Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #161
Mnabuduhe,Nashukuru kwa Majibu hayo ambayo yanazidi kunipa Maswali zaidi!
Katika kitabu chako cha Maisha ya Bwana Sykes pamoja na Interview Uliyoifanya na Bwana Gunze wa Radio Butiama,ni dhahili kabisa Unamlaumu Nyerere ambaye alikuwa kiongozi wa nchi kutomkumbuka wala kumuenzi Mzee wako wala Mchango wao!Kwanini iwapo ulikuwa na hoja nzuri na unataka kuandika kitabu kisicho na mlalio wa upande mmoja hukufanya Interview na Nyerere? Ulifanya interview na watu wengi mpaka Kenya!
Unamchukia Nyerere?
Kuhusu Kiingereza lisikupe shida wakati mwingine! labda kama andiko lipo kwa lugha ya Kiarabu au lugha zingine mbali na Kiingereza.
Asante.
Sina sababu ya kumchukia mtu yoyote kwani kufanya hivyo ni mtu
kujitishwa zigo zito kichwani ukawa linakuhangaisha siku zote.
Laiti ungekuwa umekisoma kitabu cha Abdul Sykes wala usingekuja
na maswali haya kwani nimeeleza historia nzima ya uandishi wa historia
ya TANU kuanzia African Association 1929.
Anaeleza Dossa Aziz niko nyumbani kwake Mlandizi pamoja na Ally Sykes
na mama mmoja wa Mmarekani Mweusi mwandishi wa Washington Post,
Dossa Aziz anaeleza kuwa mara tu baada ya uhuru siku moja yuko yeye,
Baba wa Taifa, Abdul Sykes na Mwalimu Kihere katika mazungumzo
ya kawaida tu ikazuka fikra ya kuandika historia ya TANU na ya uhuru.
Mwalimu Kihere
Baba wa Taifa akasema kati ya wanaoijua vyema African Association na TANU
ni Abdul kwa hiyo kazi ile akapewa Abdul na Baba wa Taifa akampeleka Dr.
Wilbard Klerruu Makao Makuu ya TANU amsaidie Abdul katika utafiti na
kuandika historia ile ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Dr. Klerruu ndiyo kwanza alikuwa amerudi masomoni Marekani.
Mpashaji wangu habari ananiambia Abdul alirudi Makao Makuu ya TANU
Lumumba na akaingia ofisi ile ile ambayo alikuwa anaitumia wakati wa
harakati za kudai uhuru, ofisi ambayo baadae alimwachia Nyerere, 1953.
Mpashaji wangu ananiambia alikuwa akitoka shule anapita pale Lumumba
kumwamkia Abdul Sykes si kwa heshima ya kuamkia ila kwa kuwa Abdul
alikuwa hawaagani hivi hivi alikuwa atamtupia vijisenti kidogo.
Baba wa Taifa alikuwa akipelekewa kila sura ikikamilika kuisoma.
Hapa ndipo ilipoanza tatizo la historia ya TANU hadi kutufikia sisi sasa zaidi
ya miaka 50.
Abdul alianza historia ya TANU na historia ya baba yake Kleist alipounda
African Association 1929.
Mnabuduhe,
Hapa ndipo lilipozuka tatizo hili ambalo hadi sasa bado linakuhangaisha
wewe na watu wengi kufikia kunighadhibikia mimi na kunitukana kwa nini
nimeandika historia nyijngine ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Mradi huu ulipoingiwa na tatizo hili Abdul akajitoa na akachukua nyaraka
zake na akamwacha Dr. Klerruu aendelee na utafiti na kuandika.
Kazi hii haikuchapwa kitabu na TANU kwa miaka mingi ilikuwa katika maktaba
ya TANU hadi, ''ilipoibiwa,'' na ''mwizi,'' akabadilisha hapa na pale akachapa kitabu.
Kitabu hiki ni sawasawa na kitabu cha Kivukoni, ''Historia ya TANU,'' (1981).
Ningeweza kuendelea kueleza kwani yako mengi lakini naamini kwa haya
niliyoweka hapa tatizo nimeliweka wazi na naamini nimeeleweka.




