Mimi ndoa ilinipotezea muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu

Mimi ndoa ilinipotezea muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu

Mmmh ! Sijamalizia simulizi pole sana..machache ya kujifunza..sijui ni seme wakarimu au wema ni wakatili sana kama simulizi inavomuelezea Sarehe..unapofika ugenini mtazamo wa kwanza wa mazingira yale kwasiku ya kwanza unakupa jibu kuwa umeingia sehemu salama au laa kulingana na simulizi..wazazi tunapotaka kuozesha tunapaswa kuijua familia ya upande wa pili kihistoria sio kuwahi kuchukua mahari tu..unapoingia kwenye himaya ya mtukatili fuata maelekezo yake kama unaona huwezi kupambana naye ila ukipata upenyo wa kusepa usisikie vitisho vyake sepa...tuheshimu na kusikiliza viungo vya mwili kwani vina kazi kubwa katika mwili...mwisho Saida kwasasa upo wapi? mengine taendelea kadri ninavofatilia mkasa.
Sikuizi kumekuwa na uvivu wa kuchunguza familia anayo enda kuolewa au kuoa mwanao pia vijana kuhalakisha mambo aswa ndoa
 
Sema shida hawezi kujua yule mzee amemwekea mtego gani,.
Kama aliweza kujua baba yake anaumwa bila kuambiwa
Ku deal na majini no rahisi kama wewe sio muislam!Hadi uasi ndio inakua rahisi!jina tu la yeshua linatosha!

Tatizo alikua muislam huwezi ku deal nayo hadi usome elimu ya kichawi iitwayo falak!

Na elim hii no ya wachache sana na ni shirki!
 
Ku deal na majini no rahisi kama wewe sio muislam!Hadi uasi ndio inakua rahisi!jina tu la yeshua linatosha!

Tatizo alikua muislam huwezi ku deal nayo hadi usome elimu ya kichawi iitwayo falak!

Na elim hii no ya wachache sana na ni shirki!
Ipoje iyo kato embu fafanua kidogo hapo
 
Ipoje iyo kato embu fafanua kidogo hapo
Maombi Kwa jina la yesu hasa usiku wa maneno saa Saba,nane,tisa!!unasema tote na kukemea hayatakusumbua coz lango la kuzimu na mbingu linakua wazi muda huo!!ndio maana wagonjwa wengi hufa usiku was manane coz no rahisi roho kutoka na kwenda kati ya sehem hizo mbili!

Jaribu hiyo hata kama wewe ni muislam jaribu hiyo!inasaidia!
 
Maombi Kwa jina la yesu hasa usiku wa maneno saa Saba,nane,tisa!!unasema tote na kukemea hayatakusumbua coz lango la kuzimu na mbingu linakua wazi muda huo!!ndio maana wagonjwa wengi hufa usiku was manane coz no rahisi roho kutoka na kwenda kati ya sehem hizo mbili!

Jaribu hiyo hata kama wewe ni muislam jaribu hiyo!inasaidia!
Hayo maombi ya vita na ukianzisha maombi ya vita uwe umejipanga
 
Sijui kwako ndoa ina maana gani lakini kwangu Mimi ndoa ilinipotezea Muda wangu, iliniacha na Maumivu na kilema cha Maisha yangu.

Sikuwahi kuwaza chochote kuhusu ndoa wala kuitamani, lakini siku moja nilikua natoka sokoni Mabibo naelekea nyumbani Magomeni Usalama, niliposhuka kwenye daladala kwa bahati mbaya niliteleza na kuanguka wakati navuka barabara. Mfuko wenye vitu nilivyonunua sokoni uliangukia pembeni.

Nilihisi aibu sana siku ile na kibaya zaidi mvua ilikua imenyesha majira ya asubuhi, lilijaa tope lililoniharibia Baibui langu. Eneo nililoangukia palikua na kijiwe cha Bodaboda. Kama uwajuavyo walianza kushangilia anguko langu kitu kilichozidi kunipa hasira lakini sikuwa na la kufanya zaidi ya kujiokotanisha pale.

“Pole sana Dada” niliisikia sauti hii nikiwa nasimama, aliyenipa pole alinipatia na mfuko wangu akiwa ameokotanisha vitu vyangu. Alikua kijana mzuri mtanashati sana, nilijikuta nikiwa na kigugumizi kumjibu

“Unaelekea wapi?”

“Nyuma ya sheli, usijali” nilisema nikiwa najipangusa tope kutoka kwenye Baibui langu jeusi, akanipa mkono wake

“Naitwa Salehe Mwinyimkuu” Alijitambulisha kwangu, nilimtazama kwa sekunde kadhaa kisha nilimjibu

“Naitwa Saida”

“Nimefurahi kukufahamu, wacha nikusogeze” alisema, kwa msaada alionipa isingelikuwa hisani kukataa alichokiomba. Taratibu tuliikanyaga ardhi kuelekea karibu na nyumbani kwetu. Kwa muda mchache nilihisi kumjua kidogo, niligundua ni mpole, mwemye hekima na busara tele licha ya kuniambia ana Miaka 27 tu.

“Mimi nina Miaka 23” nilijitanbulisha kwake huku nikianza kunogewa na mazungumzo yake. Tuliongea mengi hadi kubadilishana namba za simu kitu ambacho sikuwahi kukifanya kwa Mtu nisiyemjua.

Tulizidi kuwasiliana kwa zaidi ya mwezi mzima huku tukiwa marafiki wa kawaida tu lakini baadaye Salehe alinitongoza.

Nisiwe mwongo wala mnafiki hata kabla ya kunitongoza nilianza kumpenda hivyo kunitongoza alikua anatimiza wajibu wake kama Mwanaume kwani nisingeliweza kumwambia Nampenda isitoshe Mimi nilikua Bikra kwa wakati ule.

Tulianza mahusiano ya Kimapenzi lakini nilimwambia Salehe kuwa Mimi nimelelewa kwenye familia ya Dini sana, Baba yangu ni msaidizi wa Shekh Mkuu wa Msikiti wa Magomeni hivyo kama ananipenda kweli basi awaone wazazi wangu kwanza. Sijui tuseme alikua na kiu sana au alikua anahitaji Mke sana maana alilifanya hilo siku tatu tu baada ya kumwambia

Baba yangu alifurahi sana, Mama pia alifurahi zaidi akaniambia

“Mwanangu ndoa ni Nusu ya Dini, sisi Wazazi wako tunakutakia kila lililo jema, Mungu akuongoze” Daima Mama yangu alikua Mtu wa karibu sana kwangu, alisimama na Mimi kwenye kila jambo hata ambalo Baba yangu alipingana na Mimi.

Salehe hakutaka kuchelewesha alilipa Mahali siku iliyofuata.

“Wewe Kijana ni Mtu wa wapi?” Baba alimuuliza Salehe wakiwa katika mazungumzo ya kawaida, kama Mzazi ni lazima ahakikishe usalama wa Binti yake

“Kwetu Rukwa lakini nipo Hapa Dar Likizo” alisema Salehe

“Ooh! Unajishughulisha na nini?”

“Nimeajiliwa, Mwalimu wa Shule ya Msingi Rukwa Mjini”

“Utamtunza Binti yangu?”

Kwanza Salehe alicheka kidogo kisha akamwambia Baba

“Nisipomtunza Mke wangu nitamtunza Nani, wanasema Mbuzi unayemlisha ndiye utakaye mkamua maziwa” Basi Baba na Salehe wakaishia kuangua vicheko, ilileta raha sana.

Ndugu wa Salehe walifika tena waliazimia kuwa ndoa ipite kabla likizo ya Salehe haijaisha ili tuondoke wote kuelekea Rukwa, sikuwahi kufikiria kuwa siku moja nitaolewa na kwenda mbali kama Rukwa. Kidogo nilipata huzuni, nilimzoea Mama yangu

“Usijali, hata Mimi niliwaacha Wazazi wangu Morogoro nikaja kuishi na Baba yako Saida. Umri ukifika hakuna la kukuzuia kuanzisha Familia yako” Mama yangu hakuacha kunitia Moyo. Baba aliachia tabasamu maana tulikuwa wote sebleni

“Ngoja niwaache muongee maongezi yenu ya kike” alisema Baba akaelekea zake Msikitini, zilipita siku kadhaa hadi siku ya ndoa ilipowadia. Ndoa ilipita salama, Siku ya pili tulianza safari ya kuelekea Rukwa Mimi na Mume wangu Salehe.

Bado nilikua Bikra wala hakunigusa usiku wa kwanza wa ndoa yetu hotelini kabla ya Kuanza safari, kwakua nami nikikua mgeni wala sikudai chochote kile. Tulifika Rukwa Usiku sana tena nikiwa ninasinzia, tulichukua Taxi hadi nyumbani kwa Salehe

“Karibu nyumbani Mke wangu, jisikie uko nyumbani kabisa na hapa ndipo tutakapoishi” alisema tukiwa tunashuka kwenye taxi, tulisimama mbele ya nyumba moja iliyo giza sana, sikushangaa sababu mwenye nyumba hakuwepo kwa muda mrefu. Nilijiegemeza kwenye bega la Salehe nikamwambia

“Mume wangu, ulipo nipo na nitaendelea kuwepo siku zote” lile Taxi liliondoka, kazi ya kuhamishia mabegi ndani ilianza. Salehe alikua ametangulia nami nilibakia nyuma nikikokota begi. Sijui ni mawazo yangu au nilisikia kitu halisi kabisa, nilisikia sauti za Watoto wakiomba Msaada

“Subhannah‼” nilishtuka, sikuisikia tena ile sauti maana mwanzo ilitokea ndani ya ile nyumba ambayo tulikua tukielekea. Mapigo ya moyo yalinienda mbio, niliposikiliza vizuri wala sikuzisikia tena nikajua ni fikra zangu tu. Basi niliendeelea kuvuta begi hadi ndani, taa zikawashwa

Palikua kimya sana, uzuri sikua na njaa wala hamu ya kula zaidi ya Kulala kutokana na Uchovu wa safari. Nilisimama kusuburia Salehe anioneshe chumba chetu, akaufunga mlango kisha akaniongoza hadi chumbani, nilipofika nilijitupa Kitandani na kujilaza kama pono bila kujali kuwa kitandani palikua vumbi tupu.

Nililala Usingizi wa nusu kifo hadi mapambazuko, sauti ya jogoo kuwika niliisikia ikiniamsha na kuniambia ni muda muafaka wa kuanza majukumu ya nyumbani. Macho yalijawa na Ukungu usio kifani, nilijinyoosha kama Kinda la ndege halafu nikajikuta nikipigwa na Butwaa zito sana ambalo kiukweli nilishangazwa mno na nilichokiona

“Nipo wapi hapa?” Nilijiuliza swali hili, niliipapasa akili yangu inikumbushe jambo lakini haikua tayari kufanya hivyo, Salehe hakuwepo Kitandani. Moyo ulinienda hali Jojo, nilinyanyuka taratibu kutoka kitandani.

Nitakueleza kwanini nilipigwa na Butwaa la ajabu, kwanza harufu ya Udi wenye harufu mbaya ilizagaa kote ndani, pili nilisikia sauti ya Mtu akitwanga na kwa hakika alikua akitwangia ndani halafu sauti ya Mtoto Mchanga anayelia nilizidi kuisikia. Taratibu nilitaka kujuwa nipo wapi haswa maana tayari nilianza kupata hofu fulani

Nilipiga hatua za taratibu hadi mlango wa kutokea chumbani, ile sauti ilitoweka na palikua kimya sana. Moyo wangu haukutulia kabisa licha ya ukimya wa ghafla niliousikia, jua lilikua tayari limeshatoka

Nyumba ilikua safi sana. Ilikua na korido ndefu yenye vyumba kadhaa japo kwa wakati huo sikuhesabu kutokana na hali niliyokua nikiihisi. Basi Mimi Saida nilijiuliza

“Ah ni mawazo gani haya Jamani, Ewee Allah niepushie Mbali” nilisema kisha nilirudi Chumbani kutafuta simu yangu nimpigie Salehe aniambie alipo si unajua maisha ya Ugeni yanavyoanza. Nilikumbuka mara ya mwisho simu niliiweka kwenye mkoba wangu

Sikuwa na shaka sana kuhusu simu yangu, niliikuta lakini kwa bahati mbaya ilikua imeisha chaji. Niliketi kitandani nikiwaza mambo kadhaa lakini niliona ni bora niweke simu chaji niwasiliane na Salehe

Nilipomaliza kuweka chaji na kuhakikisha simu yangu inaingia chaji nilipata nafasi ya kukiangalia kwa uzuri chumba, kilipangwa vizuri sana hadi nilijikuta nikitabasamu, nilijuwa ni Mume wangu Salehe alikua ameamka mapema na kuweka mazingira sawa. Nilijiona ni mwenye Bahati sana kuitwa Mke wa Salehe, nilikua na nguo zangu zilezile nilizokuja nazo hivyo wazo la kubadilisha nguo lilinijia lakini kabla ya kufanya hivyo nilisikia Mlango wa nje ukigongwa.

