MtotoKautaka
JF-Expert Member
- Jul 16, 2018
- 993
- 2,045
Kuna watu thamani katika maisha yetu hapa duniani wapo na wanaweza wakawa ni wa muhimu katika negative way au positive way.
Ukiachana na ndugu wa faida na wazazi bado kuna watu baki wanaweza kuibika katika nyakati flani ambazo uliwahitaji kwa udi na uvumba.
Binafsi mimi kuna hawa watu wawili walinipa msaada special katika wakati maalumu. Hawa watu wote walijitokeza kipindi nipo kidato cha 4 mwezi wa mwisho kabla sijaingia kwenye mtihan wa mwisho.
1. Huyu wa kwanza ni madamu wangu alikuwa madam wa kiswahili. Madam huyu aliniokoa na msaada wake nisingeupata Kwa wakati ule pengine nisingekuwa hapa nilipo saivi japo hapa nilipo mwingine anaweza akapaona ni padogo ila kwangu binafsi napaona ni pakubwa sana na napachukulia kama ticket ya kufika napotaka kufika.
Ilikuwa hivi, Mimi nilipokuwa o-level nilikuwa miongoni mwa wanafunzi watukutu sana. Walimu wengi walikuwa wananisakama kwasabab ya utukutu wangu wa kijinga ambao haukuwa na faida yoyote.
Skul ilikuwa ni private ada ilikuwa imechangamka kidgo Kwa miaka ile, ningeweza kufukuzwa mapema ila private skul huwa siyo rahisi kufukuza mtu ambaye kidgo darasani anakauwezo, japo zipo nyingine hasa za seminari huwa hazibembelezi mtu hata uwe nani.
Sasa ilikuwa mwezi wa 10 utukutu umekolea, kutoroka skul kulala nje ya skul, kuiba mihogo, mayai ya kanga wa skul, kuchaji cm kwenye dali za bwenini na maujinga mengi mengi.
Headmaster akaanza kuwapa suspension wadau, akikukamata tu unafukuzwa upenge nje uwe unakuja siku ya paper ukiwa unatoka mtaani.
Mimi babaangu ni mkali sana na endapo kama ningepewe suspension kiukweli nilikuwa sina pa kukimbilia na sidhani kama ningeweza kumudu gharama za kupanga nje na na kumudu maisha ya mtaani, obviously ningechanganyikiwa na ningeangukia pia na nisingekuwa hapa kwasabab baba asingenielewa na sapot yake ningeikosa na home ningefukuzwa.
Huyu madam aliniita siku moja, ilikuwa saa12 jioni kama ya kuingia evening prep. Aliponiita akanambia Siri juu ya kinachoendelea huko ofisini. Akanambia kuwa wananijadili na wanapanga kuniweka mtegoni wanikamate ili wanisuspend namimi, yani kifupi ilikuwa ni hakuna pa kutoka, akanambia kwamba wamepanga kuniwekea spies wanifatilie na kupeleka taarifa juu ya wapi nitakapokuepo na nitakuwa nimefanya kosa gani na walipewa cm ya kuwastua walimu ili nikamatwe on the spot.
Madam alinitajia mpka hao ma spy ili nikae nao kwa tahadhari na akanishauri nitulie kabisa nisitoroke wala nisifanye kosa lolote kwasabab nitafukuzwa seriously.
Kwanzia siku hiyo nilikuwa makini sana na nikafanikisha kumaliza mitihani yangu salama na matokeo yakawa poa. Madam nilikuja kumtafuta na mpka saivi tunawasiliana na ni kama ndugu. Alinisev sana sana kwasabab ningefeli basi saiz sijui ningekuwa wapi na ningekuwa nafanya nini.
2. Huyu ni jamaa mmoja ambaye alikuwa ni bingwa sana wa hesabu. Mimi nilikuwa mzembe sana kwenye hesabu na nilikuwa napata namba za viatu. Sasa mwezi ule wa mwisho kabla ya necta nilimfata jamaa nikamuomba anielekeze topics ambazo kwangu niliona nikizisoma nitatoboa nakumbuka zilikuwa ni linear programming, probability, account na matrix hizi topics nilipiga hesabu nikasema nikiokota na zile za kawaida angalau mfano cycle, coordinate geometry, function, n.k nitakuwa na uhakika wa kupata D. Hakika yule jamaa kila siku saa4 usiku baada ya kutoka prep alikuwa anaacha kazi zake zote anajitolea kunifundisha mimi na alikuwa ananipa home work. Huyu jamaa mpka leo namshukuru sana na mpka saiv tunawasiliana na mara nyingi namkumbushaga msaada wake kwangu na nampaga maua yake sana.
Matokeo yanatoka hivi nina D kweli ya hesabu na ndo somo pekee ambalo nina D kwenye chet changu aisee asingekuwa yeye nisingeweza kusoma comb ambayo nilienda kuisoma advance na hatimaye mpka saiv nipo hapa nilipo.
Kama mjuavyo cheti muhimu hasa katika safari ya elimu bila kipingamizi ni chet cha O level kwasabab pale ukimess up ni kurisit mtihan au kwenda direction ambayo haukuwa na ndoto nayo.
Binafsi mm msomo ya arts nilikuwa nayaweza ila nilikuwa sina mpango nayo kabisa kwahiyo sayansi bila hesabu ni uongo na advance nisingeenda kwasabab nisingeweza kukubali kuona naenda kusoma comb za arts labda ningerisit hesabu.
Conclusively, nimeamini Mungu huwa anatuma malaika wake kupitia mtu yeyote ambaye atakuwa amemchagu kwani yule madam alikuwa ni miongoni mwa walimu ambao nilikuwa nawasumbua sana na ilipelekea mimi na yeye tuwe maji na mafuta. Huyu brother yeye pia hatukuwa na ukaribu kivile kwasabab yeye alikuwa mtulivu na mm nilikuwa muhuni wa kishamba kwahiyo tusingeweza kuwa washikaji lakini ndo hivo akaja kuwa msaada mkubwa kwangu.