Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

Mimi ni Mtanzania, lakini kwa huu msimamo wa Bashe kwa Malawi huu sio uungwana wala ujirani mwema

KUna watu humu kwa akili waliyonawo kuelewa hili hadi mwisho wa dunia uje, kwa sababu hawawezi kuona mbali zaidi ya mwisho wa pua zao.

Bashe kavunja sana uaminifu wa Tanzania kwa Malawi, na si Malawi tu, kwa nchi zote zinazotegemea bandari zetu. Kutumia bandari kama fimbo ni jambo la kijinga ambalo Tanzania inaweza kutumia. Kumbuka kwamba, japo Zambia waliwapinga Makaburu, bado walitumia bandari yao. Kaburu alipoanza kiutumia kama fimbo ndicho kilichozaa TAZARA.

Siku Malawi wakipata pesa basi kutakuwa na mradi wa reli kwenda Msumbiji ili waachane na bandari ya Tanzania. Malawi hawatakaa wasahau ujinga huu wa Bashe.
Nimekumbuka tulipokuwa watoto tukicheza soka mtaani. Kulikuwa na mtoto mmoja wa kishua ambaye alikuwa ana mipira mingi mizuri.

Watoto wengi walijumuika kutoka mitaa ya mbali kuja uwanjani ambao ndio ulikuwa uwanja mzuri pia kufuata mipira. Tulikuwa tukitumia mipira ya makaratasi ya kufumwa kuanza kucheza ila ikifika saa kumi na Moja jioni dogo wa kishua anamaliza ratiba ya kulala mchana na anakuja uwanjani na mpira wake, kwa hiyo tutaacha kucheza mpira wa makaratasi na kushobokea mpira mzuri wa yule dogo.

Tatizo la huyo dogo alikuwa ana nyodo sana kwa hiyo yeye ndiye alikuwa akipanga timu na wakati mwingine anaweza kuamua fulani acheze na fulani asicheze na wakati mwingine anaweza akachukua mpira wake na kuondoka katikati ya game kwa sababu za kijinga tu kama kufanyiwa faulu n.k..

Siku moja tukaona this is too much lazima tumfundishe adabu na nidhamu dogo. Tukajengana kisaikolojia na wenzangu wa kitaa na kuwaambia kama dogo akija na mpira wake hakuna kumshobokea na tutaendelea kucheza mpira wetu wa kienyeji.

Aisee siku ya siku dogo kaja uwanjani akakuta tupo bize na soka letu, ilikuwa akifika tunavunja timu tunapanga upya ila siku ile hatukufanya hivyo tukiendelea kucheza kwa furaha mpira wetu. Dogo hakuamini alikaa nje na mpira wake hakuna aliyemshobokea.

Siku zilizofuata tuliendelea na utaratibu wetu ule ule na tulikomaa kweli kweli. Baadae dogo alijiongeza akaomba msamaha na toka siku hiyo tukakubaliana kama anataka kucheza na sisi basi asituwekee masharti ya mpira wake na awe mpole. Baadae dogo akabadilika akawa mnyenyekevu na maisha yakaendelea.

Nime reflect back kwa kilichotutokea tukiwa watoto na hatua alizochukua Bashe dhidi ya Malawi.
 
Kuna watu wana uwezo wa kufikiri na tofauti na wanaosema ni pinga pinga tu hapa. Usiwe mtu wa kusukumwa tu katika maisha yako - sycophant. Ukiambiwa tunauza bandari sawaaa! Tunagawa maliasili - sawaaa! Tunapunguza kikokotoo - sawaaa! Hatubadili utaratibu wa uchaguzi - sawaaa! Tunaleta kodi za miamala - sawaaa! Tunanunua umeme toka Ethiopia hauna losses kama wa kwetu unaotoka mbali kusini - sawaaa! Tunanunua drealiner japo hatuna business plan ya Air Tanzania - sawaa! Mkurugenzi Tanesco amekufa kwa aksident wakikwepa baiskeli saa nane usiku - sawaaa! Wewe ni mtu kweli, au msukule wa Kisukuma?
Crap

Hii ni trade war and the one who blinks…. Loses it

Bashe has widen the scope na hapo ndipo ushindi ulipo

Hii si mara ya kwanza
 
Wabongo banaa kwa unafiki tu, sasa mlitaka Bashe afanyaje acheke tu huku akiwaomba Malawi watuhurumie?? Hii inaitwa jino kwa jino ,ukimwaga ugali na mimi namwaga mboga ndio China alivyomfanyia Trump sasa hivi anahaha tu.
Mh. Bashe yupo sawa 100% abane hapo hapo hadi Malawi waombe poooh waje mezani wayajadili, Yanaongeleka hayo.
 
