Miongo miwili wamekataa kubadilisha jina la mtaa wa Tandamti kuwa Mshume Kiyate

Mzee Mohamed wanaobadili hivyo vibao ni halmashauri unaweza ukawaandikia barua halmashauri au ukamueleza diwani yoyote wa Ilala awaeleze wahusika wabadili hicho kibao inawezekana nao wamepitiwa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kitulo,
Kuna mambo nyuma yake.

Labda niseme jambo.

Vipi watu hawa wampe mtaa Yusuf Makamba Gerezani wamuache Dossa Aziz na Abdul Sykes?

Kuna mtu aliwaamrisha kufanya hivyo au walipitiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee Mshume Kiyate ni shujaa wa kweli wa Uhuru.

Sijapatapo kumsoma popote nje ya historia tunayoletewa na Alama Mohamed Said.

Hizi ndiyo Lulu za kuhifadhiwa vizazi vijavyo wazikute.

Halafu anakuja punguani anaejiita Yericko Nyerere au mwengine anaejiita Mag3 au mwengine anaejiita Nguruvi3 wanajidai wanaijuwa historia ya Uhuru wa Tanganyika.

Nna uhakika hawajapato kuijuwa historia ya ukweli inayoambatana na ushahidi wa mapicha nje ya maandiko ya Mohamed Said.

Hawa ndiyo wazee wetu wa Dar. Waje watuelezee na wazee wao wana historia ipi ya Uhuru wa Tanganyika.
Hii ni sampuli ya wazee wetu wa Dar ambao bila ya kujali umaskini wao walijitoa kwa hali na mali bila kutarajia malipo ya aina yoyote yale. Kwa bahati mbaya sana hawazungumzwi hata kidogo. afadhali hata mwalimu siku akifurahi basi kwa kiasi fulani alikuwa anatoa kwa vipande vipande aina ya misaada iliyotelewa na wana darisalama wa enzi hizo.
Sisi watoto tulikuwa tukiona baba na mama zetu walivyokuwa wakihamasishana kuhusu uanachama wa tanu [ kama sikosei, asilimia zaidi ya 90 ya kina mama wa kariakoo walikuwa ni wanachama na waliona fakhari sana kujihusisha na tanu bila kujali serikali ya kikoloni].
 
Kitulo,
Kuna mambo nyuma yake.

Labda niseme jambo.

Vipi watu hawa wampe mtaa Yusuf Makamba Gerezani wamuache Dossa Aziz na Abdul Sykes?

Kuna mtu aliwaamrisha kufanya hivyo au walipitiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
HILO NALO NI NENO -SIDHANI KAMA KUNA DIWANI AU KIONGOZI YOYOTE YULE WA JIJI AMBAYE ANAYEWEZA KUTOA JIBU.
 
Kama ni kweli Mtaa wa Tandamti ulibadilishwa rasmi na kuwa Mshume Kiyate IPO haja ya ku-petition ili huo uamuzi utekelezwe. Kama Mtaa wa Somali ulivyobadilishwa na kuwa Omari Londo. Lakini nadhani pamoja na mchango wa wazee wa Dar tusiaminishwe kuwa bila wao Uhuru wa Tanganyika usingepatikana. Watanganyika wa wakati huo kwa ujumla wao walichangia.

Sent using Jamii Forums mobile app
UBINAFSI NDIYO TATIZO UKWELI SIONI SABABU YA MTAA KUPEWA JINA LA MZEE MAKAMBA[Ninamheshimu sana mzee wangu na ukweli amechapa kazi sana hapa dar na hasa yale maeneo ya gerezani magereji/sido lakini umuhimu wa kwanza wangepewa kina mzee Kiyate.
 
Abunuwasi,
Makamba anaweza kupewa mtaa Lushoto lakini si Gerezani wakaachwa wazalendo wazawa wa sehemu hiyo waliofanya makubwa katika kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika.

Hili jambo mie limenistaajabisha sana na khasa ukirejea nyuma ukaangalia historia yake kwa yale yaliyotokea Msikiti wa Mwembechai mwaka 1998.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli miaka ilipita mingi, vizuri sana kwa wao kupewa medali hizo. Shukurani kwake kwa kuwakumbusha

(Yaani nimejitahidi maneno usinikosoe.. eeeh)

MEDALI YA ABDULWAHID SYKES: MWENGE WA UHURU 1961 - 2011
Mohamed Said April 29, 2017 0
Utangulizi
''Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa, katika sherehe kubwa katika viwanja vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa. Kati ya wale ambao walipewa medali hizo alikuwa Sheikh abdallah Chaurembo. Wazalendo waliotajwa ndani ya kitabu hiki ambao walipigania uhuru wa Tanganyika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa katika orodha ile ya heshima. Baada ya siku chache kupita, Nyerere kama mtu aliyegutuka alimualika Dossa Aziz Ikulu. Dossa Aziz, wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa mtu maarufu, mwenye nafasi, na kujiweza sana. Sasa Dossa baada ya miaka kupita hakuwa akifahamika tena na ule umaarufu na utajiri wake ulikuwa umetoweka. Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kijijini Mlandizi, maili chache nje ya Dar es Salaam. Katika sherehe ya faragha Nyerere alimtunukia medali Dossa Aziz, rafiki yake wa zamani.''
(Kutoka, ''Maisha ya Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)...'')

