Mimi ni mwalimu, naacha kazi nijiajiri

Mimi ni mwalimu, naacha kazi nijiajiri

Unaweza kuifanya hobby ikawa profession ndio.....Ila tatizo linakuja kwenye malipo....mshahara was Sari unaufahamu mkuu?....kawaulize makocha was hapa bongo uone wanavyoishi kwa tabu has a hawa wazawa,wagen wengine waliondoka wamerushwa fedha zao mpk wameenda kudai FIFA,......ila nachokisema na nakikataa ni hii mentality ya kusema ualimu ni wito tu hivyo hata wasipokujali wewe uendelee kuteseka na wengine waneemekee kwako na ufe ukiwa masikini na huku hujatimiza ndoto zako...ndio maana watu wanaamua kumove on mkuu
Sarri alianza Coaching kama part time....

Ukifanya unachokipenda unaweza pia ukawa self employed au katika fani ile ile au ukatengeneza stream nyingine ya pesa kutumia ualimu wako; ile knowledge unayowapa watoto ukaifanya practically.., kama unafundisha kilimo ukawa na shamba darasa.., kama unafundisha masomo fulani ukatengeneza vitabu, electronic media n.k. kuwauzia wanafunzi n.k

Haya mambo ya kufanya kazi ili first and far most upate pesa ndio yanafanya waalimu wasiende extra mile na kuwa wabunifu.., wanafanya kile tu mtaala unasema au hata kile hawafanyi ili mradi mshahara wamepata.., ingekuwa wana wito wa kazi wangekuwa hawalali wanaangalia ni vipi wanaweza kutumia teknolojia kuwafundisha wanafunzi wazito.., na kila kukicha wana-update masomo yao kulingana na current affairs.., na kama mwalimu mzuri mzuri tu watu watanunua hizo bidhaa.., na moja ya investment kubwa kwa wazazi ni elimu kwa watoto wao
 
Da kweli hiyo kada inadharaulika sana yaani unashangaa lakini 9 kupata MWL. Sijajua unashangaa as a basic salary or take home?? Vyovyote iwavyo wengi tu wamevuka kiwango hicho
Hata mimi nashangaa sababu Mama yangu alikuwa Mwalimu primary na alifika almost 1M...sema ilikuwa gross.
 
Acha kudanganya watu wewe basic salary ya mwl mwenye degree yaani TGTSD1 ni tshs 716000 (laki saba na kumi na sita elfu tu) na take home yake haifiki laki nne na nusu
Kuna madaraja...Mama yangu alikuwa anafundisha primary na hiyo kazi alianza muda tu....baadaye alijiendeleza na salary slip zake zilikuwa zinasoma gross 1M...Baada ya makato alikuwa anapokea kilo 8 hivi
 
Kiukweli kama unataka mafanikio achana na hiyo kazi ni yakimaskini hasa kwa tanzania kazi kubwa, mazingira ya hovyo,serikali inataka matokeo mazuri wakati wewe haikujali wala mazingira ya kufanyia kazi hayayajali na imekutelekeza porin madarasa mawili bila choo wala nyumba ya mwalimu na mpo walimu 3 wanafunzi 600.

Haki zinazurumiwa kila siku ,kulaumiwa kila wakati,kudharauliwa ,mtoto unamfundisha wewe hongera na tuzo anapewa afisa elimu wakati hajawahi fika hata shulen kwako, ubabaishaji mwing sana kwenye sekta hiyo .

Ni sekta ambayo tangu tupaye uhuru bado ipo kwenye majaribio nakushauri achana nayo mil2 unaweza kufanya kitu jamaa yangu kama ukijifunga mkanda kwelikweli.
Nakazia hapa na kusisitiza .
Pambana kufa kupona.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Haina haja utangaze.... wewe piga kimya kimya, ili ukizidiwa huko uendako urudi kutafuta ajira tena upokewe, kwani haya ni maisha tu... muhimu shilingi ipatikane.
Hajatangaza ameshare experience hili jukwaa la jamii, watu kushare na kuzungumza mambo mbalimbali ya kimaisha so anafanya vizuri maana atapata challenges na ushauri hapahapa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninakaribia 30. Nafundisha sekondari, somo la Basic Mathematics. Sina furaha na kazi yangu kwa sababu kipato hakiendani na kasi ninayoipenda. Nimegundua kuwa na degree hakuendani na kipato.

Bado tunatishwa tishwa. Walimu nimegundua ni waoga. Hasa kufanya maamuzi magumu na sahihi. Mwalimu wa Tanzania anaishi kimaskini. Naacha kazi, naenda kujiajiri mwenyewe.

Kwa heri utumwa, Kwaherini walimu. KWAHERINI. Usiniige kama hujajipanga. Nina sh milioni 2. naenda kuipanda. Hii sio ndogo kwangu. Sirudi tena kufunza.
upo private au government ?? kama private sawa ila government vumilia chukua bumu la 15milion fanya biashara bila kuacha kazi
 
Ninakaribia 30. Nafundisha sekondari, somo la Basic Mathematics. Sina furaha na kazi yangu kwa sababu kipato hakiendani na kasi ninayoipenda. Nimegundua kuwa na degree hakuendani na kipato.

Bado tunatishwa tishwa. Walimu nimegundua ni waoga. Hasa kufanya maamuzi magumu na sahihi. Mwalimu wa Tanzania anaishi kimaskini. Naacha kazi, naenda kujiajiri mwenyewe.

Kwa heri utumwa, Kwaherini walimu. KWAHERINI. Usiniige kama hujajipanga. Nina sh milioni 2. naenda kuipanda. Hii sio ndogo kwangu. Sirudi tena kufunza.
Tupe mrejesho Mwl wa hesabu uliyeamua kuacha kazi.
Hope utakuwa umesonga sana
 
Umeongea ukweli mpaka umenigusa Mimi binafsi sikuwahi kuupenda ualimu kama ajira tangu nazaliwa mpaka kesho ila family ndo imeniforce but mbeleni ntakuja kuchange tu

sometimes familia zetu za hali ya chini zinapoteza sana ndoto za vijana wengi kwa kisingizio cha soma ualimu upate mkopo na ukimaliza uajiriwe mapema huku moyoni mtu haupendi hiyo carrier
Career
 
Back
Top Bottom