Mimi ndoa ilinipotezea muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu

Mimi ndoa ilinipotezea muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu

Ilipoishia “Mh! Kwani yule Kijana yuko wapi sijamuona muda, yeye alikua anachukua Mchicha hadi wa Elfu Kumi” alisema yule Mama, sikuweza kujizuia ilibidi nicheke maana Mchicha wa Elfu kumi ungetosha kulisha mifugo na siyo kula Binadamu wawili, ni mwingi Jamani.

“Usicheke kama unabisha Muulize, ni mteja wangu wa muda mrefu sana huwa anachukua hata beseni zima nakua namaliza mapema” Niliacha kucheka maana ilionekana alikua akimaanisha anachoongea, nikasema

“Sawa Mama, kwasasa hayupo amesafiri labda akirudi maana mimi sijui kuhusu hilo ila nimeshangaa huo Mchicha mwingi hivyo huwa anaupeleka wapi Mama” nilisema nikiwa nachagua Mchicha nilioutaka, mara nilisikia Mtu akikohoa nyuma yangu kama ishara kuwa nigeuke . Endelea

SEHEMU YA TATU

Alikua ni Baba Mkwe wangu, Basi yule Mama alipomwona Baba Mkwe akafurahi sana

“Afadhali nimekuona Bosi wangu, siku hizi ndio mmeamua msiniungishe si ndiyo?” aliyatupa maneno kwa Baba Mkwe

“Ah! Mama mboga mboga huyo, basi fanya kama kawaida. Saida hebu leta beseni” alisema Baba Mkwe, nilishangaa sana lakini sikutaka kuonesha chochote. Nikaelekea ndani kisha nikarudi na Beseni.

Huwezi amini yule Mzee alichukua Mchicha wote na nyanya zote ambazo yule Mama alikua nazo kwenye beseni, nilihisi kama naota vile maaana mchicha wote ule tule wawili? Halafu akatoa pesa yake mfukoni na kulipia kisha yule Mama akaondoka zake, Yule Mzee akabeba Beseni hadi jikoni halafu akaniambia

“Unapaswa kupika Mchicha wote, ukimaliza nitakuelekeza cha kufanya” Uwiii, nilihisi nachanganikiwa. Msomaji unaweza usinielewe lakini Jaribu kununua Mchicha wa Elfu Kumi halafu kaa hapo uuchambue na uupike, nakwambia utamaliza usiku mgongo ukiwa unauma, sasa fikiria tupo wawili tu halafu nipike Mchicha wote ule, haki nilihisi yule Mzee ana mapungufu fulani ndani yake.

“Sawa Baba” jinsi alivyonitazama ilinifanya niitikie tu na siyo vinginevyo ili nisije nikamkasirisha tena, halafu kwa madoido alielekea sebleni kuendelea kunywa chai, nilibaki nimejishika kiuno. Beseni la Mchicha naanzaje kuchambua Jamani halafu nipike tule wawili tu, sikuwahi kusikia kwa Watu kuhusu visa vya Baba Mkwe mara nyingi nilisikia kuhusu Mama Mkwe ila anachofanya Mzee huyu ni zaidi ya Ukatili.

Sikutaka kupoteza muda hata hamu ya Chai iliniishia, nilianza kuchambua Mchicha haraka haraka na uzuri Mungu alinipa Mkono mwepesi sana, hilo hata Mama yangu alikua akilisifia sana. Hata niwe na kazi kubwa kiasi gani nitaifanya kwa muda mfupi sana, sikutaka hata kunyanyua simu na kumpigia Mume wangu Salehe kumweleza anayonifanyia Baba yake sababu sikutaka kuwagombanisha.

Tokea saa Nne asubuhi nilimaliza Kuchambua saa kumi kasoro nikiwa nimechoka na hapo bado sijapika, halafu Baba Mkwe alikua akija kunikagua jikoni kama nimemaliza au vipi huku akinitaka kifanya haraka kupika. Nilijaribu kumwambia kua nimpikie yeye cha Mchana kidogo ili apoze njaa huku mimi nikiwa naandaa huo Mchicha wa Elfu Kumi.

Baada ya kumaliza alinionesha sufuria kubwa ambalo hupikiwa kwenye mashuhuli ili nipikie humo, halafu akaniambia

“Ukimaliza kupika usiipue sufuria hadi niwepo” Unafikiri aliongea kimzaa? Hapana alinikazia sura yake mbaya

“Sawa Baba” nilimjibu kwa sauti ya chini iliyojaa hofu kubwa, sikutaka kupoteza muda nilianza kuupika ule mchicha mwingi huku nikitamani kucheka na kulia kwa wakati Mmoja, ni vile niliambiwa mambo ya kwenye ndoa ni siri ya ndoa siyo vizuri kuyatoa nje ila nilitamani nipige picha niwatumie rafiki zangu waone kichekesho nilichokutana nacho Rukwa.

Nilipiga moyo konde nikawa napika hadi ulipoiva, nilihakikisha chumvi iko sawa kisha nilimwita Baba Mkwe ili kabla sijaondoa sufuria jikoni aone. Alipofika aliniambia

“Tia hii” alinipa karatasi yenye Unga mweusi ninyunyize kwenye mchicha, sikusita nilifanya hivyo halafu akaniambia baada ya dakika Kumi epua kisha acha upoe halafu kapumzike. Alisema akiwa anatabasamu hadi nikajiuliza

“Huyu Mzee ni Mzima kweli, sekunde kumi ananuna sekunde kumi anacheka” Sikummaliza, nilimtazama hadi alipozama chumbani kwake. Basi nilipomaliza niliepua kisha nilifanya kama alivyonielekeza kisha nikaenda zangu chumbani kulala maana nilikua nimechoka sana yaani hata njaa iliacha kuuma.

