Miongo miwili wamekataa kubadilisha jina la mtaa wa Tandamti kuwa Mshume Kiyate

Miongo miwili wamekataa kubadilisha jina la mtaa wa Tandamti kuwa Mshume Kiyate

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
Jina la Mshume Kiyate kwa sasa si geni tena katika historia ya TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Mzee Mshume alikuwa katika Baraza la Wazee wa TANU kuanzia lilipoundwa 1955.

Mshume Kiyate alikuwa kiishi Mtaa wa Tandamti na akifanya biashara Soko la Kariakoo toka miaka ya 1950. Yeye ndiye aliyekuwa dalali wa samaki wote walioletwa pale sokoni. Kazi hii ilimtajirisha kwa kiwango cha nyakati zile na yeye alitumia fedha zake nyingi katika harakati za kuijenga TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Kubwa ambalo lilimpambanua Mzee Mshume katika historia ya uhuru ni kule yeye kujitolea kubeba jukumu la chakula cha nyumba ya Baba wa Taifa kuanzia miaka ya mwanzo ya TANU hadi uhuru unapatikana mwaka wa 1961 na kuendelea kufanya hivyo hata pale Baba wa Taifa alipomwambia, ‘’Mzee Mshume sasa basi hivi vikapu vyako vya chakula, mimi sasa nalishwa na serikali.’’

Jibu la Mzee Mshume lilikuwa, ‘’Hapana Mheshimiwa sitoacha kuleta chakula nyumbani kwako kwani nataka wewe na watoto wako mle chakula hiki na hicho cha serikali wape wageni wako.’’

Huyu ndiye mzalendo mpigania uhuru wa Tanganyika na rafiki kipenzi cha Baba wa Taifa, Mzee Mshume Kiyate.

Miaka takriban 20 iliyopita aliyekuwa Meya wa Jiji ;a Dar es Salaam marehemu Kitwana Selamani Kondo katika kutambua mchango wa Mzee Mshume Kiyate alibadili jina la Mtaa wa Tandamti kuwa, ‘’Mtaa wa Mshume Kiyate.’’

Hadi hivi ninavyoandika na nimepita mtaa huu leo nimekuta kibao kipya kimewekwa lakini jina ni lile lile la zamani.

Hii nini maana yake?

Dharau, khiyana au nini?

kZ5LlMCgqPD9R9E5MUJWPN7_q0YkFwuZ732t0R3I0t0syOWSj010wSWEJ86ITul2cP47F7129sUqM_HUpVtOZjmFQio9OsxRtKebLa_HpMKZKvafFEQbCGKmZVMIAIy__ySItYdDqt7qArsJxhbL94SDaa8gHX6hoZpGwr_BZWnKCfRt5w9jmYUazcP2VmGSkm0cQcl_24UlzGW6nurImglkiFErzw2lThH2yfJqBaR1NQbLykO7Jj5X7oQ9f5mUtNQGRalLpkbPXz2fltNHdud0_qd4z41aJRz71KAJw7QNF3TBcArqWCduGyG9rZ_pmKzuTNdJwH1-8RGPhoFE2op62QgcQ4VMElKTyYSS0J_WUnDuQfHnDiy0z_NmziEGDLv400xMrWNXpeShnklbBKYS-WBI0O1mCax5BpkS7yZXOH74IUl8Iv6c1uVoDei5gxhl9uBNMnDjfNJyvnBPe9n6SLIKGbKkogeWR_0J3s0Zckv0FkQBAqwDp_5lnIg_M-bUlyjn1wfjCdxL7sX4aTo9__UZNTAt8dtxiEQwDl6wcJBmROaxXXAqfD1mFmUhz2s4644v8HFr6Ac_kVCyU9uUqngP49U=w360-h480-no


Picha hiyo hapo juu ilipigwa mwaka wa 1964 baada ya maasi ya wanajeshi na Baba wa Taifa kurejeshwa madarakani na Jeshi la Waingereza. TANU ilifanya mkutano mkubwa sana Jangwani na Mzee Mshume Kiyate siku ile alimvisha Baba wa Taifa kitambi kama ishara ya kuonyesha kuwa Wazee wa Dar es Salaam wale waliompokea na kuwa na yeye bega kwa bega kupigania uhuru wa Tanganyika bado wako nyuma yake na wanamuunga mkono.

Huyu ndiye Mzee Mshume Kiyate.

