Mimi ni mwanabaiolojia na huu hapa ndio uthibitisho wa uhalali wa Mungu(2)

umejuaje hili mkuu
Hahahahaah, nashuhudiwa rohonii🤭🤭.

Seriously inaanzia ndani ya mtu baada ya kuwa ametambua halafu baada ya hapo ndio unaanza kumuona katika mazingira unayoishi. Mfano katika watu uumbaji, akili au fani yoyote uliyopo
 
Hahahahaah, nashuhudiwa rohonii[emoji2960][emoji2960].

Seriously inaanzia ndani ya mtu baada ya kuwa ametambua halafu baada ya hapo ndio unaanza kumuona katika mazingira unayoishi. Mfano katika watu uumbaji, akili au fani yoyote uliyopo
nachelea kukuelewa mkuu. but anyway, there is nothing from nothing. absolutely there is Almighty, creater of everything , the first and the last .
 
Sawa, nikitulia nitapitia vizuri
 
Ni imani tuu, na nyie watu wa imani mnajifanyaga mna akili sana kumbe mnaonekana mataahira tuu na mnapigia watu makelele na nyimbo zenu mnazoimba usiku kucha kwenye mikesha yenu
Hasa WAISLAM na Wakristo. Hawa watu wanajiamini sana na hawajui kwamba 2/3 ya watu duniani wana imani tofauti na yao huku maisha yakisonga
 
Maombi yako yanatakiwa yawe sambamba na mapenzi yake, usifanye kosa la kutaka kumpangia Mungu cha kufanya.
Na hapa ndipo hoja ya uwepo wa Mungu inapo kufa. sababu yeye hataki kupangiwa lakini yeye anataka kutupangia sisi.kama vile tulijadiliana atulete duniani ama asitulete. Kama hakukua na majadiliano Kati yetu na yeye Basi wote tusipangiane.
 
Na hapa ndipo hoja ya uwepo wa Mungu inapo kufa. sababu yeye hataki kupangiwa lakini yeye anataka kutupangia sisi.kama vile tulijadiliana atulete duniani ama asitulete. Kama hakukua na majadiliano Kati yetu na yeye Basi wote tusipangiane.
Kuna ukakasi kidogo kwenye hoja ya anatupangia, hatupangii kila kitu per se. Japo ni kweli anao uwezo wote. So unaweza kumuomba na ukapewa mbona?

Ni kama tumepewa majibu ya kuchagua so vingi tunajipangia wenyewe kwa wenyewe. Katika hayo machaguo unaweza kuchagua kumfuata na kufuata maelekezo yake na matakwa au kukataa na kufuata maelekezo mengine. Mwisho wa kila chaguo ndo kuna matokeo yake. Kungekuwa haiwezekaniki kufanya machaguo kinyume na yeye basi kungekuwa hakuna machaguo kabisakabisa.

Ila sasa yeye akiamua anaweza kufanya chochote, japo ni mara chache anaamua hivyo. Mara nyingi anakuacha wewe ndio uamue unachukua njia ipi na unaacha ipi. Ni kwamba anatupenda saaana ndiyo maana.

Upendo ndugu kama haujajua ni pale unapoamua kutumia uwezo wako ulio nao kwa hiyari yako kutimiza matakwa ya yule unayempenda. Mfano;

Mke: Mme wangu leo nitakupikia chakula chochote unachokitaka wewe [anaonesha upendo]. Kumbuka anao uwezo wa kupika nyama, dagaa, samaki, mchicha, maharage kila kitu ila anaamua kumpa mme wake chaguo na sio kumshurutisha.

----....Kisirisiri mme anapendaga ugali na dagaa, ila mke wake hapendagi harufu ya dagaa. Yeye[mke] anapendaga samaki. Na mme pamoja na kupenda dagaa anapendaga na samaki pia na anajua status ya mke wake kuhusu samaki vs dagaa...---

Mme: Anaamua kujibu 'nipikie ugali na samaki mke wangu, nna hamu kweli na samaki'. Anaonesha upendo kwa kutumia uwezo wake wa kuchagua, kuchagua kitu ambacho ni matakwa ya mke wake pia😊. [huu ni upendo]
A. Angechagua mchicha angeona vizuri, vitamini macho.
B. Angechagua maharage angeongeza protini labda damu pia lakini pia angejaa gesi na kujambajamba yote matokeo😂
C. Angechagua nyama pia angefaidi mchuzi na mwingine ungemdondokea kwenye shati labda
D. Amechagua samaki amefaidi, wamefaidi na bado ameongeza ukaribu so watafaidi zaidi na zaidi😉
 
