Mimi ndoa ilinipotezea muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu

Mimi ndoa ilinipotezea muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu

Mwachiluwi

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2022
Posts
25,258
Reaction score
48,589
Sijui kwako ndoa ina maana gani lakini kwangu Mimi ndoa ilinipotezea Muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu.

Sikuwahi kuwaza chochote kuhusu ndoa wala kuitamani, lakini siku moja nilikua natoka sokoni Mabibo naelekea nyumbani Magomeni Usalama, niliposhuka kwenye daladala kwa bahati mbaya niliteleza na kuanguka wakati navuka barabara. Mfuko wenye vitu nilivyonunua sokoni uliangukia pembeni.

Nilihisi aibu sana siku ile na kibaya zaidi mvua ilikua imenyesha majira ya asubuhi, lilijaa tope lililoniharibia Baibui langu. Eneo nililoangukia palikua na kijiwe cha Bodaboda. Kama uwajuavyo walianza kushangilia anguko langu kitu kilichozidi kunipa hasira lakini sikuwa na la kufanya zaidi ya kujiokotanisha pale.

“Pole sana Dada” niliisikia sauti hii nikiwa nasimama, aliyenipa pole alinipatia na mfuko wangu akiwa ameokotanisha vitu vyangu. Alikua kijana mzuri mtanashati sana, nilijikuta nikiwa na kigugumizi kumjibu

“Unaelekea wapi?”

“Nyuma ya sheli, usijali” nilisema nikiwa najipangusa tope kutoka kwenye Baibui langu jeusi, akanipa mkono wake

“Naitwa Salehe Mwinyimkuu” Alijitambulisha kwangu, nilimtazama kwa sekunde kadhaa kisha nilimjibu

“Naitwa Saida”

“Nimefurahi kukufahamu, wacha nikusogeze” alisema, kwa msaada alionipa isingelikuwa hisani kukataa alichokiomba. Taratibu tuliikanyaga ardhi kuelekea karibu na nyumbani kwetu. Kwa muda mchache nilihisi kumjua kidogo, niligundua ni mpole, mwemye hekima na busara tele licha ya kuniambia ana Miaka 27 tu.

“Mimi nina Miaka 23” nilijitanbulisha kwake huku nikianza kunogewa na mazungumzo yake. Tuliongea mengi hadi kubadilishana namba za simu kitu ambacho sikuwahi kukifanya kwa Mtu nisiyemjua.

Tulizidi kuwasiliana kwa zaidi ya mwezi mzima huku tukiwa marafiki wa kawaida tu lakini baadaye Salehe alinitongoza.

Nisiwe mwongo wala mnafiki hata kabla ya kunitongoza nilianza kumpenda hivyo kunitongoza alikua anatimiza wajibu wake kama Mwanaume kwani nisingeliweza kumwambia Nampenda isitoshe Mimi nilikua Bikra kwa wakati ule.

Tulianza mahusiano ya Kimapenzi lakini nilimwambia Salehe kuwa Mimi nimelelewa kwenye familia ya Dini sana, Baba yangu ni msaidizi wa Shekh Mkuu wa Msikiti wa Magomeni hivyo kama ananipenda kweli basi awaone wazazi wangu kwanza. Sijui tuseme alikua na kiu sana au alikua anahitaji Mke sana maana alilifanya hilo siku tatu tu baada ya kumwambia

Baba yangu alifurahi sana, Mama pia alifurahi zaidi akaniambia

“Mwanangu ndoa ni Nusu ya Dini, sisi Wazazi wako tunakutakia kila lililo jema, Mungu akuongoze” Daima Mama yangu alikua Mtu wa karibu sana kwangu, alisimama na Mimi kwenye kila jambo hata ambalo Baba yangu alipingana na Mimi.

Salehe hakutaka kuchelewesha alilipa Mahali siku iliyofuata.

“Wewe Kijana ni Mtu wa wapi?” Baba alimuuliza Salehe wakiwa katika mazungumzo ya kawaida, kama Mzazi ni lazima ahakikishe usalama wa Binti yake

“Kwetu Rukwa lakini nipo Hapa Dar Likizo” alisema Salehe

“Ooh! Unajishughulisha na nini?”

“Nimeajiliwa, Mwalimu wa Shule ya Msingi Rukwa Mjini”

“Utamtunza Binti yangu?”

Kwanza Salehe alicheka kidogo kisha akamwambia Baba

“Nisipomtunza Mke wangu nitamtunza Nani, wanasema Mbuzi unayemlisha ndiye utakaye mkamua maziwa” Basi Baba na Salehe wakaishia kuangua vicheko, ilileta raha sana.

Ndugu wa Salehe walifika tena waliazimia kuwa ndoa ipite kabla likizo ya Salehe haijaisha ili tuondoke wote kuelekea Rukwa, sikuwahi kufikiria kuwa siku moja nitaolewa na kwenda mbali kama Rukwa. Kidogo nilipata huzuni, nilimzoea Mama yangu

“Usijali, hata Mimi niliwaacha Wazazi wangu Morogoro nikaja kuishi na Baba yako Saida. Umri ukifika hakuna la kukuzuia kuanzisha Familia yako” Mama yangu hakuacha kunitia Moyo. Baba aliachia tabasamu maana tulikuwa wote sebleni

“Ngoja niwaache muongee maongezi yenu ya kike” alisema Baba akaelekea zake Msikitini, zilipita siku kadhaa hadi siku ya ndoa ilipowadia. Ndoa ilipita salama, Siku ya pili tulianza safari ya kuelekea Rukwa Mimi na Mume wangu Salehe.

