Tanzania inaonekana hatuna sera ya mambo ya nje, tupo tupo tu. Lakini hata hivyo, kauli za Bashe kwa Malawi juu ya Malawi kuzuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio ya kiungwana, na haiakisi -Utanzania tulio nao.
Tukio liko hivi, katika kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni na kukuza kilimo ndani ya nchi, Malawi imepiga marufuku uingizaji wa bidhaa za kilimo ambazo zinaweza kuzalishwa Malawi. Bidhaa hizi ni pamoja na mchele, unga, tangawizi, maji ya kunywa ya chupa, nk, ambavyo vingi vinatoka Tanzania.
Bashe, waziri wa Kilimo, amewajibu Malawi kwamba kwa kuwa wamefanya hivyo basi na Tanzania inazuia bidhaa zote za kilimo toka Malawi kuingia Tanzania.
Sasa kama Bashe angeishia hapo isingekuwa Tatizo, kwa kuwa angeweza kusema ni reciprocal arrangement, na sie tunalinda bidhaa za ndani na kukuza kilimo ndani ya nchi. Hata hivo lazima utumie busara, ili usiumize wananchi kwa mihemuko ya kulipiza kisasi
Lakini Bashe kaenda mbali zaidi, akasema,
2.Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.
3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.Kwa
Sasa najiuliza
- Suala la Malawi kupitisha Mazao yake bandari ya Dar es Salaam kwenda nje linahusiana nini na wao kusema wanazuia kuagiza bidhaa za kilimo toka nje? Huku si kukomoana tu kwa makusudi?
- Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, kwa nini? Mbolea inasafirishwa kwenda Malawi kama wanavyosafirisha bidhaa nyingine kwa kutumia bandari ya Tanzania, ambayo sisi tunataka waitumie kwa sababu ni huduma wanalipia. Sasa leo tunawakomoa Malawi kuwanyima matumizi ya bandari kwa sababu tu wanataka ku-promote uzalishaji wa kilimo ndani ya nchi yao?
Ikumbukwe kwamba, Malawi imezuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio tu toka Tanzania, bali kwa nchi zote kutia ndani South Afrika, Zimbabwe nk. Sasa kwa nini tunawaingilia? Kwa mfano, sisi Tanzania tunaruhusu uingizaji wa maji ya kunywa ya chupa? Kama hapana, kwa nini?
Sasa unafanyaje uamuzi kwa Malawi, kwamba kama hununui mchele wetu wa Mbeya, basi ukiagiza mbolea toka nje usipitishe kwenye bandari yetu. Ni akili hiyo ya kiwango cha waziri?
Tunaposema Tanzania ina sera ya Ujamaa na Kujitegemea -japo sijui kama bado ipo - kuitegemea tuna maanisha nini? Tunawaadhibu Malawi kutimia bandari yetu kwa sababu wanataka kujitegemea katika bidhaa za kilimo? Mbona hata sisi Tanzania kuna wakati, ili kukuza sekta fulani fulani, tunadhibiti uingizaji wa bidhaa fulani toka nje, kwa iwe nongwa kwa Wamalawi?
Kwanza haya matamshi ya Bashe sio mambo ya wizara yake; wanaohusika ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Mambo ya Nje, sasa kimbelembele cha nini, kumshawishi Raisi Samia kwamba yeye ni tough guy?
Mimi naona katika hili Bashe amekosa busara kabisa - ame-overreact. Raisi Samia awaombe msamaha Malawi kwa kauli hizi za Bashe. Labda pia maamuzi haya ya Bashe yatakuwa na baraka za Raisi Samia. Kama ni hivyo, hivi tuseme Tanzania tumekaa tukatafakari tukaona msimamo kama huu ni wa hekima kweli? Niiteni mhaini, lakini kuna maamuzi mengine mnafanya kama viongozi yatatutia aibu.