Mimi sio kungwi ila ni mwanamke, ichukue hii

Mtoa mada Yuko sahihi sana japo maisha huwa yanatofautiana mno, kila mtu anakuwa ameumbwa na mzunguko tofaut wa maisha (life circle) .Kuna wanawake wanaolewa na miaka 13-16 hawa hawajui kitu inaitwa kula ujana.
Kuna wanaoolewa VERY late kwasababu ya vitu kama kusoma sana, shinikizo au family culture na wengine sio bahati .
NB: SIO KILA MWANAMKE ANAYECHELEWA KUOLEWA NI MALAYA AU MDANGAJI.
 
😃😃😃😃💯
 
Wanaoolewa ni wote: wenye tabia nzuri na mbaya. Wenye historia “ndefu” na “fupi”. Kudumu au kufa kwa ndoa kunategemea na hulka na akili za wanandoa BAADA ya ndoa kufungwa.

Hii haiondoi fact alizoandika mleta mada. Wanawake wengi wanapitia mikanganyiko hiyo hasa wakati muhimu (prime age) wa usichana wanaposhindwa kutofautisha kati ya KUPENDWA na KUTAMANIWA na wanaume wengi. Wanaishia kunyanyaswa na wahuni huku wakifurahia wakidhani wanathaminiwa kwa uzuri au upekee wao.

Wakishtuka ukubwani wanabakia na mahangaiko mengi na mitazamo hasi sana kuhusu wanaume. Wanaoolewa wanaingia ndoani na baggages kibao na huweza kusumbua sana wenza wao kwa mitazamo iliyopinda. It’s tragic.

To be fair. Hata wanaume wanaohusiana na wanawake wengi (kihuni) muda mrefu na kuchelewa kuoa nao huwa na mitazamo hasi sana kuhusu wanawake. LAKINI wanaume wa umri wowote wanakuwa na ADVANTAGE kubwa sana ya kuoa/kudhibiti ndoa/mahusiano kuliko wanawake. Hivyo women need a lot of help in this area tangu wakiwa mabinti wadogo. Sio kupewa false confidence and hope.
 
Mtoa mada unakabia juu sana.

#Eneweiz mtoto wa kiume hakuna kiwanda kinachotengeneza bidhaa za mtumba.
 
Reaction zako Jadda kutetea usawa wa uzani kwa wanawake unajitahidi. 😆😆
Lakini mwandishi mengi aliyo spot and address ni kweli.
 
Kila mwaka huwa nauona Uzi huu🤔🤔, anyway Wacha niendelee kukariri TU📌🔨.
 
Weeeeeeeeh sinsi when! Kuchwa kutwa wanawake this, wanawake that.... you breath women.

Wanaufanya na akina nani

Kuna kamsemo kanasemaga hivi "Kila mwanaume anaoa Malaya wa mtaa asioufahamu, na jamii asiyoijua vyema"..Binafsi sitetei upande wowote ila hii mada ni mahususi kwa makolokolo wanayofanya wanawake kwanini nisiwe huru kuchangia kwa uzoefu nilionao!? Mimi sina upeo mkubwa ni kweli lakini sio kipofu, nimeshuhudia ndoa nyingi zikitetereka na vyazo huwa ni ubinafsi wa wakinamama na hulka zao kama lipo Jambo unaona na wanaume tunakosea chapisha uzi mwingine tuje kukomenti ila hapa utupishe mamdogo feminist 🤣🤣
 
Kilichoandikwa ni uongo na watu wanakuja na shuhuda za uongo pia.
Mkuu ukute umezaliwa Masaki na kuishi ughaibuni kwa miaka kadhaa, maana ungekuwa umeishi Tanzania hii hii ungegundua haya yaliyosemwa ni reflection ya huku mitaan kwetu
 
My homie is a dead person
 
Mbona huu mwandiko wa libaba fulani lina kitambi na vinyweleo kuanzia puani mpaka kwenye kuta za masikio
 
Mkuu ukute umezaliwa Masaki na kuishi ughaibuni kwa miaka kadhaa, maana ungekuwa umeishi Tanzania hii hii ungegundua haya yaliyosemwa ni reflection ya huku mitaan kwetu
Nionyeshe feminist anayeshinda na dera na shanga pekee bila chupi anayeishi Kiwalani, Mwananyamala Kisiwani, Temeke kwa Usher, Kawe Ukwamani, Msasani Shoppers, Davis Corner.

Bonus point nionyeshe wa umri wowote siyo aliouweka OP pekee
 
Umexaliwa Tanzania ? Wapi ? Tuwe na experience basi....
Nimezaliwa Makete, Mwakauta. Nikaishi Zambia, Njombe, Makambako, Mafinga.

Nimeishi Mwananyamala, Temeke, Kigamboni, Kawe, Makumbusho, Tegeta, Masasi, Dodoma, Korogwe na sasa nipo Kondoa.

Na sijawahi kukutana na pattern ya OP.
 
Inaonekana kama umekutwa na bwana pepsi vile!
 
Miaka 12_15 kumbe watu tayar daah sijui ni malez au ni ukali wa mzeee wangu sikua naelewa chochote kuhusu mapenz looh mie michezo michezo na mim
mpaka miaka mingapi? kilichozungumzwa ni kweli, mdogo wangu wa kike alizaa mtoto akiwa na umri wa miaka 15 tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…