WAZEE+WA+TANU.jpg

Waliosimama wa pili kulia ni Mzee Mshume Kiyate





tAZ7Q0CbeIpy9U9VrFhQRXVT3KiZoLVWyGRWVQGRN9MQ2MWqQTn6Pdw3hADo7z3DvALdD5Hr-xQ=w724-h567-no

Mshume Kiyate wa kwanza kulia aliyemshika mkono Baba wa Taifa na
pembeni kwa Baba wa Taifa ni Mzee Max Mbwana akifuatiwa na Mzee

Mwinjuma Mwinyikambi

Kuna picha mashuhuri ya Mzee Mshume na Baba wa Taifa iliyopigwa Novemba 1962 wakati wa Uchaguzi Mkuu.

Picha hiyo inamuonesha Mzee Mshume akiwa amevaa koti, kanzu na kofia amemshika Nyerere mkono akimsindikiza kupiga kura.

Karika utawala wa Baba wa Taifa, magazeti ya ''Uhuru'' na ''Daily News,'' yamekuwa yakiitumia picha hii kila baada ya miaka mitano katika uchaguzi wa rais kama njia ya kuwahamasisha watu kupiga kura na kumchagua Baba wa Taifa.
 
Mzee Mshume Kiyate ni shujaa wa kweli wa Uhuru.

Sijapatapo kumsoma popote nje ya historia tunayoletewa na Alama Mohamed Said.

Hizi ndiyo Lulu za kuhifadhiwa vizazi vijavyo wazikute.

Halafu anakuja punguani anaejiita Yericko Nyerere au mwengine anaejiita Mag3 au mwengine anaejiita Nguruvi3 wanajidai wanaijuwa historia ya Uhuru wa Tanganyika.

Nna uhakika hawajapato kuijuwa historia ya ukweli inayoambatana na ushahidi wa mapicha nje ya maandiko ya Mohamed Said.

Hawa ndiyo wazee wetu wa Dar. Waje watuelezee na wazee wao wana historia ipi ya Uhuru wa Tanganyika.
 
Hii sentensi, chini ya picha, "Picha hiyo hapo juu ilipigwa mwaka wa 1964 baada ya maasi ya wanajeshi na Baba wa Taifa kurejeshwa madarakani na Jeshi laWaingereza."

Hiyo "kurejeshwa" ina maana aliondolewa madarakani, alipinduliwa au vipi?
 
Maalim Faiza,
Kwa siku tatu kuanzia tarehe 20 Januari, 1964 Baba wa Taifa hakujulikana yuko wapi.

Katika siku hizo nchi ilikuwa mikononi mwa Oscar Kambona aliyekuwa Waziri wa Ulinzi.

Baba wa Taifa alipotokeza aliulizwa na waandishi wa habari wa nje wapi alikuwa.

Mimi nilimsikia Baba wa Taifa kwa sikio langu akijibu.

Siku ile ilikuwa nimetumwa dukani nimesimama nje ya duka la Mwarabu Kinondoni Mtaa wa Wibu kona na Kinondoni Road na kulikuwa na baadhi ya watu wanasikiliza radio ile ya pale dukani na Baba wa Taifa akasema kupitia Tanganyika Broadcasting Corporation (TBC), "I was in Dar es Salaam."

Jeshi la Kiingereza ndilo liliwanyang'anya silaha askari walioasi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Maalim Faiza,
Kwa siku tatu kuanzia tarehe 20 Januari, 1964 Baba wa Taifa hakujulikana yuko wapi.

Katika siku hizo nchi ilikuwa mikononi mwa Oscar Kambona aliyekuwa Waziri wa Ulinzi.

Baba wa Taifa alipotokeza aliulizwa na waandushi wa habari wa nje wapi alikuwa.

Mimi nilimsikia Baba wa Taifa kwa sikio langu akijibu.

Siku ile ilikuwa nimetumwa dukani nimesimama nje ya duka la Mwarabu Kinondini Mtaa wa Wibu kona na Kinondoni na Baba wa Taifa akasema, "I was in Dar es Salaam."

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna tafiti zozote zinazosimulia alikuwa kwa nani kiuhalisia, hizo siku tatu alizo "potea"?

Hapa nahisi kuna historia nzuri.
 