Bashe ni mpuuzi sana aisee.
Sikutegemea hayo yatoke kwake.
Baada ya uzushi wenu kuwa anaumwa saaana kubuma, mmekuja na ujinga mwingine Sasa. Nyumbu wengi mmekimbilia tu Uzi bila kuelewa lolote kwa undani. Hii minyumbu hii mipumbavu sana, natamani JPM angelikwepo.....angekuwa ameshavifutilia mbali hivi vipumbavu viovu.
 
Crap

Hii ni trade war and the one who blinks…. Loses it

Bashe has widen the scope na hapo ndipo ushindi ulipo

Hii si mara ya kwanza
You really think Malawi will change their policy position because of Bashe's stance? If that happens nidai
 
Tanzania inaonekana hatuna sera ya mambo ya nje, tupo tupo tu. Lakini hata hivyo, kauli za Bashe kwa Malawi juu ya Malawi kuzuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio ya kiungwana, na haiakisi -Utanzania tulio nao.

Tukio liko hivi, katika kudhibiti matumizi ya fedha za kigeni na kukuza kilimo ndani ya nchi, Malawi imepiga marufuku uingizaji wa bidhaa za kilimo ambazo zinaweza kuzalishwa Malawi. Bidhaa hizi ni pamoja na mchele, unga, tangawizi, maji ya kunywa ya chupa, nk, ambavyo vingi vinatoka Tanzania.

Bashe, waziri wa Kilimo, amewajibu Malawi kwamba kwa kuwa wamefanya hivyo basi na Tanzania inazuia bidhaa zote za kilimo toka Malawi kuingia Tanzania.

Sasa kama Bashe angeishia hapo isingekuwa Tatizo, kwa kuwa angeweza kusema ni reciprocal arrangement, na sie tunalinda bidhaa za ndani na kukuza kilimo ndani ya nchi. Hata hivo lazima utumie busara, ili usiumize wananchi kwa mihemuko ya kulipiza kisasi

Lakini Bashe kaenda mbali zaidi, akasema,

2.Mizigo ya bidhaa za kilimo kutoka Malawi na Afrika Kusini haitaruhusiwa kupita ndani ya mipaka ya Tanzania, kuelekea bandari ya Dar es Salaam au nchi nyingine yoyote, hadi zuio hilo litakapoondolewa.

3.Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, ikiwa ni sehemu ya hatua za kulinda maslahi ya wakulima na wafanyabiashara wa Kitanzania.

Sasa najiuliza
  1. Suala la Malawi kupitisha Mazao yake bandari ya Dar es Salaam kwenda nje linahusiana nini na wao kusema wanazuia kuagiza bidhaa za kilimo toka nje? Huku si kukomoana tu kwa makusudi?
  2. Usafirishaji wa mbolea kwenda Malawi utasitishwa, kwa nini? Mbolea inasafirishwa kwenda Malawi kama wanavyosafirisha bidhaa nyingine kwa kutumia bandari ya Tanzania, ambayo sisi tunataka waitumie kwa sababu ni huduma wanalipia. Sasa leo tunawakomoa Malawi kuwanyima matumizi ya bandari kwa sababu tu wanataka ku-promote uzalishaji wa kilimo ndani ya nchi yao?
Ikumbukwe kwamba, Malawi imezuia uingizaji wa bidhaa za kilimo sio tu toka Tanzania, bali kwa nchi zote kutia ndani South Afrika, Zimbabwe nk. Sasa kwa nini tunawaingilia? Kwa mfano, sisi Tanzania tunaruhusu uingizaji wa maji ya kunywa ya chupa? Kama hapana, kwa nini?

Sasa unafanyaje uamuzi kwa Malawi, kwamba kama hununui mchele wetu wa Mbeya, basi ukiagiza mbolea toka nje usipitishe kwenye bandari yetu. Ni akili hiyo ya kiwango cha waziri?