Bado nilikua Bikra wala hakunigusa usiku wa kwanza wa ndoa yetu hotelini kabla ya Kuanza safari, kwakua nami nikikua mgeni wala sikudai chochote kile. Tulifika Rukwa Usiku sana tena nikiwa ninasinzia, tulichukua Taxi hadi nyumbani kwa Salehe

“Karibu nyumbani Mke wangu, jisikie uko nyumbani kabisa na hapa ndipo tutakapoishi” alisema tukiwa tunashuka kwenye taxi, tulisimama mbele ya nyumba moja iliyo giza sana, sikushangaa sababu mwenye nyumba hakuwepo kwa muda mrefu. Nilijiegemeza kwenye bega la Salehe nikamwambia

“Mume wangu, ulipo nipo na nitaendelea kuwepo siku zote” lile Taxi liliondoka, kazi ya kuhamishia mabegi ndani ilianza. Salehe alikua ametangulia nami nilibakia nyuma nikikokota begi. Sijui ni mawazo yangu au nilisikia kitu halisi kabisa, nilisikia sauti za Watoto wakiomba Msaada

“Subhannah‼” nilishtuka, sikuisikia tena ile sauti maana mwanzo ilitokea ndani ya ile nyumba ambayo tulikua tukielekea. Mapigo ya moyo yalinienda mbio, niliposikiliza vizuri wala sikuzisikia tena nikajua ni fikra zangu tu. Basi niliendeelea kuvuta begi hadi ndani, taa zikawashwa

Palikua kimya sana, uzuri sikua na njaa wala hamu ya kula zaidi ya Kulala kutokana na Uchovu wa safari. Nilisimama kusuburia Salehe anioneshe chumba chetu, akaufunga mlango kisha akaniongoza hadi chumbani, nilipofika nilijitupa Kitandani na kujilaza kama pono bila kujali kuwa kitandani palikua vumbi tupu.

Nililala Usingizi wa nusu kifo hadi mapambazuko, sauti ya jogoo kuwika niliisikia ikiniamsha na kuniambia ni muda muafaka wa kuanza majukumu ya nyumbani. Macho yalijawa na Ukungu usio kifani, nilijinyoosha kama Kinda la ndege halafu nikajikuta nikipigwa na Butwaa zito sana ambalo kiukweli nilishangazwa mno na nilichokiona

“Nipo wapi hapa?” Nilijiuliza swali hili, niliipapasa akili yangu inikumbushe jambo lakini haikua tayari kufanya hivyo, Salehe hakuwepo Kitandani. Moyo ulinienda hali Jojo, nilinyanyuka taratibu kutoka kitandani.

Nitakueleza kwanini nilipigwa na Butwaa la ajabu, kwanza harufu ya Udi wenye harufu mbaya ilizagaa kote ndani, pili nilisikia sauti ya Mtu akitwanga na kwa hakika alikua akitwangia ndani halafu sauti ya Mtoto Mchanga anayelia nilizidi kuisikia. Taratibu nilitaka kujuwa nipo wapi haswa maana tayari nilianza kupata hofu fulani

Nilipiga hatua za taratibu hadi mlango wa kutokea chumbani, ile sauti ilitoweka na palikua kimya sana. Moyo wangu haukutulia kabisa licha ya ukimya wa ghafla niliousikia, jua lilikua tayari limeshatoka

Nyumba ilikua safi sana. Ilikua na korido ndefu yenye vyumba kadhaa japo kwa wakati huo sikuhesabu kutokana na hali niliyokua nikiihisi. Basi Mimi Saida nilijiuliza

“Ah ni mawazo gani haya Jamani, Ewee Allah niepushie Mbali” nilisema kisha nilirudi Chumbani kutafuta simu yangu nimpigie Salehe aniambie alipo si unajua maisha ya Ugeni yanavyoanza. Nilikumbuka mara ya mwisho simu niliiweka kwenye mkoba wangu

Sikuwa na shaka sana kuhusu simu yangu, niliikuta lakini kwa bahati mbaya ilikua imeisha chaji. Niliketi kitandani nikiwaza mambo kadhaa lakini niliona ni bora niweke simu chaji niwasiliane na Salehe

Nilipomaliza kuweka chaji na kuhakikisha simu yangu inaingia chaji nilipata nafasi ya kukiangalia kwa uzuri chumba, kilipangwa vizuri sana hadi nilijikuta nikitabasamu, nilijuwa ni Mume wangu Salehe alikua ameamka mapema na kuweka mazingira sawa. Nilijiona ni mwenye Bahati sana kuitwa Mke wa Salehe, nilikua na nguo zangu zilezile nilizokuja nazo hivyo wazo la kubadilisha nguo lilinijia lakini kabla ya kufanya hivyo nilisikia Mlango wa nje ukigongwa.

Sikujua naanzia wapi kuitikia wito huo, nilisogea hadi mlango wa chumba na kusikiliza vizuri. Mgongaji wa mlango alikua ni Mwanamke na sauti yake ilikua karibu sana hivyo kwa haraka niliamini anagonga mlango wa Nyumba ya Salehe. Hakuna aliyeitikia ile hodi hadi pale nilipoamuwa kumkaribisha nikiwa ndani tena kwa sauti ambayo aliisikia vizuri, nilijiangalia kama nilikua nipo sawa kutoka ndani kisha nilianza safari mara moja kutembea kwenye korido kuuelekea Mlangoni.

Niliufungua mlango wa kwanza kwa kutekenya kitasa tu kisha nikauelekea mlango wa Uwani ambao ndio mgongaji alikua hapo, nilipoufungua nilikutana na Mama Mmoja aliyebeba tenga la mboga mboga kichwani, alikua ameshakata tamaa alikua akiondoka nikamwita

“Mamaaa‼” alipogeuka alirudi hadi Mlangoni

Shikamoo Mama” nilimsalimia kwa adabu, ndivyo nilivyofundishwa kwetu kwa wazazi wangu, yule Mama alitabasamu kisha akaniuliza

“Hauchukui Mboga leo?” Nilitabasamu maana aliuliza kana kwamba alishawahi kuniuzia mboga ila nilielewa Lugha ya Kibiashara huwa hivyo mara zote

“Mimi ni mgeni hapa Mama, labda kesho nikiwa nimeyafahamu vizuri mazingira naweza kuchukua. Usiache kupitisha” nilisema kisha yule Mama aliondoka huku akiitikia

“Napita kila siku Mtaa huu, Wahiiii mboga mboga” alienda mbele zaidi kisha alitokomea machoni pangu. Kuzungumza na yule Mama ni kama kulinisahaulisha kuhusu Salehe lakini alipoondoka nilijiuliza

“Salehe ameenda wapi mbona hajaniaga?” Niliufunga mlango kisha nilirudi ndani, Nyumba ilikua kubwa ya Kisasa lakini ilikua kimya sana sikusikia hata sauti ya ndege kuruka. Uwani

palikua na sehemu ya kukaa nikaona ni bora nikae hapo kwanza nipate upepo, nilijikuta nikipitiwa na Usingizi wa ghafla tu.

