Mimi Nina tatizo Moja, nataka kuanzisha biashara ya genge la nyanya, vitunguuu, mboga mboga ila naogopa watanichukuliaje?

Habari zenu ndugu zangu,

Mimi Nina tatizo Moja, nataka kuanzisha biashara ya genge la nyanya, vitunguuu, mboga mboga ila naona aibu kutoka na mazingira niliyopo na namna watu watanichukulia

Naombe ushauri wenu?
Mtu akiomba ushauri, asaidiwe kimawazo. Kama huwezi kumsaidia mawazo kaa kimya. Unapoandika maneno hasi ni sawa na kumharibu kiakili zaidi.

Watu wameumbwa na haiba tofauti, wengine ni sanguine wengine ni melancholy. Kwa mawazo ya haraka kutokana na maelezo yako ni kuwa una haiba ya aibu au status yako katika eneo ulilopo ni kubwa kulinganisha na kitu unachoenda kukifanya.

Nikivaa kiatu chako nitajaribu kukupa shauri mbalimbali utachagua mwenyewe ambao utafaa.

1. Tafuta mtu wa karibu uliyezoeana naye ambaye hana aibu ili aweze kukupa company katika kipindi cha mwanzo cha biashara ambacho unakuwa hujazoeleka machoni kwa watu.

2. Jitahidi sana kujiweka katika uhalisia wa biashara. Unatakiwa ujue muonekano wako unachangia sana katika confidence yako katika eneo husika, mavazi yako na general appearance inatakiwa iendane na kitu unachokifanya.

Katika hili siwezi kuongea sana maana unaelewa haiba yako na jinsi unavyoweza kujiweka ukaongeza confidence yako kutokana na muonekano.

3. Katika siku za mwanzoni jitahidi sana kuamka mapema sana. Hapa namaanisha usiwakute wateja wanakusubiri Bali wewe ndio uwasibiri wateja wako.

Kwa kuwa unaogopa macho ya watu, siku za mwanzo jitahidi sana kufanya mno yako mapema Ili watu wawe wanakukuta umeshafika sokoni unawasubiria.

4. Uoga / Aibu ni swala la muda tu na huwa linaisha kulingana na muda. Kinachokusumbua wewe ni mwanzo tuu ila ukishazoeleka utaona kawaida na utafurahi mwenyewe na roho yako.

5. Kama una aibu ya machoni, jitahidi sana kutengeneza mazingira (realm) yako katika taswira ya macho ambapo utajiona uko peke yako.

Jitahidi sana kuikataa aibu. Ni ugonjwa unaoua maono, ndoto na future. Mwisho wa siku yanayobaki ni majuto ambayo yatakupa mawazo ya kujiona huna thamani, ambayo vyote hivyo vitapelekea msongo wa mawazo.

Afu kuna jambo jingine unatakiwa ujue rafiki yangu. Kuhisi kwamba watu watanionaje ni illusion inayotokea ndani yako mwenyewe. Watu hawajali chochote kuhusu wewe, hiyo ni illusion umeitengeneza mwenyewe ndani yako kwenye ubongo kama mechanism to forestall you from being doing what you aim to do. Ubongo umeumbwa kutengeneza illusion Ili kutuzuia kwenye mambo ambayo wenyewe unatafsiri uncomfortable au ni hatari kwetu.

Kila mtu ana woga ila Courage ndio inayohitajika.

PAMOJA NA WOGA ULIONAO. HAVE COURAGE and START.
 
Asante sana katika majibu yote niliypjibiwa umenitia moyo na nguvu ya kufanya biashara
 
Umri ukisonga mbele baadae mzee ndio utakuja kujuta wale uliokuwa unawaonea aibu kumbe walikuwa hawana mda nawe,ndio utalia na kusaga meno
 
Hama unapoishi nenda mkoa mwingne alafu maintain low profile,na genge inalipa sana, kama mrembo utashangaa wateja wako wengi watakuwa vijana wa kiume.
 
