Ubongo(Brain) na kumbukumbu zinazohifadhiwa kwenye Akili (Mind). Sababu ni kwamba tunachanganya tofauti ya ubongo na akili. Ubongo ni mfumo endeshi (operating System upande wa Hardware yaani physical body) wa mwili wa binaadamu ambao umegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Ubongo wa mbele, wa kati na wa mwisho….. Roho (Soul) imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Mind, Intellect na Impression, tunaweza kusema soul ni mfumo endeshi wa mwanadamu ambao unashughulikia mambo ya kiroho na mazingira/Nature (operating system inayoongoza upande wa Software katika mwili wa mwanadamu). Mind ndio inahusika kwenye kufikiria, hasa kwenye kutambua lipi baya na lipi jema.
Memory ni kisehemu katika ubongo ambapo taarifa (data au information) zinachambuliwa, zinahifadhiwa na kutolewa pindi zinapohitajika. Lakini pia Memory/kumbukumbu ni uwezo wa kukumbuka mambo ya zamani kama vile tabia/habits, uzoefu/experience, maarifa/skills, hisia, facts nk. Ubongo na Akili vyote vinatumika katika kuhifadhi kumbukumbu lakini zimetofautiani katika utendaji kazi, hivyo hapa tutaangali jinsi ubongo unavyokusanya taarifa na kuzihifadhi pia na akili jinsi ikusanyavyo.