Sekondari sikwenda! Miaka ile sekondari za Kata hazikuwepo kwahiyo ufaulu ulikuwa mwembamba sana. Darasa Zima walioenda secondari hawazidi wanne!, na wote walikuwa wanatokea familia za viongozi au matajiri. Mmoja wazazi wake wote walikuwa walimu. Baba Mwalimu wa sekondari na mama Mwalimu wa primary. Wapili baba yake alikuwa mkurugenzi wa shirika la Ngara District Development Organization N.D.D.O. Watatu wazazi wake walikuwa na pesa wakampeleka shule za private, wanne alikuwa anatoka familia ya wafanyabiashara wakiarabu wakampeleka nchini Uganda kuendelea na masomo.
Mimi pamoja na ubabe niliokuwa nao, huko msikitini nilikuwa vizuri kwenye masomo ya dini kwahiyo baada ya kumaliza la 7 nikajiemdeleza na elimu ya dini na hadi sasa ni Mwalimu wa madrassa.