**

Niliamka kama saa moja na Nusu hivi Usiku, kitu cha kwanza kilikua kuangalia simu yangu kama Mume wangu amenitafuta. Hapakua na ujumbe wala Missed Call yake, nikajaribu kumpigia lakini nikaambiwa simu yake haipatikani niache Ujumbe wa Sauti, nikaitupa simu pembeni kisha nikausikilizia mwili wangu namna unavyowaka moto kwa maumivu

Pale pale nikaanza kujisikia hali ya kutapika, nikaelekea Bafuni nikatapika vitu vya Kijani mfano wa mlenda hivi. Baada ya kutapika nilianza kujisikia vizuri kiasi, nikahisi huwenda labda nilibadili mazingira. Sasa wakati namalizia kunawa mdomoni nikaona kitu kama hirizi nyekundu imeangukia chini, nilishtuka sana maana siku zote hirizi ni ishara ya Uchawi.

Nusura nipige kelele lakini nilijizuia, nikafikiria nifanyaje nimwambie yule Mzee lakini nikahofia anaweza sema mimi Mchawi, pia nikafikiria nimuulize Mume wangu Salehe atakapo rudi ila nikahisi hivyo hivyo, sikujua nifanye nini na ile hirizi. Nikaisukuma kwa mguu na kuisweka nyuma ya bomba mahali ambapo siyo rahisi kwa Mtu yeyte kujua kuwa kuna hirizi ili nione ni ya Nani na kwanini ipo Bafuni.

Kama ni ya Mume wangu basi ataitafuta na kama ni ya yule Mtu niliyefanya naye mapenzi Usiku halafu akatoweka katika mazingira ya kutatanisha ni lazima atarudi tena, nilijiona kama askari aliye vitani.

Muda huo njaa ilianza kuniuma, nikaiwaza chai yangu jikoni, basi nikavaa dera na kuelekea jikoni. Hapo giza lilikua tayari limeingia, nilitafuta zile chapati lakini sikuziona popote pale nikahisi huwenda Baba Mkwe alizichukua na kuzila. Nikawaza nipike ili nile, lakini nikapata

wazo la kumuuliza Baba Mkwe atakula nini, nilimuita sana lakini hakuitika, nikamtazama kote bila mafanikio yoyote yale

Wakati wazo la kwamba atakua ametoka liliponijia ndipo nilipoanza kusikia sauti fulani ya ajabu sana ikitokea chumba kimoja kilicho katikati, kama vile palikua na mnyama anayekula nyama ndani ya hicho chumba.

Sauti ya kuunguruma kabisa kama vile simba anakula nyama, nilishtuka sana halafu mapigo ya moyo yakaanza kunienda mbio huku nikiwa ninatetemeka, nilijiuliza ni nini kinaendelea ndani ya nyumba ya Mume wangu Salehe maana tokea nimefika ni mauzauza tu, shahuku ya kutaka kujuwa kuna nini ilinianza.

Palikua kimya hapakuwa na dalili ya Mtu yeyote kuingia ndani isipokua sauti ya ajabu ya kutafuna na kuunguruma humo ndani, pumzi za nguvu zilinitoka huku kifua changu kikipata shida ya kuzisukuma pumzi hizo zilizojaa hofu sana. Nikapata wazo jipya la kuchungulia badala ya kuufungua mlango huo, basi nilimwomba Mungu kwanza kabla ya kulianza zoezi hilo.

Taratibu nilipeleka jicho langu kubwa kwenye tundu la kitasa cha Mlango, ile sauti bado ilikuwamo lakini kilichonishtua ni kuliona lile sufuria la Mchicha likiwa tupu ndani ya kile chumba. Weee‼ nilishtuka hadi nikaacha kuchungulia, kimbelembele chote kiliniisha haraka sana.

Nikanyanyua miguu yangu kuelekea jikoni kuangalia kama lile sufuria lipo, nilipofika sikuliona hivyo nikawa na Uhakika kabisa kuwa Sufuria lipo ndani ya kile chumba, lakini limeenda kufanya nini na ule Mchicha unaliwa na Nani, ile sauti ni ya Nani?

Sikupata jibu lolote lile, hofu ilizidi kunizonga huku mwili ukiniisha nguvu, nikakimbilia chumbani ili nimpigie simu Salehe. Kiukweli woga mkubwa ulioambatana na kukosa nguvu ulinishika sana, niliichukua simu haraka sana na kumpigia Salehe huku nikiomba simu ipokelewe. Bahati nzuri safari hii simu ya Mume wangu iliita

“Salehe Pokea simu tafadhali” nilisema huku sauti ikinijia ya kutaka kulia, kabla hata haijapokelewa mara mlango ulianza kugongwa. Huo mshituko nilioupata ulinifanya nidondoshe simu yangu ikaangukia chini na kupasuka kioo kabisa. Sikujali kuhusu simu nilijali kuhusu ni Nani anaugonga mlango wa chumba changu.

“Saida” niliisikia sauti ya Baba Mkwe wangu, jinsi nilivyokua namwogopa yule nilizidi kutetemeka, akaita mara ya pili na tatu huku akizidi kukaza sauti yake ikabidi niitike kama Mtu aliyeamshwa Usingizini

“Njoo” alisema halafu nikasikia kama kaondoka pale mlangoni, nilishusha pumzi nzito sana,pumzi ambayo kama pangelikua na karatasi basi ingelipeperukia mbali kutokana na mshindo wa pumzi yangu. Nikaiokota simu, cha ajabu ni kuwa muda wote Salehe alikua anaitika

ile simu yaani alikua akiongea na kuniuliza mbona siongei, wakati naiweka sikioni akakata simu. Nikajaribu kumpigia lakini bahati mbaya nyingine simu ilikua haina uwezo wa kugusika na kufanya kazi zaidi ya kuiangalia tu.

