Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Asili ya miti au zao hili ni Asia, Waarabu na wafanyabiashara walileta zao hili Tanzania miaka ya 1600-700. Minazi ya asili hi chukua miaka 10 tangu kupanda mpaka kuvuna au kuangua Nazi. Mti wa mnazi hustaamili ukame na una maisha ya miaka 100 tangu kupandwa.
Kilimo cha minazi kiliwafaa Waarabu waliomua kuweka makazi katika Pwani za Afrika. Minazi hupaswa kufyekewa na uvunjaji ni kila baada ya miezi mitatu. Iliwawezesha wenye mashamba kufanya shughuli nyingine wakiwa wanasubiri Mavuno.
Wingi wa minazi ulisaidia watu kusuka viungo vilivyoezekea nyumba. Matapa yalitumika kulalia kuanzia kwenye vitanda hata kwenye misiba. Vifuu vya nazi vilitengeneza pawa , vifungo, shanga na hereni.
Minazi mingi iliyopandwa na wahenga imeshapita umri wa uhai (life span) na hapa katikati hakukuwa na jitihada nyingi za kupanda minazi mipya. Matokeo yake ni uhaba wa makuti ya kutengenezea viungo na matapa.
Kama kiungo cha kupikia nazi zina soko kubwa na uhaba wake unasababisha bei kuwa kubwa sokoni. Wenye mapenzi mema na hili zao tuanze kampeni ya kupanda minazi