hahaaa kumbe tuko wengi, mkuu huko ndiko kunaitwa kulea mimba na hayo ndio matokeo ya ndoa, mimi nnakumbana nayo ila nshazoea na kuna muda muda na mmisi wife nikiwa kwa Job kwa hivyo vituko, ninayokutana nayo sasa
1. kuna siku utaambiwa ana hamu na nyama choma ukileta hali
2. kuna siku apika chakula yeye hali anakunywa uji
3. siku ukishinda nyumbani ndio balaa dakika mbili mbele kimenuka, kupishana ni sekunde tuu, na ukitaka kutoka kanuna, kuna saa unaambiwa mwanao acheza njoo umguse sasa nilivyo na bahati mbaya nikimgusa tu hachezi, hapo yataanza madongo, mtoto hakupendi, ole wako atoke na masikio kama yako ( mabaya )
4. unaweza ambiwa ana hamu ya mahindi ya kuchoma saa saba za usiku usishangae,
5. hulali, unaweza amshwa mara 8 usiku kumpeleka kukojoa,
6. vikicharuka mzungu wa nne anahusika
7. unaweza rudi ukakuta hamna msosi na ukaambiwa leo nna hamu ya chakula cha mama ntilie, na ukimletea anakula kweli..
8. chakula alichokipika yeye asema si kitamu.
9. kuna wakati anakuwa karibu hadi inaboa atashinda jirani na kwapa akunuseee weee asema harufu yako inamvutia na kweli hadi anapata usingizi hapohapo sasa ole wako umsogeze,
siku ingine baba ukirudi unakaguliwa mgegedeo kama haupo used.
akianza kuumwa nyonga sijui mtoto hiyo siku kachachamaa unaweza sema sasa hivi azaa ila ndo muda bado,
utaambiwa jina la mtoto atoa yeye wakati ni kumuomba mungu mtoto atoke salama na yeye ajifungue salama lakini mwenzie ana ka listi kake ka majina ashakaandaa zamani,
kuna wakati wanakuwa viceversa alichokuwa akipenda mwanzo ndicho akichukia, mfano mimi niliombwa niweke dish la Dstv, ila hadi hivi nnavyoandika hapa haangalii na matokeo ya ni seris za kikolea kwenda mbele na kisambuzi chenyewe katupia chini ya uvungu,
nyumba sasa hata ukikwangua vocha ukaisahau mezani utasemwa wewe kwa uchafu hadi utasikia hasira,, aagh kuna raha yake man, hasa ukiwa mbali nae unamkumbuka, japo ukirudi home dakika tano ni nyingi anazingua, ila ukizoea fresh tuu, na uzuri zaidi akusumbue kama hivi uwe huna mchepuko, ukiwa nao kipindi hichi ni kigumu sana kwake, atajua tuu, sababu nawe hutokubali utaona kama mateso ila kama huchepuki wallah kuna raha yake....kwa hiyo ndugu hiyo events ni nzuri na muombee ajifungue salama akiwa fresh utamkumbusha vituko vyake kipindi cha ujauzito, naamini ni mambo ya muda tuu hayo..kaka hapo bado hujaanza kilea, utanyooka wewe...ususahau kutuletea mrejesho na kipindi cha malezi, kila la kheri...