Hayo ni maneno ya YESU kweli?
MBONA NI MANENO YA YESU YANAYO JULIKANA KABISA AU UNAOGOPA KUWA YANAWAPA POINT 12 WALE TEAM KATAA NDOA 😁😁😁😁 na ndiyo maana yesu akuoa wala kuwa na mwanamke ...huyo tunaye bishana naye anayajua hayo maana Aya kaposti mwenyewe ambayo Yesu aliongelea ndoa na kusema kiasili toka mwanzo mungu alisema mke mmoja na mume mmoja maana Mungu alisema alisema 👉 mtu na atamwacha babaye na manage na kuambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja hata si wawili tena bali mwili mmoja.
Ngoja nikukopie ile Aya yote maana nilisha post huko nyuma .
HAYA SOMA MATAYO
Mathayo 19
3. Basi Mafarisayo wakamwendea, Yesu wakamjaribu, wakimwambia, Je! Ni halali mtu kumwacha mkewe kwa kila sababu?
4. Akajibu, akawaambia, Hamkusoma ya kwamba yeye aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke,
5. akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja?
6. Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.
7. Wakamwambia, Jinsi gani basi Musa aliamuru kumpa hati ya talaka, na kumwacha?
8. Akawaambia, Musa, kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu, aliwapa ruhusa kuwaacha wake zenu; lakini tangu mwanzo haikuwa hivi.
9. Nami nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa ni kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini; naye amwoaye yule aliyeachwa azini.
10. Wanafunzi wake wakamwambia, Mambo ya mtu na mkewe yakiwa hivyo, haifai kuoa.
11. Lakini yeye akawaambia, Si wote wawezao kulipokea neno hili, ila wale waliojaliwa.
12. Maana wako matowashi waliozaliwa hali hiyo toka matumboni mwa mama zao; tena wako matowashi waliofanywa na watu kuwa matowashi; tena wako matowashi waliojifanya kuwa matowashi kwa ajili ya ufalme wa mbinguni. Awezaye kulipokea neno hili, na alipokee.