Mimi na mzee wangu hatuko sawa, na sioni dalili ya kuja kuwa sawa tena

Amini kwamba kuna namna mzee wako alikuwa sahihi kufanya alivyokuwa akifanya. Utakuja kufaham hili when itd too late.

Mzee wangu alikuwa mkali tukiona taa za gari tu zinamulika hata kama sio yeye hao tunakimbilia vyumbani kulala yani ni kama panya waonapo paka, wote wanaingia kwenye mashimo. Alikuwa na ubabe fulani ambao ulikoma baada ya sisi kukua.

Kitu kikubwa ambacho nilijifunza ni kuwa ukitaka kuishi utakavyo basi kuwa na kwako na sio uishi utakavyo na kila kitu unategemea kwenu.
 
Pole mkuu, nazani mzee wako hana ubaya ila ni katika zile kushow love kwa watoto wake, kuna wakati inabidi awe mkali kwa maslahi yako ya baadae .

Kama amekusomesha amekupa vitu vyote ulivotaka amemheshimu na mama yako hana shida yeyote..
 
Baba yako kukulinda ni ubaya?
Shukuru Mungu sana, kuna wababa walitelekeza familia zao,
Kuna watoto wanatamani wangeexperience hata hiyo care kama ya Baba yako, ila walikosa.

Na unasema Sijui baba amechangia kifo cha mama yako.
We tema mate chini!

Baba yako naye akikaa na kukwambia madhaifu ya Mama yako, unaweza kushangaza.
Ila ndio hivyo wanaume wameumbwa kubeba mambo kifuani.

Tambua wema wa Baba yako kabla hajaondoka.
Mpende Baba yako,
Ipo siku utakuja kumkumbuka sana na kuona umuhimu wake, it will be too late.
Usichezee hiyo nafasi.

Nimeandika kwa uchungu sana kama miongoni mwa watu ambao tumepoteza Baba zetu.
You'll realize that his gap is irreplaceable wakati akiwa hayupo


Ni Mungu wako wa pili huyo,
Hata awe na madhaifu kiasi Gani(japo kwa stori yako sijaona dhaifu lolote kutoka kwake)
Oyaa
Acheni kufanya mchezo na Wazazi wenu nyie.
Aisee
Acha kufanya mchezo na hiyo neema ya kuwa na mzazi.
 
We face the same issue.
Upumbavu wa wazazi wengi ni kwamba, wao hawakua na vision yoyote ya maana kwenye maisha yao, alafu wanakuja kulazimisha watoto wao waishi kwa misingi yao na mawazo yao kwa lazima, bila kujali wewe mtoto una maono gani na unapenda.

Unakuta mzazi anavuta sigara, mtoto na yeye akivuta sigara unashangaa dingi anaanza mzozo na kelele mixer ngumi,

Mwisho binafsi sina mapenzi na mzazi mpumbavu, kwani wapo wazazi wanaomwaga damu za watoto wao kaajiri ya vitu vya kidunia
 
Kaka una watoto?? Utayaoja ndugu malezi ni kazi mno
Bado sina...
Ila inshallah.. Nataka niwe baba bora kwa wanangu, nimeona na ku experience first hand jinsi malezi yalivyo magumu.. It takes courage, ila I pray to be a better one
 
Mkuu hii stori Inasikitisha sana..
Najua yameshatokea... Mzazi ni mzazi tu, nenda kaburiini kaombe msamaha na uache maumivu... It will haunt you, he is the one who brought you on earth... That alone is a gift.

Achana na mapito it is meaningless in the grand scheme
 

Pole sana mkuu๐Ÿ˜ข

Asante kwa maneno yenye hekima na nitayaishi. ๐Ÿ™
 
Mtoto hahitaji kuishi atakavyo, mtoto anahitaji malezi mazuri mkuu,watoto wako so vulnerable. Kama unaona ilikuwa ni sawa baba yako kuwa mkali hadi wakati akirudi nyumbani mnakimbia kujificha badala ya kumkimbilia kwa furaha,kazi ipoo.
 
