Mimi naona dunia iachane na mfumo dume na rasmi 50/50 ishike hatamu

Nadhani hata 50-50 sio sawa, twende na mfumo jike kabisa ndio itakuwa poa sana.
 
Kwa wanaoamini katika Biblia itakuwaje? Ni kwa nini Mungu asiwaumbe Adam na Eva kwa wakati mmoja? Ubavu mmoja wa Eva utalinganisha na mbavu za Adam?. Tuje kwa kitu kidogo, angalia masomo ya sayansi, lini itafika 50 kwa 50?
Ungesoma uzi wangu ungeelewa mada, mimi nimesema kama wanaume wanataka mfumo dume basi watimize wajibu wao kwa wanawake, lakini kama wanakimbia majukumu basi waachane na mfumo dume
 
Nadhani hata 50-50 sio sawa, twende na mfumo jike kabisa ndio itakuwa poa sana.
Hatutaki mfumo jike lakini pia hatutaki mfumo dume ikiwa wanaume wanakimbia majukumu yao, kila mtu ajitawale mwenyewe kwani ni lazima kuwepo na wa kumtawala mwenzie, hakuna mamlaka bila wajibu
 
Seems Ke wanahitaji sana kuidominate dunia, if so tuwape full authority ili tuone kama kweli mnaweza, mfanye yote ya kiume hadi vitani muende nyie sisi tulee watoto.
 
Hio haki sawa ya 50/50 hakuna siku itapatikana ngoja tuendeleee kuwazooom[emoji851]
 
Ni ninyi ndio mnaopotosha maana nzima ya 50/50 na kulazimisha ionekane kama wanawake wanataka kuwatawala wanaume, 50/50 maana yake kila jinsia ijitawale yenyewe kusiwe na wa kumtawala mwenzie kwanini wanaume mnalazimisha kuendelea kuwatawala wanawake, siku hizi wanawake wamejaa kwenye majeshi mkuu au bado mnaishi kwenye ile imani kwamba wanawake majeshini ni viburudisho tu..well hiyo ilikuwa zamani siku hizi vitani wanaenda
 
As long as men wataendelea kutimiza majukumu yao then that is totally fine
 
Ni sawa na kusema Tanzania isiwe na kiongozi, iwe autopilot. Hakuna jamii inayokosa kiongozi, mwanamke bado hawezi kuwa kiongozi wa jamii kuanzia ngazi ya familia, so nyie timizeni wajibu wenu na sisi tutimize wa kwetu ili muendelee kuwa chini ya mwanaume. There's no 50/50 madam, hakuna hiyo kitu.
 
Ungesoma uzi wangu ungeelewa mada, mimi nimesema kama wanaume wanataka mfumo dume basi watimize wajibu wao kwa wanawake, lakini kama wanakimbia majukumu basi waachane na mfumo dume
Msisahau kutongoza wanaume na kuwalipia mahari ili iwepo 50/50 na mfume dume ufe
 
As long as men wataendelea kutimiza majukumu yao then that is totally fine
  • Usisahau kumpa mwanaume hela akitaka kama mnavyofanya
  • Akiugua mpeleke hospital na ugharamie huduma zote (haki sawa)
  • Mavazi pia hata hela kodi ya mezani usisahau kutoa
  • Kodi ya pango ulipe
50/50 haitatokea mpk siku mkiweza kukojoa huku mesimama kama wanavyofanya wanaume
Haki sawa huku majukumu hamuyataki😀😀😀😀😀
 
As long as men wataendelea kutimiza majukumu yao then that is totally fine

Kutimiza majukumu unamaanisha nini?
Nikuelimishe tu kuwa, wanaume waliopewa jukumu la kutunza familia ni wale ambao Mke wake anakaa nyumbani kazi yake ni kuzaa na kuangalia familia
ILA hawa wanawake wanaotoka kwenda kufanya kazi/biashara na wengine kuacha jukumu la kulea watoto liwe la dada wa kazi/house girl, kipato chao kinatakiwa kitumike na familia (kama wanaume). sasa wakitumia kipato chao hujiona wanaume hawatumizi majukumu, wakifikiri hela zao sio za familia????.
Na tujiandae kisaiklojia kwani huko tunako elekea itafika mahala wanawake (sio wote) wawe ndio wenye kazi/kipato, na hivyo baba anabaki nyumbani kulea familia na hapo ndipo kelele zitazidi kulaumu wanaume kuwa hawatimizi majukumu wakati ndio kitu wamepigania.