Sikujua naanzia wapi kuitikia wito huo, nilisogea hadi mlango wa chumba na kusikiliza vizuri. Mgongaji wa mlango alikua ni Mwanamke na sauti yake ilikua karibu sana hivyo kwa haraka niliamini anagonga mlango wa Nyumba ya Salehe. Hakuna aliyeitikia ile hodi hadi pale nilipoamuwa kumkaribisha nikiwa ndani tena kwa sauti ambayo aliisikia vizuri, nilijiangalia kama nilikua nipo sawa kutoka ndani kisha nilianza safari mara moja kutembea kwenye korido kuuelekea Mlangoni.

Niliufungua mlango wa kwanza kwa kutekenya kitasa tu kisha nikauelekea mlango wa Uwani ambao ndio mgongaji alikua hapo, nilipoufungua nilikutana na Mama Mmoja aliyebeba tenga la mboga mboga kichwani, alikua ameshakata tamaa alikua akiondoka nikamwita

“Mamaaa‼” alipogeuka alirudi hadi Mlangoni

Shikamoo Mama” nilimsalimia kwa adabu, ndivyo nilivyofundishwa kwetu kwa wazazi wangu, yule Mama alitabasamu kisha akaniuliza

“Hauchukui Mboga leo?” Nilitabasamu maana aliuliza kana kwamba alishawahi kuniuzia mboga ila nilielewa Lugha ya Kibiashara huwa hivyo mara zote

“Mimi ni mgeni hapa Mama, labda kesho nikiwa nimeyafahamu vizuri mazingira naweza kuchukua. Usiache kupitisha” nilisema kisha yule Mama aliondoka huku akiitikia

“Napita kila siku Mtaa huu, Wahiiii mboga mboga” alienda mbele zaidi kisha alitokomea machoni pangu. Kuzungumza na yule Mama ni kama kulinisahaulisha kuhusu Salehe lakini alipoondoka nilijiuliza

“Salehe ameenda wapi mbona hajaniaga?” Niliufunga mlango kisha nilirudi ndani, Nyumba ilikua kubwa ya Kisasa lakini ilikua kimya sana sikusikia hata sauti ya ndege kuruka. Uwani

palikua na sehemu ya kukaa nikaona ni bora nikae hapo kwanza nipate upepo, nilijikuta nikipitiwa na Usingizi wa ghafla tu.

Ndoto za hapa na pale zilinifuata usingizini na kunipa hekaheka hadi nikashtuka. Niliposhtuka nilikutana na sura mbili, moja ilikua ya Salehe na nyingine ni ya Mzee mmoja mweusi aliyevalia Baraghashia nyeupe na kanzu nyeupe. Macho yao yalikua kwangu

“Eeeh imekuaje umelala hapo Mke wangu?” aliniuliza Salehe, nilijitabasamisha kidogo kama Mtu anayezuga ili asinione kuwa mvivu

“Hewa ya hapa inavutia, kaupepo nikajikuta nasinzia tu”

“Sawa, huyu ni Baba yangu anaitwa Mzee MwinyiMkuu. Ni Baba yangu Mzazi” alisema Salehe, nilimsalimia yule Mzee kwa heshima sana hata naye alifurahia na kuona ni namna gani nina heshima.

“Marhaba Mkwe wangu mzuri, hakika Mwanangu hakukosea’’ akasema kwa Utani tukajikuta tukicheka kidogo

“Samahani, najua umenitafuta ila nilienda kumpokea Baba maana aliniambia nikirudi tu atakuja kwa ajili ya kukusalimia wewe Mke wangu” alijielezea Salehe, ni kweli Mzee MwinyiMkuu alikuja na begi dogo la Mgongoni lililochakaa sana.

Aaaah! Nimefurahi sana kumuona Baba yako Salehe, karibu Baba.” Nilisema kisha nilisimama na kulishika begi la Mzee MwinyiMkuu ambalo lilikua sakafuni, kabla sijaliinua yule Mzee alinishika mkono kwa nguvu sana hadi nilishtuka, nikamtazama Usoni alikua amenikazia sura yake

“Hili begi halishikwi na kila Mtu, Salehe unajua pa kulipeleka” alisema Mzee MwinyiMkuu, nilihemwa maana sikutegemea lakini hata kama ningelichukua ningelipeleka wapi wakati na Mimi ni Mgeni pale. Nilishusha pumzi, kilinishuka nikarudi kukaa, Salehe akaniambia

“Mzoee Baba yangu ana utani sana Saida, wacha nikaweke begi lake nakuja” Mara moja alipomaliza kusema alinyanyuka Salehe na kuelekea ndani, yule Mzee hakuacha kunitazama kwa jicho kali kama vile kuna kitu nimeharibu hadi nilianza kumwogopa, ikanilazimu kumwomba Msamaha

“Samahani Baba sikujua”

“Siku nyingine uwe unauliza, umeelewa?”

“Ndiyo Baba” Nilipomjibu alinikata jicho fulani la husda kisha akatoa mguno fulani wa kicheko cha dhihaka halafu akanyanyuka na kuiburuza kanzu yake akaingia zake ndani,nilishusha pumzi zote kama Mgonjwa wa Pumu. Niliusikia moyo wangu namna ulivyoamka nakuanza kudunda tena, hata koo ilianza kupitisha mate kwa kasi. Yaani sijui nikueleze vipi unielewe namna nilivyokua nimeshikwa na woga kupitiliza, sura ya yule Mzee niliyona imekaa kikatili sana

Wakati naendelea kujiuliza mara Mume wanu Salehe alirudi kutoka ndani, akaketi mahali alipokua ameketi Baba yake

“Baba yako ni Mkali sana Salehe hadi nimeogopa. Nimefanya kipi kibaya, kumsaidia Begi ni vibaya eti?” Nilimuuliza Mume wangu, yeye akanishika bega akaniambia

“Utamzoea, si unajuwa wazee wa zamani. Pengine hakutaka wewe ushike begi kwasababu zilizo kaa kitamaduni tu za Kizamani au kabila letu lakini ni mcheshi utamzoea kwa muda atakaokaa hapa.

“Ina maana atakuwa anaishi hapa na Sisi?”

“Ndiyo, ila muda mchache tu atakua ameondoka. Vipi umeshakula?” Basi kuzungumza na Salehe kulinifanya nisahau kilichotokea, tuliongea sana hadi Mchana tuliposikia adhana. Salehe akawa wa kwanza kunikumbusha kufanya Ibada, nilitabasamu nikashusha pumzi kidogo huku dimpozi zangu zikionekana
SWAX kwa MADII
 
Ilipoishia “Kama utaendelea kunisumbua basi hapa patakuwa Jahannam yako na hutokaa utoke Milele Daima. Kingine napaswa kukuvuna viungo kila unapofanya mapenzi na Misukule, siku nikimaliza nitakuacha urudi kwenu” Nilijiuliza anivune viungo kivipi, kauli yake ilinianbia kwa haraka kuwa Kifo kilikua kimenigongea hodi, kipo karibu zaidi na Mimi.

“Unasema nini?” niliuliza nikiwa ninalia kwa sauti ya Chini.

Haraka yule Mzee akanipulizia unga fulani aliokuwa ameushikilia mkono wa kushoto, ulikua mweupe ulionifikia hadi usoni kwangu. Nikajikuta nikiwa nimelegea vya kutosha kiasi kwamba sijitambui, hatimaye giza tu lilinitanda na sikujua kilichokuwa kimeendelea nyuma yangu. Endelea

SEHEMU YA SITA

Nilikuja kupata fahamu nikajikuta nikiwa kitandani, kichwa kilikua kizito sana. Macho yangu yalikua hayafunguki kirahisi kutokana na Uzito wa Kichwa changu baada ya kupoteza fahamu zangu wakati ule

Kwanza nilihakikisha pumzi zangu zinarejea katika hali yake ya kawaida kabla ya kukumbuka kilichokuwa kimetokea, chumbani hapakuwa na yeyote yule isipokua Mimi na maumivu yangu ya Kichwa. Nilizivuta nguvu zangu hadi nikakaa kitako pale kitandani, nikawa nayasikia sasa yale maumivu ya kuchanwa huku chini na wale Misukule

Chozi likanitoka kutokana na ule unyama wa yule Mzee Mwinyimkuu, nikahitaji kuelekea Bafuni kujikagua namna nilivyoumia maana misukule walinifanya kwa fujo tena kwa Mpigo wote Watatu. Niliishusha miguu vizuri hadi Sakafuni, hapo nikahisi maumivu mengine makali mguu wa Kushoto

“Agggh‼” niligugumia, nikapeleka macho yangu Mguu niliouhisi una maumivu, Mungu wangu yule Mzee alinifanyia kitu kibaya sana. Alinikata kidole kimoja. Aisee‼ nililia kwa uchungu sana, sikuwa na kidole cha mwisho halafu damu ilikua imetapakaa mguuni, Hii siku nililia kuliko siku zote. Yaani nibakwe ma wale Misukule halafu nikatwe kidole kimoja hebu fikiria ni maumivu kiasi gani

Chozi lilinibubujika nikajikuta nikisema

“Mama yangu nateseka Mwanao, nakufa huku Mimi” Haki sikua na cha kufanya maana tayari Nilishatiwa kilema. Nikajivuta hivyo hivyo hadi nikafika Bafuni, sikujua nianze kujikagua mguu wangu au niukague Uchi wangu ambao ulikua ukiwaka moto kutokana na jasho lilivyokua

likipita. Nilivua kaniki nikaanza kuoga ili angalau nipate nguvu japo moyo ulijawa na ganzi sana.

Hiyo ilikua siku nyingine ya pili baada ya tukio la kubakwa na kukatwa kidole maana matukio haya yote yalifanyika siku moja tena Usiku. Nilifungulia maji hadi mwisho maana palikua na bomba la mvua, nikakaa sakafuni huku maji yakishuka mwilini kwa kasi sana. Nililia kuanzia moyoni mwangu hadi mwili mzima. Likaja wazo la kutaka kuondoa uhai wangu maana mateso niliyoyapata yalinikatisha tamaa ya kuendelea kuishi

Wakati wazo hilo likiwa limekolea kichwani pangu nilihisi kumwona Mtu pale Bafuni, nilishutuka nikajivuta pembeni mahali ambapo yale maji yalikua hayanipigi tena, macho yalinitoka kama fundi saa aliyepoteza nati. Mapigo ya moyo yalinidunda mithiri ya moyo unataka kutoka ndani, Mtu yule hakuonekana kuwa Binadamu wa kawaida, alikua na nywele ndefu zinazo buruza hadi chini, alivalia gauni jeupe lenye damu. Kibaya zaidi alikua ni Mtoto wa kukadiriwa kuwa na Miaka 6 hadi 8 hivi.

Hakunionesha sura yake iliyofunikwa na nywele hizo ndefu nzito na zenye uchafu wa kutosha. Alisogea hadi nilipo kisha akayafunga yale maji halafu akanisogelea zaidi na kisha nilimsikia akisema

“Kukata tamaa ni sawa na kuuza utu wako, usijione unapigana kwa ajili yako bali unapigana kwa ajili ya wengi. Amka ukashinde vita ili kuwaweka huru walio wengi ndani ya nyumba hii” alisema yule Mtoto kwa sauti ya Kukaza sana, alikua ni Mtoto wa kike, mkononi alishikilia mdoli fulani wenye manyoya.

Kiukweli sikua na ujasiri wowote wa kuongea chochote mbele ya yle Mtoto nisiyemfahamu, halafu nilihisi huwenda ni mawazo yangu tu.

“Nimesema amkaaaaa‼” yule Mtoto alipaza sauti kali ya kutisha, hadi nilijikuta nikipiga yowe la kutosha kwa hofu, niliziba masikio yangu na kufumba macho yangu, sikutaka kuendelea kuisikia sauti ya yule Mtoto wa ajabu, sijui alitokea wapi na kwanini aliyaongea yote yale. Nilipofumbua macho yangu nilikutana na Mzee Mwinyimkuu akiwa amesimama mbele yangu, kibaya zaidi nilikua uchi wa Mnyama, niliivuta ile kaniki na kuivaa

“Kwanini unapiga kelele?” aliniuliza yule Mzee, nilimeza funda zito la mate nikiwa sakafuni kule bafuni, huwa hapendi akikuuliza kitu halafu usimjibu kwa wakati.

