Mimi ni nani na ni mtu wa aina gani hilo ndio swali ambalo huwa najiuliza

Mimi ni nani na ni mtu wa aina gani hilo ndio swali ambalo huwa najiuliza

Melancholic

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2018
Posts
3,076
Reaction score
5,483
Mimi ni nani na ni mtu wa aina gani hilo ndio swali ambalo huwa najiuliza mara nyingi ninapokuwa peke yangu.

Mimi ni mzaliwa wa mkoa wa mara ni mtanzania halali ila tabia zangu zimekuwa za kipekeee sana toka nipo mdogo nimekuwa ni mtu wa kutafakari sana muda mwingi napenda kukaa peke yangu na kusoma vitabu na mara nyingi napenda kukaa kwenye fukwe za BaharI peke yangu ndio starehe yangu kubwa.

Sina marafiki zaidi nina watu wa kujuana nao tu labda majirani zangu, au wafanyakazi wenzangu sihitaji marafiki maisha yangu nayaona ni mazuri sana kuwa peke yangu.

Mimi Ni mpole huwa siongei sana japo huwa ninapenda kucheka sana ila ukinikwaza hasira zangu huwa ni mbaya huo ugomvi unaweza kuishia katika majengo ya serikali. Na kuchukizwa kwangu pia huwa sio rahisi.

Sipendi mpira wa kibongo kabisa na sishabikii simba wala yanga yani nikiona watu wanabishania kuhusu mpira wa bongo huwa nawashangaa mno.
Ninapenda mpira na ninashabikia timu moja tu duniani ni Arsenal pekee na mapenzi yangu kwa hii timu ni makubwa mno hata ikicheza saa 9 usiku nitaamka niitizame. sijui lolote kuhusu Madridi wala Barcelona, bayern au Juve pia huwa nawashangaa watu kuwa na timu mbili au 3 unakuta mtu bongo let say anashabikia simba, uingereza anashabikia liverpool ukienda uhispania anashabikia labda barcelona huwa nawashangaa sana hawa watu hivi uwezo wa kupenda timu mbili au tatu mnautoa wapi.

Pia sio mpenz wa bongo freva ya wapiga kelele bali ni muumini wa bongo freva zilizotungwa kwa IQ kubwa ambazo zipo Emotional kama penati ya mwisho ya Nash Mc, Sihitaji marafiki na Propaganda ya Fid Q, Tafakari ya suma mnazaleti, Sirudi tena na nishauri za mabeste Miss tanzania ya solo na ngoma zote za roho 7.

Na kingine nasikiliza zaidi miziki ya trance na Electronic dance hasa ambazo zipo emotional sijui labda sababu muda mwingi napenda kutafakari na waandaji wa hizi ngoma kwenye swala la emotional wako vzr mno. huu miziki nimeanza kuupenda nikiwa darasa la pili na mpaka sasa nina kama ngoma 3000 za trance na electronic dance yani simu yangu imejaa hizo ngoma sijui chochote kuhusu zuchu, diamond au mboso

Watu kama akina Craig Conelly, Cristina Novelli, Gareth emery, Ferry tayle, Ana criado , Emma hewitt, Dash berlin Ben gold, Andrew rayel na wengineo wengi hao ndio wanamuziki wangu bora.
Nimekuwa mtu wa kutafari sana mpaka naona nywele zimeanza kuisha kichwani najiona ni mtu wa kipekee sana na kuna mtu aliwahi niambia kuwa nina akili nyingi japo sikufanikiwa kusoma sana. Lakini najiona ni mtu mwenye utashi mkubwa sana kiac kwamba nineshindwa kupata watu wa kariba yangu
 
Ukikua utaona ulichoandika hapa ni unyumbu tu!.

kuzaliwa mahali fulani si kosa,kuonyesha uwezo ulionao pambana ukakae huko uholanzi lkn kutuona sisi samaki na unakuja kwenye jukwaa la samaki kutuuliza wewe ni nani..?!! basi tufanye hivi wewe ni samaki aina ya mumi.
 
Wakati naanza kusoma nilisha jua tatizo lako nikasema sitakuambia ila nilipo endelea kusoma nikakuta kweli umelitaja mwenyewe sawa sawa na nilivyo taka kukuambia ugonjwa wakoo unaitwa (self slave mind) hauna marafiki kwa sababu ujawa na marafiki ambao slave mand yako inawakubali hasa watu weupe wa ulaya. Watu kama wewe utamani sana kuwa na mke au mume mzungu na kuwa na watoto wenye uzungu kutokana na kuoa mzungu au kuolewa na mzungu, watu kama wewe wakizaa mtoto akachukua rangi nyeusi uchukia na kutamani watoto weupe au wachukue rangi za wazungu walio waoa.
 
Wakati naanza kusoma nilisha jua tatizo lako nikasema sitakuambia ila nilipo endelea kusoma nikakuta kweli umelitaja mwenyewe sawa sawa na nilivyo taka kukuambia ....ugonjwa wakoo unaitwa (self slave mind) hauna marafiki kwa sababu ujawa na marafiki ambao slave mand yako inawakubali hasa watu weupe wa ulaya....watu kama wewe utamani sana kuwa na mke au mumu mzungu na kuwa na watoto wenye uzungu kutokana na kuoa mzungu au kuolewa na mzungu ...watu kama wewe wakizaa mtoto akachukua rangi nyeusi uchukia na kutamani watoto weupe au wachukue rangi za wazungu walio waoa....
Unaongea pumba mzee mi naongelea tabia wewe unaniambia mambo ya rangi shame on you
 
Unaongea pumba mzee mi naongelea tabia wewe unaniambia mambo ya rangi shame on you
Tabia inasababu zake ....wewe tatizo lako ni rangi yako na uafrica ndiyo vimekufanya huwe disappoint na kusababisha hizo tabia ...sifa moja ya watu wenye tabia yako ni kutokukubali ukweli kuwa awapendezwi na uafrica wao .
 
Tabia inasababu zake ....wewe tatizo lako ni rangi yako na uafrica ndiyo vimekufanya huwe disappoint na kusababisha hizo tabia ...sifa moja ya watu wenye tabia yako ni kutokukubali ukweli kuwa awapendezwi na uafrica wao .
Wapi nimesema nataka kuwa mzungu chief nimesema numezungumzia tabia na sijaongelea swala la rangi hapa em jitambue kidogo
 
Wapi nimesema nataka kuwa mzungu chief nimesema numezungumzia tabia na sijaongelea swala la rangi hapa em jitambue kidogo
Uwezi kuliongelea swala la rangi kwa sababu ndiyo tatizo lako lilipo ....na unalijua ila uwezi kulikubali ni kawaida kwa watu wenye tatizo kama lako kuwa hivyo.
 
Back
Top Bottom