Changamoto KUBWA iliyopo kwenye jamii ni kuwa; watu wanapigania mfumo ambao hawaja jiandaa kukabiliana nao. Kwa mtazamo wangu, suala la ndoa (kuoa na kuachika) linaenda kuwa kama mchezo wa kuigiza (asubuhi ndoa/jioni talaka)
 
Ni sawa na kusema Tanzania isiwe na kiongozi, iwe autopilot. Hakuna jamii inayokosa kiongozi, mwanamke bado hawezi kuwa kiongozi wa jamii kuanzia ngazi ya familia, so nyie timizeni wajibu wenu na sisi tutimize wa kwetu ili muendelee kuwa chini ya mwanaume. There's no 50/50 madam, hakuna hiyo kitu.
Nafikiri mnashindwa kutofautisha kati ya uongozi na unyanyasaji sidhani kama kuna mwanamke atakataa kuongozwa na mwanaume mwenye busara na hekima wanawake wanakataa kunyanyaswa, mfano mwanaume kufanya kosa kubwa kisha kutaka mwanamke asimuulize au eti akimuuliza amuulize kwa upole hata kama anaona kabisa hapa mwanamke kakasirika huo siyo uongozi ni unyanyasaji, by the way huo mfano wa nchi siyo relevant familia na nchi ni tofauti na hata hivyo urais ni taasisi na siyo mtu hata huyo rais kuna watu wanafanya maamuzi badala yake si kila jambo anaamua yeye
 
Uongozi unaanzia ngazi ya familia mkuu, yaani familia ni taasisi kama ilivyo nchi. Ndio maana huwezi kuwa raisi kama huna ndoa(ni moja ya sababu). Ukishindwa kuongoza familia unadhani utaiweza jamii?

Hata hivyo, udikteta kwenye ngazi yoyote ya uongozi ni muhimu sana. Hizi demokrasia za kizungu mnazotaka ndio zinatufikisha hapa tulipo.
 
Msisahau kutongoza wanaume na kuwalipia mahari ili iwepo 50/50 na mfume dume ufe
Msijifanye hamjui kwanini wanawake hawatongozi wanaume siyo kwamba hawapendi ila ni kutokana na jamii zetu za kiafrika, toka enzi zinamchukulia mwanamke anayetongoza mwanaume kama malaya kwahiyo jamii zikiachana na hiyo mitazamo watakuwa huru kuwatongoza, kuhusu mahari kama pia mtakuwa tayari watoto watumie majina ya koo za pande zote mbili basi ni sawa wote kulipiana mahari au ifutwe kabisa maana hilo ndilo lengo kubwa la mahari
 
  • Usisahau kumpa mwanaume hela akitaka kama mnavyofanya
  • Akiugua mpeleke hospital na ugharamie huduma zote (haki sawa)
  • Mavazi pia hata hela kodi ya mezani usisahau kutoa
  • Kodi ya pango ulipe
50/50 haitatokea mpk siku mkiweza kukojoa huku mesimama kama wanavyofanya wanaume
Haki sawa huku majukumu hamuyataki[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
Ni misingi gani inayoamua kwamba kukojoa huku umesimama ndio kunamfanya mtu awe kiongozi, hata wanawake nao wanaweza kusema kwamba wao ndio wanatakiwa kuwa viongozi sababu wao ndio wanaleta viumbe duniani, how about that
 
Kutimiza majukumu unamaanisha nini?
Nikuelimishe tu kuwa, wanaume waliopewa jukumu la kutunza familia ni wale ambao Mke wake anakaa nyumbani kazi yake ni kuzaa na kuangalia familia
ILA hawa wanawake wanaotoka kwenda kufanya kazi/biashara na wengine kuacha jukumu la kulea watoto liwe la dada wa kazi/house girl, kipato chao kinatakiwa kitumike na familia (kama wanaume). sasa wakitumia kipato chao hujiona wanaume hawatumizi majukumu, wakifikiri hela zao sio za familia????.
Na tujiandae kisaiklojia kwani huko tunako elekea itafika mahala wanawake (sio wote) wawe ndio wenye kazi/kipato, na hivyo baba anabaki nyumbani kulea familia na hapo ndipo kelele zitazidi kulaumu wanaume kuwa hawatimizi majukumu wakati ndio kitu wamepigania.

Changamoto KUBWA iliyopo kwenye jamii ni kuwa; watu wanapigania mfumo ambao hawaja jiandaa kukabiliana nao. Kwa mtazamo wangu, suala la ndoa (kuoa na kuachika) linaenda kuwa kama mchezo wa kuigiza (asubuhi ndoa/jioni talaka)
Wanawake si kwamba hawapendi kukaa nyumbani kutimiza majukumu yao ila tatizo wakifanya hivyo, wanaume wengi wanawanyanyasa kwa kigezo cha kuwahudumia yani mwanaume anataka hata akimtendea mkewe kosa kubwa asiulizwe, na akiulizwa utasikia "yani nakulisha nakuvisha halafu unataka unipande kichwani" kisha vipigo

Hakuna kiumbe kitakubali ukinyanyase eti kisa unakihudumia, hata mnyama wako hawezi kukubali unmnyanyase eti kisa tu unamfuga ipo siku atachoka atakugeukia tu sembuse mwanamke, kwahiyo wanawake wanaona bora nao wajitafutie vyao ili walau wawe na sauti kidogo

Sasa wanapoanza kutafuta msitegemee tena wawape zile treatment kama za mama wa nyumbani, lazima tu kuna vitu vitapungua kama utii pamoja na kutimiza majukumu ya nyumbani, na hapo ndipo 50/50 inapoanzia kwa sababu huyu mwanamke tayari anakuwa kakupunguzia majukumu ya wewe kumhudumia
 
Back
Top Bottom