“Hapana Baba, labda..” nilijikuta nikibabaika nisijuwe namjibu nini

“Nakuonya Binti, Maisha ya Wazazi wako yapo mikononi mwangu. Kama unataka waendelee kuishi basi fuata niyatakayo, kila utapofanya mapenzi na misukule nitakukata kidole kimoja cha Mguu, hadi nitakapo maliza kuondoa vidole vyote vya miguu nitakuacha huru lakini kwa aharti la kukaa kimya” alisema yule Mzee, niliitikia kwa kichwa tu ili aondoke lakini sikuafiki eti anikate vidole vyote vya Miguu yangu.

Alipoondoka ndipo nami nikapata unafuu wa kupumua vizuri, nikarudi chumbani mara moja, wazo la kujiuwa halikurudi tena kwa wakati huo, wazo likawa moja tu nitawezaje kuondoka bila wazazi wangu kudhurika? Halafu kingine nilichowaza ni kuhusu yule Mtoto kule Bafuni, aliyoyaongea yalikua maneno mazito ambayo nilihitaji kuyatafakari.

Ndiyo, sikupaswa kukata tamaa, sikupaswa kulia kila siku maana machozi yangu ni sawa na machozi ya Samaki baharini huenda na maji mara zote.

Nilishinda na maumivu makali sana na nilipaswa kumpikia Mzee Mwinyimkuu na Misukule yake, siku hiyo aliniambia nipike Ugali mwingi na Maharage. Ningefanya nini, nilifanya hivyo nikiwa natembea kwa maumivu makali sana hata hamu ya kula iliniisha.

Nikiwa jikoni mchana, nilisikia Mtu akibisha hodi. Sikujali sana sababu nilishaanza kukata tamaa, fikiria naambiwa nikatwe vidole vyote ndio ataniacha huru, maana yake nitakuwa kilema. Nikamsikia akitembea kuelekea nje kumwangalia mgongaji, sijui walizungumza nini. Halafu nikamsikia akiniita

Nilijikaza hadi nikafika Mlangoni, nikamkuta Akiwa na Mwanaume mmoja mnene mwenye kitambi na ndevu zilizozagaa

“Saida Binti yangu, sogea” alisema Mzee Mwinyimkuu, aliongea kwa bashasha na tabasamu juu halafu akaniita Binti yake, hadi nilishangaa nikasogea

“Huyu ni Mwenyekiti wa Mtaa. Msikilize” Alisema kisha yeye akasogea kwa nyuma ili mimi ndiyo nifanye mazungumzo na Mwenyektii, sikujua anataka kusikia nini na kwanini niitwe Mimi.

“Majirani wanasema jana usiku na leo asubuhi zimesikika sauti za yowe kama vile kulikua na tatizo. Nimemuuliza Baba yako anasema binti pekee uliye humu ni wewe, Je, Ulipiga yowe?” aliniuliza Mwenyekiti, moyo ulinilipuka. Nikageuka kumtazama Mzee Mwinyimkuu, akanionesha ishara ya kunionya kwa kutumia macho yake. Basi nikarudisha macho kwa Mwenyekiti, nikameza mate nikamjibu

“Sikupiga yowe na wala sijui chochote kile Kaka”

“Au kuna Binti mwingine anaishi humu?”

“Hapana, naishi Mimi na Baba. Mume wangu amesafiri” nilisema ili kuondoa ngoma juani japo nilikua nautonesha moyo wangu kwa kiasi kikubwa sana.

“Basi samahani sana, pia Samahani Mzee Mwinyimkuu huwenda Majirani walisikia tofauti” alisema Mwenyekiti lakini wakati anaongea akajikuta akipeleka macho yake kwenye Mguu wangu akaona sina kidole, halafu kibaya zaidi kidonda kibichi. Yule Mzee hakunifunga chochote na wala hakukuwa na dawa yoyote ile hata Mimi ningetia ili pakauke

“Kidole chako kimeenda wapi?” akauliza, nikashtuka

“kidole?” nikajikuta nikiuliza kwa mshituko nilioupata, laiti kama angelijuwa siyo kidole tu bali hata huku chini nilichanwa na Misukule wa Mzee Mwinyimkuu sijui ingekuwaje.

“Ndiyo ina maana hujui kama huna kidole, ona kinatoa maji maji” alisema huku akianza kutilia shaka kuwa huwenda kelele walizo zisikia zilitokana na kukatwa kidole.

“Mh…Aaaah..” kigugumizi kikanijaa maana sikujiandaa na swali hilo gumu.

“Ana kisukari hivyo tulishauriwa akatwe kidole” alidakia Mzee Mwinyimkuu, yule Mwenyekiti akashusha munkali wake, akaachia kicheko fulani na katabasamu

“Aaaah! Samahani tena jamani, si unajuwa ni jukumu langu kuhakikisha Wananchi wangu wanakuwa salama” alisema.

“Hakuna shida Mwenyekiti, karibu sana. Saida si umpe Mwenyekiti hata chai?” aisee aliongea Mzee Mwinyimkuu kama vile ni Mtu mwema na kwamba tunaishi vizuri sana Mimi na yeye

“Hapana nina majukumu mengine, basi Mimi naenda” aliaga akaondoka zake, tukabakia mlangoni Mimi na Mzee Mwinyimkuu, akanikata jicho fulani la ukatili hadi nikachechemea kuelekea ndani mwenyewe. Akanifuata huko huko ndani kisha akanishika shingoni kwa nguvu hadi nikawa nashindwa kupumua vizuri

“Narudia Ole wako ujifanye una mdomo mrefu, hiyo hurka itakuponza” akasema halafu akaniacha nakohoa kwa nguvu.

“ Siku nyingine ukipiga kelele zako ndio utakuwa mwisho wako humu ndani. Halafu kuna Kaka yako anaitwa Hamidu?” aliniuliza, nikaitikia kwa kutumia kichwa

“Amepewa namba yangu na wazazi wako, amesema anapitia hapa kukuona anatokea Mbeya kisha ndio aende Dar. Sasa hakikisha hajui chochote kile hadi anaondoka, nina uhakika ametumwa kukuangalia unaishije sababu haupatikani kwenye simu wala Salehe hapatikani” Nilishtuka, sikutaka ndugu yangu yeyote yule aingie ndani ya ile nyumba ya kishetani.

Hamidu ni Kaka wa Mama Mdogo na Mkubwa hivyo ni Mtoto wa Dada yake Mama yangu. Kiukweli sikutaka Kaka Hamidu aje kwa sababu kuu mbili

Huyu Mzee siyo Mtu wa kumwamini, muda wowote anaweza akabadilika. Pili, kama itatokea Kaka Hamidu akatilia mashaka kuhusu Maisha yangu itakuwaje, si familia yangu itakuwa kwenye matatizo? Tumbo liliniwaka moto yaani kila nilivyofikiria nilihisi kuhara, hata maumivu ya kubakwa na kukatwa kidole hayakuweza kuyafikia maumivu ya kufikiria kuhusu ujio wa Kaka Hamidu.

Haki, nguvu ziliniisha Mimi. Sikuwa na simu labda ningemueleza Kaka Hamidu asije ili kuokoa uhai wake na wa wazazi Wangu. Jasho lilinivuja, moyo ulinienda kasi sana, kibaya zaidi Mzee Mwinyimkuu alinitaka niigize kuwa naishi Maisha ya furaha sana ili kuwatoa hofu ndugu zangu.

Nilifuta kwanza jasho langu kisha nilikubaliama na hali halisi kuwa ni lazima niwe muigizaji mzuri zaidi ya Monalisa, nikarudi zangu chumbani nikiwa nachechemea kisha nikavalia baibui langu na mtandio, nikakaa mbele ya kioo ili nijiweke sawa. Nikajilazimisha kutabasamu ilihali moyoni ninalia, nilipohakikisha kuwa naweza kuigiza vizuri nilikaa kitandani nikiendelea kutafakari mambo mengine yaliyonijia akilini mwangu.

Mara baada ya muda mrefu kupita Mzee Mwinyimkuu alikuja chumbani, hakuwa na heshima wala adabu na Mimi aliingia kama anaingia chooni nami wala sikushtuka sababu niliyoyapitia yalianza kunipa ukomavu. Akanipa hela, halafu alikuwa akinipa hela mpya tupu

“Ukitoka hapo nje kuna Pikipiki, atakupeleka sokoni kisha atakurudisha. Muandalie Kaka yako chakula anachopendelea, nasistiza, makosa yoyote yale yatakugharimu” mara zote anapoongea ananinyooshea kidole na kunikazia macho yake mekundu kama mvuta Bangi, nilipokea na kuitikia kwa kichwa tu. Mdomo wangu ulijawa na uzito usio kawaida sababu nilizoea kukaa kimya.

“Tabasamu” alininasa kibao na kunitaka nitabasamu, basi nikaachia tabasamu la hovyo huku chozi likinibubujika, Nyakati hizi niliona ni namna gani Mungu niliyehangaika kumuabudu akiwa amenikalia kimya akiniangalia ninavyoteseka Mimi. Nilifuta chozi na kuchapa mwendo nikiwa na kapu mkononi, moyo ulinijaa chuki. Niliyachukia Maisha yangu, nikajichukia mimi mwenyewe na zaidi nilimchukia yule Mzee.

Nilitembea kwa kuchechemea halafu kichwa kilikua kinaniuma sana, nilipofika nje nikaigiza kutembea vizuri lakini maumivu niliyokuwa nayapata hayakuwa ya kawaida. Basi, nilimuona Bodaboda akiwa amesimama na Pikipiki yake, nami nikaidandia bila hata kumsalimia kisha yule Bodaboda akaongoza kuelekea mbele kama Mtu anayejuwa nilikua naenda wapi.

Ilikua ni mara yangu ya kwanza naenda mbali na nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, sikuacha kuhuzunika ndani yangu. Niliwatazama watu wakiwa wanafanya shughuli zao kwa uhuru kabisa tofauti na Mimi mfungwa kwenye nyumba ya Misukule. Ilituchukua wastani wa nusu saa hivi hadi kufika sokoni, palikua pamechangamka vya kutosha na palikua na kila aina ya Bidhaa.

Kaka Hamidu alikua mpenzi wa ndizi za Rosti na samaki wabichi, hela ilitosha kabisa kununua vyote. Nilihakikisha namuacha yule Bodaboda mbali ili nipate nafasi ya kuomba simu nimpigie Mama yangu ili nipate namba za Kaka Hamidu kusudi nimzuie asije, mwanzo yule Bodaboda alikua akinitupia jicho kama vile alipewa maagizo ya kunichunga lakini baadaye nilimpoteza kwa makusudi kabisa.

“Samahani kaka naomba nitumie simu yako, ni muhimu sana niwasiliane na Mama yangu” nilisema haraka haraka mbele ya Muuza Samaki wabichi, akanitazama bila kunielewa nahisi alijawa na maswali mengi yasiyo na majibu

“Simu yangu?” aliniuliza kama Mtu asiyenielewa kabisa, chozi lilianza kunidondoka.

“Ndiyo kaka ni muhimu sana naomba niongee na Mama yangu japo dakika moja tu Mimi” nilisema huku chozi likinibubujika. Bado yule Mkaka alikua amepigwa na Butwa halafu dakika zilikua zinakatika.

“Wewe umetokea wapi?” naye akaanza kunihoji badala ya kunisaidia, niliihitaji hii nafasi kuokoa uhai wa Kaka Hamidu.

“Kaka nisaidie kwanza mengine utayajuwa tu, samahani nipo chini ya Miguu yako” nikasema tena, halafu pale Buchani palikua na Wateja wengine wawili ambao waliweka umakini kwangu kusikiliza, mmoja akadakia

“Bro, si umsaidie huoni Mtu hadi analia bado unamuuliza maswali?Hebu chukua ya kwangu” akasema Kaka aliyekuwa akisubiria kuhudumiwa, yaani maongezi yalichukua dakika tano za thamani ambazo zingenisaidia kumpata Mama kwanza kabla ya Kaka Hamidu. Akanipa simu

yake nikaanza kujaza namba ya Mama yangu haraka na kwa pupa hadi nikawa nakosea kosea na kurudia rudia huku mkono ukitetemeka sana hadi mwenye simu akaniambia

“Nipe simu nikusaidie” basi nikampa na kuanza kumtajia Namba. Kabla hata sijamalizia namba za mwisho nikaguswa begani, nikashtuka. Nikafuta chozi haraka, nilipogeuka nikakutana na yule Bodaboda

“Dada unafanya nini, muda unaenda?” alisema, sikuwa na la kufanya pale wala sikutaka kuendelea kuwasiliana na Mama yangu, nikatoa pesa nikampa muuza samaki, kila mmoja akajawa na bumbuwazi la kufa Mtu. Sababu ghafla tu Mtu aliyekuwa analia na kuomba msaada nikawa na nguvu ya kusema

“Kaka nipimie kilo moja nachelewa Mimi” nilisema kama Mtu mwenye haraka, cha ajabu hakuna hata aliyeongea tena pale isipokua kunitazama kwa mshangao, nikapimiwa samaki kisha nikageuka na kuongozana na yule Bodaboda, nikageuka kumtazama yule Kaka aliyekuwa na nia ya kunisaidia simu nikamtazama kwa huzuni huku chozi likianza kunibubujika. Nilikua kama nimemtumia Ujumbe kuwa nimeshikiliwa nahitaji msaada.