Tunaposema Tanzania ina sera ya Ujamaa na Kujitegemea -japo sijui kama bado ipo - kuitegemea tuna maanisha nini? Tunawaadhibu Malawi kutimia bandari yetu kwa sababu wanataka kujitegemea katika bidhaa za kilimo? Mbona hata sisi Tanzania kuna wakati, ili kukuza sekta fulani fulani, tunadhibiti uingizaji wa bidhaa fulani toka nje, kwa iwe nongwa kwa Wamalawi?

Kwanza haya matamshi ya Bashe sio mambo ya wizara yake; wanaohusika ni Waziri wa Viwanda na Biashara na Waziri wa Mambo ya Nje, sasa kimbelembele cha nini, kumshawishi Raisi Samia kwamba yeye ni tough guy?

Mimi naona katika hili Bashe amekosa busara kabisa - ame-overreact. Raisi Samia awaombe msamaha Malawi kwa kauli hizi za Bashe. Labda pia maamuzi haya ya Bashe yatakuwa na baraka za Raisi Samia. Kama ni hivyo, hivi tuseme Tanzania tumekaa tukatafakari tukaona msimamo kama huu ni wa hekima kweli? Niiteni mhaini, lakini kuna maamuzi mengine mnafanya kama viongozi yatatutia aibu.
pengine kuna nafuu fulani tanzania tumewapa malawi bandarini, ila wao hawatambui mchango wetu.
 
You really think Malawi will change their policy position because of Bashe's stance? If that happens nidai
If they didn't change their policy, who cares?? Bashe abane hapo hapo mpaka waje mezani. Moja ya mambo ambayo Nyerere alikosea ni hili la ujamaa na kuwatia upole wabongo, uwa hata wakionewa wanacheka cheka tu hawajui kua kuna kipindi lazima wawe ngangari . Hongera sana Waziri Bashe hivi ndio inatakiwa kufanywa ili tuheshimiane huko mbele.
 
Binafsi Mimi naona Bashe Yuko sawa
Haiwezekani Malawi anufaike na rasimali zetu kama bandari, miundo mbinu na soko halafu sisi atunyime soko la bidhaa na njia za kusafirisha bidhaa za TANZANIA kwenda kusaini mwa Africa
Huyo tunakufa nae kila mtu abakinna chake
 
pengine kuna nafuu fulani tanzania tumewapa malawi bandarini, ila wao hawatambui mchango wetu.
Ipo,lakini ni katika kuwavutia watumie bandari yetu. Kumbuk sio lazima watumie bandari yetu. Malawi wanahitaji mkakati mdogo sana kujitoa kutumia bandari ya Dar es Salaam. Wanaweza hata kuamua mradi wa kimkakati wa kujenga barabara kuu kutoka Blantyre hadi Beira Mozambique, ambapo ni karibu sana ukilinganisha na kuja Dar. Wanasema tatizo ni rebels eneo hili. Wanaweza hata kuwa na joint military operation na Mozambique ili kuwasafisha rebels eneo hili.

Kama tuliweka mkakati wa TAZARA ili kuwapa Zambia access ya bandari ya Dar, unafikiri Malawi watashindwa mradi wa kimkakati wa kujipa access ya bandari za Mozambique? Infact wanaweza kumshukuru Bashe kwa kuwaamsha. Angalia ramani hapo chini

1744898045731.png
 
Binafsi Mimi naona Bashe Yuko sawa
Haiwezekani Malawi anufaike na rasimali zetu kama bandari, miundo mbinu na soko halafu sisi atunyime soko la bidhaa na njia za kusafirisha bidhaa za TANZANIA kwenda kusaini mwa Africa
Huyo tunakufa nae kila mtu abakinna chake
Ndio nasema, ni watu wasioona mbali ndio wana mawazo kama hayo, ya ki-Trump. Kwa nini uwazuie katika mikakati yao ya kujitegemea kwa chakula? Mbona tunamshangilia Traole anaposema anataka Burkina Faso ijitegemee kwa chakula, na tunalaani Malawi wakichukua hatua hizo na kuwanyima access ya bandari yetu ili waendelee kututegemea kwa chakula? Sisi ni wanafiki sana basi. Traole safi sana, Malawi hapana, na tunaimba nyimbo za kujitegemea kwa chakula, eeeh!
 
Back
Top Bottom