taratibu za nchi. Na tukiangalia ktk uthubutu uliotumika ktk sakata la madawa ya kulevya hauna tija Maana hawa watu inavyoenyesha hawatafungwa kwakuwa ushahidi umeelemea ktk taarifa za kuambiwa zaidi kuliko watuhumiwa kunaswa Na madawa. Ikiwa lengo lilikuwa kuwadhalilisha watuhumiwa basi wamefaulu lakini ikiwa lengo ilikuwa watuhumiwa waadhibiwe kwa mujibu wa sheria za nchi itakuwa wamefeli.
Lakini baada ya kuanza huu mjadala wa vyeti feki wa makonda nadhani halaumiki sana Kwani njia alizotumia au anazotumia ktk maamuzi mengi aliyowahi kuyafanya yanaendana Na uwezo wake aliokuwa nao darasani Kwahiyo anastahili kusaidiwa zaidi kuliko kulaumiwa japo sheria ifuate MKONDO wake.
 
Mkuu taarifa za siri kama hizi huwezi kuzipata kirahisi kabisa. Watu wa karibu yake sana ndo watakuwa wanazitoa safi sana
Nilichogundua ni kwamba hizi habari za siri kabisa zinatolewa na watu wake wa ndani kabisa.. Tena wanachama wenzake aliowahi kuwakera!
 
Kufeli darasani siyo kufeli maisha. Wangap wanazunguka na mavyeti yao lakini hawana cha maana wengine wanauza magenge nna wengine wameajiriwa kariakoo kwenye maduka ya nguo. Ebu pale mtu anapopambania kitu usimkatishe tamaa na kutafuta sifa zisizo na maana. Wengine wanaomsema makonda kanunua cheti ukute yeye si lolote si chochote. Tujifunze kwake
 
Kaanzishe mada yako kuhusu Mbowe hii inamuhusu Paulo Makonda
VIPI CV YA KIELIMU YA MWENYEKITI FREEMAN MBOWE AU BWANA GASTURA NAE VIPI AJIUZULU UENYEKITI AU MNAMSHAURIJE??
 