Kama ni kweli Mtaa wa Tandamti ulibadilishwa rasmi na kuwa Mshume Kiyate IPO haja ya ku-petition ili huo uamuzi utekelezwe. Kama Mtaa wa Somali ulivyobadilishwa na kuwa Omari Londo. Lakini nadhani pamoja na mchango wa wazee wa Dar tusiaminishwe kuwa bila wao Uhuru wa Tanganyika usingepatikana. Watanganyika wa wakati huo kwa ujumla wao walichangia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni kweli Mtaa wa Tandamti ulibadilishwa rasmi na kuwa Mshume Kiyate IPO haja ya ku-petition ili huo uamuzi utekelezwe. Kama Mtaa wa Somali ulivyobadilishwa na kuwa Omari Londo. Lakini nadhani pamoja na mchango wa wazee wa Dar tusiaminishwe kuwa bila wao Uhuru wa Tanganyika usingepatikana. Watanganyika wa wakati huo kwa ujumla wao walichangia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sote tunaamini hivyo, hata Nyerere hakuwa Mzee wa Dar alikuja tu na kukuta harakati za kisiasa zipo na zinaendelea.

Unaweza ukatupa historia za wanaharakati wa nje ya Dar. Tutafurahi sana.

Sisi wa Dar tumejaaliwa na AlhamduliLlah tunae Mohamed Said aliyejaaliwa kutuandikia kuhusu wazee wetu wa Dar na kugusia harakati zao zilizowatoa nje ya Dar na hata nje ya Tanganyika.

Tutafurahi sana tukipata historia ya nje ya hapo. Na itakuwa ni rejea safi kabisa.
 
Leo nami nimemfahamu,
Natumaini wataibadili sasa.

Labda.

Maana kuna wazee walisahauliwa sana katika jitihada zao za kudai uhuru wa Tanganyika, mara baada ya darsa za Alama Mohamed Said tukaona historia ikiandikwa upya uwanja wa Taifa na kwa mara ya kwanza miaka zaidi ya 50 ya uhuru wakakabidhiwa na Kikwete medali za kukumbukwa michango yao katika kujipatia uhuru, "posthumously".
 
Labda.

Maana kuna wazee walisahauliwa sana katika jitihada zao za kudai uhuru wa Tanganyika, mara baada ya darsa za Alama Mohamed Said tukaona historia ikiandikwa upya uwanja wa Taifa na kwa mara ya kwanza miaka zaidi ya 50 ya uhuru wakakabidhiwa na Kikwete medali za kukumbukwa michango yao katika kujipatia uhuru, "posthumously".

Kweli miaka ilipita mingi, vizuri sana kwa wao kupewa medali hizo. Shukurani kwake kwa kuwakumbusha

(Yaani nimejitahidi maneno usinikosoe.. eeeh)
 
shukran Sana mzee Mohamed Said nimekua nikifuatilia sana nyuzi zako haswa unapoelezea jiji la DSM enzi hizo.Huu Uzi wako umekua zaid ya darasa maana Ni historia ambayo haijaandikwa Sana huyo mzee Mshume ndo kwanza namsikia Kuna haja historia kurekebishwa Na hawa wazee muhimu bwatambuliwe umma WA Watanzania.
 
Kuna tafiti zozote zinazosimulia alikuwa kwa nani kiuhalisia, hizo siku tatu alizo "potea"?

Hapa nahisi kuna historia nzuri.
Kitabu cha mlinzi mkuu wa Nyerere kilichotungwa na mlinzi wake aitwaye Peter kinaeleza kuwa Nyerere na Kawawa walifichwa Kigamboni kwenye nyumba ya mzee mmoja wakishindia mapapai.
Kitabu kizuri ingawa "kimehaririwa" sana ,kabla ya kuchapwa mwandishi alikipeleka kwa "wahusika"wakipitie kabla ya kuchapwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Mohamed wanaobadili hivyo vibao ni halmashauri unaweza ukawaandikia barua halmashauri au ukamueleza diwani yoyote wa Ilala awaeleze wahusika wabadili hicho kibao inawezekana nao wamepitiwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitabu cha mlinzi mkuu wa Nyerere kilichotungwa na mlinzi wake aitwaye Peter kinaeleza kuwa Nyerere na Kawawa walifichwa Kigamboni kwenye nyumba ya mzee mmoja wakishindia mapapai.
Kitabu kizuri ingawa "kimehaririwa" sana ,kabla ya kuchapwa mwandishi alikipeleka kwa "wahusika"wakipitie kabla ya kuchapwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyo mlinzi alikuwa nae siku hizo tatu za kuondolewa madarakani na wanajeshi au na yeye kapiga porojo tu?
 
Back
Top Bottom