Mind Illusion Projection: Jinsi ya kuidanganya mind ione vitu visivyo halisi kua ni halisi

Kiongozi kuna huyu mtu anaitwa Watchman Nee hebu tafuta vitabu vyake naamini utavipenda sana.
Jamaa nimeingia mtandaoni anavyo vitabu vingi balaa mkuu. Ingawa sijavisoma Ila naona kidogo Kama vina diverge na interests zangu. Ingawa Kuna ishu ya souls,mind na body naona Kama anavyo vinavyoelezea.
Ila ngoja nipakue nikiwa na muda napitia kimoja kuliko kumcheki Fulani leo akafanyeje
 
Ninavyo vingi sana vitabu vya huyu jamaa. Ningeweza ningekupakilia hapa
 
Mada yako ni nzuri sana. Kabla sijaendelea kujenga hoja. Yapo ninayo kubaliana na wewe na yapo ambayo nahitaji ufafanuzi zaidi. Mathalani unapo sema Wachawi wanamtia hofu mtu na si uhalisia. Naomba unipe maana halisi ya Uchawi,kisha tutamjua Mchawi au Wachawi ni kina kwa wingi.

Ama kuhusu dhana zinazo ambatana na wasi wasi kisha ukaona jambo dhahania ukasema ni halisi hili lipo. Na hili lina sababu zake,wengi wanao sema hayo huwa katika wenge la usingizi,au wamelewa na mara chache sana ukiwa timamu.
 
Uoga wa dhidi ya jambo fulani huambatana na kutolijua jambo hilo,ila kama unajua ni ngumu sana kuogopa.

Wanadamu tumeumbwa na hofu. Kuna hofu ya kimaana na hofu ya kihisia. Mathalani leo hii au wewe ukimuona Simba,lazima utamuogopa au ukiona moto ghafla. Kisha mengine hufata,hofu huambatana na tahadhari,vipi ukione kitu kisicho cha kawaida yaani hujui hakika yake ni muhali kudhibiti hofu.

Kudhurika ni matokeo tu,ambayo hayahusiani na hofu au kutokuwa na hofu. Swali litakuja,umekutana na kitu gani ? Hapa ungetupa mfano.
 
Hapa kuna Uchawi na mazingaombwe. Vyote ni uhalisia,yaani vipo.
Hili jambo unatakiwa ulifanyie utafiti zaidi,hasa ujue wapi ni sehemu sahihi ya kuchukua marejeo.

Soul bila shaka ni Roho, hii roho ni nini hasa ,na Mind bila shaka ni Akili. Unaweza kuniambia Mind katika mwili wa mwanadamu iko wapi ?
Kwa kuzingatia mfano wako wa Computer hivyo ulivyo vitaja sehemu zake kwenye Computer zinafahamika,swali langu ni Conscious na Subconsciuos Mind katika mwili wa mwanadamu ziko wapi ?
 
Hapa kuna Uchawi na mazingaombwe. Vyote ni uhalisia,yaani vipo.
Ndio vipo vyote
Hili jambo unatakiwa ulifanyie utafiti zaidi,hasa ujue wapi ni sehemu sahihi ya kuchukua marejeo.

Soul bila shaka ni Roho, hii roho ni nini hasa ,na Mind bila shaka ni Akili. Unaweza kuniambia Mind katika mwili wa mwanadamu iko wapi ?
Akili/mind ipo ndani ya Roho/soul
Kwa kuzingatia mfano wako wa Computer hivyo ulivyo vitaja sehemu zake kwenye Computer zinafahamika,swali langu ni Conscious na Subconsciuos Mind katika mwili wa mwanadamu ziko wapi ?
Kiufupi ni kwamba Soul imebaba mind na mind ina hizo conscious na subconscious mind ndani mwake. Roho ipo ndani ya ubongo (Brain)
Mind ni software part ambayo huwezi kuiona ila utaona matendo yake.
 
Akili/mind ipo ndani ya Roho/
Hili umelijuaje ?

Roho ni nini ? Yaani naomba unipe maana ambayo inazuia yote yasiyo husu Roho kuingia na inaruhusu yote yanayo husu Roho kuingia.

Hapa ndipo songombingo huanza.

