Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Synthesizer

Platinum Member
Joined
Feb 15, 2010
Posts
15,415
Reaction score
29,584
Tanzania inaonekana hatuna sera ya mambo ya nje, tupo tupo tu. Lakini hata hivyo, kauli za Bashe kwa Malawi juu ya Malawi kuzuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio ya kiungwana, na haiakisi -Utanzania tulio nao.

Tukio liko hivi, katika kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni na kukuza kilimo ndani ya nchi, Malawi imepiga marufuku uingizaji wa bidhaa za kilimo ambazo zinaweza kuzalishwa Malawi. Bidhaa hizi ni pamoja na mchele, unga, tangawizi, maji ya kunywa ya chupa, nk, ambavyo vingi vinatoka Tanzania.

Bashe, waziri wa Kilimo, amewajibu Malawi kwamba kwa kuwa wamefanya hivyo basi na Tanzania inazuia bidhaa zote za kilimo toka Malawi kuingia Tanzania.

Sasa kama Bashe angeishia hapo isingekuwa Tatizo, kwa kuwa angeweza kusema ni reciprocal arrangement, na sie tunalinda bidhaa za ndani na kukuza kilimo ndani ya nchi. Hata hivo lazima utumie busara, ili usiumize wananchi kwa mihemuko ya kulipiza kisasi

Lakini Bashe kaenda mbali zaidi, akasema,

2.Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.

3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.

Sasa najiuliza
  1. Suala la Malawi kupitisha Mazao yake bandari ya Dar es Salaam kwenda nje linahusiana nini na wao kusema wanazuia kuagiza bidhaa za kilimo toka nje? Huku si kukomoana tu kwa makusudi?
  2. Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, kwa nini? Mbolea inasafirishwa kwenda Malawi kama wanavyosafirisha bidhaa nyingine kwa kutumia bandari ya Tanzania, ambayo sisi tunataka waitumie kwa sababu ni huduma wanalipia. Sasa leo tunawakomoa Malawi kuwanyima matumizi ya bandari kwa sababu tu wanataka ku-promote uzalishaji wa kilimo ndani ya nchi yao?
Ikumbukwe kwamba, Malawi imezuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio tu toka Tanzania, bali kwa nchi zote kutia ndani South Afrika, Zimbabwe nk. Sasa kwa nini tunawaingilia? Kwa mfano, sisi Tanzania tunaruhusu uingizaji wa maji ya kunywa ya chupa? Kama hapana, kwa nini?

Sasa unafanyaje uamuzi kwa Malawi, kwamba kama hununui mchele wetu wa Mbeya, basi ukiagiza mbolea toka nje usipitishe kwenye bandari yetu. Ni akili hiyo ya kiwango cha waziri?

Tunaposema Tanzania ina sera ya Ujamaa na Kujitegemea -japo sijui kama bado ipo - kujitegemea tuna maanisha nini? Tunawaadhibu Malawi kutimia bandari yetu kwa sababu wanataka kujitegemea katika bidhaa za kilimo? Mbona hata sisi Tanzania kuna wakati, ili kukuza sekta fulani fulani, tunadhibiti uingizaji wa bidhaa fulani toka nje, kwa iwe nongwa kwa Wamalawi?

Kwanza haya matamshi ya Bashe sio mambo ya wizara yake; wanaohusika ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Mambo ya Nje, sasa kimbelembele cha nini, kumshawishi Raisi Samia kwamba yeye ni tough guy?

Mimi naona katika hili Bashe amekosa busara kabisa - ame-overreact. Raisi Samia awaombe msamaha Malawi kwa kauli hizi za Bashe. Labda pia maamuzi haya ya Bashe yatakuwa na baraka za Raisi Samia. Kama ni hivyo, hivi tuseme Tanzania tumekaa tukatafakari tukaona msimamo kama huu ni wa hekima kweli? Niiteni mhaini, lakini kuna maamuzi mengine mnafanya kama viongozi yatatutia aibu.

Tanzania hatupaswi kutumia blackmail katika negotiations, only primitive and uncultured people will resort to that. Tunatakiwa tutumie reciprocation.
 
Malawi hajazuia bidhaa hizi kutoka Tanzania peke yake, bali kutoka nchi zote

In exercise of his powers conferred by regulation 3(1)(a) of the Control of Goods (Import and Export) (Commerce) Regulations
  • Made by Minister of Trade & Industry, Vitumbiko Mumba on March 13, 2025 to expire on March 12, 2027
  • Any person who contravenes provision of the Order commits an offence and shall be liable to penalties upon conviction

By Duncan Mlanjira
Under powers conferred by regulation 3 (1) (a) of the Control of Goods (Import and Export) (Commerce) Regulations, Minister of Trade & Industry, Vitumbiko Mumba rolled out a new Order on Thursday, March 13, banning the importation of foods and other goods that are locally produced in Malawi.

With immediate effect until March 12, 2027 when the Order shall expire, the prohibited imported food items are maize flour; rice; meat products (sausages, bacon and cold meats); fruits & vegetables (except those that do not grow in Malawi); Irish potatoes; fresh milk.

Other food items are onions; garlic; ginger; peanut butter; honey; popcorn, table eggs and bottled water.

The imported goods banned are toothpicks; matches; plastic utensils; wooden furniture; mops and security boots.

Any person who contravenes the provision of the Control of Goods (Import and Export)(Commerce) Regulations Order, 2025 shall, upon conviction, be liable to penalties specified under Section 14 of the Act.

Malawians have a huge penchant for imported goods despite the call for Best Buy Malawian campaign that was suggested many years ago during the single party era of the Malawi Congress Party under former President, late Hastings Kamuzu Banda.