Ndoto za hapa na pale zilinifuata usingizini na kunipa hekaheka hadi nikashtuka. Niliposhtuka nilikutana na sura mbili, moja ilikua ya Salehe na nyingine ni ya Mzee mmoja mweusi aliyevalia Baraghashia nyeupe na kanzu nyeupe. Macho yao yalikua kwangu

“Eeeh imekuaje umelala hapo Mke wangu?” aliniuliza Salehe, nilijitabasamisha kidogo kama Mtu anayezuga ili asinione kuwa mvivu

“Hewa ya hapa inavutia, kaupepo nikajikuta nasinzia tu”

“Sawa, huyu ni Baba yangu anaitwa Mzee MwinyiMkuu. Ni Baba yangu Mzazi” alisema Salehe, nilimsalimia yule Mzee kwa heshima sana hata naye alifurahia na kuona ni namna gani nina heshima.

“Marhaba Mkwe wangu mzuri, hakika Mwanangu hakukosea’’ akasema kwa Utani tukajikuta tukicheka kidogo

“Samahani, najua umenitafuta ila nilienda kumpokea Baba maana aliniambia nikirudi tu atakuja kwa ajili ya kukusalimia wewe Mke wangu” alijielezea Salehe, ni kweli Mzee MwinyiMkuu alikuja na begi dogo la Mgongoni lililochakaa sana.

Aaaah! Nimefurahi sana kumuona Baba yako Salehe, karibu Baba.” Nilisema kisha nilisimama na kulishika begi la Mzee MwinyiMkuu ambalo lilikua sakafuni, kabla sijaliinua yule Mzee alinishika mkono kwa nguvu sana hadi nilishtuka, nikamtazama Usoni alikua amenikazia sura yake

“Hili begi halishikwi na kila Mtu, Salehe unajua pa kulipeleka” alisema Mzee MwinyiMkuu, nilihemwa maana sikutegemea lakini hata kama ningelichukua ningelipeleka wapi wakati na Mimi ni Mgeni pale. Nilishusha pumzi, kilinishuka nikarudi kukaa, Salehe akaniambia

“Mzoee Baba yangu ana utani sana Saida, wacha nikaweke begi lake nakuja” Mara moja alipomaliza kusema alinyanyuka Salehe na kuelekea ndani, yule Mzee hakuacha kunitazama kwa jicho kali kama vile kuna kitu nimeharibu hadi nilianza kumwogopa, ikanilazimu kumwomba Msamaha

“Samahani Baba sikujua”

“Siku nyingine uwe unauliza, umeelewa?”

“Ndiyo Baba” Nilipomjibu alinikata jicho fulani la husda kisha akatoa mguno fulani wa kicheko cha dhihaka halafu akanyanyuka na kuiburuza kanzu yake akaingia zake ndani,nilishusha pumzi zote kama Mgonjwa wa Pumu. Niliusikia moyo wangu namna ulivyoamka nakuanza kudunda tena, hata koo ilianza kupitisha mate kwa kasi. Yaani sijui nikueleze vipi unielewe namna nilivyokua nimeshikwa na woga kupitiliza, sura ya yule Mzee niliyona imekaa kikatili sana

Wakati naendelea kujiuliza mara Mume wanu Salehe alirudi kutoka ndani, akaketi mahali alipokua ameketi Baba yake

“Baba yako ni Mkali sana Salehe hadi nimeogopa. Nimefanya kipi kibaya, kumsaidia Begi ni vibaya eti?” Nilimuuliza Mume wangu, yeye akanishika bega akaniambia

“Utamzoea, si unajuwa wazee wa zamani. Pengine hakutaka wewe ushike begi kwasababu zilizo kaa kitamaduni tu za Kizamani au kabila letu lakini ni mcheshi utamzoea kwa muda atakaokaa hapa.

“Ina maana atakuwa anaishi hapa na Sisi?”

“Ndiyo, ila muda mchache tu atakua ameondoka. Vipi umeshakula?” Basi kuzungumza na Salehe kulinifanya nisahau kilichotokea, tuliongea sana hadi Mchana tuliposikia adhana. Salehe akawa wa kwanza kunikumbusha kufanya Ibada, nilitabasamu nikashusha pumzi kidogo huku dimpozi zangu zikionekana
 
🤔🤔
1736700972803.jpg
 
Ilipoishia “Utamzoea, si unajuwa wazee wa zamani. Pengine hakutaka wewe ushike begi kwasababu zilizo kaa kitamaduni tu za Kizamani au kabila letu lakini ni mcheshi utamzoea kwa muda atakaokaa hapa.

“Ina maana atakuwa anaishi hapa na Sisi?”

“Ndiyo, ila muda mchache tu atakua ameondoka. Vipi umeshakula?” Basi kuzungumza na Salehe kulinifanya nisahau kilichotokea, tuliongea sana hadi Mchana tuliposikia adhana. Salehe akawa wa kwanza kunikumbusha kufanya Ibada, nilitabasamu nikashusha pumzi kidogo huku dimpozi zangu zikionekana . Endelea

SEHEMU YA PILI

Ilikua ni ndoto yangu siku moja nifanye ibada na Mwanaume aliyeniowa, moyoni nilimshukuru Mungu kunipa Mume kama Salehe anayejua wajibu wa Mke na Dini yake. Basi tuliongozana hadi chumbani kujiandaa, haikuchukua muda mrefu tukawa tumeshapata udhu kwa ajili ya Ibada.

“Twende sebleni, Baba naye anatusubiria” alisema, sikuacha kutabasamu. Kwangu niliiona ni Familia bora sana, Baba alitusalisha sote hadi tulipomaliza kisha tukarudi Chumbani Mimi na Mume wangu

“Mume wangu, sijui jiko liko wapi, sijui chochote. Mimi ni Mwanamke raha yangu ni kupika chakula mle nyote” nilisema nikiwa nalivua Baibui langu na kulitupa kitandani

“Usijali, leo pumzika sote tunaelewa. Kuanzia kesho utaanza kupika na kufanya kazi nyingine, subiria nakuletea Chakula” alisema Salehe kisha aliondoka zake, aliniacha natabasamu kwa raha. Nikajisemea moyoni tu

“Kumbe ndoa ni tamu kiasi hiki” kicheko cha raha kilinitoka Mtoto wa kike, nikabdilisha nguo kisha nikawasha simu na kuzungumza na Wazazi wangu maana tokea nimefika sikuwajulisha sababu simu ilikua imezima chaji. Wazazi wangu walifurahi sana na kunisihi niwe mvumilivu.