“Nyie mmemuelewa yule Msichana?” aliuliza yule Kaka akiwa pale Buchani, kila mmoja alionesha kutonielewa mimi.

“Usikute anapitia magumu sana yule Msichana, siyo bure aombe simu halafu ghafla tu ajikaushe baada ya yule Mtu kuja” akasema Muuza samaki. Yule Kaka akawaambia

“Ngoja niwafuatilie” aliongea kisha haraka akatoka pale kutufuatilia Mimi na yule Bodaboda. Binafsi niliamini asingeliweza kuelewa chochote lakini nahisi Malaika wake walimuonesha kitu juu yangu. Wakati huo Mzee Mwinyimkuu alikua akieelekea kituo cha Daladala kumpokea Kaka Hamidu ambaye alimwambia kuwa anakaribia kufika.

Nilikuwa nimeshamaliza kununua mahitaji, nikapanda kwenye pikipiki bila kuzungumza na yule Bodaboda maana nilijuwa wapo timu moja na Mzee Mwinyimkuu hivyo sikutaka hata kuongea

chochote kile. Aliendesha kwa mwendo wa kasi sana kurudi nyumbani, sikuogopa mwendo wake sababu nilijiona kama Mfu anayeishi. Nyuma yetu yule Kaka alikua akitufuatilia na Pikipiki, Mimi wala sikujua hata yule Bodaboda hakujua kama kuna Mtu anatufuatilia hadi tunafika nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu

Yule Bodaboda alisimama na kunisindikiza kwa macho hadi naingia ndani, lakini nami sikusita kumfuatilia maana nilipoangalia mlangoni sikuviona viatu vya Mzee Mwinyimkuu hivyo nikawa na uhakika kuwa alikua ametoka, nikabana mlangoni na kumchungulia yule Bodaboda

Wasiwasi wangu ulikuwa wa kweli, akapiga simu na kumwambia Mzee Mwinyimkuu kuwa amenifikisha nyumbani halafu akasuburia kwa dakika kadhaa ndipo akaondoka, nilihema kwa nguvu kisha nikaegemea ukuta kwanza ili kumiminisha chozi langu ambalo lilikua likibisha hodi kila sekunde iendayo kwa Mungu, siyo tu kububujisha chozi bali nililia sana Mimi Saida.

Nilipomaliza kulia nilielekea jikoni ili kuandaa chakula cha Kaka Hamidu, Mzee Mwinyimkuu alikua mwenye kujiamini sana sababu aliyaweka dhamana Maisha yangu kwa ajili ya Wazazi wangu. Nikaanza kupika kwa ajili ya Kaka Hamidu.

***

Kumbe yule Kaka alikua amejificha mahali akiangalia kilichokua kinaendelea, alikua na uhakika kabisa kuwa nilikuwa kwenye mateso mazito, baada tu ya yule Bodaboda kuondoka basi akamfukuzia kwanza yule Bodaboda hadi Kijiweni. Akasimamisha pikipiki yake kando kisha akavuka barabara hadi alipo yule Bodaboda.

Akamwita pembeni na kuanza kuzungumza naye, kitu cha kwanza alichomuuliza

“Samahani Bro, hunijui, wala sikujui lakini kuna jambo nataka kukuuliza. Kwanza unanikumbuka?” akauliza, yule Mkaka alikuwa mweupe halafu alikua na rafudhi ya Kichaga. Umri wake kwa makadilio ni kama miaka 33 hivi, kwangu ni mkubwa sana hata kwa Salehe pia.

Yule Bodaboda akamtazama kwa umakini lakini hakumkumbuka kwa haraka “Sikufahamu bro, unashida gani na Mimi?”

“Naitwa Abuu, nilikuona pale Bucha ya Samaki kule Mjini. Ulikua umemfuata Msichana mmoja hivi ukaondoka naye” alipomuuliza hivi tu yule Bodaboda akaanza kutafuta majibu

“Anhaa‼ inawezekana, sasa unataka nini?”

“Yule Msichana aliniomba simu awasiliane na Mama yake, sasa hakufanikiwa ndiyo wewe ukaja ila kwa namna nilivyomuona anaonekana yupo kwenye changamoto kubwa sana na anahitaji msaada, unalifahamu hilo?” Si unajua Wachaga hawakwepeshi maneno yao, alimchapa moja kwa moja na kumwacha Bodaboda akiwa anatafakari sana

“Kaka unajua yule ni Mke wa Mtu, mimi kazi yangu ni kumpeleka sokoni tu. Hayo mengine mimi siyajui na wala sifuatilii kabisaa, sasa kama unataka kufuatilia ndoa za Watu haya, ila nakutahadharisha sana. Hii ni Rukwa” alisema kwa kujiamini sana.

Abuu alikosa cha kuongea zaidi akamshukuru tu yule Bodaboda lakini kichwani alikua na maswali mengi sana, Basi yule Bodaboda alikua akitumika kweli na Mzee Mwinyimkuu hivyo baada ya Abuu kuondoka akampigia simu Mzee Mwinyimkuu na kumueleza aliyoyasema Abuu kuhusu safari ya Sokoni, Abuu akawa amejiweka matatizoni bila kujua alikua akifuatilia jambo la hatari kiasi gani, wakamtazama Abuu kama kikwazo hivyo wakawa na mpango juu yake.

Jua lilianza kuzama, nilikua tayari nimemaliza kupika na kuweka chakula kwenye hot-pot. Nilikua na msongo wa mawazo, kichwa nacho kilikua kinaniuma sana kwa sababu ya vile vidonda. Nilipoisikia adhana sikujishughulisha nayo nikiamini Mungu ameniacha peke yangu niteseke.

Muda huo huo nikasikia mlango ukifunguliwa, mara moja nikakimbilia Uwani na kumuona Mzee Mwinyimkuu akiwa ameongozana na Kaka Hamidu, moyo ulianza kwenda mbio, nilikua nimejibanza mlangoni nikiwaangalia wakiwa wanaongea, halafu Kaka Hamidu akawa anamsaidia Mzee Mwinyimkuu kuufunga mlango wa Uwani tena kwa funguo halafu funguo akampa Mzee Mwinyimkuu.
 
Ilipoishia “Jua lilianza kuzama, nilikua tayari nimemaliza kupika na kuweka chakula kwenye hot-pot. Nilikua na msongo wa mawazo, kichwa nacho kilikua kinaniuma sana kwa sababu ya vile vidonda. Nilipoisikia adhana sikujishughulisha nayo nikiamini Mungu ameniacha peke yangu niteseke.

Muda huo huo nikasikia mlango ukifunguliwa, mara moja nikakimbilia Uwani na kumuona Mzee Mwinyimkuu akiwa ameongozana na Kaka Hamidu, moyo ulianza kwenda mbio, nilikua nimejibanza mlangoni nikiwaangalia wakiwa wanaongea, halafu Kaka Hamidu akawa anamsaidia Mzee Mwinyimkuu kuufunga mlango wa Uwani tena kwa funguo halafu funguo akampa Mzee Mwinyimkuu. Endelea

SEHEMU YA SABA

Walionekana kupiga stori za hapa na pale kana kwamba walijuana muda mrefu, nilijua hii ilikua ni tabia yake Kaka Hamidu kupenda kuongea sana na Watu tofauti tofauti pasipo kujua kua aliyekua anaongea naye alikua katili sana na laiti angelijua hata asingelikanyaga mguu wake ndani ya hii nyumba. Taratibu nilirudi ndani nikaingia chumbani, nikafunga mlango huku chozi likinibubujika

Hapakuchukua muda mrefu mlango uligongwa, halafu uligongwa taratibu sana na hapo hapo sauti ya Mzee Mwinyimkuu ikasikika ikiniita

“Mkwe” yaani nilizidi kukereka lakini kwa kuhofia uhai wa Kaka Hamidu ikanilazimu kuitikia japo kwa shingo upande

“Abee Baba” nilinyanyuka na kwenda kufungua mlango, ghafla akanisukumiza hadi ndani kisha akaufunga mlango na kunishika shingoni

“Nilikuonya lakini unaonekana hutaki kusikia si ndiyo, sasa kwa taarifa yako hakuna utakachofanya nisikijue. Ulichojaribu kukifanya leo sokoni kinaweza kukugharimu, subiri Kaka yako aondoke nitakuonesha rangi yangu halisi na yule Mtu wako anakufuatilia sasa naye arobaini yake imefika” alisema kisha akanitupa pembeni, kwakuwa nilikua mwembamba ikawa rahisi sana kwake kunisukuma, nikawa nakohoa ila nikawa nimejua kua nilichokusudia kwa yule Mwanaume kule Buchani kilifanya kazi ila sasa nikawa naogopa sababu ni lazima atadhurika tu.

“Jiandae uje uonane na Kaka yako, kumbuka nilichokwambia ukifanye la sivyo naye ataishia humu” alisema kwa sauti yenye mikwaruzo huku akimalizia na ishara ya kuweka mkono

shingoni kuwa atamuuwa. Lugha ya chozi ndiyo Lugha pekee ambayo nilikua naizungumza kila wakati, umri wangu na yote ninayoyapitia vilinizidi kabisa

Ili kumlinda Kaka Hamidu nililazimika kuigiza kuwa kila kitu kipo sawa, nilifunga vizuri kitambaa mguu ambao ulikatwa kidole kisha nikavalia na soksi, Nikanawa usoni ili kujipa utulivu wa sura yangu iliyochoka mateso na manyanyaso ya Mzee Mwinyimkuu. Nilisimama mbele ya kioo huku kwa mbali nikisikia namna ambavyo Mzee Mwinyimkuu na Kaka Hamidu walivyokuwa wakichekeshana

Nilipohakikisha nimejiweka vizuri, nilitoka chumbani nikaenda sebleni ambapo Kaka Hamidu alikuwepo, niliizima hisia ya majonzi nikaingia sebleni, Kaka Hamidu alifurahi sana sababu hakuwahi kuhudhuria harusi yangu na pia ilipita kitambo pasipo kuonana, nilimkaribisha kwa furaha ya kuigiza na kumtaka ajisikie yupo nyumbani kisha nilimuacha na kwenda kumuandalia chakula.

Niliporudi nilimpa chakula akaanza kula huku akinisifia kuwa mapishi yangu hayajabadilika, yeye alionekana kuwa na amani na furaha ya kweli sababu hakuna alichokuwa anakifahamu hadi muda huo, isipokua mimi niliyejiona nilikua ndani ya shimo refu lililoenea giza zito nisione pa kutokea, tabasamu lilitanda kote usoni pangu ili tu kumlinda Kaka Hamidu, na jinsi muda ulivyokuwa umeenda niliogopa sana kama atalala ndani ya nyumba hii ya Kutisha, nilitamani aondoke baada ya kumaliza kula tu.

Mzee Mwinyimkuu alikua ameketi anasikiliza maongezi yetu, akawa ananikumbusha stori za zamani na kumwambia Mzee Mwinyimkuu kuwa nilipokua mdogo nilikua na tabia ya kulialia, kwake alichukulia kama ni sehemu ya mazungumzo mazuri lakini kwangu niliona anapoteza muda badala ya kula akamaliza mapema aondoke, baadaye akaniuliza kama naweza kupokea simu kutoka kwake

Huwezi amini alininunulia simu ndogo ili nisikae bila simu kwa wakati ambao nilimwambia Mama kuwa namsubiria Mume wangu Salehe akirudi aninunulie simu mpya. Niliitaka sana ile simu lakini jicho alilonikata Mzee Mwinyimkuu nikajikuta nikimwambia

“Asante Kaka, muda siyo mrefu Salehe atarudi atanunua simu ni wajibu wake. Hiyo kampe Wifi yangu” nilisema kanakwamba nilikua kwenye utani lakini moyoni nilitamani angenipa kisiri ile simu ila sasa alikua hajui kuwa napitia mateso makali sana na vitisho vya kila aina. Mzee Mwinyimkuu akajikoholesha, jasiri haachi asili yake nikashtuka lakini nikajishtukia na kurudi kwenye hali ya kawaida

“Saida, Muandalie mgeni sehemu ya kulala. Apumzike akimaliza kula maana anaonekana amechoka” alisema Mzee Mwinyimkuu, nilishtuka sana sikutaka Kaka Hamidu asikie vitimbi vya Usiku vya hii nyumba, nikaitikia kwa wasiwasi sana

“Njoo Mama” akasema Mzee Mwinyimkuu, mbele ya Mtu mwingine hujionesha ni Mtu mzuri lakini tukiwa wawili ananitendea unyama na ukatili wa kutisha sana. Nilitabasamu nikiwa

namtazama Kaka Hamidu ambaye naye alikua akitabasamu huku akinitazama, ndani ya moyo wake aliiamini hii picha ya nje kuwa nina amani na furaha lakini niliamini kama atalala hapa basi ataiona picha ya ndani ya Maisha yangu kitu ambacho kitahatarisha Maisha yake.