Then the campaign was to empower Malawian entrepreneurs to be innovative by locally producing goods for the market as a substitute to imported goods, which also strain the availability of forex as well a job and wealth creation.
 
Ukishangaa ya Trump shangaa ya CCM na upumbavu wao.
Dunia ilipofika sasa watu wanataka kubadilika sio juice ya embe dodo ikatokea saudia jangwani wakati kuna ngamia sio kitimoto.
IMG_1165.jpeg
 
Ukishangaa ya Trump shangaa ya CCM na upumbavu wao.
Dunia ilipofika sasa watu wanataka kubadilika sio juice ya embe dodo ikatokea saudia jangwani wakati kuna ngamia sio kitimoto.
Bashe anataka kujifanya Trump wa Tanzania, lakini kama akili ya serikali ya Raisi Samia ndio hii na ndio inayotoa maamuzi kama mikataba ya bandari, basi Tanzania ni nchi ya kuhurumiwa sana
 
Tanzania inaonekana hatuna sera ya mambo ya nje, tupo tupo tu. Lakini hata hivyo, kauli za Bashe kwa Malawi juu ya Malawi kuzuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio ya kiungwana, na haiakisi -Utanzania tulio nao.

Tukio liko hivi, katika kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni na kukuza kilimo ndani ya nchi, Malawi imepiga marufuku uingizaji wa bidhaa za kilimo ambazo zinaweza kuzalishwa Malawi. Bidhaa hizi ni pamoja na mchele, unga, tangawizi, maji ya kunywa ya chupa, nk, ambavyo vingi vinatoka Tanzania.

Bashe, waziri wa Kilimo, amewajibu Malawi kwamba kwa kuwa wamefanya hivyo basi na Tanzania inazuia bidhaa zote za kilimo toka Malawi kuingia Tanzania.

Sasa kama Bashe angeishia hapo isingekuwa Tatizo, kwa kuwa angeweza kusema ni reciprocal arrangement, na sie tunalinda bidhaa za ndani na kukuza kilimo ndani ya nchi. Hata hivo lazima utumie busara, ili usiumize wananchi kwa mihemuko ya kulipiza kisasi

Lakini Bashe kaenda mbali zaidi, akasema,

2.Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.

3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.

Sasa najiuliza
  1. Suala la Malawi kupitisha Mazao yake bandari ya Dar es Salaam kwenda nje linahusiana nini na wao kusema wanazuia kuagiza bidhaa za kilimo toka nje? Huku si kukomoana tu kwa makusudi?
  2. Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, kwa nini? Mbolea inasafirishwa kwenda Malawi kama wanavyosafirisha bidhaa nyingine kwa kutumia bandari ya Tanzania, ambayo sisi tunataka waitumie kwa sababu ni huduma wanalipia. Sasa leo tunawakomoa Malawi kuwanyima matumizi ya bandari kwa sababu tu wanataka ku-promote uzalishaji wa kilimo ndani ya nchi yao?
Ikumbukwe kwamba, Malawi imezuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio tu toka Tanzania, bali kwa nchi zote kutia ndani South Afrika, Zimbabwe nk. Sasa kwa nini tunawaingilia? Kwa mfano, sisi Tanzania tunaruhusu uingizaji wa maji ya kunywa ya chupa? Kama hapana, kwa nini?

Sasa unafanyaje uamuzi kwa Malawi, kwamba kama hununui mchele wetu wa Mbeya, basi ukiagiza mbolea toka nje usipitishe kwenye bandari yetu. Ni akili hiyo ya kiwango cha waziri?

Tunaposema Tanzania ina sera ya Ujamaa na Kujitegemea -japo sijui kama bado ipo - kuitegemea tuna maanisha nini? Tunawaadhibu Malawi kutimia bandari yetu kwa sababu wanataka kujitegemea katika bidhaa za kilimo? Mbona hata sisi Tanzania kuna wakati, ili kukuza sekta fulani fulani, tunadhibiti uingizaji wa bidhaa fulani toka nje, kwa iwe nongwa kwa Wamalawi?

Mimi naona katika hili Bashe amekosa busara kabisa - ame-overreact. Raisi Samia awaombe msamaha Malawi kwa kauli hizi za Bashe. Labda pia maamuzi haya ya Bashe yatakuwa na baraka za Raisi Samia. Kama ni hivyo, hivi tuseme Tanzania tumekaa tukatafakari tukaona msimamo kama huu ni wa hekima kweli? Niiteni mhaini, lakini kuna maamuzi mengine mnafanya kama viongozi yatatutia aibu.
Bashe amesahau kuongea na Mama

1.Tuwafukuze hawa Wamalawi wote waliojaa hapa kwetu.

2.Piga marufuku gari zote za Malawi zisikanyage ardhi yetu.
 
Mwalimu Nyerere hakua mjinga Tanzania kuwa na chuo cha Magogoni katika lengo lake la awali. Chuo cha uongozi.
Matokeo yake ni pamoja na haya
Samia akiniteua mie waziri wa Kilimo nitakuwa bora zaidi ya Bashe x 100! Nikiwa kama raisi wa Tanzania siwezi kuvumilia akili kama hizi kuwa waziri wangu. Kwanza alipaswa angalau awasiliane na Waziri wa Mambo ya Nje, au Viwanda na Biashara kabla ya kuongea mbofumbofu hizi. Hapa anaingilia uwanja wa hawa mawaziri, yeye sio waziri wa mambo aliyoyatolea tamko
 
Kwa kweli kakurupuka vibaya. Wakae chini waweke sawa. Malawi kuingiza mbolea kupitia bandari yetu na kusafirisha mazao kupitia kwetu ni faida kwetu. Bashe anajipiga risasi ya mguu. Watahamia Beira mazima.
 
Back
Top Bottom