Salehe alikuja na chakula kinachotoa mvuke kuashiria kuwa kilitoka jikoni muda huo huo, pilau la nyama ya Mbuzi na kachumbari yenye pilipili nyingi kama nipendavyo, alinipatia na kunifanya macho yanitoke. Nilimeza mate kwa uchu

Sikutaka kuuliza alikitoa wapi na kama alikipika alipika saa ngapi, nilikifakamia kama kilivyo bila hata aibu. Sasa nimwonee aibu Mume wangu jamani si nitachekwa na Dunia nzima, sasa baada ya kushiba ndio nikakumbuka kumuuliza

“Hivi hiki chakula kimetoka wapi Mume wangu au umenunua maana kusema kimepikwa hapa ni Uwongo, pilau nishindwe kusikia harufu yake wakati kinapikwa Mmh‼” Salehe alitabasamu tu, akaninawisha Maji halafu akaniuliza

Umeshiba eeh?”

“Saaaana, asante kwa Chakula Mume wangu” nilisema nikiwa namwachia tabasamu Mume wangu. Tulikuwa chumbani wawili tu

Akaondoa vyombo bila kunipa jibu lolote lile, sikujali sana.

***

Usiku ulipoingia nilikua na uhakika kuwa Ndiyo utakuwa usiku wetu wa kwanza kama Mume na Mke, nilikua tayari kuiondoa bikira yangu kwa ajili ya Mume wangu. Sasa nikae na Bikira hadi lini na nimeshaolewa, nilijifanyia Usafi nikamsubiria Mume wangu amalize mazungumzo na Baba yake Mzee Mwinyimkuu kisha tuzagamuane kwa mara ya kwanza.

Masaa yalienda hadi nilihisi Usingizi unaninyemelea, nikajiegesha kidogo maana Jumbe zote nilizomtumia hakuzijibu. Nilikuja kushtuka nikakuta kuna Mwanaume ananikula, sikuweza kujizuia nilimpa ushirikiano. Nilijua tu ni Salehe awe nani mwingine, alikua fundi haswa na alinikula haraka haraka kama mwizi vile, nilikua nimezima Taa hivyo palikua giza tupu na sikuweza kuona taswira yoyote isipokua raha ya ajabu sana

Nilitolewa Bikira yangu kwa mazingira hayo, kisha baada ya kumaliza alikimbilia bafuni nami kwa haraka nikawasha taa kuangalia kama kuna damu inatoka ili nisichafue shuka. Hapakua na Damu yoyote ile, lakini nilikipata cha moto nikawa natabasamu tu. Nikiwa hapo nilikua namsuburia Salehe aniambie kwanini amenikula guzani tena nikiwa Usingizini hadi nimeshtuka wakati mimi ni Mke wake

Siyo kwamba aliniudhi, la hasha ila tu si unajuwa asijeniona kama Napenda sana kuzagamuana.basi nilisubiria kwa kitanbo kidogo kama dakika ishirini hivi hadi nikajiuliza

“Anakinawa kitu gani hadi sasa hatoki bafuni?” Bafu lilikua mle mle chumbani. Basi nikaikusanya shuka ili nijifunge nimfuate bafuni, mara ghafla mlango wa chumba ulifunguliwa. Nilipatwa na Mshangao mkubwa sana, eti Salehe ndiyo alikua akiingia Chumbani tena akiwa na nguo zake zilezile alizoondoka nazo kuelekea kuzungumza na Baba yake

Niliyapeleka macho bafuni huku nikijiuliza ni Nani niliyekuwa nafanya naye mapenzi muda mchache uliopita, hata Salehe alinishangaa akaniuliza

“Vipi mbona umepigwa na Butwaa unashangaa nini?” sikujua nimjibu nini, nikakimbilia bafuni, sikukuta Mtu yeyote yule na hapakua na dalili hata ya Maji pale chini, Uwii niliishiwa pozi huku mwili ukitetemeka. Salehe alinifuata Bafuni huku akiniuliza

“Wewe una nini?”

“Mh Mh niko sawa tu, ndio umemaliza muda huu kuzungumza na Baba?” nikajibalaguza kwa hofu sana kumuuliza swali hili ila moyo wangu uliniambia kuwa ndani ya ile nyumba palikua na manbo ya mazingaombwe sababu haiwezekani nifanye mapenzi na Mtu ambaye alipotea ghafla Bafuni

Huu siyo mkasa wa kujitungia, nimkasa wa kweli wa Maisha yangu. Nataka ujifunze kuhusu ndoa na Mtu usiye mjua, unaweza fikiria ni mambo ya kusadikika lakini yalinikuta haya mambo Rukwa kwenye ndoa yangu ya kwanza, sitakuja kusahau.

Basi tulirudi hadi kitandani, wenge zito likiwa limeigubika sura yangu. Wasiwasi ulizidi kutanda. Ningewezaje kumweleza Mume wangu Salehe, angemiamini? Hapana isingelikua rahisi kiasi hicho

“Mke wangu nataka tuzungumze jambo” alisema Salehe alipomaliza kuvua nguo zake, nilitikisa kichwa changu ili aniambie tu maana kichwa kilinijaa mambo mengi na maswali magumu yanayohitaji majibu ya haraka. Siku ya kwanza Rukwa ilianza kwa ugumu sana na ndiyo kwanza ni Usiku wa kwanza

“Kesho naenda Sumbawanga, kuna jambo Baba amenitaka nikalifanye ndiyo maana nimechelewa sana” alisema Salehe

“Ooh! Sawa Mume wangu, utarudi lini?” nilijikaza sana hadi kuunganisha sentensi hii na kumuuliza swali, kigugumizi cha ghafla hakikuniacha kabisa. Halafu kwa mbali nilianza kuhisi homa kali ila nilijikaza tu.