Mimi navyo fahamu ni kuwa akili mahala pake ni moyoni,na hufanya kazi sambamba na Ubongo.
Kiufupi ni kwamba Soul imebaba mind na mind ina hizo conscious na subconscious mind ndani mwake. Roho ipo ndani ya ubongo (Brain)
Mind ni software part ambayo huwezi kuiona ila utaona matendo yake.
Swali langu limemili katika sehemu mahususi ya Roho,unapo sema Roho imebeba akili,nitakuuliza vipi kwa mtoto ambaye yuko tumboni na ni hai,vipi kwa mtoto mchanga na vipi kwa chizi ? Maana yake kilicho hai kina Roho,yaani kina akili. Vipi kuhusu mimea ?

Unaposema Roho ipo ndani ya Brain hii si kweli.

Mfano wa Roho katika mwili wa mwanadamu ni kama mfano wa Mafuta katika gari.
 
Natumaini unachanganya kati ya roho na nafsi.. nafsi ndio hukaa moyoni
Je wewe binafsi unafahamu nini kuhusu Roho na akili?
 
Natumaini unachanganya kati ya roho na nafsi.. nafsi ndio hukaa moyoni
Hapa sijachanganya,sababu tamko Nafsi,nalifahamu vizuri sana tena kutokeakatika lugha yake ya asili. Nafsi ni wewe, yaani ili uipate nafsi ni uchukue Roho ujumlishe na Mwili. Yaani Roho na Mwili unapata nafsi. Na hilo tamko Nafsi kuna wakati humaanisha Roho.

Kwenye Qur'aan tunapewa majibu kuhusu Roho,mtume wetu watu wake walikuwa wana muuliza sana kuhusu Roho,na majibu ni kuwa kuhusu Roho nimepewa elimu ndogo sana.

Anasema Allah mtukufu :

85. Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo tu. (Israa : 85)

Hizi ni elimu pweke unatakiwa ujue wapi unapata elimu kuhusu vitu hivi hasa nafsi,roho na akili,watu wengi sana hawana elimu sahihi kuhusu vitu hivi.
 
Naam nakubaliana na wewe
🙏
Hizi ni elimu pweke unatakiwa ujue wapi unapata elimu kuhusu vitu hivi hasa nafsi,roho na akili,watu wengi sana hawana elimu sahihi kuhusu vitu hivi.
Ndio maana nimeeleza sehemu kwamba Dark power na Light power zote zinaweza kukupatia ufahamu sasa ni mtu mwenyewe kutambua ufahamu alionao unatoka katika nguvu gani.
Ni Mungu anifunuliaye yale nisiyoyafahamu maana anasema Ukimpokea yeye basi atakuonyesha mengi makuu usiyoyajua
 
Je wewe binafsi unafahamu nini kuhusu Roho na akili?
Umeuliza swali zuri sana. Niliwahi kuandika mada maalumu kuhusu ROHO. Nikaipa anuani hii "Ukweli kuhus Roho na yote yanayo ihusu".

Hapa nakuwekea kama ilivyo mada hiyo.



"Katika mambo makubwa mno yenye kuwatatiza watu tangu dunia inaumbwa ni hili jambo kuhusu ROHO.

Wamepita Wanafalsafa wa kale na wa sasa, Wanasayansi wa zamani na wasasa, watu wa dini, na wasio kuwa hao katika kuelezea Roho ni nini, hatimae wamekuja na mitazamo mingi yenye kutatiza watu na isiyokuwa na ithibati wala hakika yoyote.

Lakini hao wote mpaka Wakana Mungu ( Atheists) wakakubaliana ya kuwa KIFO ni ule muda ambao maisha hukoma kwa kiumbe, au Roho kuacha mwili. Suala la Roho limebaki kuwa jambo lililo fichikana kuhusu hakika yake na undani wake, na Mola wetu hakutoa elimu juu ya Roho isipokuwa kidogo mno, na jambo hili limebaki kwake kwa mapana yake.

Mola wetu anasema katika Qur'aan, juu ya ukweli kuhusu ROHO.

85. Na wanakuuliza khabari za Roho. Sema: Roho ni katika mambo ya Mola wangu Mlezi. Nanyi hamkupewa katika ilimu ila kidogo. (Israa : 85)

Hii inaonyesha ya kuwa suala la elimu juu ya Roho ni elimu kubwa mno na sisi tumepewa elimu ndogo sana juu ya ROHO na jambo hili linabaki kuwa kwake Mola wetu kwa undani wake.

Kama hali iko hivi, ni nini Roho ? Ni zipi sifa zake? Ni zipi tabia zake na ni upi uwezo wake ? Maswali haya watu hujiuliza sana.

