Habari JF members..
Nina issue huwa inanisumbua akili kidogo kuhusu Mimi mwenyewe.
Mimi Huwa nina uwezo wa kuhisi kifo kwa mtu nikimuangalia. Yaani kuna hali fulan inaniambia huyu mtu hana muda mrefu atakufa na hii hali huwa inatokea mara chache sana.
Kitu kingine, ni ndoto zangu Huwa naota kitu kinakuja tokea kweli ila sio ndoto zote ni ndoto chache sana.
Au nikifanyiwa kitu kibaya na hicho kitu kikaniumiza sana kuliko kawaida basi nikiongea neno lolote kwa yule aliyenifanyia ubaya basi lazima litamkuta jambo ambalo si zuri.
Je, hii Hali ni ya kawaida au?