Jina la Abdulwahid Sykes (1924-1968) katika historia ya uhuru wa Tanganyika kwa sasa halihitaji kuelezwa sana.
Historia yake imekuwa ni historia ya kusisimua unapomsoma kuhusu yale aliyofanya katika kuunda chama cha TANU 1954 akianza na kubadilisha mwelekeo wa TAA alipoingia katika uongozi wake 1950.
Historia ya Abdul Sykes pia ina masikitiko pale baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 juhudi za makusudi zilipofanywa kulifuta jina lake katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na kwa hili si tu kuwa lilifutika jina lake peke yake bali na jina la mdogo wake Ally na la baba yao Kleist Sykes aliyekuwa muasisi wa African Association mwaka wa 1929.

Kulia: Ilyas Abdulwahid Sykes, Daisy Abdulwahid Sykes, Mwandishi akiwa ameshikilia Medali ya Mwenge wa Uhuru
Misky Abdulwahid Sykes na Kleist Abdulwahid Sykes

Ilichukua miaka 50 kwa Abdulwahid na mdogo wake Ally kutunukiwa medali ya ‘’Mwenge wa Uhuru,’’ kama utambuzi wa mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika wakiwa bega kwa bega na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere waliyemfahamu mwaka wa 1952.
Leo nimebahatika kuiona medali ya ''Mwenge wa Uhuru'' aliyotunukiwa Abdulwahid Sykes (post homous) na Rais Kikwete katika Viwanja vya Ikulu 9 Desemba, 2011 katika kusherehekea miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.

Kuishika medali hii kwa mikono yangu kwangu kilikuwa kitu kilichokuwa na nafasi ya pekee katika moyo wangu.

Medali ya mwenge wa Uhuru aliyotunukiwa Abdulwahid Sykes katika kuadhimisha miaka 50 ya Uhuru wa
Tanganyika 2011
(Picha kwa hisani ya mjukuu wa Abdul Sykes Aisha Kleist Sykes)

Mwandishi akiwa Azam TV akifanya kipindi cha Saba Saba 2015

historia
 
Nashukuru Mohamed
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mzee Mshume Kiyate ni shujaa wa kweli wa Uhuru.

Sijapatapo kumsoma popote nje ya historia tunayoletewa na Alama Mohamed Said.

Hizi ndiyo Lulu za kuhifadhiwa vizazi vijavyo wazikute.

Halafu anakuja punguani anaejiita Yericko Nyerere au mwengine anaejiita Mag3 au mwengine anaejiita Nguruvi3 wanajidai wanaijuwa historia ya Uhuru wa Tanganyika.

Nna uhakika hawajapato kuijuwa historia ya ukweli inayoambatana na ushahidi wa mapicha nje ya maandiko ya Mohamed Said.

Hawa ndiyo wazee wetu wa Dar. Waje watuelezee na wazee wao wana historia ipi ya Uhuru wa Tanganyika.

nYaNi wA KaLe
 
Kuna tafiti zozote zinazosimulia alikuwa kwa nani kiuhalisia, hizo siku tatu alizo "potea"?

Hapa nahisi kuna historia nzuri.
Kuna mlinzi wake ametoa kitabu kitafute

Kwa ufupi inasemekana mlinzi alimtorosha kupitia geti la nyuma akapanda boti mpkaka kigamboni, huko aliishi kwa kula matunda huku akiletewa taarifa za mara kwa mara juu ya kinachoendelea

Hivi pale Ikulu "geti la nyuma" ni lipi?
 
Asante sana mzee wetu kwa history iliyo tukuka. [emoji120]
 
Ushahidi?
Unataka ushahidi upi zaidi ya alichoandika mlinzi wake au unafikiri historia hadi aandike Mzee Mohammed

Alafu Mzee Mohammed anaandika historia za wazee wa DSM waliopigania Uhuru sio historia ya kilichotokea 1964 ambacho ni watu wa karibu tu ndio wanafahamu

Punguza chuki na kufurahi Baba wa Taifa aandikwe kwa Mabaya
 
Baro,
Nimesoma hili jibu lako kwa Maalim Faiza na ningependa nami kusema jambo.

Kuhusu haya maasi na namna Baba wa Taifa alivyoweza kutoroka kutoka Ikulu
kwa salama hakika iko, ''version,'' nyingine ambayo haikubaliani na ile ya Mzee
Mbwimbo
kama alivyoeleza katika kitabu chake.
 
Baro,
Nimesoma hili jibu lako kwa Maalim Faiza na ningependa nami kusema jambo.

Kuhusu haya maasi ya na namna Baba wa Taifa alivyoweza kutoroka kutoka Ikulu
kwa salama hakika iko, ''version,'' nyingine ambayo haikubaliani na ile ya Mzee
Mbwimbo
kama alivyoeleza katika kitabu chake.

..wakati mwingine huwa nakuonea huruma sana.

..unajua vijana wa siku hizi, unaohangaishana nao, hawana mazoea ya kusoma vitabu vingi.

..mtu mwenye mazoea ya kusoma vitabu hatokuwa na shida, au hatotaharuki, akikutana na maandiko yako.
 
Back
Top Bottom