Mimi ni mwanafunzi Ufundi wa umeme wa magari. Changamoto nilizoziona mpaka sasa

Mimi ni mwanafunzi Ufundi wa umeme wa magari. Changamoto nilizoziona mpaka sasa

Kila harakati inachangamoto zake kikubwa ni kuwa mvumilivu ili kutimiza ndoto yako

Mungu abariki kazi ya mikono yako
Tanzania matusi gereji ni sawa na kanisani kusema bwana asifiwe. Nimewahi kufanya kazi nilepitch pale mwanza karibu na mwatex aisee yule muhindi alikuwa na matusi ya dunia nyingine siyo tunayoishi hii maana nilkuwa sijawahi kusikia matusi kama yale. Japo mimi alinikubali sana kujituma na nidhamu.(fani yako hii ya umeme nami ndo fani yangu )

Nikaenda gereji nyingine kwa mnyatunzu yupo barabara ya kwenda ilemela ukipita pansias unakata kulia wanapaita sabasaba karibu kabisa na mbao fc au kwa waunza mbao na feniture.

Yule jamaa alikuwa hajawahi kumuita mtu jina lake hasa hawa manyokaa
pale nilikuta mtu anaitwa kisimi imagine! na majina mengine ya aina hiyo.Ukweli nidhamu nakujituma nilikuwa napendwa sana ila sikutukanwa mimi ijapokuwa kuna matusi ya general hayo nilikuwa siya kwepi.

Komaa dogo utafika mbali sana hapo Arusha kuna jama angu ukiitaji kujifunza zaidi mimi siyo mchoyo nakuunga nae ni dogo tu anakuzidi kama miaka6 hivi yupo vzr sana kwenye umeme wa magari
 
Hongera mkuu mimi pia nimeingia garage nikiwa na umri mkubwa tena zaid yako miaka 25, we endelea kupambana tu garage kaza kwny practicals, theory jifunzie online maana kuna mda mafundi unawauliza maswali hawakupi majibu ya kurizisha wakizingua ingia google na youtube kila la kheri
 
Mkuu nashukuru sana kwa ushauri wako. Japo sijajua sana kuhusu veta ufundishaji wao. Lakini ninachompendea mwalimu ni mtu anakuacha unafanya.

Lakini pia nafikiria nitakapoendelea kujua zaidi mbeleni niende vets ili nipate vyeti kabisa officially.
hapa ndio itafeli. endelea kufanya practical
ingia youtube penda kusoma mada zako. na ukifaham.kifaa chako obd scanner. magar ya kisasa haya yenyewe inakuambia. yenyewe
 
Back
Top Bottom