“Baada ya siku tatu, sikuweza kumkatalia. Nimekubali ili Baba aridhike tu ila kukuacha Mke wangu siyojambo rahisi kwangu” Alisema, siyo kwamba nilikua namsikiliza Salehe bali niliwaza ni Nani yule nilifanya naye mapenzi

Haikua ndoto kabisa sababu niliushika mwili wa yule Mwanaume aliyepotelea bafuni. Usiku ulikua mrefu kwangu, maswali hayakuniisha Mimi hadi kulipo pambazuka, kama kawaida ya Salehe hakunigusa kabisa. Kwanza nilishukuru sababu nisingefurahia kutokana na msongo wa mawazo niliokuwa nao

Niliamka mapema kuagana na Mume wangu Salehe, alipoondoka nilienda tena bafuni kukagua huku nikijikumbusha Usiku wa jana, kwa hakika yule Mtu alikimbilia bafuni lakini kwanini hakuwepo nilipoenda lilikuwa ni swali nililojiuliza sana bila kupata jibu lolote lile. Nilibakia nimesimama mlangoni nikilitazama lile bafu

Sasa nilikua nafanya Mapenzi na Nani mbona sielewi Mimi?” sikuwa na budi bali kukosa majibu tu, nikajiwekea moyoni kuwa ipo siku nitaufahamu ukweli.

Jua lilipo chomoza nilivalia nguo za kufanya shughuli za nyumbani, kwakuwa tayari Mume wangu alinionesha mahali lilipo jiko nilielekea huko, nilikagua vitu vya jikoni kama mpishi

nikaanza na kuweka chai jikoni huku nikifikiria ni vitafunwa gani Baba Mkwe angependelea asubuhi hiyo

Nilipaswa kumuuliza kwanza hivyo nilienda kumgongea mlango huku nikiwa na hofu asije akanifokea kama alivyofanya jana, alifungua mlango haraka

“Shikamoo Baba” nilimsalimia kwa haraka sana tena kwa heshima zote huku nikipeleka na magoti yangu uelekeo wa chini kisha nikarudi juu, nilimfanya atabasamu kidogo

“Marhaba Saida, umeamkaje?”

“Namshukuru Mungu nimeamka Salama Baba”

“Usiku wako wa kwanza Rukwa umeendaje!” Nilianza kuonesha tabasamu kabla ya kumjibu

“Mungu ni Mwema Baba, samahani Baba nilikua nauliza unatumia kitafunwa gani asubuhi ya leo?”

“Ooh! Chochote tu mpendwa wangu, maandazi, chapati, mkate Mimi nakula tu” alisema, niliweka mikono yangu mbele kwa heshima muda wote nilipokua naongea naye. Niliachia katabasamu kisha nikamwambia

“Basi sawa Baba, naomba nikakuangalizie”

“Haya Mama, ukitoka tu hapo nje mkono wa Kulia kuna Mama anatengeneza Chapati nzuri sana unaweza kwenda hapo”

“Sawa Baba” Basi nilimwacha Baba Mkwe akiufunga mlango wake kisha mimi nilirudi Chumbani kuchukua pesa ambayo Mume wangu aliniachia halafu nilielekea nje kununua chapati, japo nilikua natembea lakini mwili ulikua na maumivu makali kama homa fulani hivi.

Nilijikaza hadi nilipofika kununua Chapati nilipoelekezwa, nilimsalimia vizuri maana ndiyo majirani wenyewe hao, nikachukua chapati za kututosha Mimi na Baba Mkwe wangu lakini wakati naondoka yule Mama Muuza chapati akaniita, nilikua nimeshampa mgongo hivyo niligeuka na kurudi maana nilishapiga hatua kadhaa mbele

“Abee Mama” Niliitika wito, yule Mama akanitaka nisogee zaidi kanakwamba kuna jambo analotaka nilisikie Mimi tu, basi nilisogea na kwa uzuri tulikua wawili japo kwa pembeni palikua na vijana wengine wakiwa wanatia zogo masuala ya Mpira

“Samahani Binti, ndiyo mara ya kwanza nakuona. Wewe ni Mgeni hapa mtaani?” aliniuliza ila nilianza kuhisi pengine ana jambo fulani lisilo la kawaida pengine anataka kusema, nilisita kidogo lakini nikajikuta nikiachia tabasamu kama ilivyo kawaida yangu

“Ndiyo, Mimi ni mgeni”

“Unaitwa Nani?”

“Naitwa Saida”

“Hayo maua mwilini ni ishara kuwa umeolewa siku chache zilizopita si ndiyo?” Jamani yule Mama simfahamu lakini alinidadisi ndani ya muda mfupi na kugundua yote hayo.

“Ndio, nimeolewa na Salehe wa nyumba ile pale” sikutaka kona kona maana nilijua angeniuliza naishi wapi nikaona nirahisishe maongezi tu.

“Mh! Sawa Mwanangu nisikucheleweshe” alisema halafu muda huo huo akapoa mwili mzima kama siyo yeye aliyekua akinichangamkia. Nilitamani kumuuliza kwanini ameguna ila nilihisi nitazidi kuchelewa maana niliweka chai kwenye jiko la Gesi. Haraka nikamuaga yule Mama kisha nilirejea nyumbani kuepua chai.
 
Nilikuta tayari chai ilikua imesha chemka niliiweka kwenye chupa, nakumbuka nilikua nimenunua chapati Nane, siyo kwamba mimi nilikua mlaji sana ila hofu yangu ilikua kwa Baba Mkwe sikuujua uwezo wake.

Nilipomaliza tu kuweka chai ndani ya chupa papo hapo Mlango uligongwa, nikapaza sauti

“Nakujaaa” Niliamua kwanza nimuwekee Baba Mkwe chai Mezani, nilimtengea chai sebleni na kumwekea chapati tano kisha nikamgongea mlango na kumueleza chai ipo tayari Sebleni, basi nikaelekea moja kwa moja hadi Mlangoni kuitika wito

Nilipofika nilikutanaa na yule Mama muuza mboga mboga wa jana, niliachia katabasamu nikamsalimia.

“Vipi na leo hamchukui? Jamani nyie ni wateja wangu wakubwa sana wa Mboga mboga. Tokea mmeacha kununua Biashara imekua ngumu mno” alisema yule Mama, nilicheka tu nikamwambia

“Mwenye nyumba alisafiri Mama, basi naomba Mchicha wa Elfu moja” nilisema maana niliamini ungetosheleza kwa Watu wawili

“Wa elfu Moja?”

“Ndiyo mbona umeshtuka?”

“Mh! Kwani yule Kijana yuko wapi sijamuona muda, yeye alikua anachukua Mchicha hadi wa Elfu Kumi” alisema yule Mama, sikuweza kujizuia ilibidi nicheke maana Mchicha wa Elfu kumi ungetosha kulisha mifugo na siyo kula Binadamu wawili, ni mwingi Jamani.

