Mimi nilifanya mtihani wa darasa la saba mwaka 2013, wewe je?

Hapakuwa na darasa la Saba miaka hiyo, ilikua la nne, ukifaulu unaenda middle school mpk la 8, secondary la 9 na kuendelea.
Sawa, sasa alivyosema 1961 alimaanisha ndyo mwaka aliyo maliza la nne au?
 
Mwaka 1996 Shule ya msingi Rulenge wilayani Ngara.
Hawa ambao mwaka huu wanaomaliza elimu ya msingi sio wadogo zetu bali ni watoto wetu. Wadogo zetu wamemaliza elimu ya msingi mwaka 2003 kurudi nyuma.
Pia kumbukumbu zinaniambia wakati nahitimu elimu ya msingi nilikuwa Nina umri wa miaka 19.
Kwangu mimi hao wa sasa ni wadogo zangu

Lakini mkuu kama ulimaliza na miaka 19 basi ulimaliza ukiwa kijeba kabisa.
 
Khaswaa! Hata nifanye kosa gani nilikuwa siadhibiwi na mwalimu wakike. Hao wakiume pia saa nyingine walikuwa wakinigwaya wakihofia nitawapopoa kwa mawe usiku njiani wakitoka ulevini.
 
Ulivyofika sekondari ikawaje? Nadhani huko ndipo utemi ulizidi kushamiri
 
Sekondari sikwenda! Miaka ile sekondari za Kata hazikuwepo kwahiyo ufaulu ulikuwa mwembamba sana. Darasa Zima walioenda secondari hawazidi wanne!, na wote walikuwa wanatokea familia za viongozi au matajiri. Mmoja wazazi wake wote walikuwa walimu. Baba Mwalimu wa sekondari na mama Mwalimu wa primary. Wapili baba yake alikuwa mkurugenzi wa shirika la Ngara District Development Organization N.D.D.O. Watatu wazazi wake walikuwa na pesa wakampeleka shule za private, wanne alikuwa anatoka familia ya wafanyabiashara wakiarabu wakampeleka nchini Uganda kuendelea na masomo.
Mimi pamoja na ubabe niliokuwa nao, huko msikitini nilikuwa vizuri kwenye masomo ya dini kwahiyo baada ya kumaliza la 7 nikajiemdeleza na elimu ya dini na hadi sasa ni Mwalimu wa madrassa.
 
Mkuu kwa maelezo hayo nimejifunza kwamba zamani elimu ilikuwa changamoto, pia walinufaika wale walio na uwezo pekee...

Lakini naamini Mungu alikuongoza njia sahihi mpaka sasa unafanya kazi ya kueneza na kufundisha elimu yake, Allah azidi kukupa nguvu na uwezo wa kufundisha na kuelimisha zaidi.
 
Aamiyn. Miaka ile baadhi ya shule hasa za vijijini ilikuwa yaweza pita hata Miaka 5 bila kufaulisha mwanafunzi hata mmoja. Ufaulu umeongezeka awamu ya kikwete baada ya kujengwa sekondari za Kata ndio unakuta miaka ya leo zaidi ya nusu ya darasa wote wanafaulu.
 
Sio wa
Mwaka 1996 Shule ya msingi Rulenge wilayani Ngara.
Hawa ambao mwaka huu wanaomaliza elimu ya msingi sio wadogo zetu bali ni watoto wetu. Wadogo zetu wamemaliza elimu ya msingi mwaka 2003 kurudi nyuma.
Pia kumbukumbu zinaniambia wakati nahitimu elimu ya msingi nilikuwa Nina umri wa miaka 19.
Sio wajukuu kweli😃
 
Back
Top Bottom