Milton Mahanga: RC Makonda jisafishe na kashfa hii au jiuzulu

Nakumbuka k/ndoni alisema hajaridhika na watumishi hewa waliopatikana bwana yule akamsifia sana. Nadhani huu ni muda sasa bwana yule kuwasifia waliowezesha kujua malaika mdg kafoji csee
 
Mwacheni apumue haa!
ushauri wa bure kwa Makonda tunaomba uikanushe na uweke CV yako ya kweli ili kuweka heshima yako na nafasi yako, na ili sisi wakazi wako wa Dar es Salaam tuwe na imani na wewe bosi wetu. La sivyo kama ni kweli chukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu nafasi yako ya ukuu wa mkoa.
Tuliambiwa hukuna jiwe litakalosalia bila kugeuzwa.
 
Makonda anaogopa nini kuonyesha vyeti kuondoa utata huu. Ukweli siku zote haupingiki
 
Kaka pasco hatukatai makonda anauthubutu lakini tunataka uthubutu utakaoendana Na sheria Na taratibu za nchi. Na tukiangalia ktk uthubutu uliotumika ktk sakata la madawa ya kulevya hauna tija Maana hawa watu inavyoenyesha hawatafungwa kwakuwa ushahidi umeelemea ktk taarifa za kuambiwa zaidi kuliko watuhumiwa kunaswa Na madawa. Ikiwa lengo lilikuwa kuwadhalilisha watuhumiwa basi wamefaulu lakini ikiwa lengo ilikuwa watuhumiwa waadhibiwe kwa mujibu wa sheria za nchi itakuwa wamefeli.
Lakini baada ya kuanza huu mjadala wa vyeti feki wa makonda nadhani halaumiki sana Kwani njia alizotumia au anazotumia ktk maamuzi mengi aliyowahi kuyafanya yanaendana Na uwezo wake aliokuwa nao darasani Kwahiyo anastahili kusaidiwa zaidi kuliko kulaumiwa japo sheria ifuate MKONDO wake.
 
Mkuu taarifa za siri kama hizi huwezi kuzipata kirahisi kabisa. Watu wa karibu yake sana ndo watakuwa wanazitoa safi sana
Nilichogundua ni kwamba hizi habari za siri kabisa zinatolewa na watu wake wa ndani kabisa.. Tena wanachama wenzake aliowahi kuwakera!
 
Kufeli darasani siyo kufeli maisha. Wangap wanazunguka na mavyeti yao lakini hawana cha maana wengine wanauza magenge nna wengine wameajiriwa kariakoo kwenye maduka ya nguo. Ebu pale mtu anapopambania kitu usimkatishe tamaa na kutafuta sifa zisizo na maana. Wengine wanaomsema makonda kanunua cheti ukute yeye si lolote si chochote. Tujifunze kwake
 
Mwishowe alipata degree bila kufanyiwa mtihani, kajitahidi sana ni mpambanaji haswa.
 
Kaanzishe mada yako kuhusu Mbowe hii inamuhusu Paulo Makonda
VIPI CV YA KIELIMU YA MWENYEKITI FREEMAN MBOWE AU BWANA GASTURA NAE VIPI AJIUZULU UENYEKITI AU MNAMSHAURIJE??
 
Mbona umepaniki sana jambo rahisi sana mwambieni Makonda tunaomba uikanushe na uweke CV yako ya kweli ili kuweka heshima yako na nafasi yako, na ili sisi wakazi wako wa Dar es Salaam tuwe na imani na wewe bosi wetu. La sivyo kama ni kweli chukua uamuzi mgumu wa kujiuzulu nafasi yako ya ukuu wa mkoa.
 
Baadhi ya sifa za kuwa mtumishi wa Mungu.
-Kuwa na busara.
-Weka hakiba ya Maneno.
-Usiwe mropokaji.
-Usiumie madhabahu kwa mambo binafsi.
Umeongea point mkuu, gwajima hana hekima ya kimungu, anatumia vibaya madhabau ya Mungu
 
Labda atakuelewa maana alivyoguswa daudi bashite watu wa lumumba povu linawatoka kweli...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…