“Usicheke kama unabisha Muulize, ni mteja wangu wa muda mrefu sana huwa anachukua hata beseni zima nakua namaliza mapema” Niliacha kucheka maana ilionekana alikua akimaanisha anachoongea, nikasema

“Sawa Mama, kwasasa hayupo amesafiri labda akirudi maana mimi sijui kuhusu hilo ila nimeshangaa huo Mchicha mwingi hivyo huwa anaupeleka wapi Mama” nilisema nikiwa nachagua Mchicha nilioutaka, mara nilisikia Mtu akikohoa nyuma yangu kama ishara kuwa nigeuke ……
 
Ilipoishia “Mh! Kwani yule Kijana yuko wapi sijamuona muda, yeye alikua anachukua Mchicha hadi wa Elfu Kumi” alisema yule Mama, sikuweza kujizuia ilibidi nicheke maana Mchicha wa Elfu kumi ungetosha kulisha mifugo na siyo kula Binadamu wawili, ni mwingi Jamani.

“Usicheke kama unabisha Muulize, ni mteja wangu wa muda mrefu sana huwa anachukua hata beseni zima nakua namaliza mapema” Niliacha kucheka maana ilionekana alikua akimaanisha anachoongea, nikasema

“Sawa Mama, kwasasa hayupo amesafiri labda akirudi maana mimi sijui kuhusu hilo ila nimeshangaa huo Mchicha mwingi hivyo huwa anaupeleka wapi Mama” nilisema nikiwa nachagua Mchicha nilioutaka, mara nilisikia Mtu akikohoa nyuma yangu kama ishara kuwa nigeuke . Endelea

SEHEMU YA TATU

Alikua ni Baba Mkwe wangu, Basi yule Mama alipomwona Baba Mkwe akafurahi sana

“Afadhali nimekuona Bosi wangu, siku hizi ndio mmeamua msiniungishe si ndiyo?” aliyatupa maneno kwa Baba Mkwe

“Ah! Mama mboga mboga huyo, basi fanya kama kawaida. Saida hebu leta beseni” alisema Baba Mkwe, nilishangaa sana lakini sikutaka kuonesha chochote. Nikaelekea ndani kisha nikarudi na Beseni.

Huwezi amini yule Mzee alichukua Mchicha wote na nyanya zote ambazo yule Mama alikua nazo kwenye beseni, nilihisi kama naota vile maaana mchicha wote ule tule wawili? Halafu akatoa pesa yake mfukoni na kulipia kisha yule Mama akaondoka zake, Yule Mzee akabeba Beseni hadi jikoni halafu akaniambia

“Unapaswa kupika Mchicha wote, ukimaliza nitakuelekeza cha kufanya” Uwiii, nilihisi nachanganikiwa. Msomaji unaweza usinielewe lakini Jaribu kununua Mchicha wa Elfu Kumi halafu kaa hapo uuchambue na uupike, nakwambia utamaliza usiku mgongo ukiwa unauma, sasa fikiria tupo wawili tu halafu nipike Mchicha wote ule, haki nilihisi yule Mzee ana mapungufu fulani ndani yake.

“Sawa Baba” jinsi alivyonitazama ilinifanya niitikie tu na siyo vinginevyo ili nisije nikamkasirisha tena, halafu kwa madoido alielekea sebleni kuendelea kunywa chai, nilibaki nimejishika kiuno. Beseni la Mchicha naanzaje kuchambua Jamani halafu nipike tule wawili tu, sikuwahi kusikia kwa Watu kuhusu visa vya Baba Mkwe mara nyingi nilisikia kuhusu Mama Mkwe ila anachofanya Mzee huyu ni zaidi ya Ukatili.

Sikutaka kupoteza muda hata hamu ya Chai iliniishia, nilianza kuchambua Mchicha haraka haraka na uzuri Mungu alinipa Mkono mwepesi sana, hilo hata Mama yangu alikua akilisifia sana. Hata niwe na kazi kubwa kiasi gani nitaifanya kwa muda mfupi sana, sikutaka hata kunyanyua simu na kumpigia Mume wangu Salehe kumweleza anayonifanyia Baba yake sababu sikutaka kuwagombanisha.

Tokea saa Nne asubuhi nilimaliza Kuchambua saa kumi kasoro nikiwa nimechoka na hapo bado sijapika, halafu Baba Mkwe alikua akija kunikagua jikoni kama nimemaliza au vipi huku akinitaka kifanya haraka kupika. Nilijaribu kumwambia kua nimpikie yeye cha Mchana kidogo ili apoze njaa huku mimi nikiwa naandaa huo Mchicha wa Elfu Kumi.

Baada ya kumaliza alinionesha sufuria kubwa ambalo hupikiwa kwenye mashuhuli ili nipikie humo, halafu akaniambia

“Ukimaliza kupika usiipue sufuria hadi niwepo” Unafikiri aliongea kimzaa? Hapana alinikazia sura yake mbaya

“Sawa Baba” nilimjibu kwa sauti ya chini iliyojaa hofu kubwa, sikutaka kupoteza muda nilianza kuupika ule mchicha mwingi huku nikitamani kucheka na kulia kwa wakati Mmoja, ni vile niliambiwa mambo ya kwenye ndoa ni siri ya ndoa siyo vizuri kuyatoa nje ila nilitamani nipige picha niwatumie rafiki zangu waone kichekesho nilichokutana nacho Rukwa.

Nilipiga moyo konde nikawa napika hadi ulipoiva, nilihakikisha chumvi iko sawa kisha nilimwita Baba Mkwe ili kabla sijaondoa sufuria jikoni aone. Alipofika aliniambia

“Tia hii” alinipa karatasi yenye Unga mweusi ninyunyize kwenye mchicha, sikusita nilifanya hivyo halafu akaniambia baada ya dakika Kumi epua kisha acha upoe halafu kapumzike. Alisema akiwa anatabasamu hadi nikajiuliza

“Huyu Mzee ni Mzima kweli, sekunde kumi ananuna sekunde kumi anacheka” Sikummaliza, nilimtazama hadi alipozama chumbani kwake. Basi nilipomaliza niliepua kisha nilifanya kama alivyonielekeza kisha nikaenda zangu chumbani kulala maana nilikua nimechoka sana yaani hata njaa iliacha kuuma.

