Mimi nina majumba sio nyumba, ila sitaki kuyaonyesha – Steve Nyerere

Mimi nina majumba sio nyumba, ila sitaki kuyaonyesha – Steve Nyerere

dah. hili shati ukienda kwa fundi unaweza kutoa shuka na maforonya mawili ya mito.

1472736158756-jpg.391744
 
Hahaaaaa ndo Mara ya kwanza kuskia MTU Ana Majumba alafu yeye amepanga haaha yaan watu wanapigania juu chini ili wawe na vibanda vyao kuepukana na kero za wenye nyumba yeye majumba yote hayo alaf amepanga.. [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] daah kweli bongo movie ni waigizaji hadi kwenye maisha halisi
 
Maneno yangekuwa yanaua, tungeua wengi!
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] Sana maana kuna haka ka msemo ka "wanaume wa dar " kashatrend hadi kwenye magazetu
 
Ni kweli ana majumba ila ni mapagale, hajawahi kumaliza kujenga nyumba ni kama ana kilaana fulani na anahonga sana yule mwanamke wellu
Hiyo anayotaka amia ipo madale, ndo inayokaribia kukamilika, ni nzuri kwa kweli
 
uyu steve asitudanganye aseme hyo nyumba itakayoisha ndo atahamia ndo hiyohiyo sio na majumba sitak kuonyesha we unanyumba nyingi unaenda kupanga wapi na wapi
 
xSteve-Nyerere.jpg.pagespeed.ic.pWqNEXMRHA.jpg


Msanii mkongwe wa filamu Steve Nyerere amedai yeye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanamiliki nyumba nyingi lakini hataki kuzionyesha.
Akiongea katika kipindi cha Uhondo cha EFM Jumatano hii, Steve Nyerere amedai yeye haoni ufahari wa kuonyesha mali alizonazo kama wanavyofanya baadhi baadhi ya wasanii.

“Mimi nina majumba sio nyumba ila sitaki kuonyesha instagram,” alisema Steve Nyerere. “Pia kuna nyumba kubwa ambayo ndiyo nitaamia ikiisha, kwa sasa hivi nimepanga Mkwajuni Kinondoni na naishi na familia yangu,”

Katika hatua nyingine mwigizaji huyo amewataka watanzania kuhudhuria show yake ya ‘East African STANDUP COMEDY’ ambayo itafanyika kwa mara ya kwanza Jumamosi katika hotel ya Protea jijini Dar es salaam.
Wasanii wa kibongo wanaigiza hadi kwenye maisha ya kweli............Sasa uwe na majumba halafu wewe upange si utakuwa na upungufu wa akili.
 
Labda alikua ana act wakati anaongea hahahaaa!!! majumba mchezo...
 
Back
Top Bottom