Mipaka ya Chama Tawala na Ukomo wake, Vipi kuhusu kambi kuu ya Upinzani Bungeni

Mipaka ya Chama Tawala na Ukomo wake, Vipi kuhusu kambi kuu ya Upinzani Bungeni

Kutoka CCM sio kwa kuvutwa, ni kwa kukosa nafasi wakati upinzani kwenda CCM ni maslahi.

Mkuu huwezi kuwa serious, Bashe hata kusimama na Lissu hawezi ndio useme asimame na mama?
CCM wana uhaba wa viongozi wenye mvuto kwa sasa, Mama mwenyewe ni sababu ya dola tu lakini ndio hayohayo.
Bashe kusimama na Lissu hawezi ila kusimama na Mama anaweza..
Kumbuka Bashe anaweka Kiasi kupata ushawishi ila kwa lissu kwa sasa Anakosa Mvuto sana..

Mi naona Mvuto mwingi unaanza kurudi kwa Mbowe kama ilivyokuwa mwaka 2005..Mbowe alivyokuwa wamoto..

Kuhusu Mvuto ni kwli CCM kwa sasa Viongozi wanalazimisha kupendwa ila na wenyewe wanajua hawapendwi
 
Inaonekana no hatari kwasababu chama Tawala kinawaambia wananchi Kila chaguzi kwamba mkichagua upinzani kutatokea vita!!

Aibu sana hii!!

Hakuna uhatari wore,Kwa mfano mbowe anaenda kuwa waziri mkuu au Lema hapo Kuna hatari gani !!?kama watu wenyewe hao wameshinda ikulu kila siku wakinywa chai ma kikwete na samiah Kwa nyakati tofauti!!?

Mimi ni mdau wa serikali mseto japo no mwanachama was chama Tawala najua itachochea maendeleo na kutokomeza ufisadi Kwa kiwango fulani!!
Mkuu Sikuwa na maanishi Hatari unayoisema wewe ya Vita au yoyote ile iliyofikiriwa..

Hata Hivyo Serkali mseto inakuwa Nzuri pale ambapo Naibu Rais/Makamu wa Rais ndiyo anakuwa Mpinzani ila waziri mkuu akiwa mpinzani Huwa ni kama kuna ugumu sana wa rais kutenda baadhi ya mambo
 
Nimesema rais halazimiki kuteua mawaziri wapinzani.

Ni msingi mkuu wa kuitwa chama tawala ni kushinda urais
Halazimiki ila lazima ashauriane na waziri mkuu ambaye ni Waziri kutoka Upinzani?
Kwahyo kitendo cha kushaurina na waziri mkuu ambaye sio wa chama chake huoni kama atalazimika?
Screenshot_20240221_121116_Adobe Acrobat.jpg
 
Yeah wabunge wa Upinzani watakuwa wengi..
NAtamani nijitose nichukue Jimbo langu
Jambo Zuri Ila , kama ni mtumishi wa serikali Yan (mtumwa) , akaenda upande wa chadema itakula kwako.

Jk alibadilisha Sheria ya Kwamba mtumishi wa serikali AU (mtumwa) hapasi kushiriki siasa.

Jk alirudusha Sheria ya ukoloni ya m UK , ya Kwamba ukiwa mtumishi wa ukoloni hupasi kuwafanya siasa.

Tulivyo upata uhuru nusu, Sheria ikabadilishwa MTU yoyete ana haki ya kushiriki siasa Kwa kufuata Sheria za nchi.

CCM ya jk wakabadilisha wakarudisha ile ya mkoloni, ili kuondoa ushindani kwenye siasa, kumbuka kipindi hicho wasomi wengi walingia kwenye siasa hasa vyama vya upinzani, nakuipa challenges CCM,

Kilichotokea ni Historia , kila MTU Anaye jihusisha na siasa inabidi awe chawa
 
Halazimiki ila lazima ashauriane na waziri mkuu ambaye ni Waziri kutoka Upinzani?
Kwahyo kitendo cha kushaurina na waziri mkuu ambaye sio wa chama chake huoni kama atalazimika?
View attachment 2911005
Ukweli ni kuwa kuna mengi ya kurekebishwa katika katiba iliyopo kama tungekuwa na uchaguzi huru na haki. Kama kwa mfano CCM ikashinda urais na Chadema ikawa na wabunge wengi na kuwa na Waziri Mkuu, kwa vyo vyote vile Rais atashindwa kuunda serikali anayoitaka. Hivyo kitakachotokea ni Rais kuvunja serikali na kuitishwa Uchaguzi Mkuu mpya vinginevyo Rais ataondolewa madarakani kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye na kupelekea kuitishwa kwa Uchaguzi Mkuu mpya.
 
Just imagine CCM ikapata wabunge 50 halafu wote sio wasomi..
Ila wabunge wa Chadema na vyma vingine wakawa 290 huko na wengi ni wasomi itakuwaje?
 