Mtu anaona gari anaamini limetengenezwa na mtu na kiwandani hajawahi kufika kuona likitengenezwa. Ila akiambiwa binadamu kaumbwa na Mungu anabisha anadai leteni uthibitisho, anadai binadamu amezuka tu kuliko mzuka. Ukitathmini maumbile ya binadamu ya nje na ndani ndiyo utakubali yupo aliyekaa akayatengeneza kimpangilio kikamilifu that's GOD YAHWEH.
 
Ongea na Mungu mwambie kule Ukraine watu aliowaumba Putin anawaua kinyama bila huruma yoyote. Mbona Mungu kanyamaza!
Atajibu kama alivyojibu kwa HITLER alivyofanya mauaji ili PUTIN naye aondoke kabisa na utawala wake wa kinyama.
 
Kuna ukakasi kidogo kwenye hoja ya anatupangia, hatupangii kila kitu per se. Japo ni kweli anao uwezo wote. "So unaweza kumuomba na ukapewa mbona?"
Unaongea kana kwamba unauhakika na unachokisema..Hii ni ajabu.!

Yaani unaweza kudhani mungu yupo ikulu chamwino na wewe ndio kibalaka wake, halafu upo unashangaa kwanini watu hawaji kueleza changamoto zao ili azitatue.!? Unajua hii ni aina fulani ya ugonjwa wa akili.?

Ila sasa yeye akiamua anaweza kufanya chochote, japo ni mara chache anaamua hivyo. Mara nyingi anakuacha wewe ndio uamue unachukua njia ipi na unaacha ipi. Ni kwamba anatupenda saaana ndiyo maana.
Unarudia kile kile, unapinga hoja kwa maelezo yasiyo na ulazima ili ionekane umejibu tu

Sikiliza wewe, katika Atheist ninao wafahamu wanaotoa hoja zao humu, sijawahi ona hata mmoja akitumia msingi wa maumbile katika kutete hoja zao juu ya uwepo wa huyo mungu

Kwa ufupi uzi umewatenga, na nimeona kuna mmoja aliyejaribu kuweka sawa sintofahamu yako kwa kuchanganya elimu ya kimaumbile na hiyo ya kiroho ili kuweka mambo sawa naona mmeishia kumpuuza tu, ni kama unapenda majibu fulani ya kukuunga mkono

Katika aina hii ya mtazamo huwa inatia uvivu kidogo kwenye mijadala endelevu
 
Sikiliza wewe, katika Atheist ninao wafahamu wanaotoa hoja zao humu, sijawahi ona hata mmoja akitumia msingi wa maumbile katika kutete hoja zao juu ya uwepo wa huyo mungu
Nadhani ulimaanisha theists, anyway ni kwamba kila mmoja anatumia anachokifahamu kutetea hoja yake. Sasa kuna ubaya gani mimi kutumia baiolojia. Kumbuka atheists hawazipagi uzito hoja zinazotoka kwenye vitabu vya dini[ambavyo ndio specialized sources kabisa]. Kwa nini unikataze kutumia kitu tunachoshare wote na kukikubali? Wapo watakaotumia dini, saikolojia, morality etc wote tunajenga nyumba moja.


kuna mmoja aliyejaribu kuweka sawa sintofahamu yako kwa kuchanganya elimu ya kimaumbile na hiyo ya kiroho ili kuweka mambo sawa naona mmeishia kumpuuza tu
Ungemtaja ID kwa ushahidi zaidi maana sijaona aliyepuuzwa katika huu uzi kila swali lililoulizwa humu limejibiwa ama na mimi, au mdau yeyote aliyekuwa na majibu wakati huo. Tuelekeze post namba ngapi haijajibiwa tusaidiane kujibu kuna kusahau pia.

Na kama nyongeza umesoma mfano wangu wa upendo wa mme na mke. Naongezea mke anaweza hata kumruhusu huyu mume akanunue pizza huko nje akitaka na faida zake na hasara zake matokeo atayapata sambamba na uchaguzi wake. Mungu anakuruhusu ukitaka gari kalitafute kwa bwana Kiichiro Toyoda ndiko yanakotengenezwaga na anao utaratibu wake ili akupe gari utaujua hukohuko.
 
