SIRE
Senior Member
- Feb 20, 2022
- 127
- 217
Mtu akiomba ushauri, asaidiwe kimawazo. Kama huwezi kumsaidia mawazo kaa kimya. Unapoandika maneno hasi ni sawa na kumharibu kiakili zaidi.Habari zenu ndugu zangu,
Mimi Nina tatizo Moja, nataka kuanzisha biashara ya genge la nyanya, vitunguuu, mboga mboga ila naona aibu kutoka na mazingira niliyopo na namna watu watanichukulia
Naombe ushauri wenu?
Watu wameumbwa na haiba tofauti, wengine ni sanguine wengine ni melancholy. Kwa mawazo ya haraka kutokana na maelezo yako ni kuwa una haiba ya aibu au status yako katika eneo ulilopo ni kubwa kulinganisha na kitu unachoenda kukifanya.
Nikivaa kiatu chako nitajaribu kukupa shauri mbalimbali utachagua mwenyewe ambao utafaa.
1. Tafuta mtu wa karibu uliyezoeana naye ambaye hana aibu ili aweze kukupa company katika kipindi cha mwanzo cha biashara ambacho unakuwa hujazoeleka machoni kwa watu.
2. Jitahidi sana kujiweka katika uhalisia wa biashara. Unatakiwa ujue muonekano wako unachangia sana katika confidence yako katika eneo husika, mavazi yako na general appearance inatakiwa iendane na kitu unachokifanya.
Katika hili siwezi kuongea sana maana unaelewa haiba yako na jinsi unavyoweza kujiweka ukaongeza confidence yako kutokana na muonekano.
3. Katika siku za mwanzoni jitahidi sana kuamka mapema sana. Hapa namaanisha usiwakute wateja wanakusubiri Bali wewe ndio uwasibiri wateja wako.
Kwa kuwa unaogopa macho ya watu, siku za mwanzo jitahidi sana kufanya mno yako mapema Ili watu wawe wanakukuta umeshafika sokoni unawasubiria.
4. Uoga / Aibu ni swala la muda tu na huwa linaisha kulingana na muda. Kinachokusumbua wewe ni mwanzo tuu ila ukishazoeleka utaona kawaida na utafurahi mwenyewe na roho yako.
5. Kama una aibu ya machoni, jitahidi sana kutengeneza mazingira (realm) yako katika taswira ya macho ambapo utajiona uko peke yako.
Jitahidi sana kuikataa aibu. Ni ugonjwa unaoua maono, ndoto na future. Mwisho wa siku yanayobaki ni majuto ambayo yatakupa mawazo ya kujiona huna thamani, ambayo vyote hivyo vitapelekea msongo wa mawazo.
Afu kuna jambo jingine unatakiwa ujue rafiki yangu. Kuhisi kwamba watu watanionaje ni illusion inayotokea ndani yako mwenyewe. Watu hawajali chochote kuhusu wewe, hiyo ni illusion umeitengeneza mwenyewe ndani yako kwenye ubongo kama mechanism to forestall you from being doing what you aim to do. Ubongo umeumbwa kutengeneza illusion Ili kutuzuia kwenye mambo ambayo wenyewe unatafsiri uncomfortable au ni hatari kwetu.
Kila mtu ana woga ila Courage ndio inayohitajika.
PAMOJA NA WOGA ULIONAO. HAVE COURAGE and START.