Jipe ujasiri itakua ngumu mwanzo lakini baada ya kama mwezi hivi utazoea. Kama mahusiano yako na watu hapo mtaani sio mabaya wewe fanya biashara yako tu
 
Hama unapoishi nenda mkoa mwingne alafu maintain low profile,na genge inalipa sana, kama mrembo utashangaa wateja wako wengi watakuwa vijana wa kiume.
Hata ukiamia uko mkoani mpaka uje kuzoeana na watu ni shughuli ya mida mrefu halafu kwa uzoefu wangu wa kuishi na watu uko mikoani wana ubaguzi wa kikabila.

Dada ajilipue tu hapo hapo mtaani kwake
 
Habari zenu ndugu zangu,

Mimi Nina tatizo Moja, nataka kuanzisha biashara ya genge la nyanya, vitunguuu, mboga mboga ila naona aibu kutoka na mazingira niliyopo na namna watu watanichukulia

Naombe ushauri wenu?
Ni rabisi sana. Fanya kiutofauti na wengine, mpangilio wa banda lako, usafi wa hali ya juu, mpangilio wa mboga mboga na matunda uwe tofauti kabisa na wengine, unavyoweza kuvipack au kuvifunga vizuri fanya hivyo, usiweke mamboga mboga kwenye ndoo au mabeseni ya maji kama wafanyavyo sokoni eti kuzui zisiharibike wewe fanya tofauti, hata ukiweka watu wasione.

Google ona mpangilio wa matunda na mboga mboga huko kwa wenzetu kwenye vigetable open market. Kimsingi peruzi picha nyingi kwenye mtandao au andika tuu vigetable market halafu angalia images tuu yaani picha tuu.

Haza zile meza wanazopanga ulaya huwa haziwi flat kama zetu. Nyingi huwa zimekaa ikiwa ndefu upande mmoja na mwingine fupi, yaani kama zile shelf za kuwekea vitabu au vipeperushi wakati wa maoneshe au bidhaa ili kila mtu azione, hapo ndipo utapanga mboga mboga zako na matunda kwa mtindo huo.
Na zilizo kwenye shelf hiyo au hiyo meza iliyobinuka upande mmoja au meza yenye slope basi ziwe mboga zenye mvuto na zilizofungwa vizuri ya kumvutia kila apitaye. Nyanya, vituu usirundike bila mpangilio no weka hata kwenya mabox mazuri, matunda hali kadhalika.
Kwa ufupi kuwa smart na msafi hasa. Usitupe tupe mabaki ya vyakula au majani majani au nyanya au matunda mabovu au ukaweka matenga matenga bandani mwako.

YOTE HAYO HAYAHITAJI ETI MTAJI TOFAUTI NA ULIO NAO BALI AKILI NA MAARIFA TOFAUTI NA WALIYONAYO WENZIO.
HUTA ONA AIBU UKIFANYA HIVYO BALI UTAFURAHIA NA KUPENDA SANA GENGE LAKO NA KILA MTUU ATASHANGAA NA KUKUSIFU.
BUT WATU WENYE MITAJI WATAKUANGALIA WATAIGA NA KUFANYA ZAIDI, HILO LISIKUSUMBUE. ALL THE BEST.
 
nimeshuhudia watu kuja wakitoba life kibiashara kuliko wenyeji mtu unaemfahamu yuko radhi akamuungishe stranger kuliko wewe native,akijitahd sana atakukopa.
 
I appreciate....I'll work on this
 
Habari zenu ndugu zangu,

Mimi Nina tatizo Moja, nataka kuanzisha biashara ya genge la nyanya, vitunguuu, mboga mboga ila naona aibu kutoka na mazingira niliyopo na namna watu watanichukulia

Naombe ushauri wenu?
Pole dear! Njoo pm nikupe ushauri mzuri
 
Back
Top Bottom