Nadhani ulimaanisha theists,
Hapana namemaanisha atheist, hawapendelei kutengeneza hoja katika fani za kimaumbile kutetea mawazo yao ikiwemo hii ya biolojia, kemia, fizikia, astrolojia n.k

Labda wanaepuka kukuta na wajuvi wa fani zenu kama wewe ambae umejinasibu mbailojia na pia kuepusha usumbufu wakutojadili habari husika juu ya mungu na uwepo wake na kuanza kubanana juu ya fani husika na misingi yake kitu ambacho wao hawapendi

sikukatazi kutumia fani yako kutetea imani yako

Labda ni kukumbushana tu kwamba si eneo husika sana litumikalo mara nyingi kujengea hoja atheist kupinga uwepo wa mungu.

Kwakuwa hiyo ni fani na haimpi uhalali huyo mungu juu uwepo wake, bali mawazo ya mtu ndio huweza kutengeneza hizo dhana kwenye akili yake ikitegemea kile kilichotangulia akili yake

Ndio maana vitabu vya dini haviepukiki na ndipo mminyano unapoanzia huko

Kama nitakuwa nimeshuhudia juu ya uwepo wa huyo mungu mfano wako unaweza kuwa na matokeo kwangu

Lakini kama sivyo_nitahisi una shida fulani kwenye mtazamo wako kwa kuhalalisha ujinga fulani wa mtazamo kwa jina la heshima la mungu

Hakuna kitu kama hicho kinachoitwa uhuru kwa mungu aliyekuwa peke yake akaamua vyote vitokee baada yake
 
Hakuna kitu kama hicho kinachoitwa uhuru kwa mungu aliyekuwa peke yake akaamua vyote vitokee baada yake
Kwani bro wewe ulitaka uamue vipi kabla wakati ambao hata haujakuwepo bado?

Nafasi ya maamuzi ya mwanzo ni yake mwenyewe. Lakini mengi ya sasa na baadaye una nafasi ya kuhusika nayo ni wewe tu kuchagua
 
Kwani bro wewe ulitaka uamue vipi kabla wakati ambao hata haujakuwepo bado?
Ni vema kuzungumzia wakati nipo naweza kuamua vipi.?

Hiyo kawaida ya kusafirisha mawazo katika kipindi ambacho hukuwahi kuwapo ndio husababisha matatizo mengi ya kiufahamu

Wajuvi wanafahamu tahadhari za kuchukua unapotafiti vitu vilivyo nje ya wakati wako

Nafasi ya maamuzi ya mwanzo ni yake mwenyewe. Lakini mengi ya sasa na baadaye una nafasi ya kuhusika nayo ni wewe tu kuchagua
yaani katoto kadogo kamezaliwa Ukraine kamepigwa mabomu na warusi na wazazi kamepoteza akiwa hafahamu lolote linaloendelea mpaka kufikia hali hiyo

Kesho kawa mtu mzima hana miguu halafu unakapa ufafanuzi kama huu juu ya mungu wako..!

Mimi nakuambia kweli anaweza kuwasamehe warusi kwa yote waliyomfanyia lakini si huyo mungu wako

Eti kaumba uhuru na mtu ana hiyari ya kuchagua.!? Kwani yeye aliomba kwa hiyari azaliwe Ukraine.!?

Hivi hujui katika uchaguzi wa kibinadamu ni maumivu kwa binadamu wengine.! Huu nao ni ugonjwa kutolifahamu hili
 
Bado naitafiti hii dhana ya utashi huru binafsi/free will, kweli hata wikipedia [kwa kuanzia] wametoa maelezo meeeengi sana na debate ndefu sana. Na mimi bado naendelea kutengeneza nadharia nzuri kuhusiana na hicho kitu.

Lakini tangu mwanzo nimekuwa nikiamini kuwa kuna ngazi kadhaa za mtu kujiamini kwamba anayo maamuzi. Na kila ngazi unayochagua basi unazipata faida na hasara zake wewe mwenyewe. Nilisamaraizi hivii;
 
Hivi wakati unaarchive hiyo great power from a great responsibility, While u making many shit

Hivi nani atakuwa kakaa kama jiwe la mzani kusubiria wewe ufikie unachokitaka.! Hivi umewafikiriaje wengine

Hivi uoni ni aina ya ujeuri fulani mtu aliyejizoesha kuuzoea mpaka umeroot kwenye bongo yake mpaka anajiona kuna kitu anafanikisha.?

