Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Unaandika PhD?
 
Kabla ya kuletewa dini(kipindi cha mizimu) hilo la 50-50 halikuwepo na hata zilipokuja dini pia hazijaja na hilo jambo na mpaka tutaisha(kufa) wote duniani hilo jambo halitakaa liwepo ila wakuendelea kulipambania liwepo watazidi kuwepo.

Kiufupi suala la 50-50 halitakaa liwepo na hayo ndo maumbile halisi ya binadamu.
 
50-50, kiasilia haipo hiyo, mpaka wanawake wenyewe hufikia pahala wanaikataaga wenyewe, ndo ujue alilolifanya Mungu mwanadam hawezi kubishana nalo Wala kulitangua, badala yake ataishia kujitekenya mwenyewe na kucheka alafu yanajirudia pale pale kama Mungu alivotaka iwe. Ndo maana tunasema asili ni asili tuuu

You can't fight against the nature.
 
Umemaliza kila kitu Jadda, tatizo wanaume wa Kitanzania hawaitaki hiyo kisa tu wanataka mtu wa kuwatii,

Uislam umeshaweka wazi majukumu ya Mwanamke nayo ni Kuzaa tu, kazi zote za nyumbani ni za Mwanaume kama hawezi aweke msaidizi, Uislam unamtaka Mwanaume amlipe mkewe ili amnyonyeshee watoto (haya hua hawayasemi kwenye mawaidha, wanabana kimyaaa)
 
Hiyo 50/50 unayotaka Mjukuu mtaweza majukumu yake?

Kwamba Mume atoe Kodi ya miezi 6 ya nyumba na Mke alipie miezi 6 iliyobaki ya Kodi.

Wanawake wenyewe ndiyo hawa ambao wanasema mshahara wao ni wao pekee ila wa Mshahara wa Mume ndiyo wa kutumika ndani ya nyumba?

Nina rafiki yangu ni Mzungu, wao ndiyo wanaiishi hiyo 50/50 ambapo wamegawana majukumu sawa sawa na Mume wake.

Ana watoto 2 na Mume wake, mtoto mmoja ana msomesha na kumgharamia yeye matibabu/mavazi na Kila kitu kuanzia alipozaliwa hadi Chuo Kikuu na mtoto mwingine ana gharamiwa yote hayo na Mume wake.

Nieleze kama Kuna Mwanamke Bongo hii ataweza kuyafanya hayo.

Ubunge wenyewe mnapewa bure bure na Chama
 
Hakyanani nitamuuliza mzee wa mizigo Sheikh Kipozeo kama haya uyasemayo ni kweli! πŸ˜πŸ–
 
Una ndoa? Ume practise ulichosema au nadharia... isije kua ndo yale kungwi mdomo mrefuuu kujishadadia unayajua mapenz na umefunzwa ukafunzika kumbe una talaka 4 no mume currently. Kwamba sa8 usiku likaja wazo tu la 50/50 kilichokukuta sitak ku imagine, pole πŸ˜₯
 
Basi wawe wanayasema haswaa huko kwenye mawaidha.
 

Jadda umeandika andiko refu lakini hali reference au citations ili kutetea hoja zako...

Mahusiano ya kindoa kati ya mtu mwanaume na mtu mwanamke sio partnership au mahusiano yaliyojengwa kwa mlinganyo wa kiasilimia...

Mahusiano ya kindoa kati yetu wanaume na wanawake, yamejengwa kwenye mtazamo wa utofauti wa kiutaratibu na kiutawala/nafasi...

Reference #1 Kiutawala au Nafasi
Mwanzo 2
18 Bwana Mungu akasema, Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.

Mwanzo 2
22 na ule ubavu alioutwaa katika Adamu Bwana Mungu akaufanya mwanamke, akamleta kwa Adamu.

Mwanamke ni msaidizi wa mwanamume ambaye aliumbwa kwa kufananishwa naye ili aweze kupokea majukumu toka kwa mwanamume...Mungu angeweza hata kuamua wanyama ndio wawe wasaidizi wa mwanaume, lakini hao viumbe wengine hawakuwa wamefanana na mwanaume.

Hivyo basi, mathalani wewe unapokuwa kazini na una bosi wako, je bosi wako hawezi kukukasimisha baadhi ya majukumu yake kwa nia ya kutoa usaidizi kwake kwa kutambua kuwa wewe pekee ndiye mwenye ujuzi wa majukumu ayafanyayo?

Inakuaje nongwa kwa mwanaume ambaye kapewa msaidizi wa asili, na asimjukumishe baadhi ya majukumu?


Reference #2 Kiutaratibu

Sasa utaratibu uliobainishwa kuelezea namna viumbe hawa wawili watavyoishi umeelezwa kama ifuatavyo.
#1
Mwanzo 2
24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.
#2
Waefeso 5
22 Enyi wake, watiini waume zenu (nimeukatisha kutoa maudhui ya kiimani)
23 Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe (nimeukatisha kutoa maudhui ya kiimani)

Waefeso 5
28 Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…