Niliongozana na Mzee Mwinyimkuu hadi kwenye korido, akairudisha ile sura yake ya Mbuzi ambayo niliizoea japo inatisha, kwa sauti ya chini nzito akaniambia

“Chumba cha mwisho kushoto, muandalie mazingira ya kulala.” Alisema, sijui kwanini alisistiza Kaka Hamidu alale wakati alikuja bila begi lolote lile akionekana amekuja Mara moja tu, licha ya yote sikutaka alale pale ila sikujua nawezaje kumshawishi aondoke.

“Sawa” hakunipa onyo lolote lile baada ya kuitikia aliondoka na kurejea sebleni, nilienda moja kwa moja kwenye chumba nilichoelekezwa ambacho Kaka Hamidu atalala. Sikuwahi kukifungua kile chumba wala kukisogelea, ilikua ndiyo mara ya kwanza nakifungua

Nilipoingia ndani nilianza kuona vitu vilivyoniacha mdomo wazi, huyu Mzee alitaka makusudi nione pia. Palijengwa kitu kama kaburi katikati ya kile chumba, halafu palikua na mifupa mingi sana ya Binadamu, mafuvu ukutani, halafu nikasikia sauti ya kutisha ikisema

“Hiki ni Chumba cha Hamidu” sauti hiyo ilinipa kiwewe nikajikuta nikipiga yowe nikakimbia kuelekea sebleni, Kaka Hamidu akawa Mtu wa kwanza kunidaka na kuniuliza kuna nini. Hapo akili ikanikaa sawa kuwa sikupaswa kupiga kelele namna ile, nikajitahidi kujikaza lakini tayari

nilikua nimezua taharuki halafu cha ajabu Mzee Mwinyimkuu alikua akitabasamu tu kitu ambacho kilizidi kunipa maswali yasiyo na majibu.

“Eti Babu huyu ana nini?” akauliza Kaka Hamidu akiwa amenishika bega huku macho yake akiyapeleka kwa Mwinyimkuu aliyeketi bila hata kujitingisha

“Saida Bwana, sasa nini kinakufanya unamshtua Kaka yako, hadi leo hujaizoea hii nyumba tu?” Aliniuliza Mzee Mwinyimkuu lakini swali lake lilijaa dhihaka sana kitu ambacho sikukipenda kabisa wakati alijuwa alichokua amekifanya. Bumbuwazi niliyonayo ilinifanya nishindwe kujibu swali lolote lile

“Hamidu hebu twende ukaone kilichomshitua huyu” akasema Mzee Mwinyimkuu, Moyo ulifanya kama unataka kusimama hivi kwa namna nilivyoshituka, nikajiuliza kama Kaka Hamidu ataenda kule atakiona kile chumba cha kutisha chenye kaburi ndani na hapo kizaa zaa kitaanza kwake, nikajitahidi nimzuie nikamwita

“Kaka Hamidu…” alikua tayari ameongozana na Mzee Mwinyimkuu, walikuwa wameshafika kwenye korido wakiwa wamebakisha hatua chache sana kukifikia kile chumba cha kutisha, macho yalinitoka nikiwaangalia walivyokuwa wakienda kisha walisimama mlangoni wakatazamana kwa mshangao

Halafu Kaka Hamidu akaangua kicheko huku akigeuka na kunitazama nikiwa nimesimama mlango wa kuingilia sebleni, alicheka kama Mtu aliyepandwa na wendawazimu, hapo hapo

nikaisikia simu yake ikiita maana aliiacha kwenye kochi, nikatamani kurudi niipokee ili nitoe taarifa kusudi akipotea kila Mtu ajue pa kuanzia lakini sikupata hata hiyo nguvu mara akaniita

“Saida hebu njoo” aliniita Kaka Hamidu, alikua tayari ameacha kucheka. Akaniita tena kwa kunisitiza kuwa niende, nikajikuta bila kujiuliza mara mbili naanza kupiga hatua kama Mgonjwa, kumbuka hapo nna maumivu ya Uchi wangu pia kidole kilichokatwa halafu nilishakata tamaa

Nilisogea taratibu huku nahesabu hatua zangu kama mwendawazimu, nilijua naenda kuona nini sababu nilichokiona mwanzo ni kile kile. Nilipofika nilishangaa sana, Jamani eti kile chumba chenye kaburi na mafuvu na mifupa ya Binadamu kilikua hakina chochote zaidi ya kitanda kizuri kilochotandikwa shuka safi sana na zaidi kilikua kinanukia ila chini palikua na paka aliyetulia zake.

Kaka Hamidu akanishika bega akaniuliza

“Ni lini utaacha kuogopa paka Mdogo wangu? Wewe ni Mtu mzima sasa pia ni Mke na huwenda ukawa Mama baadaye, unaogopa Paka kweli?” aliniuliza, haikuwa siri ni kweli nilikua naogopa paka lakini nilichokiona mwanzo wala hakuwa paka, sasa nikajiuliza ni mawazo yangu tu au nilichokuwa nimekiona kilikua halisi na hiki tunachokiona ni kiini macho tu.

Nilihema mfululizo kama vile moyo ulishusha pumzi na kuamua kurejea kwenye mapigo ya kawaida, basi nilikaa kimya sikusema chochote kile.

“Utalala hapa, si ulisema kesho asubuhi unarudi Mbeya?” aliuliza Mzee Mwinyimkuu

“Eeeh asubuhi narudi ili nijiandae halafu kesho kutwa niende Dar” alijibu Kaka Hamidu, akanishika mkono tukarudi sebleni nikiwa kimya. Nilimhurumia sana Kaka Hamidu maana nilianza kuwa na wasiwasi kuwa Mzee Mwinyimkuu kuna mpango fulani ameupanga dhidi yake. Muda huo huo Mzee Mwinyimkuu akapokea simu halafu akatuacha pale akaelekea nje kuzungumza ikionekana kama kuna Mtu aliyemtarajia alikua amefika nje.

Nilipanga kumshawishi Kaka Hamidu asilale ndani ya ile nyumba lakini sikujua naanzia wapi Mimi. Nikiwa natafakari Kaka Hamidu akaniuliza

“Huonekani kuwa sawa Saida, kuna tatizo gani hapa?” aliuliza kama Mtu aliyeanza kuonesha wasiwasi wa ghafla japo muda wote huo alikua akionesha kutokuwa na wasiwasi kabisa. Kwakuwa alionesha kuwa na wasiwasi nikaona ni bora nimueleze ili aokoe uhai wake sababu uhai wa Wazazi wangu ulikua mikononi mwangu.

Nilisogea na kupiga magoti mbele yake nikashika na miguu yake huku chozi likinibubujika.

“Kaka Hamidu, usilale ndani ya hii nyumba na kama utafanya hivyo basi kifo chako kitakuwa karibu zaidi na wewe” nilimwambia chozi likizidi kunibubujika, hata sauti iliyonitoka iliambatana na kilio kisicho na sauti Kubwa

“Unamaanisha nini?”

Nikavua soksi na kmwonesha Kaka Hamidu nilivyokatwa kidole ili ayaamini kwa haraka maneno nitakayo mwambia, alishtuka sana.

“Huyu Mzee siyo Mtu mzuri Kaka yangu, okoa Maisha yako bado una muda wa kufanya hivyo. Hii nyumba imejaa uchawi na mateso makali, hata kile chumba unachoambiwa ulale ni chumba chenye kaburi ndiyo maana nilishtuka. Ondoka bado una muda” Nilimueleza Kaka Hamidu, haikuhitaji elimu ya chuo kikuu kujua kua Kaka Hamidu alikua ameshanielewa.

Akajawa na taharuki na hasira sababu alikua ananipenda sana na isitoshe hakuna ndugu anayeweza kumuacha ndugu yake kwenye shida kiasi kile.

“Saida siwezi kukuacha hapa, nitamfundisha adabu huyu Mshenzi” akasema Kaka Hamidu, kimwili Kaka Hamidu alikua amejazia jazia hivyo kama utamuweka mizani moja na Mzee Mwinyimkuu basi yeye ndiye atazidi. Akanishika mkono kwa nguvu akasema

“Tunaondoka wote”

“Kaka nenda wewe tu, mimi niache hapa ili Wazazi wangu wawe salama” nilisema, sasa Kaka Hamidu akaanza kupaza sauti kitu ambacho sikukitaka kabisa. Nilichotaka ni siasa zaidi ili Kaka Hamidu aondoke pasipo Mzee Mwinyimkuu kujuwa chochote kile.

Mara tukasikia mlango ukifungwa tena siyo kufungwa kawaida ni kule kufungwa kwa kufuri kabisa halafu ni Mlango wa kuingilia nyumba kubwa, Kaka Hamidu akanipa ishara ya kukaa kimya. Alidhamilia kuomdoka na Mimi, nami niliona ni bora niondoke naye kuliko kubaki tena kwa Mzee Mwinyimkuu

Akaingia Mzee Mwinyimkuu pale sebleni, alikua amevalia suruali, singlendi na Balaghashia kama kawaida yake, hakututazama kabisa akalisogelea kabati na kuiweka funguo kwenye droo kwa mbwembwe sana huku akiwa anapiga zake mluzi.

Ilikuwa ndiyo nafasi pekee ambayo Kaka Hamidu alikua ameipata, akachukua jagi la kioo lenye maji kisha akasogea taratibu hadi nyuma kwa Mzee Mwinyimkuu, akampiga na lile jagi kisogoni kwa nguvu hadi Mzee Mwinyimkuu akagugumia kwa maumivu na damu zikaanza kutoka alipopigwa akaanguka chini huku akionekana kutaka kusema jambo lakini alikua akishindwa.

Kaka Hamidu alikua akimuangalia Mzee Mwinyimkuu alivyokua anatapa tapa, kwa sekunde kadha tu zilitosha kumnyamazisha akawa ametulia tuli pale chini kama maji ya Mtungi, ikawa ni nafasi ya dhahabu sana kuondoka ndani ya ile nyumba.

“Twende” akasema kaka Hamidu akiwa amenishikilia mkono kwa nguvu tukawa tunaelekea mlangoni ili tuondoke. Tulipofika Mlangoni tukapata akili ya ile funguo, ndiyo! Palikua na kufuri mlangoni, funguo aliiweka kwenye droo kule sebleni,.

Hapakuwa na ujanja isipokua Kaka Hamidu kurudi sebleni kuchukua funguo, alipofika Sebleni hakumuona tena Mzee Mwinyimkuu pale sakafuni wala sebleni kote, ni kama aliyayuka mithiri

ya Barafu juani. Akaniita, nikakimbilia sebleni nami nikawa shuhuda wa kutoweka kwa Mzee Mwinyimkuu, tulitazama kwa mshangao mkubwa.

Tusingeweza kurudi nyuma tena, Kaka Hamidu akafungua droo na kuikuta funguo, akaichukua kisha akaniambia tuondoke. Cha kushangaza ambacho kilitufanya tugande kama Barafu ni kuukuta ule mlango tuliohangaika kuchukua funguo ukiwa wazi kabisa, halafu nje tukisikia sauti ya Mtu kama akichakata kuni hivi.

Sote tukawa na hofu sana, Nani ameufungua ule mlango bila kusikila sauti yoyote? Hakuna aliyekua na jibu la moja kwa moja, Kaka Hamidu akaona ni bora apige simu ili aombe msaada, alishaona siyo rahisi kuondoka ndani ya ile nyumba ya kutisha, halafu ilikua mishale ya usiku mchanga kama saa 3 hivi lakini matukio yaliyotokea na ukimya uliokuwa umetanda na giza ilionesha kama vile ni Usiku mnene.

Akajipapasa na kukumbuka simu aliiacha Kwenye kochi, kabla hata hajapiga hatua kurudi sebleni, pale pale taa zote zikazima. Pakawa giza tupu hata nuru moja isionekane, pakawa kimya kabisa, sikumsikia tena Kaka Hamidu isipokua sauti ya kugugumia ambayo aliitoa kwa nguvu, papo hapo nikasikia kitu kikianguka kama Mzigo ‘Puuh’

“Aaaaah‼” niligumia kwa hofu lakini ghafla nikabanwa mdomo wangu halafu sauti ya Mzee Mwinyimkuu ikagonga ngoma za Masikio yangu, nilishtuka sana.