Kujipa maana wakati huna maana ni ugonjwa wa akili
 
Basii basii bro basii heeh! umekasirishwa sana na neno shit hadi limeziba uelewa? basi badili neno 'shit' kwa neno 'things'. Nimesema 'we' nikimaanisha mimi, wewe, yule pamoja na nguvu zote zinazotuwezesha tunashirikiana kufanya mambo yatokee.

Liliwekwa makusudi ili kila mmoja aelewe kivyake kulingana na akili yake. Na ajielewe mwenyewe je ni pessimist au optimist au realist whatever. Kama ni matatizo ya akili [ambayo umesisitiza mno kwangu] basi ajitambue automatically.

Mimi ikitokea mmarekani mweusi [au mtu yeyote] akaninong'oneza sikioni 'Make shit happen broh' ntachukulia ananitia moyo kufanya maendeleo ya maana kabisa.

Kwani wewe ikitokea mmarekani mweusi anakuambia 'Make shit happen' utaelewa nini?
 
mno kwangu] Mimi ikitokea mmarekani mweusi [au mtu yeyote] akaninong'oneza sikioni 'Make shit happen broh' ntachukulia ananitia moyo kufanya maendeleo ya maana kabisa.
Alaah kumbe.! kama vile wahuni wa huku kwetu wanavyotukanana "we ms*ng noma" unashangaa jamaa hakasiriki anachekacheka tu

Kwani wewe ikitokea mmarekani mweusi anakuambia 'Make shit happen' utaelewa nini?
Nitahisi kaniambia nijizime data niruhusu ujinga fulani upite maisha yasonge yaani kama nisitilie maanani kitu fulani kwa mkazo

Ila mimi ni mmatumbi niwie radhi
 
Alaah kumbe.! kama vile wahuni wa huku kwetu wanavyotukanana "we ms*ng noma" unashangaa jamaa hakasiriki anachekacheka tu
Yas ni mfano wake mzuri, inaonesha umeelewa. Sema bado kitukimoja ujifunze kinaitwa 'kuvaa viatu vyao' hata kama wewe hutatembea navyo. Hao jamaa hawatukanani ni wanaongea.

Basi neno lilimaanisha pande zote mbili za mambo ya maana na mambo ya kijinga. Au tuseme tu kimsingi ni mambo yote kwa ujumla;
1. Ukiishi kwa kuamini mambo yanatokea tu menyewe - unakuwa chini sana kiafya, kijamii, kihisia etc. Hutafaidi wala hutaumizwa sana na lolote sema maisha yanakosa ladha.
2. Ukiishi kwa kuamini mambo yanatokea kwa sababu fulani unakuwa umepiga hatua kubwa mambo yako yatakuwa mazuri.
3. Ukiishi kwa kuamini ni kama vile sisi wote [mtu binafsi akishirikiana na watu, na shetani, na Mungu wote] tunafanya mambo yatokee! hapo hatua uliyopo ni kubwa kubwa ajabu utakuwa na raha sana maishani. Maana unakuwa umeamini yanatokea ni kwa sababu, na wewe mwenyewe ni sehemu ya hiyo sababu. Likitokea zuri furaha yako ni maradufu, likitokea baya unaumia maradufu lakini hauna majonzi sana maana unajielewa na unajua ni kitu na we mwenyewe umehusika kujiletea.

Mfano wako wa mtoto wa Ukraine utamsikitisha zaidi kama atachukua nafasi ya kwanza akajiona hana nafasi wala hakuna sababu ya maana ya mambo yaliyompata [pole dogo😥].

Ila akiamua kuchukua ya mwisho utashangaa ikawa kwake ni motisha kubwa ajabu. Akiamua kuibeba responsibility yake atakuwa 'big man' akiamua kuibeba responsibility yake na ya wazazi wake na ya nchi yake na ya nchi majirani zake zoooote kama zake, basi atakuwa a very great man with great powers. Mi sijui atafanyaje lakini nae ajiulize si ana akili aangalie atatumiaje matukio yote kuleta kitu cha maana hapa duniani, ajitahidi tu kadri ya uwezo wake.[pole na hongera kaka mkubwa 😥👊💪]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…