Dr Dre
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 2,664
- 2,810
umejuaje hili mkuuUnaweza kuichukulia hivyo kimwili zaidi kumpata yupo mbali, lakini kiroho yupo nasi tunaishi naye kila siku yupo mahali pote ni sisi tu kumtambua
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
umejuaje hili mkuuUnaweza kuichukulia hivyo kimwili zaidi kumpata yupo mbali, lakini kiroho yupo nasi tunaishi naye kila siku yupo mahali pote ni sisi tu kumtambua
Hahahahaah, nashuhudiwa rohonii🤭🤭.umejuaje hili mkuu
nachelea kukuelewa mkuu. but anyway, there is nothing from nothing. absolutely there is Almighty, creater of everything , the first and the last .Hahahahaah, nashuhudiwa rohonii[emoji2960][emoji2960].
Seriously inaanzia ndani ya mtu baada ya kuwa ametambua halafu baada ya hapo ndio unaanza kumuona katika mazingira unayoishi. Mfano katika watu uumbaji, akili au fani yoyote uliyopo
[emoji817]nachelea kukuelewa mkuu. but anyway, there is nothing from nothing. absolutely there is Almighty, creater of everything , the first and the last .
Sawa, nikitulia nitapitia vizuriReality, tumetoka kuiweka sawa nilipomjibu kwa post namba 225. Najua ameisoma na kuikubali na hajataka tu kuitolea majibu [nimechukulia silence means yes]
Tukiachana na pande tulizoshikilia [za God or no God] kuna kitu kimoja hapa natamani kila mmoja binafsi akichallenge kwa uelewa wake kwa kile anachoona ni sensible:
Hoja kuu: Tunauishi ukweli kulingana na tunachohisi ni kweli binafsi. Yaani mimi binafsi ninaushi ukweli ninaoujua binafsi kwamba ni ukweli na ndio iko hivyo. Na wewe binafsi unauishi uhalisia wako binafsi kutokana na unachokijua kuwa ni kweli wewe mwenyewe. Mambo ya relativity.
Mfano 1.a. Yule anayeamini ukweli wa maisha baada ya kifo basi akifa ataendelea kuishi katika namna sambamba na alivyoamini. Huyu ameamini katika uhai
1.b. Na yule aliyeamini kuwa hakuna lolote la ziada ukweli ni mnyama akifa kila kitu kinasambaratika na kuwa viinilishe kwa wanyama wengine basi akifa atapata sambamba na ukweli wake binafsi. Huyu ameamini katika kifo
Mfano 2.a Yule atakayeamini kuwa ukweli ni tunaishi katika mazingira ya hatari ya, wizi, uonevu, magonjwa na vita ni vitu vya maisha ya kawaida na vingi kuliko hali ya amani basi kila kitu chake kitaitikia kwa kujiweka mkao wa vita mbeleni. Atajikusanyia bima ya rasilimali nyingi zaidi physically. Na kimwili atajiwekea bima ya rasilimali muhimu kama mafuta[nishati] na protini kujiandaa na vita inayokuja.
Na ikitokea akaamini kuwa sio hatari tu bali tayari tumo katika vita, iwe ni kuchumi, kiroho, kisaikolojia, familia, kazini etc. Basi tutashuhudia akiwa na nishati ya kutosha mwilini ili apambane sasa hivi. Namaanisha sukari. Mfano wake ni bosi wa wastani[CEO] anayeongoza kampuni kubwa yenye faida kubwa na hatari kubwa zaidi ya kufilisika ni kwa nn wanakuwa na vitambi/sukari?
2.b. Kinyume chake atakuwa ni jamaa anayeamini kwamba tunaishi na watu wa amani na upendo zaidi kwamba wengi ni wa upendo kuliko wa vita na mimi. Basi huyu mwamba hata hajiandai na rasilimali zozote za kimali binafsi physically. Na hasahasa kimwili hajiandai kwa kujirundikia mafuta[nishati] wala maprotini mwilini. Mfano ni rastamani wa wastani mwenye imani ya kirasta kwa nini wanakuwaga wembamba?