Nusura chozi linibubujike lakini sikuacha kujipa moyo, nikajikaza ili Yule Mzee asigundue chochote kuhusu Mimi, papo hapo nikaelekea kufungua mlango huku nikiigiza kanakwamba ndiyo nimetoka kuamka, sikujua yule Mzee ananiita wapi ikabidi Mimi ndiyo niite ili nijuwe alipo. Ulikua usiku mgumu sana kwangu……Tuendeleeee‼

Njoo” aliniita baada ya kusikia sauti yangu, aliniita kwenye chumba kile kile ambacho nilisikia sauti ya ajabu na kuona lile sufuria la Mchicha.

Taratibu na kwa hofu niliufungua mlango huku nikimwomba Mungu nisikutane na chochote kibaya. Nilipofika nilimkuta akiwa amesimama. Chumba kilikua na sufuria chini lakini nilipoingia niliusikia mwili wangu ukiwa unasisimka sana kitu ambacho kilinifanya nihisi hapakuwa sehemu salama

“Abeeh‼”

“Ondoa halafu uje” aliongea kwa sauti kavu, huku kidole chake akikionesha kuelekea kwenye sufuri lililo tupu halafu funiko lake likiwa pembeni, chini palikua na chembe chembe za Mchicha kama vile kuna waliokuwa wanakula kwa Pupa sana, niliinama haraka ili nitoke pale chumbani. Nilitoka haraka hadi nikajigonga mlangoni lakini sikusikia maumivu yoyote yale. Nilipofika Jikoni nilijikuta chozi likinitoka, nilitamani kumpigia simu Mama niweze kuondoka maana niliona yule Mzee alikua na mambo yasiyoeleweka, Mume wangu naye sikujua kwanini aliniacha na Baba yake.

Nilijikaza kikike hadi nikarudi tena chumbani mle na kufanya usafi kisha yule Mzee akaniambia

“Halafu uje” nilihisi nitakuwa nimemaliza kumbe ndiyo kwanza alinihitaji tena, kibaya zaidi alikua amevalia msuli mwekundu na Singlendi nyeupe iliyochanika, juu alikua na balaghashia nyeusi ndogo.

“Sawa Baba” nilisema kisha nilienda kuweka ule uchafu kwenye mfuko wa taka jikoni, moyo uliniuma sana. Siku ya pili ya ndoa yangu lakini sikuwahi kujuwa maana ya hiyo ndoa ni nini. Basi, nilirudi ndani ya kile chumba, yule Mzee akaniambia

“Ulikumbuka kuja na gauni ulilofungia ndoa?” ilinichukua sekunde kadhaa kulijibu swali hili maana sikujua anamaanisha nini.

“Ndiyo…‼”

“Kalivae uje, kuna mila za kwetu kwa Mwanamke aliyeolewa” alisema yule Mzee, niliitikia kwa kichwa safari hii, halafu niliondoka taratibu hadi chumbani kwangu. Maswali hayakuisha. Nikaufunga kwanza mlango kisha nikajaribu kuwasha ile simu nione kama itafanya kazi niwapigie wazazi wangu. Nilihitaji msaada zaidi na moyo wangu uliniambia hivyo

Simu iliwaka lakini haikukubali kubinyika , lakini muda huo huo simu iliita. Salehe alikua akinipigia, nilihangaika kuipokea lakini haikukubali hadi ilipokata, mara baada ya kukata simu ukaingia ujumbe, niliweza kuusoma kidogo sana lakini haukumalizika sababu simu ilikua imelock

“Saida nisamehe Mimi, yote ni Makosa yangu. Baba yangu…” Ujumbe uliishia hivyo, sikuelewa alitaka kusema nini kuhusu Baba yake. Nikiwa natafakari mara mlango uligongwa na sauti ya yuke Mzee niliisikia ikisema “Nakusubiri wewe muda unaenda huu”

“Nakuja Baba namalizia” nilisema kwa sauti isiyo na shaka kwake halafu nikaitafuta ile gauni, sikuwa na budi bali kuivaa tu ili nione atasema nini yule Mzee. Nilipata hisia mbaya dhidi yake. Nilivalia lile gauni haraka haraka kisha niliificha simu yangu ndani ya gauni, sijui kwanini nililipata wazo hili la kwenda na simu japo haifanyi kazi.

Nilipoingia ndani ya kile chumba, Baba Mkwe aliniambia

“Kaa katikati ya Chumba kisha jifunike huo mtandio hadi nitakaposema ujifunue” wakati anasema alikua akiwasha udi, nikaikumbuka harufu ya Udi. Niliusikia kwa mara ya kwanza siku ya kwanza naamka ndani ya nyumba hii

Hakuishia hapo akaweka Udi ule kila pembe ya chumba kisha akaufunga mlango wa chumba na kunikumbusha

“nimekwambia ujifunike huo mtandio na ubugaze macho yako hadi pale nitakapokueleza nini cha Kufanya” alisema kwa mkazo kidogo, kwakuwa tayari nilikua na woga basi nikafanya hivyo mara moja. Zikapita dakika kadhaa pakiwa kimya kisha dakika iliyofwata akaniambia

“Ondoa mtandio na ufumbue macho yako” aliposema hivyo nilipata hisia ya kuwa kuna jambo nitaliona ndio sababu ya kunitaka niyafumbe macho yangu. Mwili ulizidi kusisimka Jamani..