Katika Elimu hiyo ndogo tuliyopewa na Mola wetu, tunaipata kutoka katika vyanzo vya uhakika na kuaminika ya kuwa, Roho ni kitu kisicho onekana, chenye mafungamano ya moja kwa moja na mwili.

Lakini Roho hiyo ina sifa kadhaa kwazo huwa tunazitumia kuelezea vitu vyenye kushikika (Tangible things), kama vile hupulizwa na Malaika kuupa mwili uhai na hutolewa kipindi mja anapokufa, hukutana na kuzungumza.

Mwili unakufa ila Roho haifi, roho hubaki milele. ROHO ni katika vile viumbe ambavyo vina mwanzo ila havina mwisho.

Huu ndiyo ukweli kuhusu ROHO kwa ufupi.

Zingatia : Wasomi wakubwa na wahakiki wa mambo, wametofautiana juu ya Roho na Nafsi, ya kuwa je ni kitu kimoja au ni vitu viwili vyenye kutofautiana. Wapo walio sema ya kuwa Roho na Nafsi ni vitu viwili tofauti na kutofautiana kwake hulingana na muktadha wa hali, wengine wakasema ya kuwa Nafsi ni mjumuiko kati ya Roho na Mwili, na wapo waliosema ya kuwa Roho ni Nafsi na Nafsi ni Roho.".

Hiki ndicho nilichokiandika katika mada hiyo.

Ama kuhusu akili, akili kiasili ni tamko la Kiarabu lenye maana ya "Kizuizi", waarabu kamba ya kumfungia mbuzi asitoke nje ya eneo iliitwa "aql" . Kwa maana ya kisheria AKILI ni kizuizi kinachomfanya mwanadamu asikozee katika maamuzi. Ndiyo maana ukisoma katika elimu ya Mantiki (Logic) wanakwambia ya kuwa Mantiki ni ya kutumia akilo kwayo humfanya mtu asikosee katika kujenga hoja. Tunarudi kule kule katika maana ya msingi. Yaani akili ni kizuizi kinachomfanya mja asikosee katika kutenda mambo.

Tuendelee na mjadala kutokea hapo.
 
Kwa maana rahisi Dark Power ni nini ?

Lakini ukweli unabaki pale pale hatujui mengi kuhusu Roho ila machache ambayo ametufunulia Mola muumba.

Sasa wewe unakosea katika jambo hili sababu unatumia akili yako na maelezo ya wakubwa wako katika uliyo yasoma kuhusu vitu hivi. Huwezi kupatia hata siku moja,sababu uwezo wa akili zetu zina ukomo.

Tuko pamoja.
 
Kwa maana rahisi Dark Power ni nini ?
Mara nyingi natumia neno hilo kumaanisha Shetani/Ibirisi
Lakini ukweli unabaki pale pale hatujui mengi kuhusu Roho ila machache ambayo ametufunulia Mola muumba.
Sahihi kabisa na hatuwezi kuyajua yote
Sasa wewe unakosea katika jambo hili sababu unatumia akili yako na maelezo ya wakubwa wako katika uliyo yasoma kuhusu vitu hivi. Huwezi kupatia hata siki moja,sababu uwezo wa akili zetu zina ukomo.
Tuko pamoja.
Upo sahihi. Lakini hakuna mwanadamu aliyefanya kitu kwa asilimia 💯 yaani ukamilifu. Naamini bandiko langu linamapungufu kibao ila pia lina usahihi kiasi fulani. So kazi ni kwa msomaji kuangalia madhaifu tu au mazuri pia
 
Upo sahihi. Lakini hakuna mwanadamu aliyefanya kitu kwa asilimia 💯 yaani ukamilifu. Naamini bandiko langu linamapungufu kibao ila pia lina usahihi kiasi fulani. So kazi ni kwa msomaji kuangalia madhaifu tu au mazuri pia
Naanzia hapa. Umesema kweli kabisa. Kutokana na udhaifu wa akili yetu na baadhi ya mambo kutoweza kuyadiriki katika uhalisia wake. Mola wetu akawa anatimiliza mitume na manabii (Siyo hawa feki ambao tunaishi nao ) kwa ajili ya kujibu maswali kwa yale yaliyo fichikana,kama vile baada ya kufa hufata nini,au roho ni nini,akili ni nini au nini lengo la kuwepo duniani, chanzo cha uhai ni nini (swali hili liliwasumbua sana Wanafalsafa wa Magharibi ikatokea kila mmoja akaelezea kwa mtazamo wake).
 
Je kwanini asitimilize kwa watu wa sasa wenye kumtafuta - kutafuta hekima yake?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…