Minazi ni miti iliyo hatarini kupotea, dalili zinaonekana

Minazi ni miti iliyo hatarini kupotea, dalili zinaonekana

Mwaka 1986 hivi, Mheshimiwa Rais Mwinyi alitoa hadhari kuhusu kudharaulika kwa zao la nazi. Hasa uvunaji uliopindukia wa madafu, n.k. Akasema, itafika siku nazi itakuwa inauzwa moja sh. 100. Adjusting for inflation, bei ya nazi itakuwa imepanda kama alivyosema Mheshimiwa Mwinyi sr.
Rest in peace. Daah!
 
..wakati mwingine nadhani minazi ni investment nzuri kuliko uwekezaji ktk miti ya nguzo/mbao.

..tatizo linakuja kwenye muda wa matunzo ya minazi toka kupanda mpaka itakapoanza kutoa matunda.
Tatizo lipo wapi? Miaka mitatu? Unakumbuka sasa ni miaka mitatu toka JPM ashinde kipindi cha pili? Yaani ni 3 years lakini ni kama juzi.

Mnazi wa kisasa baada ya miaka mitatu unaanza kuvuna
 
Kuna miaka kumi ya ku sacrifice lakini baada ya hapo kama una heka moja una uhakika wa milioni 2 kila baada ya miezi mitatu.
Eka moja inabeba miti mingapi?

Upandaji hufanyika kwa umbali gani kati ya mche na mche na mstari na mstari?
 
Tatizo lipo wapi? Miaka mitatu? Unakumbuka sasa ni miaka mitatu toka JPM ashinde kipindi cha pili? Yaani ni 3 years lakini ni kama juzi.

Mnazi wa kisasa baada ya miaka mitatu unaanza kuvuna

..watafiti wanasema minazi ya kisasa sio mizuri, inashambuliwa sana na magonjwa.

..wanashauri tupande minazi ya asili / east african tall ambayo inavumilia magonjwa.

..mimi kwa mtizamo wangu east african tall inachukua muda mrefu toka kupanda mpaka kutoa matunda. Pia inatoa matunda kidogo ukilinganisha na minazi inayolimwa ktk nchi za wenzetu.

Cc Kibunango, Malila
 
naamini ktk kutunza mbegu asili, kwa hiyo nashauri tuwe na commercial farms zenye kutumia mbegu za kisasa na tuwe na mashamba ya kuhifadhi mbegu za asili.
 
Mimi bado ninaikubali hii ya kisasa pamoja na kwamba ina changamoto.

Muhimu ni kufuata matakwa ya kitaalamu ikiwemo usafi wa shamba/eneo.

Uchafu shambani ndicho chanzo kikuu cha magonjwa katika aina zote za matunda..
 
..miche ya kisasa inapatikana wapi? Na asili ya miche hiyo ni nchi gani?

..maana mimi nimekwenda kwenye kitalu cha serikali Mkuranga nikaambiwa hawana ya kisasa, wana east african tall.
 
View attachment 1767152
Asili ya miti au zao hili ni Asia, Waarabu na wafanyabiashara walileta zao hili Tanzania miaka ya 1600-700. Minazi ya asili hi chukua miaka 10 tangu kupanda mpaka kuvuna au kuangua Nazi. Mti wa mnazi hustaamili ukame na una maisha ya miaka 100 tangu kupandwa.

Kilimo cha minazi kiliwafaa Waarabu waliomua kuweka makazi katika Pwani za Afrika. Minazi hupaswa kufyekewa na uvunjaji ni kila baada ya miezi mitatu. Iliwawezesha wenye mashamba kufanya shughuli nyingine wakiwa wanasubiri Mavuno.

Wingi wa minazi ulisaidia watu kusuka viungo vilivyoezekea nyumba. Matapa yalitumika kulalia kuanzia kwenye vitanda hata kwenye misiba. Vifuu vya nazi vilitengeneza pawa , vifungo, shanga na hereni.

Minazi mingi iliyopandwa na wahenga imeshapita umri wa uhai (life span) na hapa katikati hakukuwa na jitihada nyingi za kupanda minazi mipya. Matokeo yake ni uhaba wa makuti ya kutengenezea viungo na matapa.

Kama kiungo cha kupikia nazi zina soko kubwa na uhaba wake unasababisha bei kuwa kubwa sokoni. Wenye mapenzi mema na hili zao tuanze kampeni ya kupanda minazi
Serikali iache kudanganyika.... Minazi ya asili pia miti mingine ya asili ni bora. Waitishe kampeni ya upandaji wake. Faida za mimea ya asili inajulikana
 
Indonesia na Malaysia wanasafirisha tui la nazi la makopo Ulaya, Marekani, Japan hata Australia. Kwa ardhi tuliyonayo tungeweza kukaba soko la Afrika tu linatutosha.
Kalime.basi upige pesa fursa hiyo unakaa unaiongelea tu
 
naamini ktk kutunza mbegu asili, kwa hiyo nashauri tuwe na commercial farms zenye kutumia mbegu za kisasa na tuwe na mashamba ya kuhifadhi mbegu za asili.
Sahihi, zikipotea hizi ni tabu kwa kizazi cha baadae.
 
Waswahili walikuwa kila mtoto anapozaliwa wanapanda mnazi. Wanaomba kwa Mungu kuwa mtoto akue aje kula matunda yake. Walau minazi ilikuwa inaenda na idadi ya watu.
 
Back
Top Bottom