Nilipofunbua macho sasa nilitamani nikimbie lakini haikuwezekana, nilitamani nife lakini wakati ulikua haujafika, nikatamani ardhi ipasuke niingie lakini hiyo siyo rahisi na mwisho nilitamni ingelikua ndoto niamke nikaendelee na shughuli zangu. Ilikua ni kweli nilizungungwa na Wanaume walio Uchi wa Mnyama, wanaume hao walikua wamepaka vitu kama unga mweupe usoni na mwili mzima halafu walikua wameinamisha vichwa vyao

Nilikua natetemeka kwa hofu huku sura yangu ikizidi kuwa yenye kutaka kulia, Baba Mkwe alikua ameshikilia kisu mkononi akinitazama kwa jicho kali. Yaani jinsi walivyonizunguka wakiwa wamekaa ilinizuia kurudi nyuma wala kwenda mbele bali kutetemeka tu. Sijawahi kupata woga kama ambao niliupata siku hii, moyo ulidunda kwa mapigo ya juu sana kiasi kwamba niliyasikia mapigo kama vile mdundo wa Muziki kwenye redio kubwa (Sabufa).

“Shiii‼” Baba Mkwe akanipa ishara katili ya kunitaka nikae kimya vinginevyo kile kisu kingeingia mwilini mwangu. Kisha akachuchumaa na kuniambia

“Leo utajuwa ni kwanini uliolewa Binti” Alisema halafu akayaongea maneno fulani nisiyoyaelewa, nakumbuka kabisa hayakuwa maneno ya lugha ya Kiswahili bali lugha nisiyoifahamu na wala si Kiingereza wala Kiarabu. Wale Watu wakasimama kisha wakaenda kupotelea kwenye kona za kile chumba kilichojaa harufu ya Udi.
stori ni nzuri sana
 
Ilipoishia “Shiii‼” Baba Mkwe akanipa ishara katili ya kunitaka nikae kimya vinginevyo kile kisu kingeingia mwilini mwangu. Kisha akachuchumaa na kuniambia

“Leo utajuwa ni kwanini uliolewa Binti” Alisema halafu akayaongea maneno fulani nisiyoyaelewa, nakumbuka kabisa hayakuwa maneno ya lugha ya Kiswahili bali lugha nisiyoifahamu na wala si Kiingereza wala Kiarabu. Wale Watu wakasimama kisha wakaenda kupotelea kwenye kona za kile chumba kilichojaa harufu ya Udi. Endelea

SEHEMU YA NNE

Nilikua kama naangalia filamu vile, hata wewe msomaji unaweza fikiria ilikua ni filamu na ninakusimulia hapa. Hapana ni Simulizi ya kweli, simulizi hii ikusaidie kufanya chaguo sahihi wakati wa kuolewa au Kuowa ili usije pitia kama Mimi, haya mambo siyo tu kwa Mwanamke hata Mwanaume anaweza tendewa hivi. Tuendelee sasa

Mate hayakumezeka wala pumzi hazikutulia, yule Mzee alikua amenikata jicho kali kisha kaniambia kwa maneno yenye vituo vingi kuashiria kuwa anamaanisha anachokisema, akaniambia

“Umeolewa ili uje kuishi na Misukule hapa, huu ndiyo utajiri wangu. Wewe siyo wa kwanza kuolewa na Salehe, walioenda kinyume walifia humu na kupotea kabisa wao pamoja na Familia zao” Yaani nilizidi kuishiwa nguvu, Mungu wangu jasho lilinitoka kama nimemwagiwa maji. Kisha Mzee akaendelea

“Hii ni nyumba yangu Mimi siyo ya Salehe, yule ni Mtoto wangu na ndiye anayenisaidia Mimi. Utakua unafanya mapenzi na Msukule mmoja mmoja Kila baada ya Siku tatu. Usijaribu kutoroka ndani ya nyumba hii wala kutoa siri popote, narudia kwa Msistizo ili uelewe ninachomaanisha. Utawaponza Wazazi wako kwa Ujinga wako mwenyewe” Chozi lilizidi kunitoka kisha yule Mzee akasimama akaninyooshea Kidole

“Utafanya niyatakayo ili kuilinda familia yako, hutaruhusiwa kutumia simu na hutatoka nje isipokua kwa maagizo maalum kutoka Kwangu” kisha yule Mzee aliondoka zake na kunicha ndani ya kile chumba, wala hakunifungia kuonesha kuwa anajiamini na anachokisema. Kiukweli Nililia sana kwa kwikwi, nililia Mno sababu niliona wazi kuwa ili wazazi Wangu wawe salama napaswa kutumikia Misukule ya yule Mzee na kama nataka kuwa huru basi nitawapoteza Wazazi wangu ambao hawakuwa na Hatia yoyote ile.

Katika Maisha yangu niliutunza usichana wangu kwa ajili ya Mume wangu lakini nililazinika kuutoa kwa Misukule, nilijilaumu kwa kumwamini Salehe, nilimlaani sana. Nikiwa ninalia akaingia tena yule Mzee akiwa amehamaki akaniuliza

“Simu yako ipo wapi?” alishikilia kisu mkononi, sikupepesa maneno nilimpa simu mara moja kisha akaondoka nayo. Wala hakufunga mlango aliuwacha wazi ikiwa ni ishara ya kuniruhusu kuwa huru ndani ya nyumba lakini siyo kuondoka, ndiyo kwa mara ya kwanza katika Maisha yangu niliushuhudia Uchawi wa waziwazi.

