Mimba ya wife inanitesa sana, mpaka najuta

Nas Mapesa

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2014
Posts
5,286
Reaction score
5,421
Wakuu habari za mida hii,kama mtiakumbuka kuna wakati nilileta lalamiko kuhusu huyu wife kuninyima papuchi wakati mimba ikiwa changa,sasa bora hilo,sa ivi ananisimbua sana,kwanza hataki kukaa na mimi karibu,na kwa vile muda wa kujifungua umekaribia aliniambia anataka akajifungulie kwao nikaunguza nauli mpaka kwao,

Juzi kanipigia simu hataki anataka kurudi tena sio kwangu bali nimpeleke home kwetu akajifungulie kwa mama mkwe,na hali ilivyo jamani haya si majaribu?huko alikokua ilikua kila sec simu mara naumwa mgongo, mara kiuno huku analia kabisa yaani utadhani dunia hii yeye ndio wa kwanza kupata ujauzito, nimeshafanya utaratibu aje tu,jamani wake zenu wako kama huyu?

Na nyie wanawake hebu nishaurini jamani,hali hii itanifanya akijifungua tu namfunga na kizazi potelea mbali mtoto awe mmoja tu.
 
Nikioa ntakuja na mimi kuleta yangu.... Enewei pole sana ndio ndoa hizo.
 
Itabidi ndio uvumilie hiyo inaonyesha ndio mimba yake ya kwanza kuipata na kama anakuchukia ujuwe atajifunguwa mtoto wa kiume la kama anakupenda ila anafanya hivyo vituko ujuwe ni mtoto wa kike kaka vumilia ndio ukubwa akijifunguwa atarudi hali ya kawaida na mutasahau yote yaliyopita..
 
Pole mkuu lakini mshauri kwamba kusafiri safiri na hali kama hiyo ni mbaya sana...
 
Naheshimu sana mawazo yako mkuu,asante
 
Nilizidi kuwapenda zaidi wazazi wangu pale nilipojaliwa kupata mtoto wa kwanza, pia kuwathamini sana wanawake kwa ujumla. Process nzima ya uzazi hadi malezi sio lelemama, na ukiangalia sana anaepitia maswahibu mengi ni mwanamke.
Hawa viumbe wahurumie tu, wanakua kwenye kipindi kigumu sana. Kuna kipindi alikua hataki hata kuniona, namshukuru Mungu alinipa kuelewa na kumchukulia katika hali zote nikijua ni mapito ya muda mchache tu. Mpende tu mkuu anakuhitaji sana wakati huu....Onyo, usitumie fursa hii kuchepuka na isome kwa makini signature yangu.

Ubarikiwe
 
una bahati sana mie nilikuwa naamshwa saa 9 za usiku akitaka ndizi na nyama choma na ukigoma analia sana, na ukileta ananusa tu wala hali
ikifikia huko mkuu naona mkono wangu ungehusika kuweka mambo sawa(makofi)huwezi niamsha saa 9 unataka ndizi choka kwani tupo club?
 
nadhani ni baadhi ya wanawake mm wangu tokea awe mjamzito hajawai nisumbua..niliwaisikia usumbufu huo kwa wanawake wajawazito nikawa ninahofu na wangu atanisumbua lakn haikua hvyo
 
[emoji120] [emoji120]
 
waheshimiwe sana hawa wanawake
 
mkuu natamani nikupe no umfokee kidogo,nimesema sana
Hapana usichoke mkuu tumia busara kidogo tu kwani hawa wake zetu wakiwa katika hali kama hiyo wanajiona wako saw kwa kila jambo,,so jaribu kutumia njia mbadala,,,atakuelewa tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…