Mfano wa kwanza tuachane nao kutokana na asili yake utatusumbua. Naomba muuchallenge huu mfano wa pili. Ila nahisi hapa naharibu uzi ngoja nikipata muda niuanzishie uzi wake. Ila nipeni challenge ili nijipange vizuri.
Hasa WAISLAM na Wakristo. Hawa watu wanajiamini sana na hawajui kwamba 2/3 ya watu duniani wana imani tofauti na yao huku maisha yakisongaNi imani tuu, na nyie watu wa imani mnajifanyaga mna akili sana kumbe mnaonekana mataahira tuu na mnapigia watu makelele na nyimbo zenu mnazoimba usiku kucha kwenye mikesha yenu
Na hapa ndipo hoja ya uwepo wa Mungu inapo kufa. sababu yeye hataki kupangiwa lakini yeye anataka kutupangia sisi.kama vile tulijadiliana atulete duniani ama asitulete. Kama hakukua na majadiliano Kati yetu na yeye Basi wote tusipangiane.Maombi yako yanatakiwa yawe sambamba na mapenzi yake, usifanye kosa la kutaka kumpangia Mungu cha kufanya.
Kuna ukakasi kidogo kwenye hoja ya anatupangia, hatupangii kila kitu per se. Japo ni kweli anao uwezo wote. So unaweza kumuomba na ukapewa mbona?Na hapa ndipo hoja ya uwepo wa Mungu inapo kufa. sababu yeye hataki kupangiwa lakini yeye anataka kutupangia sisi.kama vile tulijadiliana atulete duniani ama asitulete. Kama hakukua na majadiliano Kati yetu na yeye Basi wote tusipangiane.
Mtu anaona gari anaamini limetengenezwa na mtu na kiwandani hajawahi kufika kuona likitengenezwa. Ila akiambiwa binadamu kaumbwa na Mungu anabisha anadai leteni uthibitisho, anadai binadamu amezuka tu kuliko mzuka. Ukitathmini maumbile ya binadamu ya nje na ndani ndiyo utakubali yupo aliyekaa akayatengeneza kimpangilio kikamilifu that's GOD YAHWEH.Kuna mtindo wa kwenye social media watu kutosoma maelezo marefu sana. Hivyo basi nimeamua kuileta sehemu tu ya ile sehemu ya pili, enjoy;
View attachment 2174800
....................kukazia pointi kadhaa na kufunga;
Ndugu zangu, haidhuru mtu au mfumo kutokujua mwisho au mwanzo wake ili kuleta maana – ‘sense’. Maana inakuja pale kipande cha mfumo husika utakapokuwa unatenda kulingana na muelekeo sahihi ukiuchukulia mfumo mzima juu kabisa hadi chini kabisa. Sense ni ule tu uelekeo sahihi basi. Hata kama labda moyo unafahamu tu kwamba ‘ulimwengu mzima’ ni wenyewe tu na ukajijali wenyewe tu hautakuwa na maana tena mwilini. Lakini ukawa na akili ya kuelewa kwamba kuna mfumo mzima wa mishipa na kazi yake ni kuisambazia hiyo mishipa damu basi tayari utakuwa na maana na utaishi. Utaishi vizuri hata kama haujawahi kuiona mivitu migumu kama mifupa [damu yenyewe inatengenezwa huko]. Moyo ukasema wenyewe unajua kuna nyama tu na nyama ndiyo kila kitu kilichopo. Utaendelea kuishi huku ukilindwa na mifupa hiyohiyo uliyoikataa kwamba haipo na haina maana yoyote. Lakini ukitaka [ufe huo moyo] ni pale utakapofanya kitu ambacho ni non-sense yaani kinyume na ukweli wake. Mfano ukaamua kunyonya damu badala ya kuisukuma. Au kuji mwambafai na kujipa umuhimu wa kwanza badala ya kusambaza damu wenyewe ndiyo uitumie damu kukua na kuitumia zaidi. Kujitukuza kujipa umuhimu wa kwanza wewe badala ya vyote sio jambo zuri. Maana viungo vipo kwa ajili ya viungo wenzake na kwa ajili ya lengo la jumla la kuwepo kwa huo mfumo. Kwa hiyo tukirejea kwa mwili tutasema moyo ni kwa ajili ya mapafu, miguu, mikono, ubongo, moyo na mwiliwote na mtu mzima kwa ujumla. Kwa hiyo moyo unaweza kusema kuwa lile wazo la mtu ndiyo mungu. Mungu wake anaonekana kuwa tofauti kabisa na asili ya moyo wenyewe ulivyo kwanza haonekani wala hashikiki.
