Mimi ni muumini wa mfumo Dume

Mimi ni muumini wa mfumo Dume

Mama mwenyewe kakiri hadharani kuwa kafika pale kwa kudra za Mwenyezimungu akimaanisha kuwa bahati imemembeba.
Qudra za Mungu maana yake ni kwa uwezo wa Mungu. Yaani kama si Mungu basi asingekuwa pale. Hiyo ndio tafsiri sahihi ya kiswahili kile sio hiyo tafsiri yako.
 
Mungu ninayemjua hakuwahi kuweka mwanamke kuwa kiongozi, kwa hiyo sahau kuhusu swala la kudra za Mungu, fuatilia historia ya wafalme wa taifa la Israeli utaelewa ninachosema, kimamlaka aliye juu ya mwanaume ni Mungu na siyo mwanamke.

Wakati wazazi wetu wa kwanza walipoasi, Mungu alimuuliza Adamu 'uko wapi' yaani alilenga kujua kwa nini hayupo kwenye nafasi yake, unajua kwa nini hilo swali hakuulizwa mwanamke, pamoja na kwamba Mungu alijua mwanamke ndiye aliyekula dili na shetani na kupelekea mwanaume kumwasi Mungu na kuondoka kwenye nafasi yake?

Ukilitambua hilo elewa kwamba mwanamke hakukusudiwa na Mungu kuwa kiongozi wa mwanaume na kama mambo yakiharibika Mungu atamtafuta mwanaume kumuuliza 'uko wapi' kwa hiyo mambo ya kusema wanawake waongoze kisa wanaume wameshindwa ni kujitafutia laana za kujitakia maana mbali na kutokuwa utaratibu wa Mungu hata mila na tamaduni za kiafrika haziafiki hilo..............​
 
Wanaume halisi tumebaki wachache sana siku hizi... wengi wamebaki Wana mambo ya kike kike tu

Ukweli mchungu huu Last emperor Basi tupambane kila mtu kwenye nafasi yake kuanzia familia kuirudisha nafasi na heshma ya mwanaume.
Maana wanayoweza kufanya wote wanaume na wanawake; lakini kiuumbaji na asili yapo wanayoweza fanya wanawake tuu, au wanaume tuutuu.
Sasa wanaume wasipofanya yale ya kwao inakuaje😎😎
 
Habarini za leo ndugu zangu, nimetafakari sana na katika pitapita zangu kwenye maktaba mbalimbali nimejiridhisha bila shaka kuwa nafasi za uongozi wa juu ni lazima zishikwe na mwanaume ili mambo yaende.

Na hakuna ushahidi duniani wa nchi yoyote iliyowahi kufanya revolution yoyote ya maana chini ya kiongozi mwanamke, haipo narudia haipo,ndoja nirudie kwa herufi kubwa HAIPO.

Simaanishi kuwa wanawake wasiongoze, ila wanaweza kupewa nafasi Kama za ukuu wa shule kwenye shule za wasichana, uongozi wa wizara kama wizara ya afya, jinsia, wanawake, wazee na watoto nk.

Mimi naamini tunapaswa kupata rais mwanaume 2025 na makamo wake awe mwanaume.
Lipo wazi hilo this time historia inangukia tz Ili chama tawala kife huwa ni lzm rais aliyeko madarakani afie madarakani kisha anashika raisi wa mpito wa chama tawala then uchaguzi Rais wa mpito ni lzm apigwe vibaya kwenye sanduku na upinzani,hii imetokea zambia, nigeria,ghana,malawi nk.
Pia ukichek radar ccm baada ya jpm hawana mtu anaeuzika
 
Kisayansi tofauti ya mwanamke na mwanaume ni viungo vya uzazi tu. Hakana scientific proof kwamba wanawake wana inferior brain compared to women.

Nchi zilizopiga hatua zikiwa chini ya uongozi wa wanawake ni nyingi kama Liberia (Dr Serleaf Johnson), India (Indira Gandhi), Bangladesh (Bandaranaike), na recently Germany ( Angela Merkel).

Hayo mambo ya mifumo dune mubakie nayo huko kwenu Usukumani tu. Mjini hatutaki ushamba

Liberia imepiga hatua gani mkuu?? Mbona iko kwenye nchi kumi maskini zaidi duniani??
 
Liberia imepiga hatua gani mkuu?? Mbona iko kwenye nchi kumi maskini zaidi duniani??
Unasemaje kuhusu nchi kama Burundi, Mali, Sierra Leone, Mauritius , Gambia ambazo zinaburuza mkia kimaendeleo na toka uhuru zinatawaliwa na wanaume?
Hoja yako haina mashiko
 
Back
Top Bottom