Kuna kitu nime note, 2025 huenda chadema wakawa na wabunge wengi bungeni > ccm.
Hiyo iko wazi,CCM kwa upande wa wabunge watapoteza sana,hivyo kupelekea kua na wabunge wachache(kwao CCM) na wengi(kwa CHADEMA).
Watamkumbuka sana JPM wale waliobebwa kupitiliza.
Mama Samia yeye atapata kura za wastani kama atagombea.
 
Just imagine CCM ikapata wabunge 50 halafu wote sio wasomi..
Ila wabunge wa Chadema na vyma vingine wakawa 290 huko na wengi ni wasomi itakuwaje?
Rais hawezi kutawala kama hana wabunge wa kutosha kwa kuwa hata ile bajeti ya Bunge la kwanza haiwezi kupitishwa! Sasa bila fedha Rais ataendesha vipi serikali?
 
Rais hawezi kutawala kama hana wabunge wa kutosha kwa kuwa hata ile bajeti ya Bunge la kwanza haiwezi kupitishwa! Sasa bila fedha Rais ataendesha vipi serikali?
Basi katiba Mpya ipitushwe Kabla ya 2025
 
Kenya Na zanzibar ni tofauti wao walitoa Makamu wa Pili wa Rais..

Kutoa Waziri Mkuu maana yake msimamizi wa Shughuli zote za serkali awe wa chama Pinzani vipi kama akipeleka hoja Ya kutokuwa na Imani na Rais Bungeni?
Kwa hii katiba ilivyo ya kipuuzi rais anaweza kuendesha nchi bila kusikiliza bunge. Yule mwenye maamuzi na vyombo vya Dola ndio muamuzi wa Kila kitu.
 
Ila 2015 ulikuwa mwaka Bora Sana wakitaka Wapate Wabunge wengi sana kuliko Miaka yote nawashauri Watu wafuatao wawavute waende Upinzani..
A.Majaliwa
B.Ndugai
C.Bashe
Na ikiwezekana Bashe ndo awe mgombea Urais..

Nimewapa strategies hizo Bashe akisimama Na mama wanaweza kushinda
Unataka kuwaingiza mkenge hao wapinzani kama walivyoingia mkenge kwa Lowassa 2015? Hata hivyo hayo usemayo ni bure tu, maana kwa mazingira haya, Tanzania hakuna uchaguzi, Bali Kuna maonyesho ya ujinga wa mtu Mweusi kwenye box la kura. Kwanini hao wanaccm unaowataja wasianzishe chama chao waje washinde uchaguzi?
 
Rais hawezi kutawala kama hana wabunge wa kutosha kwa kuwa hata ile bajeti ya Bunge la kwanza haiwezi kupitishwa! Sasa bila fedha Rais ataendesha vipi serikali?
Hivi unafahamu Kutokupitisha Bajeti Pekee Kunaweza kumfnya Rais Avunje Bunge Lote na uchaguzi urudiwe?
 
Hivi unafahamu Kutokupitisha Bajeti Pekee Kunaweza kumfnya Rais Avunje Bunge Lote na uchaguzi urudiwe?
Ndivyo ilivyo! Kwa hiyo kama chama cha Rais kitakosa wabunge wa kutosha kupitisha bajeti, lazima serikali ivunjike!
 
Ndivyo ilivyo! Kwa hiyo kama chama cha Rais kitakosa wabunge wa kutosha kupitisha bajeti, lazima serikali ivunjike!
Kwani Rais ndo anaandaa bajeti?
Bajeti inaandaliwa na wizara kutokea majumuishi ya chini ya kusector
 
Hili swali hata mimi naomba kuuliza japo nimelikuta mahali.

Naomba kuuliza swali? Kuwa chama tawala kunatokana na kushikilia mhilili wa Serikali, mhimili wa Bunge au vyote viwili?

Mfano;
Chama cha Mapinduzi CCM kikishinda kura za urais na ndio kikaunda serikali..

ila Bungeni CHADEMA ndio ikawa na idadi kubwa zaidi ya wabunge tuchukulie Mfano Chadema ikawa na Wabunge 198 ACT 62 na vyama vingine 20 na Chama cha mapinduzi wakawa ina idadi ya wabunge 110..

kwa maana hiyo Chama cha CCM kitaunda kambi rasmi ya upinzani bungeni?
Au CHADEMA?

Hapo chama tawala ni Chama CHA MAPINDUZI au CHADEMA au CHADEMA na CCM kwa pamoja?

Cred..Thomas Kibwana..
Unfortunately Rais anaruhusiwa kuvunja bunge na wakarudi kwenye uchaguzi. Since hakuna mbunge anaweza risk hilo ina maana watahamia CCM mara baada ya tu ya uchaguzi.

Hata Kenya tuliona hili, Odinga alikua na wabunge wengi ila Ruto alishinda urais. Ikabidi tu wabunge wengi wa odinga waunge mkono juhudi otherwise wangekosa miradi ya kiserikali n.k

Hivyo tunahitimisha kwamba anayeshinda Urais ndio atahodhi bunge hivyo hata upinzani ukishinda wabunge wengi bado hawawezi mchallenge Rais sababu ya katiba iliyompa umungu mtu Rais wetu
 
Back
Top Bottom