Mimi naamini kila dhambi lazima uilipie

Nimeipata sehemu nimeamua kushare na nyinyi kwa sababu Mimi nimeipenda na at least naweza kuishi kwa kufuata hiki kilichoandikwa na sio kuangalia mambo ya karma.


Amua kuishi na amani na kila mtu

[emoji3514]Watu ambao wanaishi kwa amani na watu wengi ni rahisi kufanikiwa kuliko watu ambao hawana amani na watu wengi.

[emoji2424]Jitahidi mwaka huu kupatana na watu uliokosana nao.

[emoji3542]Jitahidi mwaka huu kuwasamehe wote waliokukosea hata kama hawajakuomba msamaha.

[emoji288]Duniani kuna makundi mawili ya watu, kundi la kwanza ni watu wanaojikita kugombana, kuchukia, kuona wivu, kutunza vinyongo na kutowasamehe wengine.

[emoji273]Kundi la pili ni kundi linalojikita katika kutafuta amani, kutafuta suluhu, kutafuta kupatana, kusamehe na kutafuta kusamehewa, kuachilia uchungu pamoja na kutafuta maelewano na maridhiano.

[emoji953]Watu walio katika kundi la pili Wana asilimia zaidi ya 70 ya kufanikiwa na watu walio katika kundi la kwanza wana chini ya asilimia 30 za kufanikiwa.

[emoji3522]Ni ngumu kuelewana na kila mtu ila jitahidi kwa kila unapoweza usiende kulala ukiwa na chuki au uchungu moyoni, hakikisha unakuwa mtu wa kusamehe watu hata kabla hawajakuomba msamaha ili uwe na moyo mweupe.

[emoji3532]Moyo ulio mweupe ni moyo ambao utakufanya upate mawazo bora ya kukufanikisha.

[emoji288]Ila moyo mchafu, moyo ulio beba makorokoro utakufanya upate mawazo mabaya ya kushindana na kulipiza kisasi kwa watu.

[emoji3589]Kama moyo wako sio msafi( sio mweupe), fanya mambo haya
1.Amua kutoka ndani kusamehe wote waliokukosea, tokea was kipindi cha nyuma hadi leo.

2.Muombe Mungu akusamehe kosa la kutowasamehe waliokukosea pamoja na kosa la kukaa na uchungu au hasira moyoni (omba msamaha kutoka ndani ya moyo wako).

3.Amua na nenda kapatane na watu ambao mlikosana, ikiwezekana wewe uwaombe msamaha hata kama wao ndo walikuwa na makosa( fanya hivyo kwa moyo ili kurudisha amani na mahusiano mazuri baina ya wewe na wao).

[emoji288]Ukifanya hayo mambo matatu kwa uaminifu(kwa kumaanisha) moyo wako utakuwa Safi na utakusaidia kupata nguvu ya kufanikiwa huu mwaka wa 2023.

[emoji762] Kwa ushauri kuhusiana na changamoto ya kimaisha inayokusumbua njoo inbox au nitafute kupitia no. 0748198856.

[emoji257] Nb.Ushauri kwa sasa ni bure kabisa, usiogope karibu upate ushauri utakaokusaidia.

[emoji3447]Badilisha fikra, chukua hatua, Badilisha maisha.

[emoji746]David Mwanguku
Mwalimu wa mafanikio
 
unamwaminisha MTU mpo safari moja kumbe umeaminisha wengi-wastage of time(hili limenipata but time will tell)
Kwa hio jamaa kala mzigo kamaliza kashiba kisha katokomea maporini?
 
Unaweza ukafanyiwa yote hayo na aliekufanyia asipatwe na chochote LIFE IS NOT FAIR so not every karma is real
 
Kaka yu are genius watu wanajidanganya et karma karma wakat na wao washawah watendea watu ubaya
 
Hakuna kitu kama hicho kinaitwa karma is just an illusion. Mtu anayeamini hivyo ni sawa na imani tu kama za dini. Mimi naangaliaga wazungu walivyodhurumu babu zetu but mpaka leo wanatoboa tu kama sio kutusua
 
Karma ipo kama na wewe hukuwahi kumtendea Mtu ubaya, ukiona umetendewa ubaya jaribu kuvuta kumbukumbu je na wewe uliwahi mtendea mtu lipi kama hakuna basi Karma itakulipia kama lipo basi Karma imekulipa.
 
TAFUTENI ELA HIZO KARMA SIJUI NIN NI MANENO YA KUJIPA MOYO😂😂UNAVOZUNGUMZIA KARMA HAKIKISHA HUJAWAH MFANYIA UBAYA MTU YOYOTE YULE
 
Karma ipo kama na wewe hukuwahi kumtendea Mtu ubaya, ukiona umetendewa ubaya jaribu kuvuta kumbukumbu je na wewe uliwahi mtendea mtu lipi kama hakuna basi Karma itakulipia kama lipo basi Karma imekulipa.
Amina
 
Hakuna kitu kama hicho kinaitwa karma is just an illusion. Mtu anayeamini hivyo ni sawa na imani tu kama za dini. Mimi naangaliaga wazungu walivyodhurumu babu zetu but mpaka leo wanatoboa tu kama sio kutusua
Amina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…