Mfano wa seli pia ni hivyohivyo mitochondria ipo kwa ajili ya ribosome, nucleus, membrane, mitochondria yenyewe na seli nzima kwa ujumla wake. Mitochondria akiongeza ujuzi wake atagundua kuwa hata ile idea nzima ya seli sio mwisho. Ni mungu wake kwa level fulani lakini sio mwisho. Atagundua kwamba zipo seli nyingine pia mwilini mamilioni na mamilioni nazo zina mitochondria zake na zoote zinafanya kazi kwa ajili ya kuuendeleza huu mwili mzima. Ndio zinaonekana kama zimaulisha ubongo wa mwili huo lakini ukitizama kwa makini utagundua kuwa hata ubongo unafanya kazi kwa ajili ya mtu ambaye ni jitu zima limalotawala seli zooote moja moja katika makundi. Lakini hapohapo ukipindisha kidogo kubadili mizania ya utazamaji unaweza kusema kuwa huyu mtu naye yupo kwa ajili ya kuvitumikia hivyo viseli [na vimitochondria] vyoote mwilini mwake ili viendelee kuishi. Nayo sio mbaya ukiamua hivyo kwa sababu huo pia ni ukweli na ni kitu kilekile tunachokisema kila siku. Na huyu mtu ameonesha kuwa yuko na upendo woote na kujali kote na uangalizi wote kwa viseli vyote vilivyo chininya uangalizi wake. Kwa hiyo kwa viseli vya mwili mtu ni Mungu wao.
Tukibakia hapohapo ona jinsi mambo yote yanavyopata majibu ya wazi kabisa. Tunaona ni sahihi kwa seli hai nyekundu za damu kufa kila zinapotimiza wastani wa siku 120. Sijui kama zinalalamika au zinaumia kufanya hivyo sijui. Lakini inaonesha kuwa zimezaliwa zimemtumikia mungu[mtu] na mwisho zimekufa zitaacha nyingine zikifanya kazi. Zitazaliwa seli nyingime. Haya ikatokea mwili umevamiwa na wadudu hatari. Tunaona rasilimali muhimu kwa matumizi ya seli nyingine zikibadilishwa njia na kupewa askari [chembe za kinga] ili zikapambane na wavamizi. Labda seli nyingine huwa zinanungunika na kuleta migomo ndio maana sababu tunaona mwili ukinyon’gonyea. Mfano ni kichwa ndio kinauma au ni damu ndiyo imeambukizwa maralia. Lakini misuli ya miguu, tumbo na viungo vya uzazi vyote vinalala, si hamu ya chakula wala ya kula inayobakia. Au mfano wa pale ambapo mwili unapoamua kuviua vipande vyake vinavyotaka kuleta shida kwa mwili mzima. Mfano; seli zilizokaidi kufa zenyewe zikaamua badala yake kukua tuu pasipo kujali zinaleta faida wala hasara kwa wenzie. Zenyewe zinachojua ni kula kunenepeana na kukua zaidi na zaidi. Kila aliye jirani nazo anaumia tena anachukizwa na uwepo wake. Muda utafika mwili utaamua kuziua japo