SoC02 Mimi ndiye adui wa maendeleo ya vijana ninayelipa kodi

Stories of Change - 2022 Competition

cupvich

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2022
Posts
408
Reaction score
247
Utangulizi.
Nimekuwa maarufu sana katika karne hii ya ishirini na moja(21). Kila mahali napokelewa kwa shangwe na walio wengi, sio vijana tu bali watu wa kila umri wananikubali na Kunipenda. Mamlaka za utawala nazo zimenipokea kwa mikono miwili na kunipatia mazingira rafiki ya kuishi. Nimekuwa na faida kubwa kwa serikali kwani ninachangia katika Maendeleo, na kufanya watawala wengi wanipigie Chapuo wakati ninapopata MISUKOSUKO.
Nimeteka watu wa kila aina VIJANA kwa WAZEE, Wasomi kwa wasiosoma, Matajiri kwa Maskini, Wanafunzi kwa wasio wanafunzi, Hakika nimekita mizizi kila eneo KANISANI nipo, MISIKITINI nipo, Maofisini nipo, Mashuleni nipo, Vyuoni, Majumbani hata katika Vyombo vya Usafiri napatikana. Umaarufu wangu umekuwa Mkubwa na kuufanya Ulimwengu wote Unigeukie. Kizuri zaidi kwangu ni kwamba NIPO KIHALALI, nafanya kazi zangu pasipo Bugudha yoyote kwasababu Nafuata sheria zote za Nchi ikiwa ni pamoja na kulipa Kodi katika Biashara zangu.

images (60).jpeg

Picha kutoka mtandaoni.

Kwa upande mwingine nimeacha MAUMIVU makali sana kwa watu, nimerudisha nyuma maendeleo ya Walio wengi, nimefarakanisha Ndoa za watu, nimeachisha masomo Vijana walio wengi, nimebadilisha tabia njema za vijana majumbani na Mashuleni. Walio matajiri nimewabadilisha kuwa masikini kwa muda mfupi, Nimefanya wale waliokuwa watumishi wa Mungu kunipenda na Kuungana nami katika Biashara zangu.Nimewaaminisha Vijana utajiri wa Haraka na hivyo kuacha kufanya Kazi. Kwa ujumla mimi sio RAFIKI mwema kwa wanaopenda maendeleo ya GHAFLA.

Mimi ni Nani?
Vijana wengi wa mjini wananifahamu kwa jina la "MKEKA", naitwa "Michezo ya KUBASHIRI" kwa kimombo ni BETTING, nina sura tofauti tofauti katika jamii, naweza kuonekana kama BETWAY, SPORTPESA, M-BET, BETPAWA, MERIDIAN BET, PARIMATCH, PREMIER BET, WASAFI BET na kadhalika. Nina simamiwa na bodi ya michezo ya kubashiri TANZANIA, ambayo ipo kwa mujibu wa sheria na imepewa mamlaka ya kusimamia na kuyaendesha na kutoa adhabu au faini kwa kampuni zitakazo kiuka kanuni za uendeshaji na pia kupendekeza utaratibu wa namna gani makampuni ya michezo ya kubashiri yanatakiwa kuendeshwa, pia imepewa mamlaka ya kusajili na kufuta makampuni yanayoenda kinyume na sheria. Nina lipa Kodi na kutambulika na mamlaka za serikali. Nina husika na michezo mbalimbali ya kubahatisha kama vile KASINO, KASINO MTANDAONI, KASINO NDOGO, MICHEZO YA KUBASHIRI MATOKEO, MICHEZO YA MASHINE, BAHATI NASIBU YA TAIFA, BAHATI NASIBU YA KUTUMIA UJUMBE MFUPI WA SIMU, MICHEZO YA VIKARAGOSI ( virtual games).

images (56).jpeg
images (58).jpeg

Vijana wakiweka mikeka(Picha zote kutoka mtandaoni).

Faida zangu kwa serikali na Watu wake.
Nimekuwa moja ya chanzo cha mapato kwa serikali kwa kulipa kodi za aina mbili, Moja ni kodi ya michezo ya kubahatisha( Gaming tax) ambayo hutolewa na mwendeshaji wa michezo hii ya kubahatisha. Pili ni kodi ya Michezo ya kubahatisha kwenye zawadi ( Gaming tax on Winnings) ambayo hukatwa kutoka kwenye Bonasi ya Mshindi. Hivyo nimechochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Nchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Miundo mbinu kama vile Barabara, Hospitali, shule na huduma zingine za Jamii. Lakini pia nimewanufainisha watu wachache ambao walinifuatilia na Kufanikiwa kushinda katika Bahati nasibu zao.