Basi, nilirudi chumbani nikiwa ninalia, nilikua mwenyewe kwenye Maisha yangu. Sikuwa na Mtu wa kumueeleza ninayopita, sikuwa na msaada na pengine kaburi langu lingekuwa ndani ya ile nyumba. Kitu cha kwanza kufanya kilikua ni kufuta chozi langu, kwanini niliruhusu lidondoke chozi langu lenye thamani kubwa. Hata ningelia vipi isingelisaidia Mimi kupona

Nilijiegemeza kwenye Mto nikatafakari mengi, nikapata jibu la uhakika kabisa kuwa siku ile nilifanya mapenzi na Msukule na ndiye aliyenitoa Usichana wangu kwa mara ya kwanza nikifikiria ni Salehe. Kitu fulani cha uchungu kilijaa kifuani pangu, hakika nilitendewa unyama sana na Salehe na Baba yake. Nilijua Baba na Mama wangekuwa na wasiwasi na Mimi kama nitakaa kwa siku nyingi pasi na kuwasiliana nao lakini ningefanya nini sasa na ilinibidi nikae nao mbali ili kuokoa Maisha yao.

“Eeh Mungu, umeniptisha kwenye Mtihani gani sasa. Hukuona mitihani mingine rahisi kwangu isipokua huu?” Nilituma lawama ma maswali kwa Mungu wangu, kumbe ukiona Mtu anamkufuru Mungu si kwa kutaka bali kwa kukosa majibu sahihi ya kuondoka kwenye matatizo.

***

Masaa yalienda, sikupata hata lepe la kuusingizia Usingizi yaani nilikua na kichwa kizito sana japo Usiku ulikua umeenda. Hakuna sauti ya kutisha niliacha kuisikia Usiku huu, yaani Mzee Mwinyimkuu alinionesha Uchawi dhahiri kabisa. Sauti za Watoto Wachanga nilizisikia bila kificho, nyimbo za ajabu ajabu ziliimbwa na kuchezwa nikajiona kama nimeshafika kuzimu. Nikazikumbuka Riwaya kadhaa nilizokua nazisoma mtandaoni na stori za hapa na pale juu ya Uchawi, nilikua siziamini lakini hatimaye nilijikuta ndani ya moja ya Riwaya ya kutisha sana.

Mimi Saida nilikosa majibu ya maswali yote hata yale madogo niliyojiuliza. Bundi walisikika Usiku kucha, hadi kuna pambazuka nilikua macho hata taa sikuizima kwa kuhofia kuingiliwa tena na yule Msukule. Kukesha macho usiku mzima haikua rahisi, macho yalivimba hasa ukizingatia nililia sana

Niliogopa kutoka chumbani, sikuwa na amani kama siku ya kwanza. Nilikaa kitandani nikipiga Mihayo, mara Mlango uligongwa, nilishtuka nkasema moyoni sasa naenda kupelekwa kwa Misukule, hofu ikaamka upya ndani yangu lakini nikamsikia Mzee Mwinyimkuu akisema

“Amka uandae chai haraka” alisema kwa jazba fulani baada ya kugonga kwa kitambo kisha nikayasikia makubhasi yake yakifanya safari kutoka mlangoni kwangu. Moyo ulinidunda sana kiukweli, sikuwa na raha wala amani yoyote ile. Ningefanya nini zaidi ya kuamka na kwenda kumwandalia chai yule Mzee, Binafsi sikuhisi njaa kabisa licha ya kutokula jana kutwa nzima.

Niliufungua Mlango taratibu sana, nikasikia kama Mtu anafanya Usafi hivi, nilipoangalia vizuri niliona tu ufagio pekee ukifagia bila kumwona aliyeushikilia ule ufagio, nusura nizame tena ndani kwa woga lakini nikapata kiu ya kuona zaidi. Huuu‼! Uchawi unatisha sana na nimeushuhudia laivu bila chenga, niliporudisha macho tena sikuona chochote isipokua nyumba ilikua safi sana

Basi nikaanza safari fupi ya kupita koridoni na kuelekea jikoni kuandaa chai ya Mzee Mwinyimkuu. Ile naingia tu nikakutana naye ndunda ndunda.

“Muda wote ulikua unafanya nini wewe?” aliniuliza kwa hasira sana kama vile tulikua tumegombana. Hofu ilinianza upya hata sikuweza kutoa sauti yoyote ile, nikainamia chini, Jamani nilikuja kushtukizwa na kibao cha shavu la kushoto hadi nikahisi giza. Alinipiga kibao kizito hadi nikapepesuka pembeni, mateso makali yalianza kwangu

Sikuweza kutoa sauti yoyote ile isipokua chozi na maumivu yaliyojaa ndani ya Moyo wangu.

“Usiniletee upumbavu, hukuja kulala hapa wala kutembea. Kumbuka maneno yangu, Utafia humu ukileta kiburi, pesa hii hapa Nunua chapati urudi haraka” alisema Mzee Mwinyimkuu, akanipa Elfu tano mpya kabisa. Kisha yeye aliondoka zake akaelekea sebleni, alionekana anajiamini na maneno yake ndiyo maana aliniruhusu nitoke nikamnunulie Chapati, wakati nataka kutoka akapaza sauti yake akaniambia ninunue chapati za hela yote

Sikuwa na maswali mengi kuwa chapati zinaenda kuliwa na Nani sababu hata ule Mchicha nilikua na uhakika kuwa unaliwa na Misukule niliyoiona Usiku. Nilihisi kukonda kwa siku moja tu ya hekaheka, nilitoka nikafungua geti kisha nikatoka ndani, taratibu nikawa naeleka kwa yule Mama anayeuza Chapati nyumba kama ya Nne hivi kutoka nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu.

