ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
mimi ni mkristo nishaamuaga sifanyi maombi yoyote sijui kuombea taifa sijui kuombea mambo mbalimbali mara kulia sijui kunena kwa lugha sijui kusali rozali mimi huwa nasali sala moja tu..ya baba yetu uliye mbinguni na huwa nasubiri ifike saa fulani kamili..07;00,08;00 n.k kwa hiyo kwa siku husali zaidi ya mara 15 hata nikishtuka usiku napiga goti chumbani kwangu nasema sala hii mara moja tu nalala anyway mambo ya kusali sio ya kujisifu kila mtu ana style yake na imani yake ,,ni sala maarufu sana toka kwa mwalimu yesu..Hii si sala ya kawaida, ni kama “muhtasari” wa mahusiano yote kati ya mwanadamu na Mungu.
ngoja tuifafanunue inaanzaga
Hapa kuna ujumbe mkubwa sana.Yesu hakusema Mfalme wa mbali,Muumba mwenye hasira bali alisema Baba yetu Mungu si wa mtu mmoja,wote tunaweza kumkaribia maanake kuna ukaribu wa kiroho na ulinzi...Na hii kusema “uliye mbinguni” ni kukumbuka kuwa pamoja na ukaribu wake bado ana mamlaka juu ya kila kitu duniani.
Hapa mtu anaanza kwanza kumtukuza Mungu kabla hajaomba mahitaji yake.Watu wengine sala zao zinaanza:nipatie,nifanikishe,nisaidie hili na lile ..Lakini mwamba Yesu akaonyesha kwanza mtambue Mungu kabla ya kujitazama wewe.Hii inafundisha nini? unyenyekevu.
Kimsingi ni unasema sitaki kuongozwa na dunia pekee, nataka mapenzi ya Mungu yaongoze maisha yangu na sio mifumo hii ya ulimwengu inayotuangusha dhambini kila dakika..
Hapa Yesu hakusema utupe utajiri wa miaka 50
Bali riziki ya leo hii Ina maana kuishi kwa kumtegemea Mungu hatua kwa hatua..kutokuwa mtumwa wa hofu ya kesho..Na “riziki” si chakula tu kuna afya,kuna amani,kazi,ulinzi,pumzi yenyewe
Hapa ndipo nguvu kubwa ya kiroho ipo na wengi hapa panatushinda kwa sababu tuna vinyongo tumeachana na wake zetu na waume zetu ila tunatakiwa tuwasamehe kwa sababu Watu wengi tu nataka kusamehewa makosa yetu tamaa zetu dhambi zetu uchafu wetu ..
lakini hatutaki kusamehe
Yesu akaunganisha vitu viwili huwezi kuomba rehema huku umejaa chuki moyoni Mstari huu unasafisha moyo wa mtu na hapa ndipo changamoto ilipo so ukifeli hapo hata uombe hivi kama moyo wako hujasamehe basi maombi yako hayaendi kumgusa MUNGU
kimsingii hii sala ni unaongea na MUNGU na unamuomba ulinzi ,toba na akuepushe na tamaa unazijua mwenyewe tamaa ulizonazo zinazonguzuka nyingi kwa sababu ya kutaka pesa na nyingine basi tu umekuwa mtumwa wa hayo unayopenda kuyafanya gizani..mangono yasiyo ya kawaida kujaribu kujaribu ambavyo hukutakiwa ujaribu...sasa ili umrudie Mungu sasa isali hii sala kwa siku mara 12 ..waislam wao si huwa wanasali mara 5 kwa siku wewe wapite nenda beyond kabla haijakufikia ile siku mbaya zaidi kwako
ngoja tuifafanunue inaanzaga
1. “Baba yetu uliye mbinguni”
Hapa kuna ujumbe mkubwa sana.Yesu hakusema Mfalme wa mbali,Muumba mwenye hasira bali alisema Baba yetu Mungu si wa mtu mmoja,wote tunaweza kumkaribia maanake kuna ukaribu wa kiroho na ulinzi...Na hii kusema “uliye mbinguni” ni kukumbuka kuwa pamoja na ukaribu wake bado ana mamlaka juu ya kila kitu duniani.