**

Niliamka kama saa moja na Nusu hivi Usiku, kitu cha kwanza kilikua kuangalia simu yangu kama Mume wangu amenitafuta. Hapakua na ujumbe wala Missed Call yake, nikajaribu kumpigia lakini nikaambiwa simu yake haipatikani niache Ujumbe wa Sauti, nikaitupa simu pembeni kisha nikausikilizia mwili wangu namna unavyowaka moto kwa maumivu

Pale pale nikaanza kujisikia hali ya kutapika, nikaelekea Bafuni nikatapika vitu vya Kijani mfano wa mlenda hivi. Baada ya kutapika nilianza kujisikia vizuri kiasi, nikahisi huwenda labda nilibadili mazingira. Sasa wakati namalizia kunawa mdomoni nikaona kitu kama hirizi nyekundu imeangukia chini, nilishtuka sana maana siku zote hirizi ni ishara ya Uchawi.

Nusura nipige kelele lakini nilijizuia, nikafikiria nifanyaje nimwambie yule Mzee lakini nikahofia anaweza sema mimi Mchawi, pia nikafikiria nimuulize Mume wangu Salehe atakapo rudi ila nikahisi hivyo hivyo, sikujua nifanye nini na ile hirizi. Nikaisukuma kwa mguu na kuisweka nyuma ya bomba mahali ambapo siyo rahisi kwa Mtu yeyte kujua kuwa kuna hirizi ili nione ni ya Nani na kwanini ipo Bafuni.

Kama ni ya Mume wangu basi ataitafuta na kama ni ya yule Mtu niliyefanya naye mapenzi Usiku halafu akatoweka katika mazingira ya kutatanisha ni lazima atarudi tena, nilijiona kama askari aliye vitani.

Muda huo njaa ilianza kuniuma, nikaiwaza chai yangu jikoni, basi nikavaa dera na kuelekea jikoni. Hapo giza lilikua tayari limeingia, nilitafuta zile chapati lakini sikuziona popote pale nikahisi huwenda Baba Mkwe alizichukua na kuzila. Nikawaza nipike ili nile, lakini nikapata

wazo la kumuuliza Baba Mkwe atakula nini, nilimuita sana lakini hakuitika, nikamtazama kote bila mafanikio yoyote yale

Wakati wazo la kwamba atakua ametoka liliponijia ndipo nilipoanza kusikia sauti fulani ya ajabu sana ikitokea chumba kimoja kilicho katikati, kama vile palikua na mnyama anayekula nyama ndani ya hicho chumba.

Sauti ya kuunguruma kabisa kama vile simba anakula nyama, nilishtuka sana halafu mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio huku nikiwa ninatetemeka, nilijiuliza ni nini kinaendelea ndani ya nyumba ya Mume wangu Salehe maana tokea nimefika ni mauzauza tu, shahuku ya kutaka kujuwa kuna nini ilinianza.

Palikua kimya hapakuwa na dalili ya Mtu yeyote kuingia ndani isipokua sauti ya ajabu ya kutafuna na kuunguruma humo ndani, pumzi za nguvu zilinitoka huku kifua changu kikipata shida ya kuzisukuma pumzi hizo zilizojaa hofu sana. Nikapata wazo jipya la kuchungulia badala ya kuufungua mlango huo, basi nilimwomba Mungu kwanza kabla ya kulianza zoezi hilo.

Taratibu nilipeleka jicho langu kubwa kwenye tundu la kitasa cha Mlango, ile sauti bado ilikuwamo lakini kilichonishtua ni kuliona lile sufuria la Mchicha likiwa tupu ndani ya kile chumba. Weee‼ nilishtuka hadi nikaacha kuchungulia, kimbelembele chote kiliniisha haraka sana.

Nikanyanyua miguu yangu kuelekea jikoni kuangalia kama lile sufuria lipo, nilipofika sikuliona hivyo nikawa na Uhakika kabisa kuwa Sufuria lipo ndani ya kile chumba, lakini limeenda kufanya nini na ule Mchicha unaliwa na Nani, ile sauti ni ya Nani?

Sikupata jibu lolote lile, hofu ilizidi kunizonga huku mwili ukiniisha nguvu, nikakimbilia chumbani ili nimpigie simu Salehe. Kiukweli woga mkubwa ulioambatana na kukosa nguvu ulinishika sana, niliichukua simu haraka sana na kumpigia Salehe huku nikiomba simu ipokelewe. Bahati nzuri safari hii simu ya Mume wangu iliita

“Salehe Pokea simu tafadhali” nilisema huku sauti ikinijia ya kutaka kulia, kabla hata haijapokelewa mara mlango ulianza kugongwa. Huo mshituko nilioupata ulinifanya nidondoshe simu yangu ikaangukia chini na kupasuka kioo kabisa. Sikujali kuhusu simu nilijali kuhusu ni Nani anaugonga mlango wa chumba changu.

“Saida” niliisikia sauti ya Baba Mkwe wangu, jinsi nilivyokua namwogopa yule nilizidi kutetemeka, akaita mara ya pili na tatu huku akizidi kukaza sauti yake ikabidi niitike kama Mtu aliyeamshwa Usingizini

“Njoo” alisema halafu nikasikia kama kaondoka pale mlangoni, nilishusha pumzi nzito sana,pumzi ambayo kama pangelikua na karatasi basi ingelipeperukia mbali kutokana na mshindo wa pumzi yangu. Nikaiokota simu, cha ajabu ni kuwa muda wote Salehe alikua anaitika

ile simu yaani alikua akiongea na kuniuliza mbona siongei, wakati naiweka sikioni akakata simu. Nikajaribu kumpigia lakini bahati mbaya nyingine simu ilikua haina uwezo wa kugusika na kufanya kazi zaidi ya kuiangalia tu.

Nusura chozi linibubujike lakini sikuacha kujipa moyo, nikajikaza ili Yule Mzee asigundue chochote kuhusu Mimi, papo hapo nikaelekea kufungua mlango huku nikiigiza kanakwamba ndiyo nimetoka kuamka, sikujua yule Mzee ananiita wapi ikabidi Mimi ndiyo niite ili nijuwe alipo. Ulikua usiku mgumu sana kwangu……Tuendeleeee‼

Njoo” aliniita baada ya kusikia sauti yangu, aliniita kwenye chumba kile kile ambacho nilisikia sauti ya ajabu na kuona lile sufuria la Mchicha.

