Habarini za leo ndugu zangu, nimetafakari sana na katika pitapita zangu kwenye maktaba mbalimbali nimejiridhisha bila shaka kuwa nafasi za uongozi wa juu ni lazima zishikwe na mwanaume ili mambo yaende.
Na hakuna ushahidi duniani wa nchi yoyote iliyowahi kufanya revolution yoyote ya maana chini ya kiongozi mwanamke, haipo narudia haipo,ndoja nirudie kwa herufi kubwa HAIPO.
Simaanishi kuwa wanawake wasiongoze, ila wanaweza kupewa nafasi Kama za ukuu wa shule kwenye shule za wasichana, uongozi wa wizara kama wizara ya afya, jinsia, wanawake, wazee na watoto nk.
Mimi naamini tunapaswa kupata rais mwanaume 2025 na makamo wake awe mwanaume.
Kumbe unajaribu kulingana na yule ambaye jina lake unatumia? Pole sana.
Sijui unsoma habari gani, ila: ninamkumbuka
Malkia Victoria; chini ya uongozi wake Uingereza iliendelea kuwa milki kubwa kabisa duniani . . . . (ikashinda China, Uhindi, nusu ya Afrika . . . );
ninamkumbuka
Angela Merkel wa Ujerumani, alibadilisha uchumi wa nchi yake na kuwa mwanasiasa duniani aliyedumu kushinda maraisa wa Marekani, wa Ufaransa, mawaziri wakuu wa Uingereza . . . .
ninamkumbuka
Margret Thatcher wa Uingereza (maarufu The Iron Lady); alileta mapinduzi ya kiuchumi Uingereza, alishinda mfumo dume wa Argentina katika Vita ya Falkland...
ninamkumbuka
Golda Meir wa Israel, aliongoza nchi wakati wa vita ya 1973, akashinda mfumo dume wa Misri na Syria...
ninamkumbuka
Indira Ghandi wa Uhindi; alitawala miaka mingi akaongoza taifa katika vita dhidi ya Pakistan akashinda mfumo dume kabisa wa Pakistan na kusaidia kuanzishwa kwa nchi mpya ya Bangla Desh
ninamkumbuka
Ellen Johnson Sirleaf, aliyeongoza Liberia na kuirudisha uhai baada ya uharibifu wa taifa hilo kutokana na mfumo dume wa vita ya wenyewe kwa wenyewe
Ninamkumbuka
Sheikh Hasina wa Bangladesh pamoja na viongozi wa kike wengine wa nchi hiyo
Ninamkumbuka
Erna Solberg wa Norwei anayeongoza taifa tajiri la Ulaya akifaulu kujenga hazina ya taifa
je niendelee?
Lakini tuna uhuru wa imani, hata kama imani ni ya kitoto ...