Mimi ni mwalimu, nje ya kazi yangu nifanye kitu gani nitoke kimaisha?

Mimi ni mwalimu, nje ya kazi yangu nifanye kitu gani nitoke kimaisha?

TEMBO WANGU

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2014
Posts
930
Reaction score
1,290
Wakuu habari za muda huu, Kuna mijadala inaendelea hapa jukwaani juu ya Hali za maisha ya walimu. Ni kweli walimu tuna maisha magumu, kwa pamoja tumelipokea.

Ndugu zangu tunaomba ushauri wenu, tufanye biashara Gani ambazo zitatuingizia angalau kiasi Cha shilingi 10000 kama faida. Natumaini nitapata michango mingi Sana kutoka kwenu wadau.

Wazo lako la biashara lizingatie yafuatayo:

*Mwalimu anatoka shule saa Tisa
*Mwalimu % kubwa wapo vijijini ndani ndani
* Zingatia mshahara wa mwalimu
LOCATION:nipo Kanda ya ziwa
Cc
Mpwayungu Village, prompwayungu village
 
Oook. Sasa fanya kitu kimoja. Kazi ya ualimu kutoboa sio rahisi wekeza kwenye ufugaji wa kuku wa nyama na mayai kazi ambayo utafanya bila kuathiri kazi Yako

Mtaji sio mkubwa sana ni million Tatu tuu pamoja na banda (au M3 ni kubwa [emoji23][emoji23][emoji23]) ukiona biashara imekuwa kubwa order unapata za kutosha zaidi ya mayai elfu tano unauza Kwa siku, kuku zaidi ya Mia unauza Kwa siku. Anzisha CHIPS SHOP utapiga sana pesa maana kuku na mayai ni yako mtaji ni viazi tuu

Baada ya hapo utaamua kuacha ualimu utoke kwenye kada ya fedheha na laana
 
Oook. Sasa fanya kitu kimoja. Kazi ya ualimu kutoboa sio rahisi wekeza kwenye ufugaji wa kuku wa nyama na mayai kazi ambayo utafanya bila kuathiri kazi Yako...
ACHA kumdanganya jamaa wewe!

Umewahi fuga kuku wewe!!?au umesikia inspiration speakers!!?

Sio rahis kutoka mkuu kwenye hiyo!hao viumbe ni risk KWA magonjwa halafu afya yao ni dynamic sio ya kutegemewa ki hivyo!!
 
Oook. Sasa fanya kitu kimoja. Kazi ya ualimu kutoboa sio rahisi wekeza kwenye ufugaji wa kuku wa nyama na mayai kazi ambayo utafanya bila kuathiri kazi Yako...
Usirogwe ukachukua ushauri huu, kufuga kuku unahitajika uwepo 100% of your time la sivyo utatoka siku moja utakuta banda zima wamekufa na uliyemuweka hana maelezo
 
Wakuu habari za muda huu, Kuna mijadala inaendelea hapa jukwaani juu ya Hali za maisha ya walimu. Ni kweli walimu tuna maisha magumu, kwa pamoja tumelipokea...
Hapo inategemeana na upo sehemu gani

Kwa upande wa kijijini.

Unaweza fanya yafuatayo ambayo USIMAMIZI wake kidogo sio mgumu.

  • Kuanzisha kibanda Cha M-pesa
  • MASHINE ya kusaga mahindi na kukoboa ya umeme.
  • Kununuaa pikipiki unampa mtu kwa mkataba.
  • Kilimo kwa kufuata mvua maana mvua zinanyesha mwezi wa kumi na mbili MDA wa likizo.
.....
 
Back
Top Bottom