Taratibu na kwa hofu niliufungua mlango huku nikimwomba Mungu nisikutane na chochote kibaya. Nilipofika nilimkuta akiwa amesimama. Chumba kilikua na sufuria chini lakini nilipoingia niliusikia mwili wangu ukiwa unasisimka sana kitu ambacho kilinifanya nihisi hapakuwa sehemu salama

“Abeeh‼”

“Ondoa halafu uje” aliongea kwa sauti kavu, huku kidole chake akikionesha kuelekea kwenye sufuri lililo tupu halafu funiko lake likiwa pembeni, chini palikua na chembe chembe za Mchicha kama vile kuna waliokuwa wanakula kwa Pupa sana, niliinama haraka ili nitoke pale chumbani. Nilitoka haraka hadi nikajigonga mlangoni lakini sikusikia maumivu yoyote yale. Nilipofika Jikoni nilijikuta chozi likinitoka, nilitamani kumpigia simu Mama niweze kuondoka maana niliona yule Mzee alikua na mambo yasiyoeleweka, Mume wangu naye sikujua kwanini aliniacha na Baba yake.

Nilijikaza kikike hadi nikarudi tena chumbani mle na kufanya usafi kisha yule Mzee akaniambia

“Halafu uje” nilihisi nitakuwa nimemaliza kumbe ndiyo kwanza alinihitaji tena, kibaya zaidi alikua amevalia msuli mwekundu na Singlendi nyeupe iliyochanika, juu alikua na balaghashia nyeusi ndogo.

“Sawa Baba” nilisema kisha nilienda kuweka ule uchafu kwenye mfuko wa taka jikoni, moyo uliniuma sana. Siku ya pili ya ndoa yangu lakini sikuwahi kujuwa maana ya hiyo ndoa ni nini. Basi, nilirudi ndani ya kile chumba, yule Mzee akaniambia

“Ulikumbuka kuja na gauni ulilofungia ndoa?” ilinichukua sekunde kadhaa kulijibu swali hili maana sikujua anamaanisha nini.

“Ndiyo…‼”

“Kalivae uje, kuna mila za kwetu kwa Mwanamke aliyeolewa” alisema yule Mzee, niliitikia kwa kichwa safari hii, halafu niliondoka taratibu hadi chumbani kwangu. Maswali hayakuisha. Nikaufunga kwanza mlango kisha nikajaribu kuwasha ile simu nione kama itafanya kazi niwapigie wazazi wangu. Nilihitaji msaada zaidi na moyo wangu uliniambia hivyo

Simu iliwaka lakini haikukubali kubinyika , lakini muda huo huo simu iliita. Salehe alikua akinipigia, nilihangaika kuipokea lakini haikukubali hadi ilipokata, mara baada ya kukata simu ukaingia ujumbe, niliweza kuusoma kidogo sana lakini haukumalizika sababu simu ilikua imelock

“Saida nisamehe Mimi, yote ni Makosa yangu. Baba yangu…” Ujumbe uliishia hivyo, sikuelewa alitaka kusema nini kuhusu Baba yake. Nikiwa natafakari mara mlango uligongwa na sauti ya yuke Mzee niliisikia ikisema “Nakusubiri wewe muda unaenda huu”

“Nakuja Baba namalizia” nilisema kwa sauti isiyo na shaka kwake halafu nikaitafuta ile gauni, sikuwa na budi bali kuivaa tu ili nione atasema nini yule Mzee. Nilipata hisia mbaya dhidi yake. Nilivalia lile gauni haraka haraka kisha niliificha simu yangu ndani ya gauni, sijui kwanini nililipata wazo hili la kwenda na simu japo haifanyi kazi.

Nilipoingia ndani ya kile chumba, Baba Mkwe aliniambia

“Kaa katikati ya Chumba kisha jifunike huo mtandio hadi nitakaposema ujifunue” wakati anasema alikua akiwasha udi, nikaikumbuka harufu ya Udi. Niliusikia kwa mara ya kwanza siku ya kwanza naamka ndani ya nyumba hii

Hakuishia hapo akaweka Udi ule kila pembe ya chumba kisha akaufunga mlango wa chumba na kunikumbusha

“nimekwambia ujifunike huo mtandio na ubugaze macho yako hadi pale nitakapokueleza nini cha Kufanya” alisema kwa mkazo kidogo, kwakuwa tayari nilikua na woga basi nikafanya hivyo mara moja. Zikapita dakika kadhaa pakiwa kimya kisha dakika iliyofwata akaniambia

“Ondoa mtandio na ufumbue macho yako” aliposema hivyo nilipata hisia ya kuwa kuna jambo nitaliona ndio sababu ya kunitaka niyafumbe macho yangu. Mwili ulizidi kusisimka Jamani..

Nilipofunbua macho sasa nilitamani nikimbie lakini haikuwezekana, nilitamani nife lakini wakati ulikua haujafika, nikatamani ardhi ipasuke niingie lakini hiyo siyo rahisi na mwisho nilitamni ingelikua ndoto niamke nikaendelee na shughuli zangu. Ilikua ni kweli nilizungungwa na Wanaume walio Uchi wa Mnyama, wanaume hao walikua wamepaka vitu kama unga mweupe usoni na mwili mzima halafu walikua wameinamisha vichwa vyao

Nilikua natetemeka kwa hofu huku sura yangu ikizidi kuwa yenye kutaka kulia, Baba Mkwe alikua ameshikilia kisu mkononi akinitazama kwa jicho kali. Yaani jinsi walivyonizunguka wakiwa wamekaa ilinizuia kurudi nyuma wala kwenda mbele bali kutetemeka tu. Sijawahi kupata woga kama ambao niliupata siku hii, moyo ulidunda kwa mapigo ya juu sana kiasi kwamba niliyasikia mapigo kama vile mdundo wa Muziki kwenye redio kubwa (Sabufa).

“Shiii‼” Baba Mkwe akanipa ishara katili ya kunitaka nikae kimya vinginevyo kile kisu kingeingia mwilini mwangu. Kisha akachuchumaa na kuniambia

“Leo utajuwa ni kwanini uliolewa Binti” Alisema halafu akayaongea maneno fulani nisiyoyaelewa, nakumbuka kabisa hayakuwa maneno ya lugha ya Kiswahili bali lugha nisiyoifahamu na wala si Kiingereza wala Kiarabu. Wale Watu wakasimama kisha wakaenda kupotelea kwenye kona za kile chumba kilichojaa harufu ya Udi.
 
Aiseh!
 
Back
Top Bottom