Kwanza Mr.Milton Mahanga, Mimi nakushangaa sana we we binafsi kuibeba hoja ya uhalali wa vyeti vya Mh. Rc Makonda, ningependa sana utujibu sisi wana Dsm kwa maswali haya yafuatayo:
1. Kwanini uhoji Elimu ya Rc Makonda baada tu ya mchakato wa kupambana na mihadarati? Tatizo lako ni nini ? Hasira yako juu ya vita hii ni nini ?
2. Kwa nini wewe utembee na madai ya Mch. Gwajima? Je kwanini malalamiko ya Gwajima unayaamini na kuyafanya ndiyo msingi wa madai yako? Kwa nini usimfuate Gwajima au yule mtoto wa Sitta ili akuthibitishie kuwa nikweli Rc alitumia cheti chake?
4.Je unamtaka Rc Makonda kujiudhuru ili uendeleze biashara yako ya mihadarati? Huoni kuwa biashara yako hii ni hatari sana kwa mstakabali WA nguvu kazi ya Taifa hili? Je kazi anazozifanya Rc Makonda ziko chini ya kiwango? Je kushughulikia vita dhidi ya madawa ya kulevya hakuna maana kwa vile tu Gwajima kaguswa?
5.Kama Rc Makonda alifeli masomo nakuishia Std 7 sasa amewezaje kujiendeleza hadi kufanikiwa kufika huko alikofikia? MTU ambaye hats Secondary amefika kwa Magumashi anaweza kuongelea mambo yanayouhusu Mkoa wetu wa Dsm kwa ufasaha kiasi ambacho huenda ni wakuu wa Mkoa wa Dsm wachache sana kuwahi kutokea ktkt historia ya Taifa hili, kwa uchace naweza kukumbusha; Rc. Mama Chipungahelo, Rc.Makamba, Rc, Kandoro na Rc Makonda.
6. Nikuonavyo Mimi We we Milton Mahanga, huenda yafuatayo nidhahili mbele yako,
(a). Huenda wewe Unajishughulusha na Madawa ya kulevya.
(b). Huenda wewe umetumwa na kulipwa na Watuhumiwa wa madawa ya kulevya akina, Mowe, Gwajima na wengineo ili ujaribu kumvunja moyo Rc Makonda jambo ambalo hatutegemei Kamwe. Makonda ni jasiri, Makonda ni Msomi wa Ukweli na ni kiongozi mahiri asiyeteteleka hats kidogo, na ni muelwa, nikiongozi sahihi na hatababaishwa na Unafiki na Uzushi wa kizandiki unaoletwa mitandaoni na watu ambao wana miyo na mitizamo ya KISHETANI, hawana Huruma na vijana, watoto, watu wetu kuangamia kwa madawa haramu ya kulevya, watu kama akina Milton Mahanga wao wanajali matumbo yako zaidi pale wanapolipwa hivyo visenti ya kununulia MB wanakuwa tayari kuuza uhai wa watu wengine, na wanadiriki kukatisha tamaa juhudi chanya za vita dhidi ya madawa ya kulevya, vita ambayo kila Mtanzania mwenye Huruma na Taifa hili hawezi kuhangaika na ujinga na upuuzi WA kuhoji Elimu ya Rc Makonda nahata kufikia hatua ya kumtaka ajiudhuru !!!!!. Huh ni ujinga na upumbavu uliopitiliza, na unafaa kupuuzwa na kila Mtanzania mpenda Maendeleo.
MH. MKUU WA MKOA MAKONDA ENDAPO UTAYAONA MAWAZO YANGU HAYA, NAKUSHAURI IFUATAVYO;
1.ACHANA NA UPUUZI HUU, HUNA HAJA YA KUJIBU UJINGA.
KAMA WAO WANATATIZWA NA ELIMU YAKO, WAO NDIYO WATHIBITISHE SIYO WEWE WANAYEKUTUHUMU NDIYO UTHIBITISHE. WAJIBU WA MTU ANAYEKUTUHUMU NIKUTHIBITISHA PASIPO SHAKA KWAMBA TUHUMA DHIDI YA MTUHUMIWA NI ZA KWELI.

ULIWAHI KUONA WAPI MTU ANATUHUMIWA WIZI, YEYE MWENYEWE TENA ATHIBITISHE KUWA NI MWIZI AU SIYO MWIZI. MAKONDA OYEEEEEEE.
Mbona umepaniki sana jambo rahisi sana mwambieni Makonda tunaomba uikanushe na uweke CV yako ya kweli ili kuweka heshima yako na nafasi yako, na ili sisi wakazi wako wa Dar es Salaam tuwe na imani na wewe bosi wetu. La sivyo kama ni kweli chukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu nafasi yako ya ukuu wa mkoa.
 
Baadhi ya sifa za kuwa mtumishi wa Mungu.
-Kuwa na busara.
-Weka hakiba ya Maneno.
-Usiwe mropokaji.
-Usiumie madhabahu kwa mambo binafsi.
Umeongea point mkuu, gwajima hana hekima ya kimungu, anatumia vibaya madhabau ya Mungu
 
Ndo matatizo ya JF kutokuweka mipaka ya umri wa kujiunga humu. Wewe mleta mada usichokijua ni kwamba miaka ya nyuma watu walipata vyeti mpaka waliokuwa na negative ( Kama ipo). Na hii sheria ya kuwanyima watu vyeti waliopata zero ni ya juzi tu. Uliza Wazazi wako Kabla ya kubandika upuuzi wako hapa.
Labda atakuelewa maana alivyoguswa daudi bashite watu wa lumumba povu linawatoka kweli...
 
Back
Top Bottom