kutokana na mapendo makubwa utafanya hivyo kwa maumivu makubwa sana. Ukisikia kansa inatesa jua kwamba kansa inatesa kweli kweli. Ni maumivu makali na ndio maana wanaoiugua huwa wanasemwa kuwa ‘they are battling cancer’ ni vita! Lakini hata yanapotokea haya tunapaswa tutambue kuwa yote ni katika upendo tu wa baba yao hizo seli mtu mwenyewe. Maana kwa upendo anaidhinisha seli mbaya ziuwawe hata kama zinazobaki zitayapata maumivu hakuna namna. Yote haya yangeepukika kama seli mbovu zitaamua kufa zenyewe kwa upendo kuwaachia wengine waishi. The key hapa ni upendo. Mungu ni pendo walishasema. Hata kama kwa upendo ataamua kwamba wacha tu vyote viishi [ambavyo mara nyingi hutokea] na mwishoni atauvunjavunja mwili wote huyu mtu katika kifo nao ni upendo. Sema tu namna hii ya pili itawaacha wale seli wengine na mateso makali hadi kufa kwao. Seli wazuri wamapoumia na mtu naye anaumia lakini kwa upendo anavumilia.
Panda hatua moja tuje kwa binadamu binadamu anaweza kujihisi kwamba yeye yupo na anajifanyia kazi kwa ajili yake kwa faida zake lakini hilo jambo haliwezekaniki. Kwanza tukianza tu kwenye kufanya kazi mara nyingi ni kuwatumikia wengine. Mfano umejiajiri unanyoa nywele unawanyoa wengine. Unapika mamantilie umawapikia wengine. Mganga anawatipu watu wenzake wanaomzunguka. Kwa kufanya hivyo unafanya kile ambacho Mungu anataka; kuwatumikia wengime na kumtumikia yeye. Na Mungu naye anajishughulisha na kuendelea kuwepo kwa sisi wote duniani pamoja na vyote vinavyotuzunguka ili tuendelee kuwepo kwa ujumla wake. Wanazaliwa wanadamu wengine wengine wanafariki. Wote tunapendezwa na kukua na maendeleonya kiuchumi. Mungu pia anayafurahia hayo ikiwa yanaleta hali nzuri kwa wote viumbe, wanadamu na mazingira. Wote wanadamu, majirani na Mungu huchukizwa pale mtu anapoamua kukua tuu hata kwa madhara kwa watu wengine. Mtu ambaye badala ya kuwatumikia watu ataamua kuwatumia watu kujikuza pasipo faida yoyote kwa watu na dunia kwa ujumla anaenda kinyume na mantiki senseless. Basi yanaweza kumpata mabaya kutokana na mifumo tuliyojiwekea labda mwizi atafungwa gerezani. Au kuugua kutokana na matumizi yaliyopitiliza ya chochote hadi akajiharibu. Au kwa upendo akaachwa aendelee kuishi japo hii itakuja kwa gharama ya maumivu ya wale wengine wote wenye kuwa wema machoni pa Mungu. Lakini mwisho wa siku utakuja na kila kitu kuvunjwavunjwa na hukumu kupitishwa.