“Shiiiii‼!” akanitaka nikae kimya. Nilikuwa nahema juu juu, mara papo hapo taa zikawaka. Nilichokiona jamani sitakuja kusahau Maisha yangu yote, nilihisi uchizi, nilihisi wendawazimu. Mwili ulipoa kama nimemwagiwa maji ya Baridi. Kaka Hamidu alikua sakafuni, damu nzito ilikua imetapakaa kila mahali.

Alitenganishwa kichwa na kiwiliwili chake, damu zilikua zinaruka kwenye shingo yake. Hata Mzee Mwinyimkuu aliponiachilia sikua na nguvu nilianguka chini nikakalia damu.

“Nilikuonya hukusikia” akasema Mzee Mwinyimkuu, alisema. Mkononi alikua ameshikilia kisu kikubwa chenye damu. Niliishia kudondosha chozi tu, mara akaingia Mwanaume mmoja na kuanza kuuvuta mwili wa Kaka Hamidu kuelekea nje, Mze Mwinyimkuu akakichukua kichwa cha Kaka Hamidu na kukipeleka kwenye kile chumba alichokua amekiandaa kwa ajili ya kulala Kaka Hamidu.

Sijui kilichoendelea baada ya hapo nilijikuta nikizidi kuishiwa nguvu, giza zito likatanda nikahisi usingizi wa ajabu. Nikapoteza uwezo wa kujitambua.

**

“Saida,Mdogo wangu amka Unisaidie” ilikua ni sauti ya Kaka Hamidu, alikua amesimama mbele yangu nikiwa nimekaa kitandani, alikua akivuja damu kila sehemu. Alikua ametisha kiasi kwamba niligugumia hadi nikapaza sauti yangu kwa hofu. Hivyo ndivyo nilivyoamka kutoka Usingizi wa kifo

Nilikua na maumivu makali sana mguuni, ndoto hii mbaya iliniamsha. Eneo lile lile nililokatwa kidole lilikua na maumivu makali sana. Niliusogeza vizuri Mguu wangu na kuangalia kidonda kinaendeleaje, nilipoangalia niliona vidole viwili vikiwa vimeondolewa. Yaani jumla ya vidole vitatu vinavyofuatana kuanzia cha mwisho vilikuwa havipo.

Maumivu yalikua makali, ni bora uyasome kwenye hii hadithi lakini yasikukute, mwili wote ulipandisha homa ya ghafla, kichwa kilikua kinauma sana. Safari hii sikuwa na uhakika kama ninaweza hata kutembea, eneo lenyewe nililopatia ufahamu sikulijua kabisa.

Nilikua sakafuni, chumba kilikua kitupu isipokuwa mimi tu na maumivu yangu. Nilipiga sakafu kwa uchovu nikasema

“Kama uliniumba niteseke hadi nife basi nitakufa na kama huu ni mpango wa shetani basi hawezi kukuzidi maarifa” nilipomaliza kusema hivi nilijikunyata, Nililia sana. Nilikua tayari nimempoteza Kaka Hamidu na sijui walimpeleka wapi

Eneo lile lilikuwa kimya sana tofauti kabisa na nilivyozoea, sikusikia sauti za Pikipiki wala mazungumzo yoyote yale. Niliona ni bora nilikague eneo lile, nilichungulia dirishani, nililiona Pori la Kubwa, nilishtuka. Nikagundua nilikua nimehamishwa kutoka kwenye nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. Nililia sana maana safari hii siwezi kukutana na yeyote yule nikapata msaada, Mzee Mwinyimkuu alishagundua kuwa kama ataniacha huru naweza kutoroka, ilifika hatua nilikua mkali nikajisemea

“Kama kuokoa uhai wangu kutafanya wazazi wangu wafe ni sawa, napaswa kukwepa haya mateso Makali. Mungu atapigana kwa ajili ya Wazazi wangu” hayo ndiyo yalikua maamuzi yangu.

Niliveshwa kaniki pekee halafu nilikua na alama fulani kwenye paja langu, ilikua alama ya ajabu iliyochorwa kwa moto, palikua na maneno ya ajabu. Huu ndiyo wakati mgumu zaidi kuwahi kuupitia katika Maisha yangu yote, haukuwa wakati rahisi kwangu, ulikuwa wakati ambao nilipoteza tumaini la Maisha yangu lakini sikuweza kufanya chochote isipokua kuugulia maumivu na kulia.

Kilipita kitambo kirefu cha Ukimya, sijui ilikua ni saa ngapi, siku gani au lile eneo ni wapi. Nilichojua ni kuwa bado naendelea kupumua, niliusikia Mlio wa pikipiki. Nikajivuta na kuchungulia dirishani, niliiona pikipiki ikiwa imesimama kando kidogo kama mita chache tu hivi kisha Mtu mmoja alisogea mbele kuelekea nyumba niliyopo

Kumbuka hapo ni Porini, tokea nimezinduka sikuwahi kumuona yeyote yule isipokua sauti za ndege zilizopita kwenye ngoma za masikio yangu yaliyochoka kusikia sauti za kutisha. Nilikua nimekonda ghafla sana Mimi Saida

Basi, yule Mtu sikuiona sura yake kwa haraka sababu hata nguvu ya kusimama kwa muda mrefu ilianza kuniisha nikajikuta nikianguka chini, maumivu yalikua makubwa halafu nilikua na njaa

sana. Nilisikia tu akifungua mlango ulioonekana kuwa na komeo nyingi, akaingia hadi chumba nilichopo

Yule Mtu nilimkumbuka kwa haraka sana, alikua ni yule Bodaboda aliyenipeleka sokoni siku ile ambayo nilikutana na Abuu. Nilikua na wenge zito lakini sikuacha kumtazama kwa makini hadi nikamtambua. Alikuwa amebeba chakula kwenye Hot-pot

Wala hakuongea chochote akaanza kuniandalia chakula nile, nilikua nahema kwa shida sana.

“Kunywa Maji” alisema, alikua haniangalii usoni, nilikua na kiu ya maji lakini kiu kubwa ilikua ni kumuuliza Nauawa lini, nilimuuliza

“Mnanimalizia lini nikapumzike?” Kiukweli sikuwa na afya nzuri, ndani ya siku chache nilikonda. Yule Bodaboda akanitazama kisha akaniambia

“Kifo ni siri ya Mungu, hakuna anayeijuwa kesho itakuwaje” alisema kisha akanipa maji, sikuwa na nguvu ya kushika kikombe akaninywesha. Jinsi alivyonihudumia alionesha anahitaji niwe hai
 
Ilipoishia “Wala hakuongea chochote akaanza kuniandalia chakula nile, nilikua nahema kwa shida sana.

“Kunywa Maji” alisema, alikua haniangalii usoni, nilikua na kiu ya maji lakini kiu kubwa ilikua ni kumuuliza Nauawa lini, nilimuuliza

“Mnanimalizia lini nikapumzike?” Kiukweli sikuwa na afya nzuri, ndani ya siku chache nilikonda. Yule Bodaboda akanitazama kisha akaniambia

“Kifo ni siri ya Mungu, hakuna anayeijuwa kesho itakuwaje” alisema kisha akanipa maji, sikuwa na nguvu ya kushika kikombe akaninywesha. Jinsi alivyonihudumia alionesha anahitaji niwe hai. Endelea

SEHEMU YA NANE

Niliyafakamia yale maji kwanza hadi yalinipalia, halafu nikahema. Akanitolea vidonge vya kunituliza maumivu. Sikusita kumeza kiukweli maana nilikua na maumivu makali sana kisha nilimshika mkono nikamuuliza

“Ningekuwa mdogo wako ungenifanyia hivi, unajua najisikiaje Kaka?’’ Chozi lilikua linanibubujika bila kuacha, akaniondoa mkono wangu kwa kutumia mkono wake mwingine kisha akasimama, akaniambia

“Kula upate nguvu” hakuzungumza tena, alisimama kisha alipiga hatua lakini alipofika mlangoni alisimama. Kama kuna kitu alitaka kuniambia lakini alighaili, hakujibu swali langu aliondoka na kuufunga mlango kwa funguo, unajua hata kama angeuacha wazi sikuwa na nguvu ya kukimbia kwa namna nilivyokua sina nguvu.

Nilisikia akiondoka, nililia sana Mimi. Hakuna siku inapita bila kudondosha chozi langu, nilimpoteza Kaka Hamidu na nilijiona ni mkosaji, nilijilaumu sababu bila kuolewa na Salehe basi Kaka Hamidu angekuwa hai hadi sasa. Kidogo zile dawa zilipunguza maumivu ya mwili lakini siyo maumivu ya Moyo wangu

Haikuchukua hata dakika nyingi nilisikia yowe la Mwanaume mmoja, yowe lile lilisikika moja kwa moja kutoka kwenye ile nyumba niliyohifadhiwa Mimi. Moyo ulinilipuka, niliamini ilikua ni nyumba ya Mateso makali zaidi hata nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu. Nilisimama hata nguvu sikujuwa ilitokea wapi

Nilisogea mlangoni ili kuisikia zaidi ile sauti, ndiyo! Ilitoka ndani ya moja ya vyumba vya ile nyumba, nilitamani kupaza sauti ila sikujua alikua akifanywa nini. Nilijiuliza

“Nani yupo ndani ya hii nyumba, anamfanya nini huyu anayepiga yowe” Ilikua ni sawa na kujitekenya kisha kucheka mwenyewe, jibu lingetokea wapi ikiwa hata mimi mwenyewe sijui nipo wapi

Yule Mwanaume baada ya kupiga yowe alianza kusema

“Msaada,Nani yupo ananisikia?” aliendelea kusema hivi, nikapata picha huwenda hata yeye mwenyewe hajui amefikaje na Nani amemleta ndani ya hii nyumba. Kupitia dirishani nilianza kuona jua namna lilivyokuwa likifanya safari ya kwenda kupumzika baada ya kuipiga ardhi kwa siku nzima.

Namna nyumba hii ilivyo ilionekana kujengwa kwa ajili ya kazi ya kuhifadhi Binadamu, hata dirisha lake lilikua kama la Mahabusu, lilikua dogo lanye nondo,hapakuwa na taa ndani ya chumba kiasi kwamba giza litakapoingia basi patakuwa giza tupu. Nilijikuta nikikaa mwenyewe bila hata kuambiwa, kwa namna ilivyo hata ukipiga kelele vipi huwezi kupata Msaada wowote.

Kwanza sikujuwa Mtu yule alikua ni Nani, sauti yake haikufanana na ya Kaka Hamidu. Wala si ya Mtu niliyehisi kuwa niliwahi zungumza naye.

**

Usiku ulipoingia ndiyo nililiona joto la jiwe, niliandamwa na ndoto za ajabu hadi niliamka, siyo Mimi tu hata yule Mwanaume alikua akigugumia nahisi naye alikua kwenye hali kama yangu. Niliamka na kukaa kitako nikaegemea ukuta

Nikiwa hapo nilianza kuona nuru ya mwanga, ikianza taratibu hadi ikaenea chumba chote, hapa nilikua na uhakika kuwa haikuwa ndoto tena bali ni tukio halisi. Nilimuona tena yule Mtoto mdogo anayetisha, safari hii alinionesha sura yake, nilikua kwenye Mshangao wa hali ya juu sana

“Umeshindwa kutoka hapa, umeshindwa kujaribu kufanya chochote. Wewe ni Mtu wa aina gani, unataka kila Mtu afe kama Kaka yako Hamidu” Ooh! Jamani nilishtuka, kama ningekua nina presha kwa haya yote ningekuwa tayari nimepotea kwenye uso wa Dunia, namna alivyokua anaongea alionesha alikua na tumaini na Mimi kwenye jambo fulani hasa la kuokoa uhai wa wengine lakini Mimi mwenyewe nilikua nimeshajikatia tamaa. Japo nilijawa na woga lakini nilimuuliza

“Wewe ni Nani, umetokea wapi?” nilipomuuliza alidondosha chozi la damu, alikua Mtoto wa ajabu sana

“Mimi ni Ashura Mtoto wa Mama Muuza chapati. Nenda kamwambie Mama yangu kuwa bado naishi kwenye nyumba ya Mzee Mwinyimkuu, Mimi sijafa” alisema kwa kupaza sauti kali ambayo ilinifanya nishindwe kuhimili zile kelele, pale pale nilijikuta nikiishiwa nguvu na kupoteza fahamu. Kitu pekee kilichobakia kwenye akili yangu ni ,kumbukumbu juu ya yule Mama anayeishi nyumba jirani na Mzee Mwinyimkuu, Mama aliyekuwa akiniuzia Chapati

Ndiyo‼ yeye ni Mama Ashura, nakumbuka alinitajia jina hili lakini sikuwahi kumuuliza huyo Ashura yupo wapi, huyu Mtoto wa ajabu alijitambulisha kwangu kama Ashura na alinitaka nimwambie Mama yake kuwa anaishi ndani ya nyumba ya Mzee Mwinyimkuu.