Hasara zangu kwa serikali na watu wake.
Pamoja na kuwa na faida, Hasara zangu kwa serikali na watu wake ni nyingi zaidi, Nimepunguza Nguvu kazi ya Taifa kwa kuwafanya vijana walio wengi kunitegemea tokea asubuhi hadi jioni wakikesha katika mabanda ya KUBASHIRI na hivyo kushindwa kufanya shughuli zingine za kuzalisha mali kama vile KILIMO, BIASHARA, na UJASILIAMALI ambao ungeweza kuwaingizia kipato na kuliingizia taifa Kipato, lakini pia Nimevunja mioyo ya Vijana walio wengi pale wanapoweka kiasi kikubwa cha Fedha katika UBASHIRI na kuangukia pua, Vijana wengi wamechukua Hatua ya Kukimbia familia zao, na wengine kufikia hatua ya KUJIUA.
images (49).jpeg

images (50).jpeg
Vijana wakifuatilia mikeka yao( picha kutoka mtandaoni)

Nimekula mitaji ya Vijana waliowengi na hivyo kuwakwamisha katika Malengo yao ya kimaendeleo, Nimekula pesa za kujikimu(BUMU) za Vijana wengi Vyuoni na kupelekea kukatisha masomo yao kwasababu ya ugumu wa maisha Vyuoni, Ndoa nyingi zimevunjika kwasababu yangu, lakini pia Nimepelekea mmomonyoko wa maadili kwa vijana wadogo kwasababu ya Kujiunga na mimi na Kusahau Masomo shuleni. Nimepelekea Vijana wengi kupata ugonjwa wa MSONGO WA MAWAZO ( SONONA) kwa sababu ya kukosa matarajio ambayo walikuwa nayo. Mimi ni Chanzo cha migogoro mingi miongoni mwa Vijana.
images (51).jpeg

Mkeka umechanika ( picha kutoka mtandaoni)

Vita dhidi yangu.
Nimekuwa nikipigwa vita kila mahali MAKANISANI NA MISIKITINI, baadhi ya serikali zimeshindwa kuniruhusu kutokana na itikadi zao. Lakini pia watu mbalimbali duniani wamekuwa wakinipiga vita, Viongozi wa Dini, wanamichezo mashuhuri wote hao wamekuwa adui kwangu. Mwaka 2019 Bodi ya Michezo ya Kubashiri nchini KENYA ilipiga marufuku Matangazo ya mchezo huo mitaani, kwenye mitandao ya kijamii, na Kwenye runinga ( Kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku), Pia ilizuia watu maarufu kupigia chapuo( endorse) ubashiri na kampuni za Ubashiri.(Chanzo, www.Muungwana.co.tz/2019). Na hadi leo vita dhidi yangu inaendelea kila mahali Duniani.

Ombi langu Kwa Vijana wa Kitanzania.
Pamoja na kupigwa vita kila mahali, Bado mimi ni rafiki kwa watawala serikalini, hii ni kutokana na Mchango wangu mkubwa katika Maendeleo Nchini kupitia kodi yangu, Hata katika sekta ya michezo nimekuwa Nguzo kubwa katika maendeleo ya Michezo nchini ikiwa ni pamoja na Kudhamini michuani mbalimbali lakini pia kudhamini Klabu zetu kwa kutoa fedha nyingi. Hivyo SI RAHISI MIMI KUONDOKA. Vijana wote wanatakiwa kunielewa na kunizoea na Kutotumia MUDA mwingi na fedha nyingi kunihangaikia. Wanapaswa kuwa na KIASI na kunichukulia mimi kama BURUDANI kwao na Sio kama CHANZO CHA MAPATO, Hivyo watafute shughuli zingine za kufanya ili kujikwamua KIUCHUMI wakikumbuka kuwa VIJANA ndio NGUVU YA TAIFA.
 
Upvote 41
Safi sana kwa Makala hii Nzuri. Nimekuwa nikikufuatilia na kuzisoma makala zako, hakika unastahili pongezi Mwandishi.

Huu ndio uhalisia wa maisha ya vijana wengi siku hizi. Kura yangu umeipata
Asante kwa mrejesho huo mwanajukwaa.
Nakuelewaga sana mwandishi wewe nakiri wazi kuwa Umekuwa ukiandika MAKALA BOMBA SANA. umepata kura yangu.
Tupo pamoja mwanajukwaa. Ahsante sana
 