Mtoto hahitaji kuishi atakavyo, mtoto anahitaji malezi mazuri mkuu,watoto wako so vulnerable. Kama unaona ilikuwa ni sawa baba yako kuwa mkali hadi wakati akirudi nyumbani mnakimbia kujificha badala ya kumkimbilia kwa furaha,kazi ipoo.
Sijaeleza mengi ila kwa kifupi mbio zilikiwa zinasababishwa na mengi. Kwa mfano uzembe wa kushindwa kukamilisha kazi alizowaachia, muda wa kusoma sisi tupo bize na kuangalia tv, ukorofi n.k.
 
Wazazi mafala ni wengi niamin mm
 
Bado sina...
Ila inshallah.. Nataka niwe baba bora kwa wanangu, nimeona na ku experience first hand jinsi malezi yalivyo magumu.. It takes courage, ila I pray to be a better one
Mim binti yangu ananinunia kabisa kisa namkazia anataka awe huru , ananiona snitch na mnoko afanye anachotaka ,malezi ni kazi ngumu aiseee kuwa positive
 
Mim binti yangu ananinunia kabisa kisa namkazia anataka awe huru , ananiona snitch na mnoko afanye anachotaka ,malezi ni kazi ngumu aiseee kuwa positive
Kaa nayee.. Mfanye awe rafiki in a more stric way... Sometimes naona wazazi wengi wanakuwa kama watoto wawaone wa kuogopwa which inamfanya awe na nidhamu ya uoga
 
Let things go..
Something we can't control, ndo maisha kaka
 
Hivi vitu vinaharibu future ya mtu ukubwani asee, Mimi mamangu alikuwa anashirikiana na kaka zangu kunichangia kunipiga na mikanda na waya za umeme utotoni eti mi mtundu sana... sasa hivi nimekuwa mtu mzima hata siwapendi yaan๐Ÿ˜๐Ÿ˜.....wao wanadhani nimesahau kumbe kila kitu kiko ubongoni kama jana tu...mtoto hasahau kitu๐Ÿ™Œ๐Ÿ™Œ
 
Kwa mwandiko huu ulikuwa mtundu kweli.
 
Bado sina...
Ila inshallah.. Nataka niwe baba bora kwa wanangu, nimeona na ku experience first hand jinsi malezi yalivyo magumu.. It takes courage, ila I pray to be a better one
Binafsi sijaona makosa yoyote kwa huyo mzee wako!

Kwa mim ninavyojua mzazi anawajibu wa kuwalea watoto wake kwa kuwatiisha (kuwafanya watoto waish maisha siriasi), maana haijulikan mtoto katka maisha (ukubwan) yake atapitia nin, mzaz anapaswa kumuandaa mtoto kupambana changamoto yoyote katka maisha!


Binafs mim nimelelewa na mjomba wangu (huyu mzee ni mkali sana, kipgo mixer kitu kidogo unafokewa). Kipndi tupo wadogo nilijua tunateswa ila kwasasa nimeshamuelewa mjomba wangu!
 
Mkuu, jilazimishe, kuwa karibu na mzee.

Kama alitoa fedha yake ukapata huduma hiyo inatosha sana sana sanaaa.

We piga simu nenda kamchomee nyama mpige story hata mara moja kwa wiki.

Mkisha kaa mara mbili tatu story zitakuja nyingi tu na parts za story zinaweza kuwa hizi hizi ulizozipiga hapa kumhusu. Anaweza kukupa upande wake wa hadithi ukamuelewa sana.

LIFE IS SHORT, KUNA SIKU HUTAKUWA NA HIYO NAFASI ACHA MARINGO.
 
Aisee.. ๐Ÿ˜”
Pole sana, kumbe watu mmebeba maumivu Daah.. Kama kwa sasa umesha kuwa mtu mzima, let that shit go, yameshapita.. Waambie kuwa uliumia na bado hujasahau Itakusaidia...

Mimi mzee wangu huwa namkumbusha sana, na huwa na tendency ya kumwambia sijasahau kitu.. He knows now na ni yeye ndo ananitafuta ni rudi ila sio rahisi kama a navyo dhani.. Ila mwishoni forgiveness is the only option lazima kusamehe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