***

Baba yangu aliendelea kuumwa, Mama alikua anamuuguza huku akinitafuta Mimi kwa simu lakini aliendelea kutonipata, zilipita wiki mbili bila kupata mawasiliano yoyote yale. Salehe hakupatikana, hata Mzee Mwinyimkuu hakupatikana, Kaka Hamidu naye ilikua kama ndiyo

kichocheo kipya cha hofu kwa Familia yangu. Mara ya mwisho aliwaeleza anakuja kuonana na Mimi lakini baada ya hapo hawakujua kilichomfika na kupelekea kutopatikana kwenye simu kwa wiki mbili.

Vikafanyika vikao vya kututafuta Mimi na Kaka Hamidu maana hawakujua naishi Rukwa sehemu gani na pia Kaka Hamidu alikutwa na nini. Ni Mimi pekee ndiye niliyekuwa najua Kua Kaka Hamidu alikua ameuawa.

Familia ikamtuma Mjomba wetu aliyeitwa Kambona, alikua Mtu mzima na mwenye busara zake.

Akasafiri kutoka Dar-es-salaam hadi Rukwa akiwa na picha yangu, akaanza kunitafuta bila mafanikio kwa zaidi ya siku kumi. Mwishowe akaenda kituo cha Polisi maana sasa hakuna aliyekua na amani bila kujua tupo wapi, wote waliamini wakinipata Mimi watajua mahali alipo Kaka Hamidu maana mara ya mwisho aliwaambia anakuja kwangu. Polisi wakaanza kunitafuta kila kona ya Rukwa lakini hakuna aliyeweza kujua niko wapi, lakini kupitia jina la Mwinyimkuu Ambalo Salehe alilitaja alipokua ananichumbia, ikawawezesha kufika hadi nyumbani kwa huyu Mzee.

Hapa ndipo mahali ambapo nilikuwepo kabla ya kuhamishwa, nyumba hii ndimo alimouawa Kaka Hamidu tena kikatili sana na Mzee Mwinyimkuu. Walipofika walimkuta tena wala hakuwa na wasiwasi kabisa, najua alitumia akili sana kunihamisha vinginevyo polisi wangenikuta mle

“Wewe ndiye Mwinyimkuu?” aliuliza polisi baada ya salamu fupi

“Mnasemaje?” aliwauliza, alikua haogopi chochote wala Mtu yeyote yule, jeuri na katili mno “Saida anaishi hapa?” akauliza Polisi mmoja.

“Yeye ni Nani?” akawauliza

“Unajibu kwa dharau kiasi hicho Mzee, Saida ni Mpwa wangu Mimi. Ameolewa na Kijana anaitwa Salehe, upelelezi umeonesha kuwa ni Kijana wako huyo Salehe halafu unauliza ni Nani?” akaingilia kati mjomba Kambona na kumshika shati Mzee Mwinyimkuu, Polisi wakaokoa

“Unanivunjia heshiam si ndiyo?” akauliza Mzee Mwinyimkuu kwa hasira

“Siyo heshima tu, ntaivunja hata hii nyumba kama hutonipatia Saida wangu” Mjomba Kambona hakupoa kabisa, alijawa na hasira sana.

“Huyo Salehe unamfahamu?” Polisi wakamuuliza Mjomba Kambona

“Ndiyo, nimeozesha mwenyewe. Picha si hii hapa ya ndoa” akatoa picha, ile picha akapewa Mzee Mwinyimkuu.

“Umemtambua mtajwa pichani?” akauliza Polisi mmoja, Mzee Mwinyimkuu akaangua kicheko kisha akaita kwa sauti

“Salehe, hebu njoo uone maajabu ya Dunia” akaitikia Mtu kutokea ndani na kuwafanya Polisi na Mjomba Kambona wakae mkao wa kula kumuona Salehe. Ikachukua kama sekunde kadhaa tu Kijana mmoja akatoka ndani, Kijana aliyekuja hakufanana na Salehe wa kwenye picha.

“Unamfahamu Saida?” akauliza Mzee Mwinyimkuu akimuuliza huyo Kijana aliyemtambulisha kama Salehe, kiukweli hakuwa yule Salehe aliyeniowa kabisa yaani sura tofauti.

“Hapana, kuna nini?” akauliza huyo Salehe, kiukweli Mjomba Kambona alinywea. Lakini Polisi mmoja akasema

“Ongozana na Mimi Kijana” akamshika mkono Salehe na kwenda naye nje. Lengo la Polisi ni kutaka utambuzi kwa Majirani maana Upelelezi wao uliwaambia Salehe wa kwemye picha anapatikana kwa Mzee Mwinyimkuu. Wakafika hadi nyumbani kwa Mama Ashura maana ndipo palikua na Watu nje

Walipomuona Yule Kijana akiwa na Polisi vijana walikimbia hadi yule Polisi akashangaa, hata Mama Ashura naye alikua anataka kukimbia ila Polisi akamzuia Mama Ashura na Kumwambia asikimbie ana maswali kadhaa anataka kumuuliza, ndipo Mama Ashura akabakia lakini kwa hofu sana

“Unamtambua nani pichani?” Yule Polisi akampa picha yule Mama, Mama Ashura akaipokea picha japo kwa wasiwasi lakini alipoiangalia ile picha alishtuka sana, akameza funda la mate.

“Hapana’’akajibu lakini kwa hofu sana kiasi kwamba yule polisi akahisi pengine kuna jambo analificha. Kilichomshtua Mama Ashura ni kuniona Mimi kwenye ile picha ya ndoa ambayo Mjomba Kambona aliwapatia polisi

“Na huyu Kijana hapa?” akauliza Polisi, Mama Ashura akamtazama yule Kijana. Akaachia tabasamu la hofu kisha akajibu

“Ni Salehe, anaishi pale” akaonesha na kidole kabisa. Majibu haya yakamuacha yule polisi kinywa wazi, basi akarudi hadi nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu. Hakuna ushahidi wa anachosema Mjomba Kambona. Lakini Mjomba akawaaambia

“Nina namba ya huyu Mzee alikua anawasiliana na Mama yake Saida, hii namba nimepewa na Mama Saida. Jina ni hilo la Mwinyimkuu” akasema Mjomba japo kwa sauti ya kupoa, ikabidi Polisi waipige ile namba.

Ikapokelewa na Mtu mwingine kabisa tena Mwanamke akimuuliza yule Polisi Nani wewe? Yalikua kama maigizo ya Filamu lakini lilikua tukio la kweli, nyakati zote hizo Mzee Mwinyimkuu alikua akitabasamu akiwa anamtazama Mjomba Kambona.

“Mnaona anavyo nitazama, huyu anajua kila kitu” akasema Mjomba lakini hakuwa na ushahidi, maneno yake yalikua ni sawa na kuupaka upepo rangi. Muda wote Mzee katili alikua akitabasamu kwa mpango fulani ulio kichwani pake

Polisi walikosa ushahidi, ikaonekana kuwa Mjomba Kambona aliyakosea maelezo yake. Kibaya zaidi hata picha aliyowaonesha Polisi kuwa ndiye aliyeniowa ilikanwa kwa kuoneshwa Salehe mwingine na kilichotia nguvu kukosekana ushahidi ni maneno ya Mama Ashura. Angefanyaje Mjomba wangu zaidi ya kutoa kitambaa na kujifuta jasho ila moyoni aliamini Mzee Mwinyimkuu alikua anajua wapi nilipo, pia hapakua na ushahidi mwingine sababu Mzee Mwinyimkuu hakuhudhuria ndoa yangu

Polisi wakamwambia Mjomba Kambona

“Tutaendelea na Uchunguzi, kwasasa wewe liachie jeshi la Polisi. Tutakupa taarifa ya Uchunguzi juu ya Saida pia huyo Kaka yake” haikua kauli yenye matumaini, ilimvunja moyo sana Mjomba Kambona. Akamwambia Mzee Mwinyimkuu

“Saida hawezi kutoweka kirahisi, lipo unalolijua. Siondoki Rukwa hadi nihakikishe nampata Mpwa wangu” alisema hivyo kisha aliongozana na Polisi kuondoka, Salehe feki na Mzee Mwinyimkuu wakatazamana kisha wakawa wanawatazama namna Polisi na Mjomba Kambona walivyokuwa wanaondoka.

Wala hawakufika mbali, kabla hata hawajapanda kwenye gari ya Polisi. Mjomba Kambona alianguka na kufariki papo hapo akitokwa na Mapovu mdomoni. Licha ya jitihada za jeshi la polisi kumkimbiza Hospitali lakini alikua tayari amefariki

Taarifa ikarudi Dar-es-salaam kuwa Mtu waliyemtuma kuja kututafuta Mimi na Kaka Hamidu alikua tayari ameshafariki. Yalikua ni majonzi juu ya Majonzi, taarifa hii ilipomfikia Baba yangu alifariki pia kwa presha. Bundi aliizingira familia yangu, misiba miwili ndani ya siku moja, Mzee Mwinyimkuu akashinda tena kwa kishindo kikubwa sana.

**

Nilihesabu siku ambazo nilikua ndani ya ile nyumba ya mateso, zilitimia siku saba ngumu. Nilikonda nikawa kama Mtoto mdogo, niliishiwa nguvu. Kilichokuwa kimebakia kwangu ilikua ni kufa tu. Kila nilipoamka nilijikuta nimeshaondolewa kidole kimoja, pumua yangu ikawa ya

shida sana. Nikakosa uwezo wa kuwatambua Watu kirahisi, yule Bodaboda aliendelea kuniletea chakula kila siku lakini pia sauti ya Mwanaume mmoja kugumia ilikua ni sauti ya Kila siku

Lilikua ni jambo la kawaida sana yeye kupaza sauti, sikuwahi kufahamu alikua akipitia mateso gani, ila dakika za mwisho niligundua kuwa naye alikua akipelekewa chakula na huyu huyu Bodaboda anayeniletea Mimi chakula.

Sikuweza kusimama tena, vidonda vilianza kutoa funza sababu sikuwa na dawa yoyote isitoshe joto la mle ndani liliniathiri kwa kiasi kikubwa, Mwenzenu niliwahi kufika Jehannam nikiwa Hai.

Basi siku moja yule Bodaboda alikuja, siku yenyewe palikua na mvua kubwa. Aliingia akiwa ameloa sana anatetemeka kwa Baridi, japo nilikua katika nyakati za mwisho kabisa za uhai wangu lakini niliweza kugundua kuwa Baridi lilikua tatizo kubwa kwake. Alikua akiniandalia chakula huku akitetemeka nikagundua anasumbuliwa na tatizo linalo sababishwa na Baridi.

Akajikaza, akaniwekea chakula. Alipaswa kunilisha sababu Mimi nilikua siwezi tena hata kushika kijiko, nilikonda mno hadi mishipa ya Damu ilikua ikionekana. Akajitahidi kuniinua ili kunikalisha kitako niweze kuegemea ukuta anilishe vizuri, siku hii nilipanga kuacha kula ili nife mapema maana mateso yalinizidi kabisa, Jamani naposema nilikonda basi ujue nilikonda nikawa na kilo chache sana halafu kichwa kikawa kikubwa.

Nilitamani kumuuliza ana shida gani, huyu Mtu hakuwahi kunitesa wala hakuwahi kunisemea jambo baya isipokua alikua hajibu maswali yangu yote niliyokuwa namuuliza.

Hali yake ilianza kuwa mbaya, akashindwa hata kunishikilia akaanguka chini na kuanza kugala gala kwa maumivu Makali sana, mlango ulikuwa wazi hakuufunga sababu alipoingia alikua tayari ana hiyo hali ya Maumivu, niliona ni nafasi ya kutoroka lakini sikuwa na akiba yoyote ya nguvu iliyobakia

Nikatamani kuendelea kuishi ghafla tu, namna pekee ya kuendelea kuwa hai ni kutoroka. Huko nje mvua ilikua ikinyesha na kusababisha kelele kubwa sana kwenye Bati. Sikuwa na nguvu ya kusimama, nikaona ni bora nijiburuze nione kama naweza kufika nje

Yule Bodaboda alipoona naanza kujiburuza akajua nataka kumtoroka, akili yake ikatamani anizuie lakini mwili ulimsaliti, nguvu zilimwisha akiwa sakafuni anapumua kwa shida sana. Nikaendelea kujivuta taratibu huku nikiwa ninasali Mungu niliyemkatia tamaa azidi kunipa nguvu, unajua kwanini niliamini naweza kuondoka pale?