Baada ya kufa sasa ndiyo kila kipengele kitajihukumu kutokana na kiwango kilichofuata hiyo mantiki. Kama kilifanya vyema ni furaha tuu milele na kama kilifanya visivyo ni shida tuu milele. Kama ambavyo sisi binafsi hufanya makosa na kuumia nafsini. Na wakati mwingine kutamani kurudi nyuma na kurekebisha makosa. Labda ni kweli huwa zinatolewa nafasi za pili ili kuja kurekebisha makosa hilo sina hakika japo uwezekano ni mkubwa wa ukweli huo. Au labda kile kilichotenda vibaya kinarudishwaga tena levo ya chini ili kikajifunze kutenda mema baadaye kitapandishwa. Kwa usemi huohuo na kile kilichotenda vema basi kitarudishwa katika levo ya juu yake maana kimeuthibitishia mfumo kwamba kinafahamu lengo lake. Aliye mwaminifu kwa kidogo tunaweza kumuongeza majukumu zaidi maana tunamuamini au sio? Wapo watu wanaoamini hivyo. Mfano labda kwenye ufufuo ile kuvikwa miili mipya itakuwa na zile taarifa za seli zilizofanya vizuri wakati wa uhai wake. Maana tofauti na kufanyiana kazi hapa duniani tupo pia kwa ajili ya kujifunza kitu fulani.
Basi ndugu zangu nahitimisha; kama ambavyo neutroni zipo kwa ajili ya protoni, nyutroni wenzake zenyewe na ulimwengu mzima kwa ujumla. Ndivyo ambavyo atomu nzima ipo kwa ajilinya atomu wenzake, lengo fulani la uwepo wa maada na ulimwengu mzima kwa ujumla. Ndivyo ambavyo seli zipo kwa ajili ya seli wenzake, viungo na tishu mtu na dunia na ulimwengu mzima kwa ujumla. Ndivyo ambavyo sayari zipo kwa ajili ya zayari nyingine, vimondo, jua na lengo zima la kuanzishwa kwa sayari na mfumo wa jua na ulimwengu mzima kwa ujumla. Ndivyo hivyohivyo ndugu zangu magalaksi yapo kwa ajili ya magalaksi mengine na gesi, na nafasi na ulimwengu mzima kwa ujumla. Basi kwa mfananisho huo mimi nasema wazo la Mungu ni wazo halali kabisa na linaleta mantiki kuliko ile kuwepowepo tu bila lengo lolote, bila jukumu lolote. [Ili unielewe basi rudia hii aya ya mwisho ukibadili [replace] neno ulimwengu mzima kwa ujumla na neno Mungu.] Mungu yupo ndugu zangu Mungu yupo. Nakubali kuwa anaweza kuwa katika muonekano tusioweza kuung’amua kisawasawa hadi inapelekea kuambizana sisi kwa sisi kuwa hachunguziki. Ni sawa lakini lile wazo la kwamba yupo linabaki palepale. Na sifa zake za kuwa na upendo wote na ujuzi wote ni sahihi kabisa. Kuwepo pote hiyo ndiyo haswaa imejionesha katika makala hii ndefu. Hata kama sayansi au watu wataamua kumficha mbali juu kabisa infinity au kumficha chini kabisa infinitesimall bado Mungu ataonekana tu kwa sababu yeye ni mwanzo na mwisho, hana mwanzo wala mwisho ni hamna na ndo kila kitu. Ukivichunguza vitu vikubwa juu kabisa yako utamkuta mungu. Na hata ukivichunguzwa vitu vidoogo vya wewe na chini yako utamkuta Mungu pale. Somo lolote ukilichukua ukalifafanua ukalisoma na ukalichunguza mpaka mwisho wake utamkuta Mungu. Kwa hiyo iwe ni baiolojia, fizikia, filosophia mwisho utamkuta Mungu. Nawasilisha.
View attachment 2174803
Atajibu kama alivyojibu kwa HITLER alivyofanya mauaji ili PUTIN naye aondoke kabisa na utawala wake wa kinyama.Ongea na Mungu mwambie kule Ukraine watu aliowaumba Putin anawaua kinyama bila huruma yoyote. Mbona Mungu kanyamaza!
Unaongea kana kwamba unauhakika na unachokisema..Hii ni ajabu.!Kuna ukakasi kidogo kwenye hoja ya anatupangia, hatupangii kila kitu per se. Japo ni kweli anao uwezo wote. "So unaweza kumuomba na ukapewa mbona?"