Utangulizi.
Nimekuwa maarufu sana katika karne hii ya ishirini na moja(21). Kila mahali napokelewa kwa shangwe na walio wengi, sio vijana tu bali watu wa kila umri wananikubali na Kunipenda. Mamlaka za utawala nazo zimenipokea kwa mikono miwili na kunipatia mazingira rafiki ya kuishi. Nimekuwa na faida kubwa kwa serikali kwani ninachangia katika Maendeleo, na kufanya watawala wengi wanipigie Chapuo wakati ninapopata MISUKOSUKO.
Nimeteka watu wa kila aina VIJANA kwa WAZEE, Wasomi kwa wasiosoma, Matajiri kwa Maskini, Wanafunzi kwa wasio wanafunzi, Hakika nimekita mizizi kila eneo KANISANI nipo, MISIKITINI nipo, Maofisini nipo, Mashuleni nipo, Vyuoni, Majumbani hata katika Vyombo vya Usafiri napatikana. Umaarufu wangu umekuwa Mkubwa na kuufanya Ulimwengu wote Unigeukie. Kizuri zaidi kwangu ni kwamba NIPO KIHALALI, nafanya kazi zangu pasipo Bugudha yoyote kwasababu Nafuata sheria zote za Nchi ikiwa ni pamoja na kulipa Kodi katika Biashara zangu.

View attachment 2354508
Picha kutoka mtandaoni.

Kwa upande mwingine nimeacha MAUMIVU makali sana kwa watu, nimerudisha nyuma maendeleo ya Walio wengi, nimefarakanisha Ndoa za watu, nimeachisha masomo Vijana walio wengi, nimebadilisha tabia njema za vijana majumbani na Mashuleni. Walio matajiri nimewabadilisha kuwa masikini kwa muda mfupi, Nimefanya wale waliokuwa watumishi wa Mungu kunipenda na Kuungana nami katika Biashara zangu.Nimewaaminisha Vijana utajiri wa Haraka na hivyo kuacha kufanya Kazi. Kwa ujumla mimi sio RAFIKI mwema kwa wanaopenda maendeleo ya GHAFLA.

Mimi ni Nani?
Vijana wengi wa mjini wananifahamu kwa jina la "MKEKA", naitwa "Michezo ya KUBASHIRI" kwa kimombo ni BETTING, nina sura tofauti tofauti katika jamii, naweza kuonekana kama BETWAY, SPORTPESA, M-BET, BETPAWA, MERIDIAN BET, PARIMATCH, PREMIER BET, WASAFI BET na kadhalika. Nina simamiwa na bodi ya michezo ya kubashiri TANZANIA, ambayo ipo kwa mujibu wa sheria na imepewa mamlaka ya kusimamia na kuyaendesha na kutoa adhabu au faini kwa kampuni zitakazo kiuka kanuni za uendeshaji na pia kupendekeza utaratibu wa namna gani makampuni ya michezo ya kubashiri yanatakiwa kuendeshwa, pia imepewa mamlaka ya kusajili na kufuta makampuni yanayoenda kinyume na sheria. Nina lipa Kodi na kutambulika na mamlaka za serikali. Nina husika na michezo mbalimbali ya kubahatisha kama vile KASINO, KASINO MTANDAONI, KASINO NDOGO, MICHEZO YA KUBASHIRI MATOKEO, MICHEZO YA MASHINE, BAHATI NASIBU YA TAIFA, BAHATI NASIBU YA KUTUMIA UJUMBE MFUPI WA SIMU, MICHEZO YA VIKARAGOSI ( virtual games).
View attachment 2354518
Vijana wakiweka mikeka(Picha zote kutoka mtandaoni).

Faida zangu kwa serikali na Watu wake.
Nimekuwa moja ya chanzo cha mapato kwa serikali kwa kulipa kodi za aina mbili, Moja ni kodi ya michezo ya kubahatisha( Gaming tax) ambayo hutolewa na mwendeshaji wa michezo hii ya kubahatisha. Pili ni kodi ya Michezo ya kubahatisha kwenye zawadi ( Gaming tax on Winnings) ambayo hukatwa kutoka kwenye Bonasi ya Mshindi. Hivyo nimechochea kwa kiasi kikubwa maendeleo ya Nchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Miundo mbinu kama vile Barabara, Hospitali, shule na huduma zingine za Jamii. Lakini pia nimewanufainisha watu wachache ambao walinifuatilia na Kufanikiwa kushinda katika Bahati nasibu zao.

Hasara zangu kwa serikali na watu wake.
Pamoja na kuwa na faida, Hasara zangu kwa serikali na watu wake ni nyingi zaidi, Nimepunguza Nguvu kazi ya Taifa kwa kuwafanya vijana walio wengi kunitegemea tokea asubuhi hadi jioni wakikesha katika mabanda ya KUBASHIRI na hivyo kushindwa kufanya shughuli zingine za kuzalisha mali kama vile KILIMO, BIASHARA, na UJASILIAMALI ambao ungeweza kuwaingizia kipato na kuliingizia taifa Kipato, lakini pia Nimevunja mioyo ya Vijana walio wengi pale wanapoweka kiasi kikubwa cha Fedha katika UBASHIRI na kuangukia pua, Vijana wengi wamechukua Hatua ya Kukimbia familia zao, na wengine kufikia hatua ya KUJIUA.
View attachment 2354519
Vijana wakifuatilia mikeka yao( picha kutoka mtandaoni)