Kwasababu hapakua na mtu mwingine aliyekuwa anakuja isipokua yeye, hivyo hakuna tena wa kunizuia, halafu niliwaza kufika chumba ambacho yule Mwanaume anagumia ili kama yeye ana nguvu tusaidiane kutoroka.

Nilijiburuza kama nyoka hadi nilipotoka nje ya chumba kile, palikua na funguo kwenye kitasa. Nikapata akili ya dharura kuwa huwenda funguo ile inaweza nisaidia kufungua milango mingine

maana ilikua na funguo tatu zilizowekwa sehemu moja, naipataje Funguo ni lazima nisimame niichomoe

Kivumbi kilianzia hapo, nilikonda Mimi kiasi kwamba upepo unaweza nipeperusha, Malaika Mtoa roho alikua amenisimamia akiniuliza nasimama au achukue roho yangu, sijui nguvu zilitoka wapi nikasimama kwa kuyumba huku nikitetemeka. Nikachomoa funguo, ile nataka kupiga hatua nikaanguka

Basi nikagugumia kwa maumivu, nilihitaji kufanya haraka maana kama yule Bodaboda atapata nguvu basi sitaweza tena kuondoka, nikamkumbuka Mama na Baba yangu, nikamkumbuka Kaka Hamidu. Ghafla nguvu zikaamka

Nikajikaza na kuanza kujiburuza sakafuni kama nyoka vile, kwa mwendo huo huo nilijikuta nikikiacha chumba kwa mbali kidogo, sikuufunga ule mlango wa chumba nilichomuacha Bodaboda.

Basi nilipofika kama chumba cha tano hivi nikasikia Mtu akiugonga mlango kwa nguvu huku akisema

“Njoo unitoe humu Mshenzi wewe, mtauwa wangapi. Siku ikifika mtakufa kama Kuku” alisema kwa hisia sana lakini hakujuwa kuwa Mimi nilikua tayari nipo mlangoni. Mlango ulikua umefungwa, korido lilikuwa refu halafu vyumba vilikua mbali mbali. Nilijitahidi sana kusimama nifungue mlango lakini nilikua nakosa nguvu, nilijaribu kama mara tatu lakini niliishia kuanguka

Wakati nikiwa nimeanguka nikageuka nyuma, ndipo nilipomuona yule Bodaboda akijikongoja kwa maumivu kuja nilipo, alikua amelishikilia tumbo lake. Hapo sasa yule Malaika mtoa roho nikamuona kama anachukua koleo kwa ajili ya kuichukua roho yangu.

Sauti ya yule Mwanaume ilizidi kusema, kibaya zaidi Mimi ndiye mwenye funguo halafu sauti yangu ilikua haitoki. Nikasema kama sisimami basi siondoki. Yule Bodaboda akawa anazidi kuja upande wangu kwa kasi akionekana kuanza kupiga hatua za nguvu. Nikamtaja Mungu nikasema

“Mungu nipe nguvu niishinde hii vita” nikajivuta haraka nikasimama nikiwa ninayumba, nikaanza kusaka tundu la kuweka funguo maana nguvu yenye ilikua sifuri, nikawa najitahidi huku nikiwa natetemeka. Mara naingiza mara nakosea, huku yule Bodaboda akizidi kunisogelea, hata nilipopaatia nilikua nimeingiza funguo isiyo yake.

Akawa karibu zaidi kiasi kwamba akipiga hatua tatu anakuwa amenifikia na kunizuia kuufungua mlango, nikapapasia kwa bahati nzuri nikapatia funguo nikavuta nguvu za mwisho nikatekenya kitasa lakini tayari Bodaboda alikua ameshanivaa na kuniangusha chini, Bahati nzuri ule mlango ulikua tayari umeshafunguka

Akatoka mwanaume mmoja na kuanza kumkita mateke yule Bodaboda hadi akamtupilia mbali huko akiwa hoi sana anatokwa na damu mdomoni, eneo la Korido lilikua linawaka taa isipokua

vyumbani tu. Sikuamini macho yangu Mtu ambaye nilikuja kumuona na kumtambua japo nilimuona mara moja tu

Alikua ni yule Mwanaume niliyemuazimaga simu kule Buchani, Ndio! Ni Abuu, masikini naye alikua mateka wa Mzee Mwinyimkuu baada ya kujulikana ananifuatilia Mimi, kwa muda mfupi naye alikua amepungua sana japo alikua na nguvu.

Hakuniuliza chochote zaidi ya kuninyanyua na kuweka mkono wangu kwapani kwake tukawa tunaelekea nje, mvua bado ilikua inanyesha. Tulipokua tunakaribia kutoka kabisa tukamuona Mtu anakuja Mbio, tena akikimbia kwenye mvua, ikatubidi tujifiche nyuma ya Mlango wa kutokea

Yule Mtu alipofika, breki ya kwanza ilikua vyumbani kisha akamrudia yule Bodaboda aliyekuwa anagala gala. Akamuuliza kwa hasira

“Umefanya nini Mpuuzi wewe?” aliuliza kwa sauti ambayo niliitambua, ilikua ni sauti ya Mzee Mwinyimkuu. Nilishtuka na kupata nguvu, nilipokumbuka kuwa yeye ndiye mtesi wangu basi mkojo ulinibana. Ghafla tu nikajiona ni Binadamu ninayehitaji kujitetea

“Nenda, hatuwezi kuondoka wote. Kaiambie Dunia kuhusu huyu Mzee, kama nitarudi tutakutana na kama nitafia hapa basi Roho yangu itakua salama” alisema Abuu, roho iliniuma. Sikua na uwezo wa kuzungumza. Mdomo wangu wa juu na chini nilihisi kama vimeungana sababu nilikua na vidonda mdomoni hivyo kukaa kimya ndiyo yalikua maisha yangu.

Nikaitikia kwa kutumia kichwa kisha nikasimama kama Mzimu, Mungu akaamua kunikumbuka. Akanipa nguvu na ujasiri, alichotaka Abuu ni kumzuia Mzee Mwinyimkuu. Wakati naanza safari Mzee Mwinyimkuu akaja mbio nahisi alikua anaanza kutusaka, sijui alijuaje kuwa tunatoroka. Huyu Mzee alikua Mchawi haswa, aliponikaribia tayari Abuu alimdaka Mzee Mwinyimkuu wakaanza kupalangana, muda huo nami nikaanza kujivuta kuondoka pale taratibu hadi nikaingia kwenye mvua.

Ulikua mchana lakini anga lilikua na wingu la kutosha kiasi kwamba palikua na giza fulani isitoshe palikua Porini. Nilipopigwa na mvua nikapata nguvu ya kuanza kuchanganya Miguu yangu vizuri. Nikaanza kukimbia huku nikiyumba kama mlevi

Sijui nilikimbia umbali gani lakini nilikimbia bila kuangalia nyuma, nilikimbia sana hadi nilichoka kabisa nikaanguka na kupoteza fahamu zangu.

Nilirudisha fahamu na kuanza kujitambua nikiwa naburuzwa kwa kasi sana, watu walikua kama vile wamenizunguka. Walikua na mavazi ya kufanana, nilikua kwenye kitanda kiendacho kwa kasi mno, nikawasikia wakisema

“Apelekwe ICU Haraka sana, kazi ianze mara moja” niligundua nilikua Hospitalini, wale wauguzi walionekana kunikatia tamaa sababu nilikua na hali mbaya sana. Lakini mimi

mwenyewe nilijiona ni mzima wa Afya zote, mahali nilipokuwepo palikua ni hatari zaidi ya Kuzimu.

Chozi lilinibubujika nikafumba macho yangu huku nikimshukuru Mungu. Madaktari walifanya kazi yao kwa wiki tatu kuhakikisha najitambua zaidi, wakaniweka kwenye uangalizi maalum kwa kipindi chote hicho hadi nilipokumbuka yaliyonisibu.

Nikawaandikia jina Langu, mahali nilipotoka maana nilikua siwezi kuzungumza tena, Hospitali ikasambaza jina na taarifa zangu ndipo Mama yangu alipokuja Mbeya akiongozana na Ndugu wengine kunitambua. Mama alilia sana, sikuwahi kumuona Mama yangu akilia namna ile, yale Maisha yaliniathiri sana kisaikolojia. Nikapoteza uwezo wa kuzungumza kabisa. Taarifa ya Kifo cha Baba ilinihuzunisha mno, ikanitoa chozi.

Polisi walipokuja niliandika maelezo yangu, ilikua baada ya wiki sita. Mwezi mmoja na siku kadhaa, afya yangu ilianza kukaa sawa lakini sikuwa na Uwezo wa kuzungumza chochote isipokua kuandika. Polisi walinichukua ili nikawapeleke mahali nilipoteswa yaani nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu

Mimi na Mama tulienda, palikua ni pale pale kwa Mzee Mwinyimkuu. Namba ya nyumba ilikua ni ile ile, mazingira yale yale, chozi lilinibubujika sana hadi Mama akashindwa kujizuia.

Nilikua natembezwa kwenye kiti cha Walemavu maana bado miguu ilikua haipo sawa pia sikua na vidole nilikua najiuguza. Nikampa ishara Mama yangu kuwa anipeleke kwanza nyumba jirani, pale kwa muuza chapati, nilimkuta Mwanamke mwingine kabisa akitengeneza chapati, nikaandika kwenye karatasi

“Mama Ashura yupo wapi?” nilikua na ujumbe wa Mtoto wake Ashura nilitaka kwanza nimpe ujumbe, wakati huo polisi walikua wameizingira nyumba ya Mzee Mwinyimkuu. Mama akamsomea yule Mwanamke, lakini cha ajabu eti akadai yeye ndiye Mama Ashura, nilishtuka alafu kingine kilichonipa mshituko ni kumuona Ashura mwenyewe, alikua ni Ashura yule yule niliyemuona Nyumbani kwa Mzee Mwinyimkuu

Haya mambo yalinifanya nianze kuonekana akili yangu bado haiko sawa, nikajitahidi kuwaambia kwa maandishi lakini niliishia kupewa pole tu, kisha nikapelekwa kwa Mzee Mwinyimkuu. Nako nikakutana na stori mpya kabisa

Kwanza ile nyumba si ya Mzee Mwinyimkuu, hawamfahamu. Wao wanaishi hapo Kwa Miaka mingi, nilitokwa na Mchozi, nyumba ile ile mazingira yale yale lakini stori tofauti. Nikaomba niingizwe ndani, nikapelekwa kwenye chumba nilichokuwa nalala

Nikakuta magunia ya vyakula, tena kilikua chumba chenye makorokoro mengi sana na hakikuonekana kua chumba cha kulala Mtu. Mama akaniambia

“Saida, najua umeteseka sana huku lakini hukumbuki chochote tena. Siku ukikumbuka nakuahidi tutarudi, yule Kijana na Baba yake watalipa” Kauli ya Mama yangu ilinimaliza akili yangu,

nilifikia hatua nikakubali kuwa akili yangu haipo sawa, inawezekanaje kila kitu kibadilike kwa haraka vile. Hakuna aliyeniamini

Lakini sasa wakati natoka nikajikuta nikipeleka macho yangu jikoni, nikaiona ile sufuria kubwa ambayo kwa mara ya kwanza nilipika mchicha mwingi, nikashtuka alafu nikauona Mchicha mwingi ukiwa kwenye Beseni. Kilichonishtua ni kwamba nilimuona Msichana wa umri wangu akiutengeneza.

Nilijikuta nikipiga yowe kali sana. Hali ya afya yangu ikawa sio nzuri nikarudishwa tena Hospitali. Tokea siku ile nilikua Msichana ninayekaa kimya hadi leo hii nawasimulia hiki kisa, sikumpata Mzee MwinyiMkuu wala Salehe, lakini sitakubali. Siku moja nitarudi Rukwa ili walipe kwa maumivu na mateso makali ninayoyapitia hadi sasa.

Kwasasa nimerudishwa kwetu Dar-es-salaam, niko Magomeni. Maisha yangu yamekuwa ya Ukimya sana, Sijazungumza tena tokea siku ile nilipozungumza kwa mara ya mwisho Rukwa, sijaandika chochote na wala sitaki kusema chochote kile ila kupitia mkasa huu nataka ujifunze.

Kamwe kwenye Maisha yako usiolewe au kuowa Mtu usiye mfahamu, Dunia ni Kichaka cha Mateso. Wasichana wengi wanayapitia mateso niliyoyapitia, wengi wanauawa, wengi wanapata ugonjwa wa akili. Hata wanaume wapo waliopoteza kila kitu, Siku nikifungua kinywa changu nitawasimulia mengi, kwasasa naishia hapa, naweka kalamu yangu chini.

AHSANTE……….MWISHO
 
Back
Top Bottom