Macho yangu yaliitazama sana ile nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, nje Watu walikua wakiendelea na shughuli zao, niliamini hakuna anayejuwa kinachoendelea. Nilitamani nimsimulie Mtu pengine nimwombe msaada lakini nikakumbuka onyo nililopewa na Mzee Mwinyimkuu, Ah! Hamu iliniisha……….
 
story ni nzuri saaaana
 
Ilipoishia “Sikuwa na maswali mengi kuwa chapati zinaenda kuliwa na Nani sababu hata ule Mchicha nilikua na uhakika kuwa unaliwa na Misukule niliyoiona Usiku. Nilihisi kukonda kwa siku moja tu ya hekaheka, nilitoka nikafungua geti kisha nikatoka ndani, taratibu nikawa naeleka kwa yule Mama anayeuza Chapati nyumba kama ya Nne hivi kutoka nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu.

Macho yangu yaliitazama sana ile nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, nje Watu walikua wakiendelea na shughuli zao, niliamini hakuna anayejuwa kinachoendelea. Nilitamani nimsimulie Mtu pengine nimwombe msaada lakini nikakumbuka onyo nililopewa na Mzee Mwinyimkuu, Ah! Hamu iliniisha. Endelea

SEHEMU YA TANO

“Karibu Binti” alisema yule Mama, sikuachia tabasamu kama lile la siku ya kwanza nililompa huyu Mama, moyo wangu ulikataa kuigiza furaha wakati napitia nyakati ngumu sana na za mateso makali sana.

“Ahsante, nataka chapati za hii hela” nilisema kwa sauti isiyo changamka, yule Mama akapokea pesa kisha akawa ananichukulia chapati alizozitengeneza tayari, lakini akaacha akaniuliza

“Upo sawa?” swali hili liliniumiza sana, nikawaza nimjibu nini ila nilishaonywa kuwa nikisema chochote Wazazi wangu watauawa. Kwa simulizi nilizosikia kuhusu Uchawi inawezekana kabisa wakauawa wakiwa Mbali hivyo niliogopa sana. Wakati nawaza yule Mama akanishtua kwa kunitikisa maana nilishazama kimawazo

“Upo hapa kweli Binti?” nikashtuka na kujibaraguza kama Mtu aliye sawa huku nikijuwa fika kuwa nausaliti moyo wangu.

“Ndiyo, nipo Mama. Samahani naomba chapati niwahi nimeacha chai jiko la gesi” nilisema, nilishakuwa na uhakika kuwa pengine Mzee Mwinyimkuu aliweka mtego wake kwangu ndiyo maana akaniacha huru nje

“Mh!” akaguna tu kisha hakusema kingine, halafu akanifungia chapati za Elfu tano akaniwekea kwenye mfuko.

“Karibu tena, Naitwa Mama Ashura. Ukikwama usisite nitakupa msaada” alisema yule Mama akanipa mfuko, Uwii‼ alinigusa ndani ya Moyo wangu kwa jinsi nilivyokua natamani kupata msaada Mimi kwa yanayonisibu lakini sikujua napataje msaada Mimi, naanzaje? Nikajichekesha tu kama mwehu kisha nikageuka na kuondoka pale.

Kitendo cha Kumpa mgongo Mama muuza chapati aliyejitambulisha kama Mama Ashura, chozi lilinilenga. Safari ya kurudi ndani ilijaa maumivu makali sababu narudi tena kuivaa hofu na mateso ndani ya Nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. Nilitamani kukimbia lakini niliwaza Wazazi wangu, sikuwa na tumaini kiukweli.

Nilifungua geti na kuingia ndani kisha nikafunga geti, nilivyofunga geti chozi lilinibubujika sana nikalifuta kwa kutumia mtandio wangu. Ilikua kama Mishale ya saa Tatu na dakika zake hivi, nilichemsha chai na kumpa Mzee Mwinyimkuu sebleni

“Kula chapati moja, zilizobakia peleka kwenye kile chumba. Weka na maji ya kunywa kisha ondoka, ukimaliza njoo” alisema akiwa anakula chapati zake, nilifuata maagizo sababu hapakua na jambo jipya. Nilishajua zinaliwa na Misukule ambao Mzee MwinyiMkuu ameniambia nifanye nao mapenzi.

Nilipomaliza sikula, nikarudi sebleni kumsikiliza.

Kaa hapo” akaniamuru niketi kwenye kochi la kizamani, akagida funda kadhaa za chai kisha akasema tena

“Hii simu imekumbana na Nini?”

“Ilianguka Baba” nilijibu kwa heshima na woga

“Utaongea na Wazazi wako kwa kutumia simu yangu, Baba yako anaumwa na kama utafanya zihaka nitamwondoa. Wasalimie waambie simu imeharibika ili wasisumbue, ole wako uoneshe wasiwasi wowote ule” Nilishtuka, likanitoka neno bila kutarajia sababu nilikua nampenda sana Baba yangu Jamani, sijui alipata wapi namba ya Mama yangu

“Baba anaumwa?” Weee, nilikiona cha moto, alinimwagia chai ya moto usoni. Nilitapa tapa kwa maumivu

“Kimya‼ mshenzi wewe, unauliza ulichokisikia?” alisema Mzee MwinyiMkuu, sijui nikwambie nini Msomaji. Huyu Mzee alikua katili haswaa kuanzia sura yake hadi matendo yake, Watu kama hawa nilikua nawaona kwenye filamu tu na wala sikutegemea kama wangekuwepo kweli hapa Duniani.