Unarudia kile kile, unapinga hoja kwa maelezo yasiyo na ulazima ili ionekane umejibu tuIla sasa yeye akiamua anaweza kufanya chochote, japo ni mara chache anaamua hivyo. Mara nyingi anakuacha wewe ndio uamue unachukua njia ipi na unaacha ipi. Ni kwamba anatupenda saaana ndiyo maana.
Nadhani ulimaanisha theists, anyway ni kwamba kila mmoja anatumia anachokifahamu kutetea hoja yake. Sasa kuna ubaya gani mimi kutumia baiolojia. Kumbuka atheists hawazipagi uzito hoja zinazotoka kwenye vitabu vya dini[ambavyo ndio specialized sources kabisa]. Kwa nini unikataze kutumia kitu tunachoshare wote na kukikubali? Wapo watakaotumia dini, saikolojia, morality etc wote tunajenga nyumba moja.Sikiliza wewe, katika Atheist ninao wafahamu wanaotoa hoja zao humu, sijawahi ona hata mmoja akitumia msingi wa maumbile katika kutete hoja zao juu ya uwepo wa huyo mungu
Ungemtaja ID kwa ushahidi zaidi maana sijaona aliyepuuzwa katika huu uzi kila swali lililoulizwa humu limejibiwa ama na mimi, au mdau yeyote aliyekuwa na majibu wakati huo. Tuelekeze post namba ngapi haijajibiwa tusaidiane kujibu kuna kusahau pia.kuna mmoja aliyejaribu kuweka sawa sintofahamu yako kwa kuchanganya elimu ya kimaumbile na hiyo ya kiroho ili kuweka mambo sawa naona mmeishia kumpuuza tu
Hapana namemaanisha atheist, hawapendelei kutengeneza hoja katika fani za kimaumbile kutetea mawazo yao ikiwemo hii ya biolojia, kemia, fizikia, astrolojia n.kNadhani ulimaanisha theists,
sikukatazi kutumia fani yako kutetea imani yakoanyway ni kwamba kila mmoja anatumia anachokifahamu kutetea hoja yake. Sasa kuna ubaya gani mimi kutumia baiolojia. Kumbuka atheists hawazipagi uzito hoja zinazotoka kwenye vitabu vya dini[ambavyo ndio specialized sources kabisa]. Kwa nini unikataze kutumia kitu tunachoshare wote na kukikubali? Wapo watakaotumia dini, saikolojia, morality etc wote tunajenga nyumba moja.
Kama nitakuwa nimeshuhudia juu ya uwepo wa huyo mungu mfano wako unaweza kuwa na matokeo kwanguNa kama nyongeza umesoma mfano wangu wa upendo wa mme na mke. Naongezea mke anaweza hata kumruhusu huyu mume akanunue pizza huko nje akitaka na faida zake na hasara zake matokeo atayapata sambamba na uchaguzi wake. Mungu anakuruhusu ukitaka gari kalitafute kwa bwana Kiichiro Toyoda ndiko yanakotengenezwaga na anao utaratibu wake ili akupe gari utaujua hukohuko.
Kwani bro wewe ulitaka uamue vipi kabla wakati ambao hata haujakuwepo bado?Hakuna kitu kama hicho kinachoitwa uhuru kwa mungu aliyekuwa peke yake akaamua vyote vitokee baada yake
Ni vema kuzungumzia wakati nipo naweza kuamua vipi.?Kwani bro wewe ulitaka uamue vipi kabla wakati ambao hata haujakuwepo bado?
yaani katoto kadogo kamezaliwa Ukraine kamepigwa mabomu na warusi na wazazi kamepoteza akiwa hafahamu lolote linaloendelea mpaka kufikia hali hiyoNafasi ya maamuzi ya mwanzo ni yake mwenyewe. Lakini mengi ya sasa na baadaye una nafasi ya kuhusika nayo ni wewe tu kuchagua
Bado naitafiti hii dhana ya utashi huru binafsi/free will, kweli hata wikipedia [kwa kuanzia] wametoa maelezo meeeengi sana na debate ndefu sana. Na mimi bado naendelea kutengeneza nadharia nzuri kuhusiana na hicho kitu.Ni vema kuzungumzia wakati nipo naweza kuamua vipi.?