2. “Jina lako litukuzwe”
Hapa mtu anaanza kwanza kumtukuza Mungu kabla hajaomba mahitaji yake.Watu wengine sala zao zinaanza:nipatie,nifanikishe,nisaidie hili na lile ..Lakini mwamba Yesu akaonyesha kwanza mtambue Mungu kabla ya kujitazama wewe.Hii inafundisha nini? unyenyekevu.
3. “Ufalme wako uje”
Hii si tu kuhusu mwisho wa dunia.Ni kuomba haki ishinde,amani iongezeke,uovu upungue,Mungu atawale maisha yako kuliko tamaa zakoKimsingi ni unasema sitaki kuongozwa na dunia pekee, nataka mapenzi ya Mungu yaongoze maisha yangu na sio mifumo hii ya ulimwengu inayotuangusha dhambini kila dakika..
4. “Mapenzi yako yatimizwe duniani kama mbinguni”
Huu mstari naupenda sana na ndio mstari mgumu zaidi kwa watu wengi.Kwa sababu hapa unajiweka pembeni ni kama unasema si kila ninachotaka au kukiwish ndicho sahihi...Mungu anaweza kuona mbali kuliko mimi..Ni mstari wa kujitoa kabisa kwa Mungu na kuacha nature iamue Mungu mwenyewe akufikishe unapotakiwa..5. “Utupe leo riziki yetu ya kila siku”
Hapa Yesu hakusema utupe utajiri wa miaka 50
Bali riziki ya leo hii Ina maana kuishi kwa kumtegemea Mungu hatua kwa hatua..kutokuwa mtumwa wa hofu ya kesho..Na “riziki” si chakula tu kuna afya,kuna amani,kazi,ulinzi,pumzi yenyewe
6. “Utusamehe makosa yetu kama nasi tunavyowasamehe waliotukosea”
Hapa ndipo nguvu kubwa ya kiroho ipo na wengi hapa panatushinda kwa sababu tuna vinyongo tumeachana na wake zetu na waume zetu ila tunatakiwa tuwasamehe kwa sababu Watu wengi tu nataka kusamehewa makosa yetu tamaa zetu dhambi zetu uchafu wetu ..
lakini hatutaki kusamehe
Yesu akaunganisha vitu viwili huwezi kuomba rehema huku umejaa chuki moyoni Mstari huu unasafisha moyo wa mtu na hapa ndipo changamoto ilipo so ukifeli hapo hata uombe hivi kama moyo wako hujasamehe basi maombi yako hayaendi kumgusa MUNGU
7. “Usitutie majaribuni lakini utuokoe na yule mwovu”
Hapa kuna kukubali kuwa mwanadamu ni dhaifu.Ni kuomba usianguke kwenye tamaa ukamezwa na mausharerati ya dunia hii yaliyojaa mitandaoni.usimezwe na hasira...usiharibiwe na uovu wa dunia hii mbaya kabisa.. Kimsingi ni sala ya ulinzi wa kila siku.simu yako mwenyewe unaikemea isikupeleke majqribuni..UTAWEZA???kimsingii hii sala ni unaongea na MUNGU na unamuomba ulinzi ,toba na akuepushe na tamaa unazijua mwenyewe tamaa ulizonazo zinazonguzuka nyingi kwa sababu ya kutaka pesa na nyingine basi tu umekuwa mtumwa wa hayo unayopenda kuyafanya gizani..mangono yasiyo ya kawaida kujaribu kujaribu ambavyo hukutakiwa ujaribu...sasa ili umrudie Mungu sasa isali hii sala kwa siku mara 12 ..waislam wao si huwa wanasali mara 5 kwa siku wewe wapite nenda beyond kabla haijakufikia ile siku mbaya zaidi kwako