Mimea tiba kupitia mimea ya majumbani

Mimea tiba kupitia mimea ya majumbani

Ahsante sana 😍

Sasa

Kisonono na chango
Na mengineyo unaweza andika kwa lugha ya kiingereza kwa mabano

Maana kama mie wa kijijini ngachoka kuhighlight na ku Google.. 🤗
Shukran sana mkuu Kwa kushukulu ila nimeweka Kwa kiswahili Ili watu wote waweze kupata faida hii mkuu🙏🏽
 
Sida Acuta

Mmea huu ni mgumu sana kung'oa nadhani wengi tunaujua au tumeshawahi kuuona.sijui kilugha wala kiswahili chake.

Huu mmea

*Chai ya mizizi yake inaongeza nguvu za kiume

*Ukiponda majani yake kwa kuchanganya na kitungu swaumu ni dawa ya jipu

*Chai ya majani yake inasaidia mwanamke kujifungua haraka bila maumivu makali sana

*Chai ya mmea huu ni nzuri kwa mwanamke ambaye uzazi umegoma. Kunywa hii kwa siku 5 kuanzia unapoona damu ya hedhi
Mungu atajaalia

Je umeutambua mmea huu? Unajua niini kuhusu huu mmea kwa zaidi ya niView attachment 3225405liyoyaelezaa??
Umenikumbusha kitambo hicho enzi za kujipikilisha hayo majani tulikua tunaponda tunaweka maji yanateleza sasa na sisi tulikua tunasema ni mlenda ila hatuli ukweli tunaishia kwenye kidevu
 
1000236371.jpg
 
Mmea ni majabu ya Mungu kwetu .

Mmea hapo kwenye picha :

🥬Kisukuma unaitwa Mjorwambogo.
🥬Kikamba unaitwa Ithaa.
🥬Kikikuyu unaitwa Mwino au mwinu.
🥬Kijaruo unaitwa Ovino au owinu.
🥬Kimeru unaitwa Kirao au Murao.
🥬Kitaita unaitwa Mbinu au Mshua.
🥬Kiiraq unaitwa Nkharerei.
🥬Kihehe huitwa Mulimuli.
🥬Kisambaa huitwa Mzangazi.

Kuhusu matibabu :

🥬 Huo mti hutibu magonjwa ya ini...
🥬Hutibu vidonda vya tumbo. Hutibu malaria, typhoid na ameba.
🥬Hutibu kisonono. Huondoa sumu zote mwilini na kupunguza mafuta.
🥬Mtidawa huu hushusha shinikizo la damu yaani presha ya kupanda.
🥬Hutibu chlamydia. Hutibu magonjwa ya mifupa. Magonjwa yote ya mfumo wa uzazi wa mwanamke hutibiwa na mti huu...
🥬Mti huu humwezesha mwanamke kushika ujauzito ikiwa hajakoma hedhi.Hii hufanyika kwa kuondoa uvimbe wowote kwenye mfumo wa uzazi, ini, bandama, figo, kusafisha kizazi, kurutubisha mayai na kuongeza uwezekano wa kupata ujauzito

🥬 Mti huu hurudisha mzunguko wa hedhi na kuuweka uwe sawa ikiwemo kuondoa maumivu kipindi cha hedhi...
🥬Mti huu huondoa uvimbe wa aina yoyote ndani ya mirija ya uzazi, ovari, uterus au kizazi kwa muda wa wiki tatu tuu..

NAMNA YA KUTENGENEZA

🥬Chukua majani yake. Hakikisha huchanganyi na mbegu zake. Chukua majani tuu. Chukua mengi kadri uwezavyo. Yaanike mahali safi ndani, Yasambaze kabisa. Baada ya siku tatu kama mahali hapo pana joto la kutosha (hapo ndani na siyo nje kwenye jua) yatakauka.Saga ili kupata unga laini, Waweza kusaga hata kwa kufikicha tuu kwa mkono. Ni malaini na yanasagika kwa haraka mno ikiwa yamekauka vizuri. Waweza kusaga kwa kutumia brenda pia...

NAMNA YA KUTUMIA

🥬 Isipokuwa ugonjwa wa kisonono, tumia kijiko kidogo ndani ya maji ya moto nusu kikombe cha chai asubuhi na jioni kwa muda wa week mbili. Baada ya hapo, nenda ukapime hutaona kitu.

🫐Kumbuka: Mtidawa huu utakufanya uharishe kama mara tatu kila unapokunywa. Kadri tatizo linavyoendelea kuisha mwilini, kuharisha nako kunapungua na mwisho kupotea kabisa. WagonjwaView attachment 3225379
Nimeshasapuskraipu hii page
 
"🌿MLONGE HUMALIZA TATIZO LA PRESHA

ℹ️ Kwa zaidi ya miaka 1,000, Mlonge umeendelea kuwa tiba ya kiasili inayotegemewa na vizazi vyetu vya Kiafrika.

ℹ️ Sasa, tiba hii ya kiasili imekuwa msaada mkubwa kwa wagonjwa wengi wa presha na inaweza kukusaidia pia!

Wenda nawe ulishawahi kusikia hili

Faida za Mlonge kwa Presha ni pamoja na 👇

✅ Kupunguza presha kwa kupanua mishipa ya damu Kwahiyo mzunguko damu utaimarika na kuwa vizuri.

✅ Kusaidia kupunguza cholesterol mbaya, chanzo kikuu cha presha ya juu.

✅ Kuimarisha afya ya mishipa ya damu na kupunguza msongo wa mwili.

Na Hii Ndio Namna Rahisi ya Kutumia Mlonge..

1️⃣ Saga majani makavu ya mlonge hadi yatoe unga laini(Hakikisha Yameanikwa katika kivuli ili yasipoteze virutubisho vyake)

2️⃣ Chukua kijiko 1 cha unga na changanya na kikombe cha maji ya uvuguvugu.

3️⃣ Kunywa mara moja au mbili kwa siku na uone mabadiliko!

1738692752647.jpg


● Ni tiba ya asili, salama, na bila athari za kemikali.

● Imetumiwa kwa maelfu ya miaka hauhitaji kusubiri uthibitisho!

● Wagonjwa wengi wa presha tayari wameona matokeo mazuri na haraka.

NB: Ili Kupata Faida za mlonge Chuma wakati ambao jua limetoweka kwani huwa linapoteza ama kupunguza virutubisho vyake jua linapokuwa kali..

#Dogoli kinyamkela _ninakuletea afya yako kwa njia salama na asili!..
 
Mti wa mwembe unatibu

🌿Kisukari
🌿Shinikizo la damu
🌿Mawe kwenye nyongo
🌿Mawe kwenye figo
🌿Kaswende
🌿Malaria
🌿Cholesterol nyingi
🌿 Ini kushindwa kufanya kazi vizuri
🌿Upungufu wa damu..

Matumizi:

Chemsha vijiko viwili vya unga wa majani makavu ya mti wa mwembe . Au chemsha magome ya shina la mwembe kwenye maji.

Kunywa kikombe mara mbili kwa siku.
1738692902642.jpg


Olds is Gold 🥇
 
Back
Top Bottom