Wanawake si kwamba hawapendi kukaa nyumbani kutimiza majukumu yao ila tatizo wakifanya hivyo, wanaume wengi wanawanyanyasa kwa kigezo cha kuwahudumia yani mwanaume anataka hata akimtendea mkewe kosa kubwa asiulizwe, na akiulizwa utasikia "yani nakulisha nakuvisha halafu unataka unipande kichwani" kisha vipigo
Hakuna kiumbe kitakubali ukinyanyase eti kisa unakihudumia, hata mnyama wako hawezi kukubali unmnyanyase eti kisa tu unamfuga ipo siku atachoka atakugeukia tu sembuse mwanamke, kwahiyo wanawake wanaona bora nao wajitafutie vyao ili walau wawe na sauti kidogo
Sasa wanapoanza kutafuta msitegemee tena wawape zile treatment kama za mama wa nyumbani, lazima tu kuna vitu vitapungua kama utii pamoja na kutimiza majukumu ya nyumbani, na hapo ndipo 50/50 inapoanzia kwa sababu huyu mwanamke tayari anakuwa kakupunguzia majukumu ya wewe kumhudumia