Niliacha Kulia lakini maumivu ya moto yalikua makali sana japo taratibu yalianza kupoa, kisha nikasikia simu ikiwa imeshapigwa inaita, aliweka Loud Spika ili naye ayasikie mazungumzo, hapo ndipo nilipoisikia sauti ya Mama yangu, chozi lilikua linanibubujika tu. Mama aliita

“Hello”

“Abee Mama” nilimwitika Mama yangu kwa sauti niliyoshindwa kujizuia kabisa, nililia kwa mengi sana. Kwanza niliwakumbuka sana wazazi wangu japo ni muda mchache tu umepita na pili ninayoyapitia sikuwa na Mtu wa kumwambia wakati wazazi wangu wapo

“Hee! Saida Mwanangu, Unalia nini Mama na hii namba ya Nani?” Mama aliitambua sauti yangu na pia aligundua ninalia, yule Mzee akanikazia macho yake

Jamani sauti ya Mama yangu ilizidi kunichoma Moyoni, nilishindwa hata kuongea, laiti kama Mama yangu angelijua nipo chini ya Ulinzi sijui ingekuwaje.

“Saida unalia nini Mwanangu, Mumeo amekufanya nini?” Si unajua ndoa ina siku tatu tu hivyo ni lazima Mama ahisi pengine nina tatizo na Salehe, nikafuta chozi nikasema neno moja tu kwa Mama kisha niliangua Kilio

“Nimewakumbuka sana Mama na Baba…” Nililia kama Mtoto mdogo, Mama naye akalia, Mimi ndiye Mtoto wao pekee na pendwa hivyo hawakuwahi kukaa mbali na Mimi nami sikuwahi kukaa mbali nao hata mara moja, walinilea kama mboni ya Jicho.

“Saida hata sisi wazazi wako tunakuwaza sana, nyumba imepooza mno lakini hakuna jinsi ni lazima Maisha yendelee. Usilie najuwa utazoea hayo unayoyapitia, najua una upweke sana” Mama alisema, laiti angejua kuwa naishi nusu mfu na nusu Mtu angelia sana.

“Sawa Mama lakini siwezi kuacha kuwawaza kila siku ziendazo kwa Mungu, naomba sana muwe na afya njema siku zote” angalau kidogo sauti ya kilio ilianza kuniacha, kimafua kwa mbali tu ndiyo kilikuwepo.

“Amen Mwanangu, hata hivyo Baba yako anaumwa” alichokisema Mama ndicho alichokua ameniambia Mzee Mwinyimkuu, halafu safari hii akajifanya hana habari na mimi bali anaendelea kunywa chai, nilimtazama kwa jicho baya la hasira lakini sikuwa na cha kumfanya

“Eeh imekuwaje tena Mama?”

“Asubuhi ameanguka chooni, yupo amelala na anahisi mkono mmoja hauna nguvu” alisema Mama, Roho iliniuma sana. Chozi tu ndilo lililokuwa linanibubujika kwa wingi

“Mungu ni Mwema Mama, atapona Insha Allah” nilisema kwa hisia huku nikijuwa ni fitina za kichawi za Mzee Mwinyimkuu.

“Amen, hii namba ya Nani? Nimejaribu kukupigia hupatikani.”

“Hii namba ni ya Mkwe Wangu. Nilidondosha simu ikapasuka, hata hivyo Mume wangu amesafiri kwa dharura jana hivyo akirudi nitapata simu nyingine. Ukinihitaji piga humu Mama”

“Sawa Mwanangu…ndoa unaionaje Saida?” Lilipofika hili swali moyo wangu ulisinyaa ghafla, niliumia sana kuulizwa kuhusu ndoa wakati nayoyapitia ni magumu kuliko magumu ya ndoa. Mzee Mwinyimkuu akanikata jicho huku akinionya kwa kidole

“Nina furaha sana Mama, familia inanionesha upendo wa hali ya juu sana. Samhani Mama naelekea jikoni mara moja” nilisema na kumuaga Mama, nilijijua kuwa ningeangua kilio cha Mtu mzima sababu nilisema uwongo kitu ambacho sikipendi hasa kumuongopea Mama yangu.

Nilikata simu kisha niliiweka mezani.

“Kama utaendelea hivyo basi hatutagombana Mimi na wewe lakini kama utakuwa mkaidi basi utakiona cha Mtema Kuni” alisema Mzee Mwinyimkuu, nilinyanyuka taratibu nikatembea hadi jikoni

Chai ilikuwa hapo inaniangalia lakini njaa haikuwepo kabisa, Taswira ya Maisha yangu ilibadilika mno. Nikajuta kwanini niliolewa Mimi Huuuh‼

Nilikaa kwenye kigoda na kuanza kulia kwa sauti ya chini, huh‼ nilishindwa kujizuia kusema ukweli, maumivu yalikua makubwa kiasi kwamba chozi lilinibubujika bila hata kubisha hodi.

**

Baada ya kupita siku mbili, zikatimia siku tatu ambazo Mzee Mwinyimkuu aliniambia kuwa napaswa kufanya mapenzi na Misukule wake, hiyo siku nilisoma kila aya kwenye Quraan tukufu, nilipiga kila goti ili Mungu aniondoe ndani ya ile nyumba lakini haikua hivyo. Aliniambia Usiku ndiyo nitafanya kitu hicho, akanipa dawa fulani alizozijua yeye akasema napaswa kunywa kabla ya kuingiliwa na Msukule ili nisije pata Ujauzito

Akanipa pia Kaniki nyeusi nijifunge bila kuvaa chochote ndani, kisha akaniambia

“Jiandae saa moja Usiku utaingia kwenye kile chumba. Una uwezo wa kuhudumia Wanaume wangapi kwa mara moja?” Aliniuliza, haki ya Mungu nilijawa na hasira isiyo kifani. Kwanza sikuwahi kufanya mapenzi kabla ya kuingiliwa na yule Msukule Usiku ule nikifikiria ni Salehe hivyo sijui chochote kile kuhusu Mapenzi

“Nakuuliza wewe!” Akanishtua, nikashtuka haswa maana nilijua kama nitaendelea kuwa kimya pengine ningekutana na kofi lake, nikajikuta naropoka tu

“Watatu” Nikaliona tabasamu kwenye uso wa Mzee Mwinyimkuu.

