Parallel inawezekana. Kama njia tunazotumia hazikutani au kugusana sehemu yoyote, hizo ni parallels.
Misingi ya vipimo na imani huwa haikutani. Huwezi abudu halafu umalize uchungulie telescope au microscope kumtafuta huyo mungu. Mwisho wa siku either una amini au unajua. Huwezi kuunganisha vyote. Ukijua kitu huhitaji tena kuamini. Imani haina msaada kwenye taaluma au ujuzi wowote.
Mimi na wewe tuko parallel kwa msingi huo. Wewe mtu wa imani wakati mimi mdadisi. Nahoji kila kitu hadi uhalisia wa hizo imani. Sijajiwekea mpaka. Siwezi kuabudu kitu nisichoelewa. Hata iwapo moja ya aina nilizopata kuona kuhusu mungu ni kweli bado sitoabudu. Zote zimejaa ujinga. Mambo ya kale. Mimi sio mtu wa kale. Pamoja na kupitwa na wakati nahisi kuna watu walihoji hata kipindi hicho. Walikuwa imara kukataa ujinga. Kuabudu ni udhaifu ambao nitajionea aibu kufanya. Kuna wanaona ufahari kuabudu sio mimi. Utumwa, uvivu, ujinga, upotevu wa muda kwa zoezi lisilo na faida.... itoshe kusema bongo zetu ziko tofauti.
Naweza nikakuheshimu kama mtu japo una mawazo nayojua ni imani potofu. Imani yako hiyo ni sehemu ndogo ya utu wako. Unaweza kuwa mtu mwema na hodari kwenye mambo mengine ya msingi. Kwani unadhani hakuna wataalamu wanaoamini hizo imani? Wanaheshimika kwenye field zao lakini inapokuja kwenye imani nao dhaifu. Kuheshimu imani zao itakuwa unafiki. Tunavumiliana tu sio kuheshimu imani yenyewe. Hata ikisemwa tunaheshimu imani, ukweli ni kwamba kauli hii ya "kisiasa" ina maana tunaheshimu watu wanaoamini ujinga fulani maana wao ni zaidi ya ujinga wao huo mmoja. Binafsi tunajua hatuwezi kufata ujinga wao ila mambo mengine ya msingi tutashirikiana.
Sijui umenielewa au tumeenda parallel tena? Nimejitahidi kuandika namna utakayoelewa Synonym.
Ni nani aliyekukaririsha kwamba mtu akiwa mwanasayansi au mwanafalsafa ni lazima asiamini uwepo wa Divine Being kwa sababu ni fani zenye misingi tofauti? Eti huwezi kuunganisha vyote, yaani mtu kuwa mwanahistoria au mwanajiografia ndo kumpokonye haki ya kuamini? Nani kakufunza mambo haya, ni viashiria vya fikra limbukeni
Unayejadiliana naye humjui acha kunitengenezea nadharia tete, niweke mimi pembeni ambaye sijadhihirisha wazi wasifu wangu. Uhakika Bro ni mdadisi na pia ni muumini. Kuna jamaa ana username Mpare2 - rejea comments za juu amejidhihirisha wazi kwamba ni mwanasayansi na anaamini uwepo wa Mungu, sasa wewe sijui hilo sharti la kutokuwa mwanasayansi na muumini kwa wakati mmoja sijui umelipatia wapi!
Kwenye maelezo yako umediss ulivyotaka imani kwa ujumla wake, mara ni kale, upuuzi, kuabudu ni kupoteza muda, ni ujinga, upotofu na maneno ya kebehi kibao! Sawa ngoja hayo tuyapokee kwa mikono miwili japo hamna hoja ya msingi uliyojenga dhidi ya imani zaidi ya kuonyesha mitizamo yako hasi inayoishi kwenye kichwa chako. Kwa kuwa unajinadi wewe ni mwerevu sana kuliko watu takribani bilioni 7, mimi sitaidogosha sayansi kwa mitazamo hasi au maneno matupu kama wewe, badala yake nitaweka challenge ndogo sana kukufunza!
Niliwahi kukuuliza sayansi kama fani, unajua madhaifu yake? Ulichezacheza na maneno na hamna cha maana ulichojibu.
Hivi hata katika akili ya kawaida tu, mambo/hali/mienendo/tabia zote zilizopo ulimwenguni au vitu vyote vilivyomo/vinavyotuzunguka vinaweza kuelezwa kwa ufasaha/kweli na kuvielewa kwa kuegemea kwenye fani moja tu ambayo ni sayansi? Hivi kweli fani moja ndo itupe majibu ya mafumbo yote ulimwenguni?
Sayansi kama fani msingi wake mkuu umejijenga kwenye experimentation, sasa ngoja tuone implication ya hiyo approach na udhalili wake kwa mifano kwenye baadhi ya mambo (Challenge I): Uchawi upo au haupo? Unaweza kuthibitisha uwepo wa uchawi kisayansi? Sayansi kushindwa kuthibitisha uwepo wa uchawi ndo kunaufanya uchawi usiwepo?
Challenge II: Tusaidie kufanya utafiti wa kisayansi kuthibitisha uwepo wa akili tambuzi 'consciousness', kwamba ipo au haipo kwa muonekano na sifa zake! Eti uchukue telescope/microscope umchungulie Mungu! Kwa nini usichukue telescope/microscope uichungulie akili?
Tafakuri: Ni kwa nini sayansi ikishindwa kuthibitisha jambo hukimbilia kwenye hitimisho la kutokuwepo kwa hicho kitu! Wakati huohuo kwenye fani yetu yenyewe kuna mambo tunaitakidi yapo na hayathibitishiki lakini tunakomaa kutetea uwepo wake au tunajisahaulisha kama hayo mambo hayapo hivi kwa lengo la kuitakasa fani na madhaifu yake
Halikadhalika, kuna mambo yapo wazi lakini jinsi sayansi inavyoeleza ni kana kwamba imekuwa conflicted, au kuna deficit ya concepts, au concepts zake ni incomplete, hali inayopelekea kutoelewa jambo kwa kina au kupotosha kabisa, nimeona kwenye comment yako hapo chini umemtaja Darwin: sijui ni tahira gani wa karne hii unayeweza kumuelezea nadharia zake za evolution akakuelewa