Nimesikia Rais wetu Mhe Kikwete akisema akisema, serikali haitaanzisha Mahakama ya Kadhi na kwamba ni Jukumu la waislamu wenyewe kuianzisha na kuihudimia.
Waislamu tumekuwa tukiburuzwa na kugaragazwa katika mambo ya msingi hasa pale wenzetu wa dini nyingine wanapoweka ngumu.
Tuliomba sensa iwe na kipengele cha dini, tukashindwa baada ya usaliti wa BAKWATA. 2005 tulidanganywa ktk ilani ya CCM, tukawachagua. Lakini Hola.
Mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya ulipoanza, tukaona ndipo pa kupatia Mahakama ya Kadhi. Rasimu ya Kwanza na ya pili, zikaja bila ya Mahakama ya kadhi.
Tulipokuja juu, Waziri Mkuu akaahidi Mswaada wa Mahakama ya Kadhi utapelekwa Bungeni februari. Kiini macho kikafanyika eti kupata ridhaa na muafaka na ndugu zetu wa upande wa pili.
Na katika Mchakato wa kuurudisha bungeni mswaada April hii, viongozi wa wenzetu wametia munda. Hawaitaki Mahakama ya Kadhi. Wamehamasisha waumini wao, wajiandikishe kwa wingi na muda ukifika, wapige kura ya HAPANA kwa Katiba Pendekezwa.
Serikali imeogopa nguvu ya wenzetu wakristo. Imesema HAPANA kwa Mahakama ya kadhi, licha ya Tafiti nyingi kuonesha, Mahakama ya kadhi haina madhara (Waziri Mkuu, Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu) waliuthibitishia Umma.
Kutokana na kudharauliwa na kupuuzwa kunakofanywa na serikali mara kwa mara dhidi ya waislamu na Uislamu, binafsi nitapiga kura ya HAPANA KWA KATIBA PENDEKEZWA.
Ewe Muislamu na ndugu zangu wa dini nyingine, tuungane tupige kura ya HAPANA kwa katiba pendekezwa