“Haya pumzika hakikisha umekula vizuri, tuna masaa mawili tu kufika Usiku” alisema kisha aliniacha chumbani kwangu nikiendelea kukonda kwa mawazo. Kaniki ilikua mkononi mwangu nikiwaza eti nakuwa mtumwa wa mapenzi kwa Misukule, kipindi hicho nilishaacha kumuwaza Salehe sababu Baba yake aliniambia kuwa walikua timu moja kuniingiza matatizoni.

Yale masaa mawili yalikwisha, roho iliniuma na hofu juu, nililia jamani. Halafu sasa huyu Mzee alianzisha tabia moja, aliacha kugonga mlango wa chumba changu badala yake aliigia tu kama upo wazi. Alinikuta nimekaa

“Jitayarishe Binti” alikuja kuniambia hivyo tu, nilimeza funda zito la mate. Laiti kama ningelikua huru basi ningeli mrushia tusi la nguoni lakini nilikua kifungoni japo nilikua na uhuru wa kuchagua kati ya kupoteza Wazazi wangu au kujipotza mimi mwenyewe ndani ya ile nyumba ya Kichawi

Basi, nilifanya kama alivyosema. Niliivaa ile kaniki kama khanga vile nikiwa nimeyafunga matiti yangu. Sijui aliona nachelewa basi akaja mkuku-mkuku na kunipeleka kwenye kile chumba ambacho siku ile niliwaona Misukule.

“Saida, kama utakua Binti mzuri nakuahidi utaishi kwa raha sana na wazazi wako watakuwa hai. Unatakiwa utambue jambo moja kuwa unapofanya mapenzi na hawa Misukule wanapata nguvu zaidi ya kunipa utajiri na nguvu za Kichawi. Huu ni ufalme niliourithi kutoka kwa Baba yangu, nami nitamrithisha Salehe hivyo ni lazima hizi nguvu zitunzwe na kulindwa zaidi ya chochote kile. Usiogope ila nitakuwa mkali kama utanifanya nisuburi zaidi” alisema Mzee Mwinyimkuu akiwa anatoa sauti ya kawaida iliyojaa Ulaghai mtupu

Akawasha zile udi zake akaweka kila pande ya chumba kisha akaniambia nikae katikati ya Chumba kama siku ile ya kwanza. Sijui nikwambiaje uelewe kuwa Mzee Mwinyimkuu alikuwa na sura mbaya ya kutisha kiasi kwamba akikutazama kwa macho yake mekundu ni lazima uogope na ujasiri ukuishe, na kingine yeye kukupa pigo ni dakika moja tu wala hawazi.

Chozi lilinitoka siwezi kuongopa, haikua kawaida. Mara ghafla wakatokea misukule Watatu wakiwa uchi wa Myama, ilikua kama filamu ya maigizo hivi lakini ndiyo ukweli wenyewe unaouma zaidi moyoni, nahisi walikua wanajuwa walichoitiwa. Niliona Midudu yao ikiwa imesimama sana, halafu ni mikubwa Jamani Ooooh‼

Nilianza kuogopa huku nikimwambia yule Mzee

“Samahani Baba naweza kufanya kila kitu lakini hii siwezi, nihurunie Mtoto wa mwenzako Mimi. Niache nirudi kwetu” nilisema nikiwa ninalia, Msukule mmoja akanivaa kwa nguvu na kuniondoa ile Khaniki, nikabaki Uchi wa Mnyama kama alivyotaka Mzee Mwinyimkuu. Niliingiliwa kwa nguvu na wale Misukule huku nikipiga kelele za kuomba Msaada, kwa jinsi nilivyogumia nina uhakika kuwa majirani walisikia maana nilikua na maumivu makali sana

Walinichana huku chini, damu zilinitoka nikiwa nimelala sakafuni. Nililia kwa kwikwi sitakuja kusahau namna nilivyojisikia Usiku ule. Yule Mzee akanifuata na kunitaka nikae kimya vinginevyo angenichoma kile kisu, nilijinyamazisha haraka sana huku nikimuomba yule Mzee

“Kwanini unanitendea unyama kiasi hivi, nimekukosea nini Mimi? Naomba nirudi kwetu Mimi siwezi jamani Aaaah‼” yaani kama angelikuwa ni Mtu mwenye roho nzuri basi angelinihurumia mara moja na kuniacha niondoke lakini akanipa Mtihani mwingine mgumu sana ambao uliniacha na kilema cha Maisha hadi hivi leo

Kitu cha kwanza alichofanya ni kuzungumza maneno yake wale Misukule wakaondoka kama walivyokuja kupitia pembe za ukuta, lakini pili Mzee Mwinyimkuu aliniambia

“Kama utaendelea kunisumbua basi hapa patakuwa Jahannam yako na hutokaa utoke Milele Daima. Kingine napaswa kukuvuna viungo kila unapofanya mapenzi na Misukule, siku nikimaliza nitakuacha urudi kwenu” Nilijiuliza anivune viungo kivipi, kauli yake ilinianbia kwa haraka kuwa Kifo kilikua kimenigongea hodi, kipo karibu zaidi na Mimi.

“Unasema nini?” niliuliza nikiwa ninalia kwa sauti ya Chini.

Haraka yule Mzee akanipulizia unga fulani aliokuwa ameushikilia mkono wa kushoto, ulikua mweupe ulionifikia hadi usoni kwangu. Nikajikuta nikiwa nimelegea vya kutosha kiasi kwamba sijitambui, hatimaye giza tu lilinitanda na sikujua kilichokuwa kimeendelea nyuma yangu.
 
Back
Top Bottom