Hiyo kawaida ya kusafirisha mawazo katika kipindi ambacho hukuwahi kuwapo ndio husababisha matatizo mengi ya kiufahamu
Wajuvi wanafahamu tahadhari za kuchukua unapotafiti vitu vilivyo nje ya wakati wako
yaani katoto kadogo kamezaliwa Ukraine kamepigwa mabomu na warusi na wazazi kamepoteza akiwa hafahamu lolote linaloendelea mpaka kufikia hali hiyo
Kesho kawa mtu mzima hana miguu halafu unakapa ufafanuzi kama huu juu ya mungu wako..!
Mimi nakuambia kweli anaweza kuwasamehe warusi kwa yote waliyomfanyia lakini si huyo mungu wako
Eti kaumba uhuru na mtu ana hiyari ya kuchagua.!? Kwani yeye aliomba kwa hiyari azaliwe Ukraine.!?
Hivi hujui katika uchaguzi wa kibinadamu ni maumivu kwa binadamu wengine.! Huu nao ni ugonjwa kutolifahamu hili
Hivi wakati unaarchive hiyo great power from a great responsibility, While u making many shitBado naitafiti hii dhana ya utashi huru binafsi/free will, kweli hata wikipedia [kwa kuanzia] wametoa maelezo meeeengi sana na debate ndefu sana. Na mimi bado naendelea kutengeneza nadharia nzuri kuhusiana na hicho kitu.
Lakini tangu mwanzo nimekuwa nikiamini kuwa kuna ngazi kadhaa za mtu kujiamini kwamba anayo maamuzi. Na kila ngazi unayochagua basi unazipata faida na hasara zake wewe mwenyewe. Nilisamaraizi hivii;View attachment 2225742
Basii basii bro basii heeh! umekasirishwa sana na neno shit hadi limeziba uelewa? basi badili neno 'shit' kwa neno 'things'. Nimesema 'we' nikimaanisha mimi, wewe, yule pamoja na nguvu zote zinazotuwezesha tunashirikiana kufanya mambo yatokee.Hivi wakati unaarchive hiyo great power from a great responsibility, While u making many shit
Hivi nani atakuwa kakaa kama jiwe la mzani kusubiria wewe ufikie unachokitaka.! Hivi umewafikiriaje wengine
Hivi uoni ni aina ya ujeuri fulani mtu aliyejizoesha kuuzoea mpaka umeroot kwenye bongo yake mpaka anajiona kuna kitu anafanikisha.?
Kujipa maana wakati huna maana ni ugonjwa wa akili
Alaah kumbe.! kama vile wahuni wa huku kwetu wanavyotukanana "we ms*ng noma" unashangaa jamaa hakasiriki anachekacheka tumno kwangu] Mimi ikitokea mmarekani mweusi [au mtu yeyote] akaninong'oneza sikioni 'Make shit happen broh' ntachukulia ananitia moyo kufanya maendeleo ya maana kabisa.
Nitahisi kaniambia nijizime data niruhusu ujinga fulani upite maisha yasonge yaani kama nisitilie maanani kitu fulani kwa mkazoKwani wewe ikitokea mmarekani mweusi anakuambia 'Make shit happen' utaelewa nini?
Yas ni mfano wake mzuri, inaonesha umeelewa. Sema bado kitukimoja ujifunze kinaitwa 'kuvaa viatu vyao' hata kama wewe hutatembea navyo. Hao jamaa hawatukanani ni wanaongea.Alaah kumbe.! kama vile wahuni wa huku kwetu wanavyotukanana "we ms*ng noma" unashangaa jamaa hakasiriki anachekacheka tu