Nimekula mitaji ya Vijana waliowengi na hivyo kuwakwamisha katika Malengo yao ya kimaendeleo, Nimekula pesa za kujikimu(BUMU) za Vijana wengi Vyuoni na kupelekea kukatisha masomo yao kwasababu ya ugumu wa maisha Vyuoni, Ndoa nyingi zimevunjika kwasababu yangu, lakini pia Nimepelekea mmomonyoko wa maadili kwa vijana wadogo kwasababu ya Kujiunga na mimi na Kusahau Masomo shuleni. Nimepelekea Vijana wengi kupata ugonjwa wa MSONGO WA MAWAZO ( SONONA) kwa sababu ya kukosa matarajio ambayo walikuwa nayo. Mimi ni Chanzo cha migogoro mingi miongoni mwa Vijana.
View attachment 2354522
Mkeka umechanika ( picha kutoka mtandaoni)

Vita dhidi yangu.
Nimekuwa nikipigwa vita kila mahali MAKANISANI NA MISIKITINI, baadhi ya serikali zimeshindwa kuniruhusu kutokana na itikadi zao. Lakini pia watu mbalimbali duniani wamekuwa wakinipiga vita, Viongozi wa Dini, wanamichezo mashuhuri wote hao wamekuwa adui kwangu. Mwaka 2019 Bodi ya Michezo ya Kubashiri nchini KENYA ilipiga marufuku Matangazo ya mchezo huo mitaani, kwenye mitandao ya kijamii, na Kwenye runinga ( Kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 4 usiku), Pia ilizuia watu maarufu kupigia chapuo( endorse) ubashiri na kampuni za Ubashiri.(Chanzo, www.Muungwana.co.tz/2019). Na hadi leo vita dhidi yangu inaendelea kila mahali Duniani.

Ombi langu Kwa Vijana wa Kitanzania.
Pamoja na kupigwa vita kila mahali, Bado mimi ni rafiki kwa watawala serikalini, hii ni kutokana na Mchango wangu mkubwa katika Maendeleo Nchini kupitia kodi yangu, Hata katika sekta ya michezo nimekuwa Nguzo kubwa katika maendeleo ya Michezo nchini ikiwa ni pamoja na Kudhamini michuani mbalimbali lakini pia kudhamini Klabu zetu kwa kutoa fedha nyingi. Hivyo SI RAHISI MIMI KUONDOKA. Vijana wote wanatakiwa kunielewa na kunizoea na Kutotumia MUDA mwingi na fedha nyingi kunihangaikia. Wanapaswa kuwa na KIASI na kunichukulia mimi kama BURUDANI kwao na Sio kama CHANZO CHA MAPATO, Hivyo watafute shughuli zingine za kufanya ili kujikwamua KIUCHUMI wakikumbuka kuwa VIJANA ndio NGUVU YA TAIFA.
Asante kwa kusoma na KUPIGA KURA yako katika andiko hili. Kama bado hujapiga kura yako piga sasa kwa kubonyeza sehemu iliyoandikwa VOTE chini ya andiko.
 
Mbna iyo vote siion
Fungua hili andiko kisha angalia mwisho wa andiko kuna alama ya V na neno linasomeka VOTE. Bonyeza Sehemu hiyo italeta rangi nyekundu na kukuandikia VOTE APPROVED. Hapo utakuwa umepiga kura yako.

Ahsante sana mwanajukwaa kwa kusoma andiko hili Muhimu.
 
Habari mwanajukwaa. Tafadhari usiache kusoma makala hii na kuipigia KURA.
 
Fungua hili andiko kisha angalia mwisho wa andiko kuna alama ya V na neno linasomeka VOTE. Bonyeza Sehemu hiyo italeta rangi nyekundu na kukuandikia VOTE APPROVED. Hapo utakuwa umepiga kura yako.

Ahsante sana mwanajukwaa kwa kusoma andiko hili Muhimu.
Screen shot ilipo iyo V utume humu mm Sion mwisho wa andiko Kuna neno Quote
 
Mkuu umetisha sijaona sehemu hata moja ya kukukosoa ila bahati mbaya mimi sio mpenzi wa betting mkuu. Hivyo najishughulisha na kilimo na ufugaji maporini.
Asante mwana JF. Mungu akuongoze katika kazi zako hizo. Tafadhari usiache kupiga kura yako Katika andiko HILI.
 
Nielekeze namna ya Kupiga kura Katika andiko hili.
Asante mwana JF Kwa kusoma andiko hili. Ili uweze kupiga kura yako fungua andiko hili kisha utaona kwa chini kuna sehemu imeandikwa VOTE, ukibonyeza sehemu hiyo utakuwa umepiga kura yako.
 
Back
Top Bottom