Mind Illusion Projection: Jinsi ya kuidanganya mind ione vitu visivyo halisi kua ni halisi

nazungumzia movie ndg.
Naijua.. Sema yenyewe imeBase kwenye Spells/mazingaombwe zaidi.
Ila ni vitu vinaendana na yanayotokea kwenye jamii.
Unazika mgomba ukiwa unajua ni mtu kumbe sio...
 
Hivi wazungu wameshindwa kutengeneza movies za 3D? kuziangalia sio kwa TV tena hapa itahitajika projector iliyokaa viertical
Mkuu teknologia kama hizo sio kwa ajili ya matumizi ya sisi wananchi hizi zinatumika na vyombo vya usalama mpaka wakishaichoka ndio inatufikia sasa. Nadhani haiwezi kutengenezwa kua mbadala wa TV ili wasiue ajira na viwanda vya watu. Ila ngoja tuone huko mbeleni mambo yatakuaje
 
Nimeipata hii elimu kwa uzuri kabisa, nataman nifaham natural power kama inaweza kuwa learned na kuwa practiced
 
Nimeipata hii elimu kwa uzuri kabisa, nataman nifaham natural power kama inaweza kuwa learned na kuwa practiced
Pamoja sana Kiongozi, ndio unaweza kujigunza. Sasa itategemea unajifunza kwa udhamini wa nguvu za giza au za mwanga
 
Ukijiangalia kwenye kioo kwa muda wa dakika moja unakua unajiona wewe halisi ikizidi dakika moja Mind yako inaanza kukudanganya kwaba wewe ni mzuri. Ndio maana kadri ya jinsi unavyojiangalia kwenye kioo muda mrefu ndio unaanza kujiona mzuri. Kwanini??
Ubongo wako unachoka kuangalia kitu kimoja tu muda mrefu hivyo unaanza kukuletea sifa zingine mpya usoni mwako ambazo si halisi ili uridhike kwamba wewe ni mzuri uache kujiangalia au inafanya hivyo ili kukutia hamasa kwamba nawe ni mzuri.
Kumbe ukweli wanajua wakuonao, so ukijiangalia kwenye kioo usijisifu Kwamba ni mzuri acha watu wakuambie.
This is scientific correct!
 
Moja ya mfano wa ubongo kuonyesha illusion ni pua lako.

Ukiwa unaangalia kawaida huwezi kuliona pua mpaka utulie uangalie kwa umakini ndio utaliona. Kwanini? Macho yanaliona pua ila Mind yako inalipuuza (ignoring) pua lako ili lisikuzibe kuona mbele yako.. hii inasaidia watu wenye mapua makubwa tuone vizuri, Kwa umbali uliopo Kati ya pua na Macho na pua lilivyokaa basi tusingewez kuona mbele.

So akili hupuuza tu kuliona pua lako na sio kwamba halionekani na macho.
Kitu hiki kinafanyika tena Kwenye Miwani na Darubini
Ukivaa miwani ule mstari unaotenganisha kioo kimoja na kingine huwezi kuuona unakua kama haupo ila upo bali Mind yako ina Ignore hiyo mistari ili uone vizuri sio kuona vipande vipande.
Bado nachunguza kwanini jicho langu la kushoto ndio liko active sana kuliko la kulia!
[Mimi nikivaa miwani natumia jicho la kushoto kuona ]
 
Worries makes your mind shrink, and your brain crumble to fear. Hence you will see anything you want to see (Illusion)
 
ngoja nitulie nisome
 
Mfano 3 jinsi Ubongo unavyo-Ignore vitu.
Ukienda sehemu labda sehemu yenye harufu kali kwa muda kama dakika 3 halufu itakua kali ila baada ya muda harufu itakata/utaona ile hali ni ya kawaida (Chukulia mfano vyoo vya shule au vya Sokoni😆)

Ukikaa muda mrefu chooni Ubongo wako una ignore ile harufu unakua unasikia tu harufu ya kawaida. Ubong unafanya kuipuuza hiyo harufu ili uepukane nakero ya harufu...
Kisayansi kitendo hicho huitwa Diffusion ambapo ni mjongeo wa vitu kutoka sehemu yenye mgandamizo mkubwa kwenda kwenye mgandamizo mdogo (Movement of particles from the area of higher concentration to lower concentration)
 
Sio kwamba pua iko chini ya macho ndo maana haionekani
Kama kilivyo kidevu hakionekani na macho 4 real
 
Sio kwamba pua iko chini ya macho ndo maana haionekani
Kama kilivyo kidevu hakionekani na macho 4 real
Pua linaonekana hasa ncha yake, ila kidevu hakionekani kwa sababu macho yanaona kwa nyuzi 120. Macho na kidevu yapo kwenye nyuzi sawa 0° ndio maana hayawezi kuona kidevu. Angalia macho yako na kidevu kama havipo usawa mmoja.
Nimeeleweka?
 
Upo sahihi mkuu,

Lakini kuna aina mbili za memory
Short term memory
Long term memory

Hizo unazozizungumzia ni long term memory ndio huwa zinahifadhiwa hazipotei, lakini short term memory kama vile majibu ya hesabu za logarithm ulizozifanya ukiwa form two majibu yake yote unayakumbuka?

Kiufupi ni kwamba kuna taarifa ndogo ndogo hua zinakuwa filtered kabla ya kupakiwa kwenye long term memory mfano namba majina n.k zisipofanikiwa zinakuwa erased ndio maana unaweza kumkumbuka mtu ila usikumbuke jina lake.
 
Ahsante kwa kuongezea..
Lakini mkuu kwa wale wenye kumbukumbu kali inakuaje?? Mfano mimi nikisoma kitu nakua naona kama kilivyo ndani ya kichwa changu
Nikiamua kumkumbuka kitu nakumbuka every detail...
Watu wasiosahau vitu vidogovidogo si wapo??
Uwezo mkubwa wa kutunza kumbu kumbu unategemea mambo yafuatayo
  • Umri
  • Lishe
  • Trauma kama vile ajali inayohusisha kichwa au kupigwa na kitu kizito kichwani kinaweza kuathiri uwezo wa kutunza kumbu kumbu
  • Magonjwa kama vile Malaria, HIV/AIDS, parkisons disease, stroke, Delirium, dementia n.k yanaweza kupunguza uwezo wa kutunza kumbu kumbu
  • Kubanwa kichwa wakati wa kujifungua kunaweza kujeruhi ubongo, inasemekana watoto njiti na wanaozaliwa kwa opereaheni wengi ni ma genius
  • Uvimbe kwenye ubongo au kansa
  • N.k
Mkuu wewe ni mtoto njiti? Au ulizaliwa kwa oparesheni?
key point ni kwamba jambo lolote linalo athiri ubongo huhatarisha afya ya akili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…