Well.
Kwanza kabisa tuelewa kwamba, "Hakuna sayansi bila dini, na dini bila sayansi imepungukiwa".
Sayansi inafanya kazi ya kutafuta na kuona: Je, yale yote ambayo dini au imani imesema yapo; au je, ni kweli.
Sasa, hakuna sayansi au mwanasayansi ambaye anakataa kwamba ulimwengu umefanyika kwa akili nyingi na ya hali ya juu sana.
Sayansi inakubali na inaona kila kitu kinachoonekana kimefanyika kwa akili nyingi sana kuanzia na muundo wao wa nje na hata utendaji kazi wao, ni wa akili ya hali ya juu.
Sasa, ni nini au hali gani ambayo imesababisha vitu kuwepo, na kuwepo kwa akili hivi?
Hapo ndipo nadharia ya "Mlipuko Mkubwa" (The Bing bang theory), ambayo ni msingi wa nadharia karibu zote za sayansi, inafafanua kuwa ulimwengu umetokana na mlipuko mkubwa. Maana ya maneno "Mlipuko Mkubwa", ni Nishati (Energy). Kwahiyo kwa maneno mengine: ulimwengu umetokana na nishati.
Ingawa nadharia hii ina maswali mengi, lakini ndio inayokubaliwa na wanasayansi wengi.
Sasa, hoja ni "Nishati" (energy) kwa upande wa sayansi na "Mungu" au "Roho" kwa upande wa dini.
Sayansi inasema Nishati. Je, hii nishati ambayo sayansi inasema kama chanzo cha vitu ni nini?
Dini inasema, ulimwengu umeumbwa na Mungu. Na Mungu ni roho. Je Mungu maana yake ni nini? Na roho maana yake ni nini?
Muhimu sana. Dini na sayansi: vyote vinashughulikia "Kweli za Akili".